The Flesh Pt.2

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript

Galatians 5:20

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano vs.20. Kwa wiki chache tumeona Paulo kuwaambia Wakristo wagalatia kuenendeni kwa Roho na wakifanya hii hawatazitimiza tamaa za mwili. Tunajua walimu wa uongo waliingia kanisa na walianza kufundisha ni lazima kutayarishwa kuptata wokovu wao. Wakati uongo kidogo inaingia inaleta shida mingi, kumbuka kama Paulo alisema kwa Wagalatia 5:9 Chachu kidogo huchachua donge zima. Bila shaka kwa hawa ambao walijua Yesu kristo walikuwa na ukweli walijua wako na uhuru Katika Yesu Kristo walianza kudangaywa na wale walimu wa uongo na walianza kutumia uhuru wao vibaya. Kusema ukweli labda hawajajua Yesu kweli kweli na yeye hajabadilisha mioyo na mawazo yao. Kwa sababu ya hii walianza kufanya mambo mingi na Paulo alisema labda wanatenda matendo ya mwili na si Yesu. Ikiwa mtu anaweza kuendelea kwa matendo ya mwili wako na shida kubwa. Hii ni sababu Paulo aliwaambia kanisa la korintho kwa waraka wa pili wa korintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. ni mzuri kwetu sote kujijaribuni kujua ikiwa tumekuwa katika imani.
Paulo hajataka hawa kuwa na shaka yo yote kuhusu matedno ya mwili. Alitoa orodha kwao na Paulo ametoa ordodha mingi kwa kanisa mingi lakini kwa Wagalatia tunaona anaongea kuhusu mambo ya ngono, kuibada sanamu na mahusiano ya kibinafsi. Wiki iliopita sisi tuliangalia vitu vya tatu ya kwanza, vitu vya ngono. Unakumbuka alisema vitu hivi vyote ni dhaihiri, kila mtu anajua matendo ya mwili kwa sababu ni wazi. nataka pia kutukumbusha kama tulisoma wiki iliopita kama Yohana alisema kwa waraka wa kwanza wa Yohana 3:4-10 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Tena watu wengi hawapendi hii sehemu ya maandiko kwa sababu watu wanataka tamaa zao za mwili na Yesu pamoja na haiwezikani. Ikiwa wewe unajipata unjaribu kuishi naam na hiyo ninaomba sana unatubu na ongea na sisi badaye.
Tusome hizi mistari ya Wagalatia 5:19-21 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tuombee: Baba Mungu wetu tunasema asante kwa nafasi hii ya leo, kufika mbele yako na kutoa sifa kwa jina lako. Tusaidie sasa wakati tunaingia neno lako, fungua mioyo yetu na mawazo yetu kushika, kujua na kutenda kama umesema. Tunaomba hii yote katika jina la Yesu, Amin.
Baada ya Paulo luwaeleza Wakristo Wagalatia kuhusu matendo ya mwili na mambo ya ngono anaingia vitu vya kuibada sanamu. Angalia Wagalatia 5:20a. Ibada ya sanamu, uchawi. Kumbuka Paulo alisema hii ni matedno ya mwili na ni dhahiri, ni wazi kwa kila mtu kuona. Ibada ya sanamu ni dhambi ya kuabudu kitu ambacho kimeundwa na binadamu.
Mara ya kwanza mimi niliona sanamu ya kuabudu ilikuwa wakati nilifika Kenya. Amerikani maisha yangu yote sijaona. Hapa Kenya uko na dini mingi tofauti na wako kila mahali. Ukiingia duka ya mwindi unaweza kuona sanamu mingi. Iko kwa calendar, iko kwa ukuta na mara mingi unaweza kuona nyuma ya dirisha. Ni kama kitu utaona kwa movie, iko na sehemu mingi ya binadamu, wanyama na vitu viingine. Na hawa watu wanapiga magoti mbele ya hii kitu na wanaomba kwa kitu kuwasaidia. Hata Mungu anaongea kuhusu hii kwa neno lake. Angalia Isaya 44:14-18 Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha. Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia. Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto; na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu. Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. Halafu anagalia Zaburi 135:15-18 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,Zina masikio lakini hazisikii, Wala hamna pumzi vinywani mwake. Wazifanyao watafanana nazo, Na kila mmoja anayezitumainia.
