The Fruits of The Spirit Pt.2
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 1 viewNotes
Transcript
Galatians 5:22
Galatians 5:22
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika 5:22. Kwa wiki mingi tumeangalia Mtume Paulo kuwaambia wakristo wagalatia kuhusu matendo ya mwili na tuliona alisema ni dhahiri, ni wazi kwa kila mtu kuona si siri , na tuliangalia vitu vile sana sana na tumeona hakuna Mkristo wa kweli anaweza kuishi kwa vitu vile, ikiwa mtu anaishi kwa tamaa za mwili wake yeye hajaokoka kweli kweli. Wiki iliopita tulianza kuangalia tunda la roho. Ikiwa sisi tunaendeni na Roho ya Mungu tutaona vitu hivi maishani ya Mkristo. Ni mzuri kukumbuka maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa kitabu cha Mathayo 7:16-17 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti.? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Halafu vs.20 anasema Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Utajua ikiwa mtu anafuata tamaa za mwili au anaongoza na Roho kwa njia ya matunda ya Roho maishani yake. Kumbuka walimu wa uongo wameingia kanisa la galatia na walianza kufundisha ni lazima mtu anatayarishwa kupata wokovu, waliharibu neem ya Mungu na wokovu wake kusema mtu anaweza kupata kwa njia ya matendo yake. Hii ni uongo sana lakini hata siku zetu watu wengi sana wanaishi maisha yao naam na hiyo. Ni mzuri sisi tunakumbuka wokovu ni ya Mungu. Kitabu cha Yona 2 mwisho ya mstari wa tisa inasema Wokovu hutoka kwa Bwana. Ingekuwa vizuri kwetu kukumbuka hii Paulo alisema kwa kitabu cha waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Sitaki sisi kusahau hii.
Wiki iliopita tuliangalia upendo, furaha na amani. Vitu hivi vi tatu ni misingi ya yote, Upendo nii kuu kulioko yote na wakati mtu ako na upendo maishani yake atakuwa na furaha na amani. Kumbuka tulisema vitu hivi iko kwa sehemu tatu. Vitu vile vya kwanza ni kumhusu Mungu. Upendo, furaha na amani huwezi kupata mahali ingine, ni mungu peke yake anaweza kupea mtu vitu hivi. Sehemu ya pili ni kuhusu wengine na ya mwisho ni kuhusu wewe mwenyewe. Leo tumefika matunda ambao ni kuhusu wengine.
Tusome mistrai yetu kwa muktadha yao Wagalatia 5:22-24 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tuombe:
Ya kwanza tunaangalia leo ni uvumilivu. Maana ya hii ni uvumilivu wa uchungu au mgonjwa wa maumivu au kutokuwa na furaha. Ni mtu ambaye ako tayari kuvumilia chini ya majaribu na dhiki. Mtu amabye ako na uvumilivu maishani yake ni ngumu sana kusikia yeye kulalamika kwa sababu anajua ukweli na uopendo wanatshinda. Hii ni kitu ambacho wasioamini hawana. Na ni rahisi sana kuona maishani ya mtu. Yesu alikuwa na uvumilivu sana. Hata wakati alideal na watu. Kila mtu alitaka kitu kutoka Yesu, hata rafiki zake. Labda unakumbuka Mathayo 20:20-23 Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. Ni ajabu sana kufikiri kuhusu mama ya hawa aliuliza Yesu na kama hawa walisema, hawa wanaweza kufanya kama Yesu. Hii ni ujinga wa watu lakini bado Yesu alivumilia na hawa na aliwapenda.
Hata kuteseka bado Mkristo ako na uvumilivu. Angalia Yesu kwa kitabu cha Luka 23-33-34 Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Hata wakati anajua yeye ni bila dhambi bila hatia na wanamwua bure alisema Baba uwasemehe. Yesu ni mfano mkuu kwetu kufuata, lakini labda unasema anaweza kufanya hii kwa sababu yeye ni Mungu. Hii si ukweli sisi sote tuko na hii uwezo na tumeona kwa miaka elfu mbili wakati watu wanateseka kwa jina la Yesu. Watu walipelekwa mbele ya mifalme na viongozi na walisema kughairi imani yao katika Kristo na wamekataa. waliletwa viwanjani meble ya watu wingi, wingi wanyama waliwararua vipande vipandw, wengine walichomwa motoni, walipgwa na mawe hadi wakufe na bado hawajarudi nyuma kusema Yesu si ukweli. Hawajakasirikia na watekaji wao. Ni ajabu kufikiria Nigeria. Kila masaa mbili mkristo anakufa kwa ajili ya imani yake. Hii ni kumi na tatu kila siku, mia tatu sabini na mbili kwa mwezi, elfu nne mia sita hamsini kwa mwaka. Kwa sababu ya imani yao katika Yesu kristo. Deborah Samuel, msichana ambaye alikuwa miaka kumi na tisa alikuwa univeristy na alipita exams yake na aliulizwa amepita naam na gani na aliweka kwa chatroom kusema YESU amemsaidia yeye. CLassmates yake ambao ni waislamu walisema kwake kutoa hii post na alikataa. Walimopga yeye na mawe halafu walichoma mwili wake, kwa sababu ya Yesu. Hii mwaka angemaliza university. Labda unasema kwa nini hajatoa post yake kupendeza hawa watu? Kwa sababu alikuwa mkristo na alikuwa na uvumilivu kujua ukweli na upendo itavumilia.
