The Character of False Teachers Pt.3
Galatians • Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 5 viewsNotes
Transcript
Wagalatia 5:10-12
Wagalatia 5:10-12
Leo tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano mstari wa kumi hadi kumi na mbili. Kweli kweli tumeona kitabu hiki imejaa na mambo mingi sana na ni tamu kwetu wakristo kuona na kujua vitu hivi. Natumaini sana unaina faida ya kufundisha bibilia kwa kila mstari na kutoa mizigo ndani yake. Sisi tunasema ni kama tuko na mfuko na tunatoa kila kitu kwa hii mfuko kuona ni nini iko ndani. Hakuna tofauti kwa bibilia, sisi tunataka kutoa kila kitu kwa kila mstari ili tunaweza kujua maana ya Mungu, unajua kitabu hiki ni neno lake, na sisi hatutaki kukosa kujua anatuambia nini? Hii ni shida ya kanisa mingi, ya wahubiri wengi, wanatoa kwa neno la Mungu vitu ambavyo Mungu mwenyewe hajaweka ndani, hii ni sababu tuko na uongo wingi sana kwa makanisa siku zetu.
Kusema ukweli wakati tunakosa kupata Mungu anasema nini kwa neno lake tunaweza kujipata kama tumesoma kwa wiki mbili kwa kitabu hiki na walimu wa uongoi wanaingia na wanadanganya kanisda la Yesu kristo na baada ya muda unapata kama tumesoma wiki iliopita walimu wa uongi wanaingia kwa siri na wanafundisha uongo na watu wanaanza kufuata hii uongo na vs.9 ya Galatia 5 inasema Chachu kidogo huchachua donge zima. Na wiki iliopita tuliangalia sana maana yake ya hii na kama kiazi moja inaharibu gunia nzima na viazi kwa sababu ya kuoza, hata mtu moja ama mbili ya uongo wanaweza kuharibu sisi sote.
Leo tunaona Paulo anaendelea kusema kwa vs.10a. Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. . Kwa hii mstari tunaona Paulo anasema ako na Matumaini kwa hawa wakristo kwa kanisa hili. anajua wamefundishwa vizuri, anajua hawa wanajua ukweli, wanajua Yesu ni nani na wanajua Yesu ameleta huru kwao. hii neno matumaini hapa inaweza kuwa imani pia. Ako na imani na sii kwa hawa lakini ukiona mstari inasema katika Bwana. Kwa sababu hawa wamefundishwa ukweli na wanajua ukweli ako na tumaini kwamba watafuata Mungu na ukweli wake.
Ni mzuri ninyi yote unajua kitu. Kwa sisi ambao ni pastor ya kweli, na tunajaribu kufundisha watu wetu neno la Mungu, na tunataka hawa kuwa na uhusiano na Mungu na kutii neno lake, tuko na tumiani kama Paulo. Tuko na tumaini kwamba Yesu ameingia maisha yako kweli kweli na amekubadilisha, tuko na tumaini kwamba Roho Mtakaitfu anaishi ndani yako na wakati unaanza kuona hii uongo na walimu wa uongo utajua ukweli, na ikiwa unaanza kufuata hii uongo, utarudi haraka kwa sababu ya Roho ambaye anaishi ndani yako na kwa sababu ya ufahamu wako kuhusu ukweli wa neno la Mungu utarudi haraka. Hii ni tumaini la Paulo hapa na ni tuamini langu kwako. NA tuko na hii tumaini kwa sababu ya Mungu wetu. Tumaini letu ni utakumbuka kama Paulo alisema kwa vs.5-6 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo. Kama vs.7 ilisema walipiga mbio mzuri, walijua kukimbia vizuri na walitoka njia kidogo na alikuwa na tumaini watarudi kwa hii njia ya kweli.
