The Battle within Pt.1

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 12 views
Notes
Transcript

Galatians 5:17-19

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango 5:17-18. Hii sehemu ya maandiko vs.17-26 tutaona mambo mingi sana, mimi ninapenda kuita hii sehemu vita ambaye ni ndani. Ni vita ndani ya kila Mkirtso, Ikiwa wewe unapumua saa hii na wewe ni Mkristo, ukovitani. Hizi mistari zinatuonyesha hii vita ni nini na ni nani tunapigana. Pia tunaweza kuona mtu ambaye ni Mkristo kweli kweli namtu ambaye si Mkristo. Kwa wiki mingi tumeona Wakristo wagalatia walikuwa na shida, hii shida ilikuwa walimu wa uongo wameingia na walianza kuwaambia hawa ni lazima kufanya tohara kujua mtu ameokoka. Hii ilikuwa uongo sana, hawa walimu wa uongo kama wingi leo wameongeza matendo ya binadamu kwa wokovu, sisi tunajua hakuna kitu cho chote tunaweza kufanya kuoata wokovu lkaini kama Bibilia inasema ni zawadi au neema ya Mungu na ni yeye Alitupea. Tuliona Paulo kusema kwa nini umedanganywa, ulikua ukweli, ulikuwa na uhuru kufuata Yesu bila hi uzito wote. Hata leo asabuhi sisi sote tuko na hii uhuru kuwa watoto wa Mungu bila hii uzito wote watu wanajaribu kuweka. Huwezi kufanya matendo mazuri ya kutosha, huwezi nunua kwa pesa zote za dunia, rangi yako, kabila yako haina maana, Hakuna mtu hata moja anaweza kusema angalia kama niemfanya kupata hii, kwa sababu yote ni ya Yesu, kila kitu cha maisha haya ni kumhusu Yesu si wewe.
Tumeona tuko na uhuru katika Yesu lakini wengi wanatumia hii uhuru vibaya na wanajileta shida mingi, na dawa ya hii yote ni upendo. Kupenda wenzetu kama nafsi zetu, na bila kufanya hii tutapigana ndani, tutaharibu jirani yetu na tutaleta ayibu kwa Bwana wetu.
Leo Paulo anaendelea kusaidia Wakristo wagalatia kujiangalia, kujipima na kutembea kama wakristo. Tusome Wagalatia 5:16-24 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tuombe: Baba wetu tunasema asante kwa wakati wetu leo kuingia mbele yako na kukuabudu kwa njia ya kuomba na kuimba na kufungua neno lako, tusaidia kuweka kila kitu ambacho tumeingia hapa naye leo asabuhi kando, na kuweka mawazo yetu kwako na neno lako, tafadhali fungua macho na mioyo yetu kusikia kama unasema leo na nisaidia kudfundisha kama neno lako inasema. Tunaomba hii yote katika jina la Bwana wetu Yesu kristo, Amin.
