The Flesh Pt.5

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript

Galatians 5:21

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha wagalatia na tumefika 5:21. Tumeona kwa wiki mingi Paulo kuonyesha wagalatia matendo ya mwili. Tumeona ni mambo mingi sana, shida mingi sana hii mwili wetu inatuleta. Tumeona Paulo alisema kwetu wakristo enendeni kwa Roho. Sisi tuko na Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu, lazima sisi tunafuata yeye. Hawezi lazimisha sisi ni kwetu kumfuata. Tumeona kwa hii orodha Paulo alisema matendo ya mwili ni dhahiri, ni wazi kabisa. Si kitu ambacho ni siri ni rahisi sana kuona. Sisi sote tunaona vitu hivi kila siku ya maisha yetu. Shida ni wakati wakristo wako na vitu hivi maishani yao. lazima tunajiuliza ikiwa kweli kweli Yesu anajua hawa ama hawa wanajua Yesu tu. Kiatbu cha Waefeso 5:3 ya sema Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; Sisi watakatifu hatuwezi kupatikana kama vitu hivi ni tabia ya maisha yetu.
Tusome mistari yetu kwa muktadha take. Kitabu cha Wagalatia 5:16-21 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,  ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tuombe:
Leo tumefika mwisho ya orodha ya Paulo kwa matendo ya mwili na tunaona vs.21 ansema Ulevi. Hii si ngumu, nafikiri sisi sote tunajua maana ya hii. Lakini kumbuka Paulo anaongea na Wakristo wagalatia. Kumbuka walikuwa mataifa na madesturi yao yalikuwa tofauti sana na mahali walikuwa wamezoea kufanya karamu za ulevi na ngono. ilikuwa kama kawaida kwao, hakuna dhamiri ya vitu vya Mungu. Kama hapa tunaona watu wingi wanaishi maisha yao kama hakuna mungu. Kulewa ni kama kupumua kwa wingi. Kwa dunia ya mataifa siku zile kunywa pombe na kulala na wengine na kuibada sanamu ilikuwa kitu ya kawaida. Hata Petro anaongea kuhusu hii. Angalia Waraka wa kwanza wapetro 4:3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; Hii ilikuwa sisi sote. Kabla ya Yesu tulitenda mapenzi ya mataifa. Kusema ukwlei tulikuwa wajinga, na hii mwili na tamaa zake zilikuwa mungu wetu. Lakini Yesu alituokoa na yeye ni Mungu wetu, yeye ni Mungu wa maisha yetu na tunataka kumpendeza yeye. Petro anaendelea vs.4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. Wewe uko na Bwana wengine sasa, unafuata Yesu na hawa wengine, wazazi wako, watoto wako, Bwana ama bibi yako, rafiki zako wanashangaa kwa sababu huendi pamoja na hawa kwa hii yote tena na unaona wanafanya nini wakiwatukana. Wanakudhihaki na wanakucheka.
Sasa hawa si rafiki zako, hata kusema ukweli hawataki kuwa karibu na wewe. Kwa nini? Kumbuka hii yote tunaangalia ni vita vya roho na mwili, nuru na giza. Yesu alisema kwa kitabu cha Yohana 3:19-20 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Wakati wewe unafuata Yesu umekuwa jeshi la ufalme wa nuru. Kila mahali unaenda unaonyesha watu ukweli wa mfalme wako na inainyesha watu hawa wako gizani na wako na mfalme mwengine. Angalia Waraka wa pili wakoritnho 2:15 Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; Hii ni mzuri sana. Nafikiri sisi sote tunataka kuwa manukato, lakini vs.16 inasema katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Hawa ambao bado wako gizani wewe ni harugu ya mauti, unakumbusha hawa ya dhambi zao na hukumu ambaye inakuja. Nilijua kijana moja kitambo sana, yeye na baba yake walikuwa marafiki sana. Kila mahali uliona kijana na baba yake pamoja hata walikunywa pombe pamoja kila ijumaa, walikuwa wamelewa kila ijumaa na siku moja Mungu aliokoa kijana na ilileta shida kubwa sana kati kati ya yeye na baba yake. Kwa mwisho baba alimfukuza kijana kwa nyumba yake. Hata hajataka kuona yeye. Ni ajabu sana.