Paulo aliwaambia wakristo wafilipi kitu kama hii pia Wafilipi 1:6-7 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kutetea Injili na kuithibitisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii. tumaini la hii ni ikiwa mtu ni Mkristo atavumilia. Hawataangamia. Ikiwa mtu ni Mkristo kweli kweli, kumbuka wakati ninasema kweli kweli ni kummanisha si Mkristo ya mdomo tu, si mkristo kwa sababu baba na mama na pastro yake lakini mtu ambaye Yesu kristo amebadilisha mioyo na akili yake, kweli atavumilia. Yesu alisema kwa kitabu cha Yohana 10:27-28 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Ikiwa Yesu ni Mungu na Mungu ni juu ya kila kitu na Mungu ni Mkuu nani anaweza kututoa kwa mikono wake. Ni yeye ametuokoa, wakati sisi ni wake, sisi ni wake. Kusema ukweli Yeye ni Mchungaji wetu, tunafuata yeye, Angalia Yohana 10:4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Hii ni Yesu na sisi halafu angalia vs.5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. Sisi ambao tunafuata Yesu ukweli hatuwezi kufufata mwengine. Hii ni ngumu, lakini tena ni rahisi. Sisi tunaina watu wengi sana wanasema hawa ni wakristo lakini wanafuata uongo zaidi, tutasema nini? Mchungaji wao si Yesu kweli kweli na wanafuata mgeni amabye ni uongo, hawajui Yesu, Hawajaokoka kweli kweli. Ukifahamu bibilia inatusaidia sana kujibu maswali mingi, kuhusu maisha haya, watu wengine, wokovu wa kweli.
Hii ni sababu Paulo alisema kwa wakristo wagalatia ako na tumaini, kwamba wataendelea, watavumilia katika ukweli, watarudi haraka ikiwa wameanza kutoka kwa sababu ya Mungu, hawezi kupoteza hata mtu moja ambaye ni wake ukweli.
Rudi kwa Wagalatia mlangio wa tano na Paulo anaendelea kwa vs.10b kusema Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote. Walimu wa uongo mbele yao si mzuri. Walimu ambao wanaongoza watu wa Mungu kwa njia nyingine hatima yao, mbele yao ni hukumu. Yesu alisema kwa kitabu cha Mathayo 18:6 bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. Kufanya hii si kitu kidogo. Paulo anasema huyu mtu ambaye anafanya hii atachukua hukumu yake. Kusema ukweli ni mzuri kwetu sote kusikia hii, mimi zaidi, kwa sababu mara mingi unaangalia kila mahali na iko na hii uongo na unashangaa. Hata unajaribu kuonyesha watu ukweli na wanataka uongo zaidi, kwa nini? Kwa sababu mafundisho ya uongo inasema ikoswa kujipendeza na kufanya kama unataka. Ukiangalia ndani unaona haraka, hawataki Yesu, wanataka vitu vya mwili wao, tamaa za hii dunia. Inaweza kuhimiza mioyo yetu kujua, siku moja hata hawa watasimama mbele ya Mungu kutoa majibu kwa maisha yao. Siku ile inakuja na watabeba hii uzito wa hukumu yao. Hata Petrio anaongea kuhusu watu wale anagalia Waraka wa pili wapetro 2:2-3 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
Wagalatia 5:11 Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika! Mafundisho ya uongo ni kitu ambacho inaleta shida mingi sana kwa kanisa la Yesu Kristo. Kusema ukweli kwa dunia, wasioamini, watu wa nje, hawa wote wanaona sisi sote ni kitu moja. Wanaona hii uongo wa Mombassa na kwa sababu iko na jina kanisa kwa ile nyumba wanasema sisi oste ni the same. Wanaona mapastor wingi wanaweka mimba kwa wasichana na wanadanganya watu kuiba pesa zao na wanasema sisi sote ni moja tu. Kwa sababu watu wako na jina “Kanisa” mbele ya nyumba kwa macho yao sisi sote hakuna tofauti. Hii ni sababu ni mbaya sana wakati hii uongo wote inafanyika kwa sababu hata sisi tutateseka kwa sababu ya hawa.