Kama nilisema hii sehemu ya maanadiko inatuonyesha vita ambavyo imekuwa ndani ya watu tangu mwanzo, na hata leo inatusaidia kufahamu sbabu watu wanafanya kama wanafanya. Tukiangalia Historia yote kusema ukweli imekuwa vita ya viwango vya Mungu na Mwili wa mwanadamu na tamaa zake. Sasa kwa Mkristo, sisi sote ambaye tumeokoka kweli kweli na tunatii neno la Mungu masihani yetu tumekuwa kiumbe Kipya, maana ya hii ni nini? Angalia Kitabu cha Ezekieli 36:26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Tuko na mistari tatu kwa agano la kale zinatuambia hii, maana yake ni wakati sisi tulikuwa wasioamini mioyo yetu yalikuwa kama jiwe, ngumu, baridi lakini Mungu alitupea mioyo mipya. Unajua jiwe ni kitu ambacho haina uhai, ni wafu, iko tu, na Mungu alitoa ile moyo wa mawe na alitupea mioyo wa nyama, nyama iko na uhai, nyama si baridi. Na pia alisema nitatia roho mpya ndani yao. Roho zetu zilikuwa wafu kabisa na kama Mungu anafanya kwetu kama alifanya kwa Adamu. Angalia Mwanzo 2:7b. akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Mungu anapumua uhai ndani yetu, Anatupea Roho yake. Angalia Waefeso 2:1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; Moyo ilikuwa jiwe, hakuna uhai. halafu vs. 4-5 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Hii Roho ni Nani? Ni Roho Mtakatifu. Ni Roho ile ile tunasoma kwa umbaji wa dunia kwa Mwanzo 1:2b Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Ni Yeye. Kumbuka wakati Yesu anaongea na wanafunzi wake na aliwaambia hawa baada ya yeye atatoka Yohana 15:26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. Hii Roho wa kweli ni Roaho Mtakatifu. Halafu tunasoma kwa Waraka wa kwanza wakorintho 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Tunaona hapa Huyu anaishi ndani yetu, inasema Anakaa ndani yetu. Si wakati unaingia kanisa jumapili na pastor fulani anakumwaga na fresh fry na unapokea, hii ni uongo, kusema ukweli ni roho ingine anaingia watu si ROho ya kweli. ROho ya kweli anakaa ndani yetu kwa sababu sisi wakristo ni hekalu ya Mungu.
Halafu tunafika mstari yetu ya leo na Paulo anawaambia wakristo wagalatia Kwa 5:17a. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, Roho gani? Roho Mtakatifu. Tuko na hii amri kumpea Roho Mtakatifu udhibiti wa maisha yetu, ako juu ya mwili wetu, na roho zetu. Wakati tunafanya hii atatusaidia kushinda mwili wetu na tabia yetu ya zamani. Paulo anasema Enendeni. Maana ya hii ni kila kitu cha maisha yetu, hii inaweza kuwa Mkristo na msioamini, sisi sote tunaenda. Maana yake ni maisha yetu, ni tabia ya maisha yetu kila mtu anaona. Tunaweza kusoma hii kama Mwenendo wenu utawaliwe na roho, au ishi maisha yako yote katika roho. Ni kama kutembea, ni hatua moja baada ya nyingine, ni maendeleo ya maisha yetu. Bila shaka tutaanguka mara kwa mara lakini tunaamka na tuendelee mbele. Na tunaweza kufanya hii kwa sababu ya Roho Mtakatifu. Mtu ambaye ni msioamini hawezi fanya hii lakini anaendelea kuenda chini.
Enendeni ni tabia ya maisha yetu, na hii ni amri hapa. Kama nimesema ni maendeleo ya maisha yako. Ikiwa wewe umeokoka miaka kumi au hata miaka moja iliopita na bado maisha yako hakuna tofauti tunaweza kusema Roho Mtakatifu hayupo ndani yako. Na bado wewe ni msioamini. Kumbuka ile kitu inaitwa utakaso. Hii ni kila siku ya maishs yako unakwa zaidi na zaidi kama Bwana wako Yesu kristo. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu kutusaidia kuwa kama Yesu. Hii ni kwa kila njia ya maisha yetu, hii ni sababu anaishi ndani yetu, tunabeba yeye kila mahali na sisi, hii ni sababu Paulo anasema enendeni kwa Roho. tunapojinyenyekeza kwa roho, lazima tutasonga mbele, utakaso itakuwa na tutaanza kuwa kama Mungu anataka sisi kuwa. Roho Mtakatifu ni chanzo cha maisha mtakatifu, lakini ni sisi wakristo tuko na hii amri ya enendeni, kutembea, na roho. Ni mzuri kujua sisi tumeitwa kuwa watu watakatifu, waliotengwa na Mungu. Ukitaka kujua kazi yetu kama wakristo tunapata kwa kitabu cha Warumi 6:11-13 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Sasa hii ni kazi yetu, na tunaweza kufanya hii kwa sababu ya roho mtakatifu ndani yetu. Ikiwa dhambi inaishi vizuri sana ndani yako na dhambi ako nyumbani ndani yako uko na shida.