Najua ni ngumu sana kwetu, sisi bado tunapigana na hii mwili na tamaa zake. lakini Mkristo usikasirike, usikufe moyo. Vumilia. Kumbuka Wahebrania 12:1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu. Ni mzuri kwetu wakristo tunakumbuka Mungu wetu anataka sisi kuwa mfano kwa wengine, tuonyeshe hii dunia kama Mungu wetu ako na uhai na anaishi ndani yetu. Zaburi 86:15 ya sema Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli. Kwetu wakristo ni lazima tukuwe kama Paulo alimwambia Timotheo kwa waraka wa pili wa timotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Ni mzuri kukumbuka mtu ambaye hana uvumilivu maishani yake, watu hawataki kusikia yeye.
Kitu cha pili tunaona leo ni UTU WEMA. UtuWema ni mtu ambaye ni mkarimu. Nafikiri sisi sote tunajua mtu kama hii. Akotayari kusaidia hata na kitu kidogo. Huyu mtu ni mtu ambaye anaonea mema katika kila hali. Unajua tabia yetu ya binadamu ni kuona mabaya katika kila hali. Labda unakumbuka nilisema unaweza kuwa na shamba ya acre kumi na ni mara dari sana lakini mtu anaweza kuona kitu kimoja kidogo ambaye ni mbaya na ataongea kuhusu hii. Hii ni tabia yetu. Unaweza kusponsor watoto elfu moja kwa shule lakini bado hujasponsor huyu moja na wewe si mzuri sana. Lakini UTU WEMA ni mtu ambaye hata wakati mtu analala na uginjwa mbaya sana, anaweza kupata mema kwa ile shida. Ni mtu ambaye anajua sana kuhimiza moyo ya mtu mwengine. Roho yake ni nyenyekevu. Hii ni ngumu sana kusema na hata ni ngumu zaidi kuona lakini utu wema ni mtu ambaye anatoa baraka kwa mtu ambaye anapomlaani. ni ngumu sana, hii ni sababu hii ni tunda la Roho,kwa sababu bila roho mtakatifu anaishi ndani yako huwezi. Sisi tunataka kufanya nini? Tunataka kujitetea kwanza, tunataka kulipiza kisasi. Hii ni tamaa za mwili. Mara mingi sisi tunaona mtu ambaye ni utu wema na tunaona huyu ni dhaifu, lakini huyu mtu ako na nguvu zaidi ya watu wengi. Tamaa ya huyu mtu ni kuwatenda wengine kwa upole kama vile Bwana Yesu Amemtendea.
Tunaona kwa ordodha ya Paulo kutuambia uoendo ukweli ni nini kwa waraka wa kwanza wakoritnho 13:14 kitu cha pili cha upendo ukweli ni nini? Wema? ni neno letu hapa kwa utu wema. Pia tunaona ikiwa sisi ni watu wa Mungu Paulo anasema kwa kitabu cha wakolosai 3:12 kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu. Unaona anasema jivikeni moyo wa vitu hivi na tunaona utu wema. Ni lazima tunafanya hii, bila kufanya hii watu wataona Yesu kristo naam na gani? SIsi ni watu wake, sisi ni chumvi na nuru kwa hii dunia. Lakini shida ni hata mapastors siku hizi wanapigana na wenzao kama watu wa dunia. Wakristo ninaomba sana, kuwa wakristo wa kweli. Utu wema ameshika kabisa maana ya mithali 15:1. Ni mzuri sisi sote tukiweza kushika maana ya mithali 15:1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Wakati moto mingi iko na mtu anakasirika na wewe na anaongea vibaya sana, dawa ni nini? Kwako Mkristo hii itasaidia wewe sana, Jawabu la upole. Jibu yeye vizuri na upole, ni ajabu sana na nimeona mara mingi sana hii ni ukweli. Lakini shida sisi hatuwezi kufanya hii na sisi tunafanya kama mstari inaendelea kusema Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ni ukweli ama uongo?