Walimu wa uongo wanawatesa walimu wa kweli. Kwa nini? Kwa sababu hawataki sisi ya kweli kufichua matendo ya maovu. Ni mzuri ninyi unajua Shetani anapigana na Mungu, na dini ya kishetani inapigana na imani ya kweli. Sisi tunajua ni bure kabisa kwa sababu shetani hawezi kushingda lakini bado anajaribu. Hawa walimu wa uongo kwa kitabu cha Galatia wamejarubu kusema Paulo amefundisha kutahiriwa kama hawa. Labda unakumbuka Timotheo, Paulo alimtayarisha kwa sababu alikuwa half cast, alikuwa myahudi nusu na mgiriki nusu. Na Paulo alijua hii itakuwa shida ikiwa Timotheo alifanya kazi na wayahudi. Lakini Paulo hajafundisha kama hawa ya uongo kwamba ni lazima kutahiriwa kuokoka. Paulo anasema ikiwa ninafundisha kama hawa, kwa nini bado anaudhiwa? Ni swali nzuri. Kwa nini wanaleta shida kwake ikiwa yeye ni kama hawa? Paulo alijua ikiwa anafundihsha kama hawa, wokovu wa Mungu haingekuja kwa njia ya neema yake lakini kwa sheria. Ameshaa waambia hawa Kwa Wagalatia 2:21 Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, na njia ya sheria ni nini? Ni kufuata torati na kutahiriwa na hii mambo yote ya agano la kale, na ikiwa haki au wokovu inakuja kwa hii njia anaendelea kusema basi Kristo alikufa bure. NA sisi tunajua Kristo Hajakufa bure na wokovu ni neema ya Mungu.
Paulo anasema mwisho ya Wagalatia 5:11 Hapo kwazo la msalaba limebatilika! Sasa maneno haya ni muhimu sana, na ni muhimu sana kwetu kushika hata kwa siku zetu. Ikiwa Paulo hajafundisha ukweli, ikiwa hajabishana na wapenda sheria, maisha yake ingekuwa sawa. Hata sisi mara mingi sana tuko na nafasi kusimama kwa ukweli wa Yesu na tunanyamaza. Hii si kusema kuingia na kuoigana na watu kupigana tu, lakini wakati tunasikia uongo au vitu amabvyo watu wanaongeza kwa neno la Mungu na wokovu wake, ni lazima katika upendo tunasimama na tunasema ukweli.
Hawa wapenda sheria wamekataa Masihi Alikuwa Yesu, hawawezi kubali, alikuwa maskini, dhaifu na alikufa msalabani, msalaba ilikuwa ayibu na Masihi yao hawezi kufa naam na hiyo. Msalaba ilikuwa kikwazo kwao. Kitu kiingine msalba ilifanya, ilitoa vitu vya nje kwa hawa, au matendo yao kupata haki mbele ya Mungu, sheria ya Musa na tohara. Msalaba ilikuwa shida kwa wayahudi kwa sababu haijalazimisha watu kutii sheria za mababu. Labda unakumbuka wakati waliua Stefano. Unakumbuka shida yao na Stefano? Unakumbuka walisema nini wakati walianza kutupa mawe na kupiga yeye? Angalia Matendo 6:13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati; Mahali hapa ni heakalu na torati ilikuwa sheria zao. Wamekasirika na Stefano si kwa sababu ya Mungu lakini kwa sababu ya vitu amabvyo wameweka imani yao, vitu ya nje. Ukiangalia vs. 14 maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa. Yesu na Mslaba wake kilikuwa kikwazo kwao. Paulo alwaambia kanisa la korintho kwa waraka wa kwanza wakoritnho 1:23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; Hata leo hii inaendelea kwa dunia yetu.