he Character of False Teachers. Galatians 5:8-9 Pt.2

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 6 views

The Character of false teachers Pt.2

Notes
Transcript

Mapitio:

Leo tunaendelea na mafundisho yetu kwa kitabu cha Wagalatia. Kitabu hiki kimejaa na mambo mingi sana kwa maisha yetu ya sisi wakristo. Lakini kitu cha umuhimu zaidi tumeona kwa kitabu hiki na ni mandhari ya kitabu cha Wagalatia ni kuhesabiwa haki kwa imani. Kila dini kwa hii dunia iko na kitu unafanya, iko na matendo lazima unafanya kupata wokovu, lakini kwa Ukristo ni kitu moja tu na ni kuamini, ni kuweka imani yako katika Yesu kristo. Maisha yake aliisha hapa wakati alikuwa. Alikuwa kamilifu, hajatenda dhambi hata mara moja na Biblia inasema bado alikuwa kama sisi, alikuwa na hii mwili, alijaribiwa, alijua njaa, alijua kuwa na kiu mingi, alijua kufanya kazi na kutoa jasho, alikuwa kama sisi lakini bado bila dhambi. Pia ni kuamini katika kifo chake na maana yake. Yesu hajatenda kitu moja kibaya, hajakosea na mwengine lakini bado walimwua yeye. Kifo chake ilikuwa lazima kuokoa watu wake kutoka dhambi zao. Wajeshi waroma walimpiga yeye hata Bibilia inatuambia walmpiga mpaka hata huwezi jua uso wake. Tunasoma Kitabu cha Isaya 52:14 (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), Na Yesu alikuwa bila dhambi, baada ya hii alibeba msalaba wake, ilikuwa uzito karibu 70kg kwa mgongo wake meter mia sita mpaka alifika mahali inaitwa Golgotha, Yaani Fuvu la kichwa.
Alifika na walimweka msalabani na alikaa hapo mbele ya watu wote kuteseka maa saa sita na alikufa. Maneno yake ya mwisho zilikuwa “IMEKWISHA”. Wokovu ilinunuliwa dakika ile. Damu ya kondoo ya Mungu ilimwagika siku ile, sadaka imetolewa juu ya madhabahu kwa dhambi za watu wake. Mwili wa yesu iliwekwa kaburini na baada ya siku tatu Mungu alimfufua katika wafu. Kifo na mauti ilishindwa na Yesu kristo, nguvu ya kaburi ilivunjwa siku hiyo na alikaa hapa siku arobaini na watu zaidi ya mia tano walimwona yeye hata waliongea na yeye. Siku moja Yesu alisema anarudi tena kuchukua watu wake na kuleta hukumu kwa wasioamini na hii dunia itaharibika kabisa na atajenga mbunguni na dunia mpya. Hii yote, kuamini hii yote na kuweka imani yako yote kwa vitu hivi ni kuhesabiwa haki kwa imani. Uikona hii yote hakuna kitu cho chote sisi tumefanya, kila kitu ni kumhusu Yesu na ushindi wake. Hakuna kitu mimi ninaweza kuongeza kwa hii, nikijaribu kuongeza kitu itakuwa taka taka, itaharibu neema ya Bwana wangu. Nitauliza, na wewe je, umehesabiwa haki kwa imani? Au bado unajaribu kuongeza vitum bado unajaribu kuongeza matendo yako kusaidia ushindi wa yesu kristo? Natumaini sana unasema hii ni ujinga na sisi hatuna kitu tunaweza kuleta kusidia wokovu wetu, tunaamini tu.
