The Fruits of The Spirit Pt.3
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 4 viewsNotes
Transcript
Galatians 5:23
Galatians 5:23
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano mstari wa ishirini na tatu. Kwa wiki mingi tumeona Paulo kuwaamabia Wakristo wagalatia kuhusu matendo ya mwili na tunda la roho. Kwa nini ni muhimu sisi tunajua vitu hivu? Kwa sababu Paulo aliwaambia sisi tuko vitani. Hii vita ni kali sana na mshindi anapata roho zetu. umilele wetu iko mbele yetu na si mchezo. Watu amabo wanaishi kwa hii mwili na tamaa zake mwisho yao ni hukumu halafu jehanamu, nakuambia saa hii hii mahali inaitwa jehanamu ni ukweli kama mimi ninasimama mbele yako. Ikiwa unacheza kanisa kama wewe ni Mkirsto ukweli na wewe sio kweli nataka kujua nini inakuongojea. Tunapata Yesu kuongea kuhusu hii kwa kitabu cha Marko 9:43-44 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Ananedelea kusema kwa mguu wako na jicho lako likikukosesha ling’oe ulitupe kwa sababu mahali inaongojea mtu ambaye ni msioamini ni mabaya sana. Mathayo 22:13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mahali hapa ni uchungu tu, kuteseka kama mtu hata hawezi kufikiria kwa milele na milele na milele. Mafikirio yako kwa wakati ulikuwa hapa kwa hii dunia utafikiria kila nafasi ulikuwa nai kuweka imani yako katika Yesu, kufuata yeye lakini ulifuata tamaa za mwili. Motoni, bila kifo, bila shaka jehanamu imejaa na watu wengi sana, na utaguzana uko, bila kulala, na watu watakuwa wakipiga kelele na kuteswa. Kwa kitabu cha Luka tunaona mtajiri moja alikufa na alienda kwa hii mahali mbaya na tunasoma kwa kitabu cha Luka 16:23-24 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Hii ni sababu mimi na familia yangu na Robertsons na familia yao wamefika hapa. Si kwa sababu tunataka kuishi hapa, hatujatoka kila kitu tunajua, familia, nyumba, mashamba, kazi na maisha yetu Amerikani kufika hapa kusihi tu lakini kukuambia kuhusu hii yote, na ni njia moja kutoka hii umilele ambaye inakuja na ni Yesu Kristo. Habari njema ni Yesu kristo, habari njema kwa hii habari mbaya yote, na sisi tutalipa kwa dhambi zetu kwa milele kwa mahali inaitwa jehanamu na tutakuwa chini ya ghahadhabu ya Mungu, ni Lakini Mungu. Waefeso 2:4-5 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda, hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Hii ni habari njema, hii ni ile vita tunapiga kwa roho na umilele wa watu. SI kila mtu ataamini, si kila mtu anaamini kama tunasema. Tuko na watu wanaketi hapa saa hii leo asabuhi hawataweka imani yao katika Yesu kristo na kila kitu nimesema inaongojea hawa na hii ni uchungu kwangu kama huwezi amini. Na watakuwa kwa kuteseka na kukumbuka kila jumapili walikuwa na nafasi kufuata Yesu na maisha yao na wamekataa. Angalia kama Yesu alisema kwa Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Hii ni uchungu sana kusikia. Kwa sababu tunaangalia kila mahali na tunaona watu wako kwa bara bara mpana, na hawajali nini inaongojea hawa.
Wakati sisi tunaingia kitabu kama wagalatia matendo ya mwili na tunda la Roho ni footi kupima maisha yako na kujua ikiwa wewe ni msioamini au wewe ni mfuasi wa Yesu na siku moja utasikia sauti yake kusema Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ingia katika furaha ya bwana wako. au utasikia Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Tusome mstari yeti ya leo kwa muktadha yake Wagalatia 5:16-23 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Hii ni neno la Mungu.