Kama unaona ibada ya sanamu ni kitu kubwa sana. Wakati mtu anafanya hii anavunja amri kumi kuu. Unakumbuka kitanu cha kutoka 20:3-5 Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako. Hii ni amri ya kwanza Mungu anawapea kwa amri kumi kuu. Kwa nini? Kwa sababu wakati sisi tunaabudu sanamu ni kama kupiga uso wake. Hakuna kitu kiingine unaweza kufanya kwa Mungu ni mbaya zaidi ya kuabudu miungu miingine. Unasema Mungu wa dunia na mbinguni si ukweli.
Hata wakati Musa alikuma kwa mlima na Mungu na Mungu anampea amri kumi kuu, unakumbuka watu waisraeli wanafanya nini? Musa alikaa kwa mlima siku mingi na watu walianza kusema labda amekufa. Wayahudi walimwaambia Haruni katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu. Na Haruni hajasema usifanye hii, ni mbaya, ni Mungu moja, lakini aliwaambia kumpea pete zote za dhahabu na Haruni aliunda sanamu ya ndama na alisema hiyo ndiyo miungu yako, iliyokutoa katika nchi ya Misiri. Ni ajabu sana. Unaweza kusoma hii yote kwa kitabu cha kutoka 32. Tunaona kwa kutoka 32:7 Mungu aliwaambia Musa Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, Halafu vs.8-9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, Hii ni watu wa Mungu, wayahudi, aliongoza hawa, alichunga hawa na siku chache tu wanaanza kuabudu miungu ya mikono yao yameunda. Na walikuwa watu wa Mungu lakini unaona si mchezo kwa sababu Mungu alitaka kumaliza hawa, hawezi kubali. Na kwa sababu ya hii dhambi tunasoma kwa vs.27-28 Akawaambia, Hawa ni wana wa lawi, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu. Watu elfu tatu walikufa kwa sababu ya hii. Si mchezo.
Kama Paulo aliwaambia Wagalatia, ni dhahiri. Ni rahisi kuona watu kufanya hii. Na labda unasema Mimi nikosawa. Mimi siwezi kuingia dhambi ya ibada ya sanamu, mimi sina miungu nyumbani yangu, siwezi kupiga magoti mbele ya kitu ambacho haiwezi kuongea, haiwezi kusikia. Hii ni kweli? Unaamini hii? Sawa. Labda nisaidia sisi kidogo. Sisi tunapiga magoti na tunabudu hii kila siku ya maisha yetu. Hii ni nini? Hii ni karatasi. Karatasi tu na iko na maandiko. Ni watu waangapi wamejiuza, wameuza watoto wao, wametoa maadili yao yote kupata hii karatasi? Ni waangapi hata wanaketi hapa leo asabuhi wamesema uongo kupata hii karatasi? Ni waangapi hapa hawawezi kufika kanisa na kuabudu mungu wao kwa sababu hawa ni mgonjwa, au mtoto ni mgonjwa au kichwa inauma, lakini saa mbili kesho asabuhi utaona hawa kwa kazi. na wako kwa kazi kwa sababu gani? Kupata hii karatasi. Wakristo sisi tuko na sanamu mingi sana maishani yetu. Kazi ni sanamu, pesa ni sanamu, watoto wetu wanaweza kuwa sanamu. Wazazi, ikiwa mtoto wako anaishi dhambini na wewe hutaki kusema kitu kwake, huyu ni kijana first born, umekubali kwake kusihi dhambini kwa sababu hujasema kitu kwake hii ni kumaanisha unaweka yeye juu ya Mungu. Mungu anasema Kuonyesha watoto wako njia zake na Mithali 22:6 ya sema Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Sanamu ya siku zetu ni hii kitu inaitwa simu. Ukiangalia watu siku hizi na ni wote, lakini youth zaidi hata hawawezi kubeba siku kwa mfuko wanabeba kwa mkono. Kila saa, kila dakika. Wamepima na wamepata mtu anaangalia simu yake mara 352 kwa siku, hii ilikuwa average. Wanasema mtu ako kwa simu yake karibu maa saa nne kila siku. Hata unaweza kupata kanisani mtu ako kwa simu, unatoka ba mtu ameweka statu yake na kumbe ni saa sita, na unajua unahubiri kwa saa sita. Kusema ukweli shetani ameweka sanamu mingi sana maishani yetu siku hizi, si ya mbao na mawe lakini vitu ambavyo tunatumia kila siku. Sanamu ni kitu cho chote unaweka juu ya Mungu. Ikiwa unaweka kitu juu ya Mungu unaabudu ile kitu. Mara mingi sisi tunajiweka kati kati ya kila kitu na tunajiabudu zaidi ya kila kitu. Nitoe list kidogo kukusaidia vitu ambavyo ni sanamu kwa siku zetu. Pesa, kazi, mafanikio, Teknologia, michezo na burudani, simu, umaarufu, miili yetu, Uhusiano, familia yetu, watoto, rafiki zetu, tamaa zetu. Hii ni chache sana. Ni mzuri sisi sote tunajipima kujua ikiwa vitu hivi tumeweka juu ya Mungu wetu. Na ikiwa kitu moja kwa hii orodha inaweza kukuzuia usije kanisani, Sunday School, Bible study halafu umeshaa pata jibu lako.
