The Flesh Pt.1

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view

The Flesh Pt.1

Notes
Transcript

Galatians 5:19-20

Leo asubuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano mstari ya kumi na nane hadi kumi na tisa. Kumbuka mandhari ya kitabu hiki cha Wagalatia ni kehesabiwa haki kwa njia ya imani. Tumeona Paulo kuandika vitu vingi sana kwa wakristo wagalatia vitu ambavyo vinaendelea hata kwetu leo. Uzuri wa neno la Mungu ni Neno la Mungu haibadiliki kwa sababu Mungu si kama sisi, leo Mungu haisemi hii na kesho anasema kitu tofauti. Neno lake ni ya milele na ni kwa kila kizazi. Dunia yetu ni tofauti sana siku hizi hata ukiangalia miaka ishirini ilioptia hapa Kenya, hakuna simu, hakuna smart phone. Mambo mingi ni tofauti sana, lakini bado neno la Mungu ni the same tu, na ikiwa Yesu hajarudi itakiwa the same kwa watoto wa watoto wa watoto wako. Tunaweza kuamini kila kitu inasema kwa sababu ni kamilifu. Watu wingi hata watu ambao wanaenda kanisa kila jumapili hawajui hii hazina tukonai inaitwa Bibilia.
Kwa Wakristo wagalatia Walifundishwa vizuri sana, walijua injili ya Yesu Kristo, waliamini alikuwa Masihi wao na Mtume Paulo mwenyewe alikuwa mwalimu wao, lakini kama kawaida shetani alituma watu wake, walimu wa uongo, kuingia na kujaribu kuharibu neema ya Yesu na walianza kuongeza matendo kwa neeam ya Yesu ili kupata wokovu. Na kama kawaida kwa kila kanisa dunia nzima walikuwa na watu ambao walianza kufuata hii uongo, ilianza kuleta shida kanisani na hii ni sababu Paulo aliandika hii barua kwao. Kwa wiki mbili tumeangalia hii vita ambaye ni ndani ya sisi sote, kila mtu ya Roho na Mwili, tumeona hawa wa wili wakovitani kila dakika ya kila siku na ikiwa umeokoka kweli kweli hii vita inafanyika ndani yako. Kweli kweli hii mwili iko na nguvu sana, na ni ya ule mtu wa zamani na alizaliwa katika dhambi zake na hajui kitu kiingine lakini Mungu kwa sababu ya rehema yake alipea watu wake wokovu na alituma Roho Mtakatifu kuishi ndani ya hawa. Sasa kwa nyumba moja ndani yetu kwa roho zetu tumekuwa kiumbe kipya lakini bado roho yetu iko ndani ya hii mwili na tamaa zake na hatutakuwa bila hii mwili mpaka siku ile hii mwili inakufa na tunaenda kuwa pamoja na Yesu mbinguni. Wakati tunafika uko tuatkuwa kamilifu na hakuna vita itakuwa. Siku ile kufikiria ni tamu sana.
Kwa watu na hii dunia tuko na wengi sana wanajribu kujitetea na kutufafanulia, dhambi ni nini. Au tunaweza kusema wameweka viwango vyao vya jinsi matendo ya mwili yalivyo. Lakini kwetu wakristo sisi tunataka kujua neno la Mungu inasema nini kuhusu hii.
Paulo aliandika orodha ya matendo ya mwili ili sisi tunaweza kujua bila shaka ikiwa tunafanya vitu hivi au hii ni tabia ya maisha yetu tutajua hii si Yesu lakini ni mwili na ni dhambi. Mtume Yohana aliandika kuhusu tabia ya maisha ya mtu, nafikiri ni muhimu sana tunasoma hii kabla ya tunaingia kwa hii orodha Paulo aliandika Wakristo wagalatia. Angalia Waraka wa kwanza wa Yohana 3:4-10 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Watu wengi sana hawapendi hii sehemu ya maandiko na inakuwa hata mbaya zaidi kila mwaka, kwa sababu watu wanataka tamaa za mwili na Yesu pamoja na hii haiwezikani. Lakini kwa hii wiki chache tunaangalia hii orodha ya matendo ya mwili tafadhli kumbuka maneno haya ya Yohana.
Tusome kitabu cha Wagalatia 5:19-21 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tuombee: Babu Mungu tunasema asante sana kwa hii siku ya leo ambaye umetuleta hapa kukuabudu. Hii ni lengo yetu ya maisha haya kuleta sifa kwa jina lako, kusema ukweli sisi si kitu na hata tunajua ibada yetu kwako si safi kama unastahili lakini tunaomba utaaidia udaifu wetu. Wakati tunasoma orodha kama hii tunajua ndani yetu ya sisi sote tunapigana na vitu hivi, tunaomba utatusamehe, saidia sisi leo kujua neno lako na kutoka hapa na kuitii maishani yetu. Tunaomba hii yote katika jina la Yesu, Amin.
umeona hii orodha ni kubwa na ni vitu vingi ndani yake, kusema ukweli tunaweza kukaa kwa miezi mingi na tunaweza kuangalia kila moja kwa jumapili yake lakini nitajaribu kuenda haraka kidogo. Nataka ninyi kujua bila shaka Paulo anasema nini hapa na maana yake. Tunaona anaanza vs.19 kusema Basi matendio ya mwili ni dhahiri. Hii neno dhahiri iko na maana sana. ni kusema ni kitu ambacho kila mtu anajua. Paulo anasema matedno ya Mwili ya ni wazi, hakuna shaka yo yote ni nini, ni kama taa kubwa imewekwa gizani na wakati watu wanaona wanajua ni taa. Labda unakumbuka wakati Yesu aliongea kuhusu walimu wa uongo kwa kitabu cha Mathayo 7:16-18 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. halafu vs.20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Wakati Yesu alisema Mtawatambua ni kama Paulo anasema dhairi, utajua. Huwezi kuona mti ya ndizi na kusema hii ni machungwa.
Wakati unaona matendo ya hii mwili unajua si ya Yesu. Na sisi sote ni mafundi ya matendo ya mwili. Sisi si wajinga. Ni rahisi sana kutoka hapa na kuenda center na bila shaka matendo ya mwili yatakuwa dhahiri mbele ya macho yetu. Utaona walevi, wizi, wivu, hasira na mambo mingi sana na tuasema kweli hii si ya Yesu ni ya binadamu.
Related Media
See more
Related Sermons
See more