Wakati sisi Tunaenendeni kwa Roho ni kama tunavaa silaha za Mungu na anakuwa ngao kwetu. Tunafanya kama Warumi 13:14 inasema Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
Paulo anaendelea kwa mstari yetu ya leo Wagalatia 5:16 Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Wakati sisi tunaenendeni kwa roho tunaenda kwa ni kufanya kama Warumi 13:13 ya sema Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu, Lakini bila kufanya hii tuatashinda kwa kwa tamaa za hii mwili. Hii mstari ya Warumi inaendelea kusema si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Na si vitu hivi peke yake. Kwa wiki chache tutaangalia vitu amabvyo tunapata kwa mtu amabaye anatembea kwa mwili na tamaa zake. Tabia hizi mbili ni kinyume kabisa za kila mmoja. Hata ni mzuri kujua ikiwa wewe ni Mkristo una chaguzi mbili, Unenendeni kwa Roho au unaishi kimwili na unaishi dhambini, huwezi kufanya yote mbili pamoja. Kuishi kwa mwili wetu na tamaa zake si shida kwetu, kila mtu anaketi hapa leo asabuhi ni fundi ya kuishi kwa tamaa zake. Hata leo asabuhi bila shaka umeona kitu kibaya, umesema kitu kibaya, umesikia kitu kibaya, umefikiri kitu kibaya, umetenda kitu kibaya, kwa nini? Kwa sababu ni tabia yetu na tumezaliwa na hii shida, tunatenda kama tunajua.
Hii ni sababu wakati Mungu anatuokoa anatupea roho mpya kama tuliona wakati tulianza leo. Sasa ndani yetu huyu ya zamani ameenda na tumekuwa kitu kipya, lakini tumekuwa kitu kipya kwa roho zetu na bado tunavaa hii mwili, na hii mwili haijakuwa mpya, bado mabaki ya huyu zamani ako na anapigana na huyu ambaye ameingia. Hii ni sababu sisi wakristo ni lazima tunajaza mawazo yetu na ukweli, upendo na kuweka macho yetu kwa Yesu kristo. Ni mzuri kukumbuka sisi tunaishi misha yetu wazi mbele ya Mungu, anaona kila kitu, ni muhimi sana tunafanya kama Wakolosai 3:16a. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, ni mzuri tunasoma na tunajua maisha ya Yesu kristo hapa kwa hii dunia kwa sababu yeye ni mfano kuu kwetu. Mkristo huwezi kubali na tamaa za mwili wako. Ni ngumu ninajua, lakini ni lazima kupigana na huyu ya zamani yako. pole sana kwa sababu ni vita ambavyo itakuwa mpaka siku ile unapumua pumzi yako ya mwisho. Ni mistari mbili zimenisaidia maisha yangu yote ya kujua Yesu na ni Yakobo 4:7-8a. mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. hii ni ahadi kubwa sana.
Paulo alijua hawa wagalatia watakuwa na shida bila kuenendeni kwa roho. Kwa sababu ya walimu wa uongo waliingia na ha hawajali umoja kanisani, wako na lengo ingine, na Paulo alijua bila upendo wakristo wangekulana. Watakuwa na wivu, uvumi itakuwa mingi, watapigana kuhusu vitu ambavyo si ya Yesu. Vitu hvi vimeandikwa kwetu pia na maana yao hakuna tofauti.
Ninaomba sana sisi tuenendeni kwa roho, tuonyesha community yetu, area yetu hata nchi yetu sisi ni wakristo wakweli, sisi ni watu ambao tumeua tamaa za mwili na tunaishi kwa Roho.
Leo asabuhi labda wewe umesikia neno la Mungu na umeona wewe hujui Yesu kristo, hujaweka imani yako katika yeye na maisha yake na kazi yake. Nataka wewe kujua Yesu Kristo alikuja na alikuwa pamoja nasi hapa, alikuwa kama sisi lakini bila dhambi, aliishi maisha kamilifu na alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na baada ya siku tatu, Mungu alimfufua katika wafu. Ikiwa unaamini hii na uko tayari kutubu kwa dhambi zako na kufuata Yesu kwa njia ya kutii neno lake, tafadhali ongea na sisi baada ya ibada yetu.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe, na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more