Paulo aliongea kuhusu hii shida pia kwa kitabu cha Warumi 1. Hii mlango ni mzuri sana lakini angalia vs.23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Hii kwa mfano wa sura ya binadamu ni sanamu. Vs.25 waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Matokeo ya hii tunaona kwa vs.24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Naukiendelea kusoma hii mlango unaona wakati Mungu anacha mtu katika tamaa zake za moyo wake ni mbaya sana uko na wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili , wanaume hakuna tofauti, wanatamani wanaume wengine. Matokeo ya kuabudu sanamu na si Mungu tunasoma kwa vs29-31 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; Kumbuka Paulo kusema matendo ya mwili ni dhahiri, nafikiri utakubali wkati ninasema tunaona vitu hivi kila mahali siku hizi, na yote kwa sababu tumetoa Mungu kwa kila kitu na tumeweka kwa nafasi yake sanamu.
Pia tunaona Kwa hii ordha ya matendo ya mwili baada ya ibada ya sanamu Paulo anasema kwa wagalatia 5:20 Uchawi. Uchawi ni nini? Hapa Kwa kigiriki ni Pharmakeia. Na kutoka neno hili tunapata neno letu Pharmacy. Ilitumiawa kwa dawa ya ulevi ambaye inachanganya akili za watu. rafiki zangu wakati nilikuwa kijana walitumia dawa ya ulevi kali sana. Hata wanaanza kuona vitu ambavyo havipo. Wanaona ukuta na inapakwa na rangi mingi tofauti ni mara darti sana, lakini hii ukuta ni nyeupe tu. Halafu hofu wanashika hawa kwa sababu wanaona buibui na nyoka kwa ukuta na inajaribu kushika hawa, na kweli hakuna kitu kwa ukuta. Nimeweka hawa kwa gari na ninaenda na mbio sana na hawa wanapiga kelele kusema rangi amabye iko kati kati ya bara bara inapanda kama ukuta na sisi tutagonga. Ni ajabu sana lakini ile dawa ya ulevi ni mbaya. Wakati wa Paulo watu watatumia hii dawa kwa sherehe za kale za kidini na watafikiri wanaongea na miungu yao.
Kusema ukweli siku zetu hata Abortion, kuua mtoto tumboni ya mama ni hii. Watu wanachukua dawa na vitu viingine kuua mtoto. Kwa miaka mia moja Abortion imekuwa sawa kwa dunia karibu nchi 136 wanasema iko sawa. Karibu watoto billioni moja wameuawa tumboni la mama yao. Kila mwaka karibu watoto milioni sitini wanauawa tumbobi la mama. Hii ni uchawi pia. Badaye hii neno ilianza kutumiwa kama witchcraft na black magic. Najua hapa Kenya nimesikia story mingi sana kuhusu laana juu ya watu na desturi ya kabila fulani na wanacheza na vitu hivi, kusema ukweli karibu yote ni uongo na watu hapa wanaamini kila kitu. Lakini bado shetani na mapepo yake si kama sisi na wako na nguvu, na mtu anaweza kutumiwa na shetani na ako nguvu zaidi ya kawaida. Si watu wengi lakini inawezikana
Related Media
See more
Related Sermons
See more