Mambo ya ulevi ni ngumu sana. Kusema ukweli inaharibu hii jamii sana. Hata siku zetu vijana hawana heshima kwa wazee, lakini wazee amabo wanalewa kila siku wanastahili heshima? Ni ngumu sana. Kulewa imeharibu familia mingi sana kwa dunia hii. Kwa nini watu wanalewa? Wengi kusema ukweli wako na shida mingi maishani yao na insaidia hawa kusahau shida zao. Wengine hawapendi hali zao ya maisha, labda ni bibi au watoto wao na wanataka kuacha ukweli wa maisha yao na wanadhani itawaleta amani. Ikiwa hii ni wewe nataka kusema msaada iko, amani iko. Ikiwa hii ni wewe tuko hapa kusaidia na tukona maneno ya tumaini hapa kwako. Ni Yesu Kristo.
Neno lingine tunaona kwa hii orodha ya Paulo ni Ulafi. Walikuwa na sherehe mingi siku zile na kubwa, watu watakuwa pamoja kula na kunywa na kulala pamoja. Kila mtu analal na mtu mwengine. Sijui ikiwa wanafanya hii hapa lakini bado uko na mahali zingine siku hizi na zinakuwa zaidi kusema ukweli watu wanafanya hii. Siku za Wagalatia wengi wao waliabudu miungine miingine na sehemu ya kuabudu miungu yao ilikuwa kufanya hii, ibada za kipagani ni ajabu, ni kujazwa na tamaa ya mwili. Shetani anapenda sana kudanganya watu kufikiri kila mitu cha maisha haya ni kujipendeza, ni kujifurahisha. Ukiangalia siku zetu, walimu wa uongo wanadanganya watu naam na gani? Wanahubiri iko sawa kujipendeza, utapata baraka za pesa, hakuna matokeo ya dhambi zako, amambo mingi kama hii. Ni hatari sana na hii ni sababu makanisa yao yamejaa na watu. Ikiwa wewe au watoto wako unaenda kanisa kama hili tafadhali jitoe haraka na pata kanisa ambalo inafundisha ukweli wa neno la Mungu, inafundisha maisha haya si kuhusu wewe lakini Yesu na kutii neno lake.
Paulo anaendelea kwa Wagalatia 5:21 kusema kitu ambacho ni ngumu sana kusikia na kufikiria. Kwa sababu sisi sote tunajua watu ambao wanasema hawa ni wakristo na wanaenda kanisa lakini maisha yao imejaa na matendo ya mwili. Angalia vs.21 ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Kitu cha kwanza tunaona hapa ni Paulo kusema hii orodha ya mwili tumeangalia na mambo yanayofanana na hayo. Hii ni kusema bado ni vitu vingi na kwa orodha zingine Paulo anasema ni matendo ya mwili. Hata kwa vs.26 anaogeza vitu viingine anasema Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Hata hii ni matendo ya mwili, majivuno, kuharibu ushiriki wetu na wivu tena. Tutaangalia hii jumapili ingine. Na tunaona Paulo anaendelea kwa vs.21 kusema katika hayo nawaambia mapema, kama nlivyokwisha kuwaambia. So kama hii orodha ni dhambi Wagalatia walianza kufanya lakini hii ni dhambi wamefanya kwa muda na bila shaka zilikuwa kama kawaida katika utamaduni wao. Vitu hivi nje ya kanisa zilikuwa kila mahali, kama kupumua. Kusema ukweli hata kwa utamaduni wetu vitu hivi vimeanza kuwa kawaida. Hata hujashangaa kusikia mtu amelala na mtu ambaye si bibi ama bwana wake, ama huyu ni mtu ya hasira au ule ni mtu ya wivu na mwengine ni mtu ya fitina. Hii yote imejaa kila mahali na unaoana hata kanisani na inakuwa zaidi na zaidi. Kwa kiingereza hii mstari vs.21 inasema ninawaonya kama nilivyowaonya. Ni kali zaidi ya kumwaambia mtu kitu wakati unawaonya.
Natumaini sana tunaposikia onyo hili, litatutia moyo wetu sana. Natumaini italeta sisi kujua hii si mchezo Paulo anasema watu ambao watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Ikiwa vitu hivi ni tabia ya maisha yako, ikiwa hii ni wewe kila siku uko na shida kubwa. Nataka ninyi kujua bado sisi wakristo tunaanguka mara kwa mara, bila shaka tuko na wivu na hasira mara kwa mara lakini ikiwa vitu hivi zinaashiria maisha yako na vitu hivi vinaishi ndani yako kama wako nyumbani uko na shida, na ile shida ni kwamba hutaingia ufalme wa Mbinguni. Nataka kuwa wazi kabisa hapa. Hii ni kumaanisha ikiwa vitu hivi ni tabia yako wewe hujaokoka, Yesu hakujui. Mbele yako hukumu na jehanamu inakuongojea. Ikiwa vitu hivi ya hii orodha ni tabia yako wewe ni adui ya Mungu.