Turudi kwa ile ordodha ya Paulo ya tunda la Roho, kitu cha tatu cha leo ni Fadhili. Utu wema na fadhili hao ni mapacha. Wanaenda pamoja na huwezi kuwa na moja bila ingine. Ni mtu ambaye ni wema. ni mtu ambaye ako na kiroho na kimaadili bora. Mtu ambaye ako na hii tunda maishani yake anajaribu kusaidia watu wote kwa utukufu wa Mungu. Fadhili unahusiana na ubora wa kiadili na kiroho ambao unajuliakana kwa utamu wake na fadhili zake tendaji. Mtu ambaye anabeba fadhili naye ni mtu ambaye hata rafiki zake wako tayari kijitoa kwake. Tuko na mfano mzuri ya mtu kama hii. Yusufu, baba ya Yesu. Alipata Mariamu alikuwa na mimba alifikiri MAriamu hajakuwa mwaminifu kwake, kwa sababu alikuwa mtu mwadilfu hawezi mwoa Mariamu. Laini kwa sababu alikuwa mtu mwema hakutaka kumdhalilisha Mariamu. Mathayo 1:19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
Angalia Waefeso 5:8-9 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru, kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; Tulikuwa giza, sisi sote tunakumbuka siku zile bila shaka. Labda kwako ilikuwa kitambo au juzi tu lakini unakumbuka. Sasa sisi ni nuru na tunda la nuru ni katika wema wote, hii ni neno letu fadhili hapa. Ikiwa wewe si mtu mzuri katika Yesu kristo wewe si Mkristo. NA tutaona kwa njia ya maisha yako.
Tunda la nne leo kwa orodha ya Paulo Ni Uaminifu. Hii ni nini? Ni mtu ambaye ni mwaminifu. Kupata hii siku hizi imekuwa ngumu sana na kusema ukweli wakati unaoata mtu ambaye ni mwaminifu huyu mtu ni hazina. Lakini shida ya hii ni Paulo anasema hii ni tunda la Roho, ingekuwa kila Mkristo. Ikiwa wewe unasema umeokoka na imani yako iko kwa Yesu ni lazima utakuwa na uaminifu maishani yako. Ikiwa huwezi kuwa mwaminifu na ndugu na dada zako utakuwa mwainifu kwa Mungu naam na gani? Tangu sisi tumefika Kenya tumeona kudanganya mtu hapa ni kama kawaida. na kila mtu kwa jamii wamekubali hii iko sawa. Wakati mtu anasema Hii ni Kenya my friend, maana yake ni nini? Ni watu si waaminifu, wanakudanganya. Na watu hapa wanaishi maisha yao kila siku kujua huwezi kuaamini kama mtu anakuambia. Ni ukweli ama uongo? Na zaidi ya wote watu wanasema makanisa ni mabaya sana kufanya hii. Unajua mimi ni pastor, na watu wanasema mapastor ni wakora zaidi ya wote siku hizi, hii ni aibu kubwa sana. Sisi tungekuwa watu ambao wako na uaminifu maishani yao. Tukisema kitu utajua itafanyika. Tukisema saa tatu tutakuwa unaweza kujua bila shaka saa tatu huyu atakuwa. Bwana wetu, Yesu kristo, na yeye ni kiongozi yetu alikuwa mfano kwetu kufuata. Kwa sababu Yesu alikuwa mwaminifu Wafilipi 2:7-9 ya sema bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa sababu Yesu ni mwaminifu tunaweza kuamini atarudi siku moja, angalia Matendo 1:11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Ni swali nzuri sana Luka aliuliza kwa kitabu cha Luka 18:7-8 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Wakati unaangalia wakristo siku hizi hata tunauliza swali hili. Wakatu Yesu atarudi atapata imani duniani? Tunaona kanisani siku hizi kama dunia inafanya kusema ukweli tunaona kanisani vitu ambavyo hata dunia hawezi kufanya. Lakini nataka kusema kwetu wakristio lazima tukuwa na uaminifu. Tumeitwa kuwa kama Bwana wetu yesu kristo, na hii tunda itakuwa maishani ya mkristo wa kweli. Waraka wa kwanza wakorintho 4:1-2 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. Uaminifu si hiari ni lazima. Ni mstari moja imenisaidia kwa miaka mingi wakati ninaongea na mambo ya maneno yangu. Mathayo15:18 vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. unaona shida hapa ni moioyo yetu. Ikiwa yamebadilishwa tutakuwa tofauti sana, maneno yetu yatakuwa ukweli, maisha yetu yatakuwa ukweli , matendo yetu yatakuwa ukweli. Na utaona matunda ya roho. Ni watu ambao wamezaliwa tena na wanakuwa viumbe vipya watakuwa na vitu hivi maishani yao.
Ikiwa leo asabuhi umepata huna vitu hivi maishani yako ya tunda la Roho na maisha yako imejaa na matendo ya mwili nitasema tubu, weka imani yako katika Yesu Kristo, kwa sababu hakuna kitu kiingine inaweza kuleta tumaini, na ushindi kwa mtu. Ukitaka kuongea tuko hapa, karibu mbele baada ya ubada yetu.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.