Tuombe:
Tumefika kwa hii orodha vitu mbili ambao ni mwisho ya tunda la Roho. Ni Upole na Kiasi. Upole ni nini? Ni mtu ambaye ni nyenyekevu. Watu wingi kwa hii dunia wanaangalia mtu ambaye ni upole na wanafikiri huyu mtu ni dhaifu, kwa sababu mara mingi si mtu ya maneno mingi na anasimama mbele ya watu lakini mtu ambaye ako na hii maishani yake ako na nguvu mingi sana na tunda moja ya kuonyesha Roho anaishi ndani ya ule mtu. Lakini pia nitasema nafikiri ufahamu wetu kuhusu neno hili upole na kama tunasoma kwa bibilia ni tofauti sana. Kitabu cha Hesabu 12:3 ya sema Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Umeshika hii, Musa alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote. Hakuna mahali ingine kwa agano la kale nzima inasema hii kumhusu mtu. Ni Musa tu. Lakini wakati tunaangalia maisha ya Musa si mtu ambaye utasema ni mpole, kwa ufahamu wetu ya hii neno. Kumbuka Musa Aliua Mmisiri, Alikuwa kasirika na alituoa mawe ya amri kumi kuu na zilivunjika, kwa sababu ya hasira alipiga jiwe ya maji na Mungu alisema kuongea na jiwe. Mtu moja alisema “upole wa kibiblia ni kujidhibiti kwa nguvu ambayo hutufanya kuwa wana-kondoo katika sababu zetu wenyewe na simba kwa sababu ya Kristo.” Kama Musa, na upole yake inalazimisha sisi kufanya kitu wakati Mungu na neno lake inachafuliwa, tuko na unyenyekevu mbele ya Mungu, na tunweka vitu vya watu wa Mungu juu ya sisi. Bila upole maishani yako huwezi kufanya kama kitabu cha Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Hii dunia imejaa na mtikisiko lakini upoke inaleta utulivu wa utulivu kwa roho zetu. na inaweka mtikisiko kuwa sawa. Upole inaltea faraja kwetu kwa sababu inaleta ushindi juu yetu wenyewe. Ni fujo mingi sana kwa hii dunia na hata mtu anaweza kuwa na wasi wasi na anaweza kufa moyo kwa sababu ya taka taka ambaye iko kila mahali, lakini upole inaleta utulivu katika maisha yetu.
Kitu kiingine upole inaltea ni ujasiri, kwa sababu lazima unafanya kama tumesoma na unaweka wengine mbele yako, na ukotayari kusaidia mwengine hata ikiwa ni ngumu kwako. Wewe umekuwa chombo muhimu kwa ufalme wa Mungu. Ikiwa wewe ni Mkristo kweli kweli utakuwa na hii tunda la upole maishani yako, hii ni sababu Zaburi 37:11 ya sema wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani. Musa alikuwa mtu ya upole kwa agano la kale lakini tunaona Yesu kristo alikuwa upole kwa agano jipya. Wafilipi 2:7-8 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Yesu alikuwa mfano kuu ya upole na bado tunaona akazipindua meza za hekalu, Aliwaita Mafarisayo wa bruta, nyoka, na akaomba si mapenzi yangu, bali yako yatimizwe. Ni ngumu sana lakini kwetu wakristo ni lazima tunakuwa na upole maishani yetu. Waraka wa pili watimotheo 2:24-25 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; Hii ni sisi sote. Ikiwa haukna upole maishani yako ni mzuri ujipme kujua ikiwa wewe ni Mkirsto kweli kweli.
Tunda la mwisho tunaona kwa hii orodha ya Paulo ni Kiasi. Kiasi ni nini? ni uwezo wa kuzuia tamaa zetu. Kusema ukweli mimi ninaona wakristo wanakosa hii tunda zaidi sana. Kiasi ni nidhambu kubwa. Mtu ambaye ako na kiasi analinda kila hatua. Mtu moja alisema kiashi ni “mwendo wa kipimo ambamo wema wa Kikristo hushika njia ya uzima na kunyoosha kupita kwa miguu inayojikwaa na kupotea.” Hii ni ukweli kabisa. Kiasi au self control ni mwisho kwa hii orodha ya Paulo ni kama anajumlisha hii yote na kiasi kwa sababu bila kiasi huwezi fanya vitu hivi. Maisha haya imejaa na majraibio na chafu na mtu ambaye hana kiasi maishani yake ataanguka mara mingi, kusema ukweli ataishi dhambini. Siku hizi tunajaribiwa kila dakika, kwa television, kwa simu kwa watu mbele yetu. mtu ambaye hana kiasi kwa siku zetu ni rahisi kuona. hanavita maishani yake ya wema na mabaya anakula tamaa zake mpaka anashiba. Ni mwisho ya orodha ya Paulo ya tunda la Roho na karibu kitu cha kwanza kw kiongozi ya kanisa. Waraka wa kwanza watimotheo 3:2 ya sema Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara. Bibilia imejaa na mistari kuhusu hii tunda la rohpo kwa sababu ni muhimu sana. Sulemani kwa kitabu cha Mitahli 25:28 anasema Asiyetawala roho yake, na hii ni kusema mtu ambaye hana kiasi maishani yake, Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta. Kumaanisha unafungua maisha yako kwa kitu cho chote bila kiasi, unakribisha adui yako ndani kwa sababu hakuna ukuta kwa maisha yako, fisi wanaingia na wanakula kondoo wote. Hii ni sisi bila kiasi.