Nafikiri nu muhimu sana kwetu kusom na kusikia maneno ya waraka wa kwanza wa Yohana 3:4-10 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Yohana ni wazi na hajaogopa kusema ukweli. Hii vita ambaye ni ndani yetu si mchezo na iko na matokeo ya milele. Roho za watu ziko hatarini. Shetani amedanganya watu kufikiri wako sawa wakienda kanisa, wakiomba, wakiongea vizuri lakini mioyo yao na akili zao hazijabadilishwa. Pasto yao hawezi kuokoa hawa, wazazi wao hawawezi kuokoa hawa, ndugu, dada rafiki zao hawezi kuokoa hawa, seri kali yao hawawezi kuokoa hawa, shule ambaye wamepata na ni mzuri haiwezi kuokoa hawa na watu wameweka tumaini lao kwa vitu hivi, hawawezi kuangalia mbele na kujua siku moja watakufa, labda leo, labda kesho labda baada ya miaka sitini. Hii ni ngumu kusikia lakini baada ya miaka tisini karibu kila mtu amabye anaketi hapa saa hii ameshaa kufa, jina lake limesahuliwa, shamba lako imeuzwa mara mingi na kila ngombe, mbuzi na kondoo ulikuwa imekufa kitambo, Waaah Travis watu watakufa moyo kusikia hiio, ndiyo ni mzuri unakufa moyo na kufungua macho yako kujua umilele uko mbele ya kila mmoja wetu. hii vitu vyote ambaye tunashika na nguvu yetu na tunapgana na watu kwa sababu ya vitu yote siku unasimama mbele ya Mungu haitakuwa na maana.
Angalia kitabu cha ufunuo 20:11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Kila kitu imeshaa isha, muda mwenyewe hakuna tena na Mungu anaketi kwa kiti cha enzi na kila kitu milima mbingu zinakimbia uso wake, kila kitu ni wazi mbele yake. Vs.12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Wakati tunasoma hii mstari, moja ya mambo mawili yatakushika, tumaini, ikiwa wewe ni Mkristo, au hofu, ikiwa wewe ni msioamini. Umeshika hii mstari? Wafu, watu wote wakubwa na wadogo amabo wameshaa kufa, mwanzo wa dunia hadi mwisho wanasimamam mbele ya Mungu. Halafu vitabu vikafunguliwa. Moja ni cha uzima. Na hawa wote ambao wamekufa wakahukumiwa katika mambo hayo yalioandikwa katika vitabu vile, sawa sawa na matedno yao. Matendo yao yako na maana mingi sana. Vs.13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Tena wote amabo wamekufa watafufuka wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matedno yake. Hufikiri kwamba matedno yako hayana maana yoyote? Ikiwa matedno yako ni ya hii mwili na unatedna vitu hivi tunasoma kwa kitabu cha Galatia uko na shida kwa sababu hii si matendo ya Mkristo na jina lako haijandikwa kwa kitabu cha uzima angalia vs.15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Sijali kama unafikiri kama umefundishwa kwa kanisa lako hii ni neno la Mungu na siku ile inakuja. Wakati inafika kwako utasema nini kwa Mungu? Bila Yesu wewe ni mtu bure. Hakuna tumaini lo lote nje ya Yesu, yeye alibeba hukumu ya dhambi zako zote juu yake msalabani, ni kuamini na kuweka imani yako katika yeye na kutii neno lake.
Ukianagalia nje kwa jamii yetu hata hapa, wengi hawaturithi ufalme wa Mungu, wengi wa kanisa mingi sana hawataurithi uflame wa Mungu kwa sababu hawamjui yeye, unaona kwa matendo yao. Mimi ninaomba sana leo asabuhi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Unafanya hii naam na gani? Kuamini, kuweka imani yako katika Yesu kristo kutubu kwa dhambi zako na kuenendeni na Roho yake. Ikiwa unataka kuongea zaidi tuko hapa, ikiwa uko na maswali yo yote karibu mbele baada ya ibada yetu.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more