The Battle Within Pt.2
Galatians • Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 5 viewsNotes
Transcript
Galatians 5:17-18
Galatians 5:17-18
Leo tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano vs.17-18. Kitabu Hiki kimejaa na vitu ambavyo vinatusaidia sana. Natumaini imesaidia maisha yako ya Mkristo na pia imelisha roho yako. Bibilia sii kitabu kama vitabu viingine. Ni maneno ya Mungu mwenyewe. Inajua sisi sana kwa sababu Muumba wetu aliiandika. Bibilia iko na uhai na inajua kila kitu kuhusu sisi. Wahebrania 4:12 ya sema Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Tukifanya kama tumeambiwa kwa agani jipya tutakuwa watu tofauti kabisa. Fikiria hii, ikiwa tumefuata kama inasema, hakuna corrution, hakuna chuki, hakuna wasi wasi, hakuna hofu, tutakuwa na upendo, ujasiri, tumaini na mambo mingi mengine. Lakini nataka kusema Mkristo bado hii yote unaweza kuwa nai. Ni kufuata na kutii kama inasema.
Wiki iliopita Tulianza kuangalia vita ambayo ni ndani yetu. Tulisema kila siku ya maisha ya Mkristo ni vita na hii ni ukweli. Kwa sababu kama tuliona wikiliopita tuko na mwili ambaye inataka tamaa zake na tuko na Roho mpya Mungu ameweka ndani yetu na mwili na roho hivyo viwili viko vitani wakati wo wote. Hii mwili yetu imezaliwa dhambini na haijui kitu kiingine ni kutenda dhambi tu kwa sababu ni tabia yake, hii ni sababu tunafanya kama tunafanya, hii ni sababu wakati unaona mtu anaiba mbele yako, au anasema uongo mbele yako, au anafanya kitu cha ajabu na ni mbaya sana mbele yako, anafanya kama anajua. Halafu Mungu anatuokoa na anaweka Roho yake ndani yetu, Bibilia inasema Anakaa ndani yetu, sisi ni hekalu ya Mungu na Roho yake anaishi ndani yetu, na ROho yake ni kamilifu kwa sababu ni Roho Mtakatifu, ni Mungu. Sasa tumekuwa viumbe vipya, mawazo yertu ni tofauti, moyo wetu imebadilishwa. Tunaona votu tofauti sasa, ni kama tumeweka miwani tofauti kuangalia kila kitu. Sasa tumeshika sababu tulifanya ile mambo ypote mabaya na hatutaki kutenda lakini mara kwa mara mwili inakuwa na nguvu sana na tunaanguka tena, lakini roho yetu iko na uchungu wkatai tunatenda dhambi na tunaanza kujua kweli kwwli tuko vitani.
Wiki ilopita tuliona Paulo kuwaambia Wakristo Wagalatia Kwa vs.16 Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. tuliangalia hii sana. na tuliona bila kufanya hii tutashindwa kabisa, huyu ni msaada wetu Yesu alwaacha sisi. Msaada ya kujua neno lake, msaada kusihi maisha mpya, msaada kushinda hii mwili na tamaa zake.
Leo Paulo anaendela kueleza zaidi kuhusu hii vita ambao ni ndani ya sisi sote. Najua wakati tunasoma hii kila mtu ambaye ni Mkristo anaketi hapa leo asabuhi atajua ni ukweli. Tusome Wagalatia 5:16-18 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
Tuombe. Baba Mungu tunasema asante kwa hii nafasi kuingia pamoja na kukuabudu. Asante sana kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kazi yake amefanya mioyoni mwetu, na kwa sababu ya hii sisi sote ambaye ni wakrito tunaweza kuwa na umoja kwa ibada yetu leo asabuhi. Asante kwa neno lako na tunaomba utafungua masikio na mawazo yetu kujua na kutenda kama inasema . Tunaomba hii yote katika jina la Yesu Kristo, Amin.
