The Fruits of The Spirit Pt.1

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Galatians 5:22

Leo asabuhi tunaendelea kwa masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika 5:22. Tumeona Paulo kuwaambia Wakristo wagalatia Kenendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa wiki saba sisi tumeangalia vizuri sana vitu hivi Paulo ansema ni tamaa za mwili. Ikiwa umekosa kuwa hapa na sisi nitasema enda kwa kweli kweli ministry online na angalia uko. Paulo alieleza hawa kwamba sisi wakristo tuko vitani na ni vita kwa roho zetu. Wakati Mungu alituokoa aliweka roho yake ndani yetu na hii ilileta vita, kwa sababu bado hii mwili iko pia na inatamani sana tamaa zake. Paulo alisema kwa Wagalatia 5:17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Hii inafanyika ndani ya kila mkristo. ikiwa wewe ni Mkristo unajua. Wakati tulikuwa wasioamini tulijipendeza, tulijifurahisha lakini Mungu alibadilisha mioyo yetu na akili zetu kutamani vitu vyake si ya mwili wetu. Lakini mwili iko na nguvu pia na mara kwa mara unaweza kuona ndugu ama dada wanaanguka na mwili inawashinda. Shida ni ikiwa tunaina ni tabia ya maisha ya mtu kuishi kwa tamaa za mwili wake huyu mtu si Mkristo kweli kweli. Hii ni sababu Paulo alionyesha hawa vitu hivi. Anasema Kwa waraka wa pili wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. Hii ni mzuri sisi sote tunafanya hii na mara mingi.
Leo tunaanza kuangalia matunda ya roho na tutaona ni tofauti kabisa kuwa matendo ya mwili. Tusome mistari yetu kwa muktadha yao. Wagalatia 5:16-23 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Hii ni neno la Mungu.
Tuombe:
Hii sehemu ya maandiko ni muhimu sana kwetu wakristo kwa sababu Bwana wetu yesu kristo alikuwa wasi wakati aliongea kwa kitabu cha Mathayo 7:16-20 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Anasema mara mingi hapa utajua watu kwa matundo yao. matunda ni nini? Matendo yao. Watu wengi siku zetu wanataka kuokoka lakini hawataki Yesu kuwa bwana wa maisha yao. Wanataka kuokolewa kutoka hukumu na jehanamu lakini hawataki kufuata neno la Mungu kama inasema. Hii ni sababu walumu wa uongo wengi ni watajiri, kwa sababu wanapea watu tumaini la uongo kwamba wanaweza kuwa na Yesu na tamaa za mwili wao pamoja na hii ni uongo sana, ni kwa sababu ya hii mafundisho watu wengi wanafikiri wako sawa na hawajaokoka kweli kweli. Watu hawataki kusikia kama Yesu alisema utajua mti kwa njia ya matunda yake, utajua msioamini na mkristo kwa njia ya matunda yao. Tutaona baada ya wiki chache Paulo kusema kwa kitabu cha Wagalatia 6:8 yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tunaona hii kila mahali. Tunaona watu wanapanda sana kwa mwili wao na pia tunaona matokeo ya uharibifu maishani yao na pia tunaona wengine si wengi wanapanda kwa Roho.
Kwa wiki chache sisi tutaangalia matunda ya mtu ambaye anasema yeye Mkristo. Na ikiwa huyu mtu ni mkristo kweli kweli vitu hivi vitakuwa maishani yake. Tutaona kwa hii orodha ya Paulo matunda tisa na kwa hii tisa wapo katika makundi matatu. Upendo, furaha na amani ni kuhusu Mungu. Halafu Uvumilivu, utu wema, fadhili na uaminifu ni kuhusu wengine na upole na kiasi ni kuhusu wewe mwenyewe. Tunaona tunda la kwanza ni upendo. Upendo ni Alfa na Omega kwa mafikrio ya Paulo wakati anafikiria maisha mpya katika Yesu kristo. Bila upendo wewe si Mkristo. Waraka wa kwanza wakorintho 13:13 ya sema sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo. Upendo si kitu moja kwa ordodha ya vitu vingi lakini upendo ni misingi ya kila kitu. Ni ubora wa juu kuliko wema wote, na misingi wa utauwa wote. Ni jumla na kiini cha maana ya kuwa Mkristo. Ni Upendo ili timiza sheria. Kusema ukweli Habari njema ni upendo wa mungu kutuma Yesu kristo hapa kwetu. Angalia Yohana 3:16
Related Media
See more
Related Sermons
See more