The Flesh Pt.3

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

Galatians 5:20b.

Leo tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano vs.20. Kwa kitabu hiki iko na kila kitu kwa maisha ya Mkristo. Tumeona mambo mingi sana. Tunajua mandhari ya wagalatia ni kuheasbiwa haki kwa imani. Si kwa sheria au matendo yetu. Walimu wa uongo waliingia na walianza kufundisha wokovu kwa njia ya matendo. Walisema lazima mtu kutayarishwa ikiwa ataokoka. Tumeona Paulo kueleza hawa kuhusu uhuru wao na hawakochini ya torati lakini wako chinbi ya neema. Halafu alianza kuongea kuhusu lazima sisi wakristo tunaenendeni kwa Roho tukitaka kushinda hii mwili na tamaa zake. Halafu hajataka mtu kuwa na shaka ya matendo ya mwili ni nini na alisema ukweli matendo ya mwili ni dhahiri. Ni wazi kwa kila mtu kuona. Na kusema ukweli sisi sote ni fundu ya vitu hivi, bila kufundishwa kitu cho chote kila mtu kwa asili hufuata mwili. Sisi sote tumezaliwa na hii tabia. Kuvunja hii tabia maishani yetu inahitaji nguvu isiyo ya kawaida ya Mungu. Na wakati Yeye anampea mtu hii zawadi ya wokovu Anatupea Msaada kuishi maisha kama inavyopaswa kuishi. Hii ni Roho Mtakatifu, lakini lazima tunafuata yeye wakati anatuongoza.
Tumeona hii orodha ya Paulo iko na vitu vingi, wiki ya kwanza tuliangalia vitu vya ngono uasherati, uchafu na ufisadi. Wiki iliopita tuliona ibaday ya sanamu na uchawi. Ikiwa hujakuwa hapa au hujasikia naomba uende kwa kweli kweli ministry na kusikia uko halafu sisi sote tutakuwa pamja kwa mafundisho haya.
Leo Paulo ananza kwa orodha yake vitu ambavyo ni kuhusu uhusiano wetu na wengine. Hatutafanya yote leo kwa sababu ni muhimu sana tunashika kama Paulo anasema na tutaangalia pole pole. Tusome tena hizi mistari kwa muktadha yao Kitabu cha Wagalatia 5:19-21 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe: Baba, Mungu wetu tunasema sante kwa hii nafasi ya leo kuingi mbele yako pamoja na watoto wako na kuimba na kuomba na kufungua neno lako la uhai na kujua kama wewe unasema. Vitu hivi si rahisi lakini tunaomba utusaidie kushika kama unasema na kutii ili tunaweza kuwa wato wako ambao tunaishi kwa hii dunia maisha mtakatifu na tutakuwa nuru kwa wote kuona na watakusifu. Tunaomba hii yote katika jina la Yesu. Amin.
Wakati unaona hii orodha ya Paulo ni kubwa na ni vitu vingi ndani yake na pia natumaini sana hakuna mtu hapa ako na vitu hivi maishani yake na ikiwa unajipata kama vitu hivi vinaishi ndani yako utatubu na kurudi kutembea na Roho. Pia natumaini sana hujasoma mbele na unaona dhambi moja ambaye imekushika na utapanga kukosa kufika kanisa jumapili ile wakati tunaongea kuhusu ile dhambi.
Tuanze. Kitu cha kwanza tunaona kwa uhusiano na watu ni Uadui. Hii neno iko na maana mingi tofauti. hata inaweza kuamnisha chuki, mtu ambaye anapenda kupigana na wengine. Hii ni watu ambao hata hawajui wewe lakini wanataka kuharibu jina lako kwa sababu ni watu ambao wako na chuki moyoni mwao. Kila kitu unafanya wanachafua, ukitaka kusaidia wengine, haitoshi. Ni kama kila mitu mtu anajaribu kufanya hawa watakuwa kinyume kabisa. Wakati mtu ni adui yako hana upendo kwako, hana rehema au neema kwako na lengo ya moyo wake ni kuhaikisha wewe unaanguka na umeangamizwa. Hii neno imetumiwa mara ishirini na tano kwa bibilia. Ni mzuri tuangalia kama inatumiwa halafu tutaona sisi hatutaki kuwa mtu mabaye ako na uadui maishani yake. Warumi 8:7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni, hii ni neno letu yaorodha ya Paulo, uadui, juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Hapa anasema wakati tunaishi kwa hii mwili na tamaa zake zimejaza nia yetu sisi tumekuwa adui ya Mungu. Kwa sababu mawazo yetu yanapigana na njia za Mungu na kama anasema kufanya. Chunga sana wakati uko na vitu hivi maishani yako. Hutaki kupigana na Mungu na kuwa adui yake. Yakobo 4:4 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa, Hapa ni neno letu tena, adui wa Mungu. Tunaona ikiwa unataka kuwa rafiki ya hii dunia wewe utakuwa adui wa Mungu.