Paulo anatuonyesha umuhimu ya kuenendeni kwa roho kwa vs.17. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Tunaona hapa Roho na mwili ni maadui. Wamekuwa maadui tangu mwanzo na watakuwa maadui mpaka Yesu atarudi na sisi tutakuwa kamilifu tena. Wale maadui wawili hakuna siku, hakuna dakika, watakoma kupigana. Hakuna mtu mwengine ataingia kujadili amani. Huwezi kupata moja anachoka, hakuna kulala na lengo yao ni kuwaangamiza wengine. Na hii yote inafanyika ndani yetu, ndani ya mwili wetu, ndani ya mioyo yetu na ndani ya mawazo yetu. Bila Yesu Kristo na tumaini letu katika yeye nafikiri sisi sote tutakuwa kama wazimu. Mbele yetu tuko na ufalme wa giza na ufalme wa nuru, tuko na mema na mabaya. Yesu Kristo ameweka utawala wake mioyoni mwetu lakini nguvu yake inapingwa na tamaa za mwili. Kila tamaa, kila tendo au mawazo ya ouvu ni kinyume na mamlaka ya Roho Mtakatifu. Ni mzuri tena kujua wakatoi Paulo anatumia neno hili, Mwili, anaongea kuhusu hii mabaki ya mtu ya zamani ako ndani yetu.
Hata Paulo mwenyewe alikuwa kama mimi na wewe. Yeye si kama Yesu, hajakuwa kamilifu na alisema Kwa kitabu cha Warumi 7:15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Anaendelea kusema vs. 17-19 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Tunaweza kuona Paulo ako na hii vita ya Roho na mwili ndani yake. Anajua hakuna kitu kizuri iko ndani ya mwili wake, lakini kama anasema kwa kuwa kutaka nataka, anataka kufanya mema, hii ni roho lakini lile jema nilipendalo, silitendi. SIsi oste tunajua kama anasema. Anaendelea vs.23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Hii ni mwili wake, na tamaa zake. akili yake imebadilishwa lakini ni kama amekuwa mfungwa ndani ya mwili wake, unaweza kuona hii vita ndani ya Paulo, na anajua huyu ya zamani amechaduliwa angalia vs.24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Ni mzuri sisi sote tunafika hii mahali kusema ole Wangu, maskini mimi. Pia ni swali nzuri sana kwa sisi sote kujiuliza Nani atatuokoa na mwili huu wa mauti? Vs.25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi. Yesu kristo. Hii ni jibu letu ya hii vita ndani yetu. Hakuna kushinda bila yeye, hakuna tumaini bila yeye.
Nataka sisi kushika kwamba, Hii neno Mwili inatumiwa mara mingi tofauti bibliani. Maana yake inaweza kuwa kama ngozi, damu, misuli na mifupa. Pia tunaweza kuona neno hili mwili inaweza kutumiwa kwa wasioamini, Utasoma kama Warumi 7:5 inasema tulipokuwa katika hali ya mwili. Watu kama hii wakochini ya udhibiti wa tamaa mbaya, wanaishi kama wanajua. Hapa wakati Paulo anaongea na wagalatia anatumia neno hili tofauti tena, maana yake ni udhaifu wa kimaadili na kiroho, mtu ya zamani bado ako kwa roho amabye imekombolewa. Maana ya mwili hapa kwa wakristo ni udhaifu wao ya kutenda dhambi lakini ndani yao hawa ni kiumbe kipya. Mwili inapinga kazi ya roho moyoni ya mtu.
Hata wasioamini wanaweza kusikia vibaya wakati wanatenda kitu kibaya, labda kwa sababu ya hatia au matokeo ya hii mbaya wametenda, lakini yeye hanavita ndani yake. Ni maishnai ya wakristo, watu ambao Mungu amebdilika, ROho itapigana na Mwili, kwa sababu hakuna mahali ingine roho anaishi, ni ndani yetu. Kama nimesema sisi sote tunaweza kusema na Paulo kama tumesoma kwa Warumi 7. Na unawza kuona wakati vita iko ndani ya mtu, unaweza kuona matuda ya roho maishani yao, na tutaongea sana kuhusu matunda y a roho baada ya wiki chache. Lakini unaweza kuona matunda ya roho maishani ya mtu naam na gani? Wakati wanapigana na mwili wao. Ikiwa wewe unaweza kutenda dhambi bila hata kusikia kitu ndani yako hiyo ni ishara nzuri kwamba roho haipo ndani yako. Ikiwa wewe unawea kusema uongo kwa mtu, au kuiba kitu au kulewa au kulala na mtu amabye si bwana au bibi yako na unaweza kulala usiku vizuri, uko na shida, kwa sababu kuna kitu kinakosekana na ni Roho ya Mungu.