Sasa tunafika mahali hapa kwa kitabu cha Wagalatia na Paulo anasema wakristo wa kanisa hili walijua hii yote, walisikia kila kitu sisi tumesikia saa hii na waliamini na tuliona wiki ilioptia Paulo aliuliza hawa Wagalatia 5:7 Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Na sisi tuliona ilikuwa walimu wa uongo waliingia na wametoa macho ya watu kwa yesu na wanajaribu kurudisha hawa chini ya sheria. Hawa walimu wa uongio wanajaribu kusema huwezsi kuwa Mkristo bila kutahiriwa. wamefanya nini? Wameongeza tohara kwa ushindi wa yesu. Fikiria hii. Baada ya hii yote tumesema kumhusu Yesu, Aliishi maisha kamilifu, alikufa msalabani na alifufuka kutoka wafu, watu wanajaribu kusema kwa sababu ya ngozi kidogo lazima inakatwa kuokoka. Tutaona baada ya wiki mbili kama Paulo alifikiri kuhusu hawa watu lakini angalia vs.12 Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao! Hii likuwa kali sana. Lakini hata mimi wakati ninasikia walimu wa uongo au watu kujaribu kusema lazima unafanya hii, ama hii ama hii, lazima unaomba hii sali fulani, ni lazima pastor yako anakuombea, lazima unakufa njaa kuona yesu, hata mimi nataka kusema kitu kali pia, kwa sababu ni uongo na inaongeza vitu kwa kazi ya Yesu, na yeye hana hitaji kwa msaada wako. Ni kama kufikiri unaweza kuleta roho mtakatifu kwa mtu kwa njia ya fresh fri! Roho Mtakatifu ni Mungu, sijajua yeye anasihi kwa mafuta. Natumaini sana umeanza kuona uongo wa hii ujinga wa binadamu. Sitaki kusema siku moja kwa kanisa hili Mlikuwa mkipiga mbio vizuri, ni nani aliyewazuia msiitii kweli?
Kwa mistari yetu leo tunaona Paulo anaendelea kueleza kuhusu hii na tutaona matokeo ya hii kwa kanisa lao. Wagalatia 5:8-9 Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.  Chachu kidogo huchachua donge zima. Tunaona hapa kwamba tabia ya wale walimu wa uongo ni mbaya, si mzuri. Kwa sababu Paulo hapa anasema hii mafundiisho yao haijatoka Mungu. Hawa walimu wa uongi walikuwa na wivu mingi sana kwa sababu kabala ya Yesu walikuwa na kazi mingi sana kufuata sheria ya Mungu, sasa Yesu alikuja na alitimiza sheria Mungu kwetu na alileta uhuru kwetu na sisi hatuna hitaji kwa hawa na kazi yao. Sasa ni wewe na yesu, wewe unaweza kuongea na Mungu peke yako, wewe wakati uko dhambini unaweza kutubu kwa dhambi zako bila mkuhani. Hawa watu wamejiapata bila kazi na walitaka kuendelea kuongeza vitu kwa wakristo ili hawa wenyewe wanawezi kuwa muhimu tena.
Lakini tunaona Paulo anasema Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. Anakumbusha hawa kwanza wameitwa. Ni hawa wameitwa kwa wokovu, wameitwa hata kuingia hii mbio za ukristo. Ni Mungu amebadilisha mioyo yao na Paulo ameshaa waambia hawa Mungu anafanya hii naam na gani. Kumbuka Wagalatia 1:6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Waliitwa katika neema ya Kristo, kama sisi sote. Ikiwa wewe unaketi hapa leo asabuhi na wewe ni Mkristo, umeitwa na Mungu katika neema ya Kristo. Hii neema ni kitu mabacho hakuna mtu anastahili. Ni kitu ambacho umepata bila kufanya kitu cho chote. Hii kitu ni kwa wenye dhambi na hawa watu wameamini na wameweka imani yao katika Yesu kwa samaha. Yeye amabye anaitwa ni Mungu, watu ambao wameitwa ni wenye dhambi a njia ambaye anaita hawa ni neema yake. Hii ni sababu Paulo anasema hii mafundisho wanasikia na wanafuata haijatoka Mungu lakini ni walimu wa sheria na ni uhalali (legalism). Mafundisho ya uhalali inatoka baba ya uongo na hii ni shetani. Ikiwa ni mtu ambaye anataka sisi kujiamini na kuweka imani yetu katyika matendo yetu ni shetani. Yeye anajua kazi yetu, matendo yetu tunafanya haziwezi kutusaidia kufika mbinguni, wakati tunaanza kuamini tunaweza kutenda matendo ya kutosha kupata wokovu, kuliko kuweka imani yetu katika Yesu peke yake, hii ni mafundisho ya mapepo. Ikiwa wewe unaenda kanisa ambalo wanafundisha hii, tafadhali kimbia haraka, ikiwa unajua watu ambao wanaenda kanisa ambalo linafundisha matendo yako ni lazsima kupata wokovu, waambia hawa kukimbia haraka.
Hii si mchezo na siku moja hawa watu watasimam mbele ya Mungu na watafikiri wako sawa kwa sababu wameishi maisha mzuri, wametenda matendo mazuri sana na watasikia sauti ya Yesu na watashangaa. Kumbuka Mathayo 7:22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Hakutufanya, na kwa jina lako na kwa jina lako, matendo, matendo , matendo, Tumefanya hii, tumefanya hii katika jina lako Yesu, Hawa watu ni watu ambao wamefikiri wanafanya kazi ya Yesu na kwa matendo yao bila shaka hata sisi tutafikriri wako sawa, wamefundisha, walitoa mapepo bila shaka katika jina la yesu, wametenda miujiza mingi, katika jina la yesu. Na vs.23 Yesu anasema Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Shida yao ilikuwa nini? Hawajaweka imani yao katika Yesu peje yake, hawajaamini katika neema yake, walijaribu kuongeza kwa kazi ya Yesu. Walijaribu kusema ni mimi na Yesu pamoja, nataka wewe kujua, si wewe na Yesu pamoja, na ninyi wawili unjaribu kuokoa wewe, si mimi na Yesu pamoja na sisi tunaniokoa, ni Yesu peke yake na hii kazi imeshaa fanyika, sasa ni wewe kuamini na kuweka imani yako katika Yesu.
Sasa labda swali lako ni hii, Travis unasema nikienda kanisa haiwezi kusaidia wokovu wangu? Ndiyo haiwezi, Travis nikitoa pesa zangu kusaidia jirani yangu haiwezi kusaidia wokovu wangu? Ndiyo haiwezi. Travis ikiwa mimi nitaenda bible school miaka nne na ninahubiri neno la Mungu na mimi nitakuwa pastor ya kanisa kubwa, haiwezi usaidia wokovu wangu? Ndiyo haiwezi. Hii yote ni vitu ambavyo unafanya kwa sababu Yesu ameshaa fanya kazi yake moyoni mwako, wewe umeokolewa tayari. Sasa hii inaitwa matunda ya wokovu wako, hii ni matunda ya wokovu si vitu amabavyo unatenda kupata wokovu. Kweli kweli bila matunda haya maishani yako, bila kuwa na matunda ya roho maishani yako, ni mzuri kuuliza ikiwa wewe ni mkristo ukweli, bila kuwa na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi maishani yako ni kusema Yesu hajafanya kazi moyoni mwako, hujakuwa kiumbe kipya. Lakini kufanya vitu hivi hakuna siku utapata wokovu wako. Kama Paulo anasema kwa hawa ya Galatia, Tohara haiwezi kusaidia mtu kuokoka. Na hii haijatoka yeye ambaye aliwaita na neema yake kupata wokovu.
Hii iko na matokeo mingi sana kwa kanisa la yesu. Paulo anaendelea kusema, mafundisho kama hii, walimu wa uongo kuingia na kuharibu watu iko na matokeo mingi sana. Angalia vs.9 Chachu kidogo huchachua donge zima.
Related Media
See more
Related Sermons
See more