Kama nimesema mara mingi ikiwa kila mtu ni rafiki yako, uko na shida. Kwa sababu huwezi kufanya kama Yesu alisema kufanya na kila mtu atakupenda, kwa sababu ikiwa wewe ni Mkristo kweli kweli wewe ni nuru, na wasioamini ni giza, wewe ni mtoto wa Mungu hawa ni watoto wa shetani, ni sisi hatuchezi pamoja vizuri. Hii tendo la mwili uadui ni tabia za chuki. Bila shaka sisi sote tunajua watu kama hii, na tumaini sana wewe ni mtu kama hii.
Wakati uko na uadui inaleta neno la pili kwa orodha ya Paulo Ugomvi. Ugomvi ni wakati shida inaingia kati kati ya watu. Ni ngumu sana, na wakati ugomvi iko kila mtu anachunga panda yake na yeye anasema ukweli na wengine wanasema uongo. Wakati ugomvi iko hakuna amani hakuna umoja. stress tu. Bibilia inasema kwa Zaburi 133:1 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. hii ni ukweli kabisa. Wakati sisi sote tunaendelea pamoja, ushiriki wetu ni tamu sana lakini wakati ugomvi inaingia, unaanza kufa moyo na shetani anaoenda sana ugomvi kuingia kwa wakristo, kwa sababu inaonyesha watu wa dunia, wasioamini sisi hakuna tofauti na hawa. Na ikiwa sisi hakuna tofauti na hawa, kwa nini watataka kujua Yesu.
Tunaona kwa bibilia mahali mingi watu walikuwa na ugomvi lakini tunaona kwa kanisa la Filipi tulikuwa na wanawake wa wili walikuwa na shida. Angalia kitabu cha wafilipi 4:2-3 Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana. Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima. Hatujui shida yao ilikuwa nini lakini imefika mpaka Paulo alisikia na alandika majina yao hapa. Na majina yao yameandikwa kwa milele kwa kila mtu kusoma kuhusu hawa. Hawa walikuwa waaamini hata Paulo alisema walikuwa pamoja na yeye kushindania injili ya Yesu. Na amesema hata majina yao yamo katika kitabu cha uzima. Na tunaona anaomba huyu anaita yeye Mjoli wa kweli kusaidia hawa kurekebisha hii ugomvi wao.Ni mzuri kwetu kuona kwa hii ugomvi ilikuwa kwa kanisa la Filipi kwa Euodia na Sintike. Kitu cha kwanza Paulo alipenda umoja kanisani sana kuliko kuweka kila kitu kama iko sawa. Hajasema waacha nifike tuketi pamoja nisikie hawa wawili. Abgalia alisema nawashi nini? kuwa na nia moja katika Bwana. Hajachukua panda moja ama ingine. Unajua sisi tunataka kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo. Bila shaka hii haijakuwa kama mtu anafundisha uongo kanisani kwa sababu Paulo angechapa mtu sana, lkaini labda hii ilikuwa kitu kidogo na inaleta aibu kwa injili ya Yesu na anasema kuwa kwa nia moja. Iko sawa ikiwa huwezi kubaliana kwa vitu vidogo, bado unaweza kuwa dada na ndugu, lakini usiharibu kanisa la Yesu kristo kwa sababu ya rangi, ua viti au vitu kama hivi. Na pia Paulo hajasema kwa wengine kuwaachana na hawa lakini kwa watu kanisani kuleta hawa pamoja. Ni kazi ya Wakristo kuleta wengine pamoja wakati shida inaingia. Kama utafanya kwa familia yako unafanya kwa familia ya Mungu.
Wakati Paulo alianza barua yake kwa kanisa la Filipi alionyesha hawa njia kutoa ugomvi na hata kwetu leo angalia Wafilipi 2:2-4 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Kitu cha Yakobo ni wazi kabisa shida yetu na sababu tuko na ugomvi inaingia angalia Yakobo 4:1-2 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, Hii ni ukweli kabisa. Hii ni chanzo cha ugomvi. ni tamaa za watu, ni wivu na watu wanaanza kuongozwa na mwili kuliko Roho. Chunga sana. Mithali 13:10 inasema Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. ni nini inaleta mashindano au ugomvi kati ya watu, kiburi.
Kitu kiingine Paulo anaandika kwa ordotha yake ya matendo ya mwili kwa Wagalatia 5:20 ni Wivu. Wivu, tunaweza kufanya jumapili mbili kuhusu hii peke yake lakini nitajaribu kufipisha. nani hapa anajua wivu ni nini? nani amekuwa na wivu hapa? Nani amekuwa na watu kuwa na wivu kwa sababu ya hawa? Wivu ni tendo la mwili sana, na kama Paulo anasema ni dhahiri. ni rahisi sana kuona wivu ya watu. Hapa nimeona ikiwa mtu anafaulu kila mtu anakuwa na wivu sana, hata rafiki zake wanaanza kuwa na chuki moyoni mwao. Kusema ukweli karibu hii yote tumeangalia leo, chanzo yake ni wivu. Unajua wakati wewe ni mtu wa wivu ni kama chuki kwa sababu mtu mwengine ako na kitu wewe unataka. Wakati wewe ni mtu ya wivu unavunja amri kumi ya amri kumi kuu Kutoka 20:17 ya sema Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. Wakati unatamani kitu cha jirani yako uko na wivu moyoni mwako.