Mtu ambaye ako na kiasi maishani yake ni mtu wa nidhamu binafsi. Huyu mtu anajijua na anajua mwili wake ni dhaifu, anajua akiona hii au anaenda mahali fulani inaweza kuleta yeye kuanguka na haendi na haangalii. Ni mtu ambaye amejenga kuta za usalama ya security karibu na mawazo na moyo wake. Ni mtu ambaye anavaa silaha za Mungu kwa sababu anajua bila silaha atakufa. Ni mzuri tuangalia haraka silaha za Mungu kusema ukweli ni mafundisho ya wiki sita saba lakini mtu ambaye ako na kiasi utaona wanavaa silaha za Mungu. Waefeso 6:14-17 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; Kiasi ni kuamuka kila asabuhi na kuvaa vitu hivi ili ukotayari kuingia vita ya maisha haya. Tunaona dirii ya haki kifuani, hii inalinda moyo wako, na chapeo ya wokovu, hii ni kulinda mawazo yetu na ngao ua imani yetu ni kulinda mwili yetu yote. Lakini ikiwa unashau kuweka hata sehemu moja ya hii silaha uko na shida, na ikiw ahujui kutumia silaha zako uko na shida kubwa zaidi. Neno la Mungu ni upanga wetu, ikiwa hatujui neno halafu sisi tutashindwa na kila kitu. Sulemani aliwaacha sisi na maarifa mingi kw kitabu cha Mithali. Ikiwa sisi tunataka kuwa na kiasi maishani yetu ni lazima tunafanya kama alisema kwa Mithali 7:1-4 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Fana hii utakuwa na kiasi. Ni vita kusema ukweli, dunia na mwili wetu yanasema jifurahisha, jipendeza, wewe unastahili hii na Mungu anasema kwa Warumi 8:13 kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Tofauti kubwa sana, hii ni sababu ni rahisi kuona watoto wa Munguna watoto wa ibilisi. SI ngumu.
Kwa mwisho ya hii orodha ya paulo aliandika kwa Wagalatia tunaona kwa 5:23 juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Hata wasioamini hawawezi kuweka sheria juu ya watu ambao wako na hizi mataunda ya Roho. Kwa sababu haiwezi kuleta shida kwa mtu mwengine, inaleta upendo na msaada kwa wengine. Wakati vitu hivi viko kwa jamaa, hata jamaa inafaulu, lakini wakati matendo ya mwili yako yanaharibu jamaa, angalia tu, tunaona kila mahali. Paulo aliwaamabia hawa wakristo wagalatia kwamba uko na watu wanajaribu kuingia na kusema lazima kufanya hii ama hii kupata wokovu lakini wakati sisi wakristo tunaendeni kwa Roho, hatuna hitaji ya mfumo fulani, mfumo wa sheria kwa sababu mawazo na mioyo yetu yamebadilishwa na vitu hivi vinafanyika kama kawadia. Sisi ni mbegu ya Mungu na mbegu inapoota hutoa vitu hivi. Si kwa lazima ya sheria lakini kwa sababu ni kawaida. Ikiwa unajaribu kupata wokovu wako kwa njia ya kufuata sheria hii ni kuweka imani yako kwa matendo yako na wewe hunatumaini. Jitoe kutoka chini ya uzito wa sheria na onja uhuru wa yesu kristo.
Nitakuuliza leo asabuhi, gani iko ndani yako? Hii yopte ya kikristo ni kwa sababu umelazimishwa? Umelazimishwa kuja kanisa, hofu imepandwa ndani yako tangu ulikuwa mtoto kwamba ikiwa huendi kanisa utaenda jehanamu? Au uko hapa kwa sababu gani? Unafuata Yesu Kristo kwa sababu gani? Labda hujui Yesu na humfuati nitaomba sana mpatanishwe naye, tubu kwa dhambi zako na fuata yeye kwa akili yako yote na nguvu zako zote. Milele iko mbele yetu, labda miaka hamsini kwa wengine labda siku moja kwa wengine labda hata leo ni siku yako, hatujui. Tena ninaomba weka imani yako katika Yesu na fuata yeye.
Ikiwa leo asabuhi huna uhusiano na yesu Kristo, hujatubu kwa dhambi zako au umeishi maisha yako yote kufikiri unafuata yeye lakini unaishi dhambini na matendo ya mwili ya jaza maisha yako nitasema kuja ongea na sisi baada ya ibada yetu, hakuna kitu cha umuhimu zaidi ya hii.
Asanteni Sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.