Wakristo sisi ni wana wa Mungu, watoto wake hatuna deni la mwili kama sisi tunalipa yeye, lakini ni mzuri kujua Warumi 8:12-14 ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Nataka ninyi kusikia kitu cha umuhimu sana, tukitaka kushinda mwili na tamaa zake ni lazima kuwaua kwa njaa. Hatuwezi kulisha hii mwili wetu, utashindwa kila wakati ukifanya hii. Warumi 13:14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. Ukitaka kuanguka dhambini njia nzuri ni kujiweka mahali mbapo dhambi ni mingi. Ikiwa unaenda pub na mahali ya makahaba bila shaka utapata shida na ni rahisi kuanguka dhambini. Lakini kama hii mstari ya Warumi inasema msiuangalie mwili, maana ya hii ni usipe nafasi kwa mwili wako kuingia dhambini, usiende mahali mbapo unajua vitu hivi viko. Majaribu ni mingi sana, sisi oste tunajua hii. Hii ni sababu Yesu wakati alifundisha wanafunzi wake kuomba litu moja alisema ni Usitutie majaribuni. Kwa mkristo ni lazima kwetu kufanya kama Paulo alisema kwa kitabu cha Wakolosai 3:5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu. Kwa Mkristo tumeua tamazaa zetu.
Pole kusema lakini ikiwa mtu anafikiri yeye ni Mkristo na maishani yake hakuna vita ya kupigana na mwili na tamaa zake, amejidanganya, hajaokoka na bado ako kwa ufalme wa giza. Kwa sababu tunajua hakuna mtu anaweza kushinda hii mwili na tamaa zaka peke yake, ni Mungu tu anaweza na utaona mtu ambaye ako na roho ndani yake kupiga vita na kushinda.
Kwa bibilia huwezi kupoata neno Utatu, lakini tunaona mara mingi mistari kutuonyesha Baba, Mwana na Roho, ni tatu lakini Mungu moja. Tuko na utatu ingine ambao wanapigana na Baba, Mwana na Roho ni dunia, mwili na shetani. Tunaweza kuona Baba na dunia wanapigana kipenyo, Tunaona hii kwa mistari mingi sana lakini tuangalia mbili tatu. Ya kwanza Yakobo 4:4 hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Huwezi kuwa rafiki na hii dunia na rafiki ya Mungu. Nilikuwa pastor moja aliniambia kablya alikuwa raifiki yangu hajakuwa na shida na mtu yo yote na baada ya kujua mimi imeleta yeye shida mingi na watu. Nitasema hii, ikiwa wewe ni Mkristo, Pastor na wewe ni rafiki ya kila mtu na kila mtu anakupenda, wewe ni fake kabisa. Wasioamini ni ya hii dunia na baba yao ni shetani, wewe ni ya Mungu na unabeba ukweli na wewe, hawa ni giza wewe ni nuru, utakuwa marafiki naam na gani? Mstari ingine ni waraka wa kwanza wa Yohana 2:15-16 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Ya pili ya hii vita vya utatu ni Mwana, Yesu, na shetani. Ukisoma agano la kale unaweza kuona lengo ya Shetani ilikuwa kuzuia kuzaliwa ya Yesu, alijaribu kuchafua watu waisraeli ili waangamizwe. Aikuwa karibu kufaulu. Kumbuka wakati Musa alikuwa kwa mlima na anapata amri kumi kuu, Haruni na Wahebrania wakochini na walitengeneza sanamu na wakaanza kuiabudu. Unaweza kusoma hii kwa kitabu cha kutoka 32:7-14 lakini angalia vs.9-10 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu, basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, Hii yote ilianza kwa kitabu cha Mwanzo 3:15 Mungu alisema nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Hii ilikuwa Yesu na shetani. Hata Shetani alijaribu kutumia Herode unakumbuka wakati Yesu alizaliwa kwa kitabu cha Mathayo 2:16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. Shetani almjaribu Yesu, na alishindwa na tunasoma kwa Waraka wa kwanza wa Yohana 3:8 Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
Halafu kwa vita vya Utatu tuko na Roho na Mwili.