Wivu ni kitu ambacho ni hatari sana. Nataka ninyi kusikia mistari michace kuhusu wivu. Mithali 14:30 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Husuda ni wivu. Hapa inasema ni ubovu wa mifupa, Tafsiri zingine zinaema wivu ni kuoza kwa mifupa. Wakati mtu ako na ugonjwa ya mifupa unaona kwa mwili wake wote, kwa uso, kwa afya. Fikiria watu ambao unajua hawa wako na shida na wivu, ni kama wako na ugonjwa fulani. Wako chini, uso wao iko tofauti. Kusema ukweli ule mtu wa wivu, kazi yake ni kuleta fitina kwa watu, ni kuleta uvumi wingi. Watu ambao wako na wivu, maisha yao si mzuri na hawataki watu wengine kuwa na maisha mzuri. Labda mtu anaona Bwana na Bibi yake na wako na furaha kwa ndoa yao, na huyu mtu wa wivu ndoa yake ni fujo na ako na wivu ya furaha ya ndoa ya wengine, ataenda kuanza kutandaza uongo kuhusu hawa, anajaribu kuleta hawa kuwa kama yeye. Ni mzuri kukumbuka ikiwa wewe ni mtu ya uvumi wewe uko na shida ya wivu pia.
Mstari ingine ni Yakobo 3:16 hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Unaona wivu inabeba rafiki zake pamoja naye. Ogomvi, machafuko na matendo mabaya. Kumbuka aliwaambia wagalatia vitu hivi ni dhahiri. Ni wazi. Nafikiri kila mtu hapa amekuwa mwathirika wa wivu. Bila shaka sisi sote tumeonjwa wivu ya mtu mwengine. Sisi tumeongea hapa kwa mission na ninyi unajua tumekuwa na shida mingi sana ya maneno ya watu kujaribu kuchafua hii mission, kanisa na mimi. Karibu kila mtu wakati unaongea na hawa wanasema watu wako na wivu mingi. Unashangaa kwa sababu wivu ya nini? Kwa sababu tunasaidia watu? Imagine hata wivu iko wakati mtu mwengine anasaidiwa. Kwa kitabu cha ulimbo ulio bora 8:6 anasema upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Wivu ni kali kama ahera. ahera ni nini? Ni kuzimu, ni kaburi, mahali watu ambao wamekufa wako. Ni baridi, hakuna uhai, hakuna tumaini lo lote. Wakati wewe ni mtu ya wivu unakuwa kama hii.
Ni mzuri sisi sote wakati tulikuwa wasioamini tulikuwa naam na hiyo. Mstari ya mwisho ni Tito 3:3 hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Hii mstari inatuonyesha kabisa kabla ya Yesu tulikuwa nani. Kitu cha kwanza inasema ni tulikuwa hatuna akili. hii ni kusema tulikuwa wajinga. Na tuliishi kwa mambi yote ya hii ordoha ya vitu vibaya sana hata utaona tumedanganywa. Tumedanganywa na nani? Sheatani na hii mwili wetu na tamaa zake za dunia. na tulikuwa watumwa wa tamaa zetu na kujipendeza na tulijaza wakati wetu wa maisha katika uovu na nini? Neno letu husuda, wivu. Angalia kama anasema kuhusu mtu ambaye tulikuwa tukichukiza. Hii ni mtu wa kudharauliwa na amejaa na chuki kwa wengine.
Kanisa nataka kusema hii, huwezi kuishi kwa vitu hivi vi tatu tumeona leo, Uadui, Ugomvi na wivu. Ikiwa hii ni tabia ya maisha yako, wewe si Mkristo, bado unaishi gizani na mwisho yako ni hukumu si uhai. Paulo alipenda kanisa wagalatia na hii ni sababu aliandika vitu hivi kwao, kujua na kupima ikiwa wanaishi kwa Roho ama kwa Mwili.
Leo asabuhi ikiwa wewe unaishi kwa mwili nataka kusema tumaini liko. Ni kuweka imani yako katika Yesu kristo, kutubu kwa dhambi zako. Kila mtu ambaye anaketi hapa keo asabuhi tulikuwa kama tumesoma leo asabuhi, tulikuwa na uadui, na ugomvi na wivu, watu wa giza na chuki. Hatujamaliza kusoma Tito 3 na anaendelea kusema kwa vs. 4-7 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. Hata wewe unaweza kuwa na hii tumaini na uhakika kwamba umesemehewa na unaweza kupata nguvu ya kuongozwa na Roho kuliko Mwili. Ukitaka kuongea tafadhali kuja baada ya ibda yetu na ongea na sisi.
Asanteni sana Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe, na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more