The True Christian

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript

Galatians 5:24

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa tano vs.24. Kwa wiki mingi tumeona Paulo kuwaambia Wakristo wagalatia kuhusu Matendo ya mwili na tunda la Roho. Natumaini sana wewe hunashaka yo yote kuhusu vitu hivi. Kama Paulo alisem avitu hivi ni dhahiri, ni wazi kwa kila mtu kuona. Ni mzuri kuona ikiwa tabia ya maisha yako ni matendo ya mwili wewe si Mkristo. Lazima Mkristo atakuwa na tunda la Roho maishani yake kwa sababu Roho mwenyewe anaishi ndani ya watoto wa Mungu. Mtume Yohana alisema wazi kwa waraka wa kwanza wa Yohana 3:7-10 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Huwezi kuwa wazi zaidi ya hii. Watu hawapendi hizi mistari lakini ni ukweli.
Usishanga kuona watu ambao wanasema hawa ni wakristo, hawa ambao wanaenda kanisa kutoka na kuishi kama wasioamini, kwa nini wanafanya hii? Kwa sababu hawa ni wasioamini, Yesu hajabadilisha miyo na mawazo yao. Knaisa mingi dunia nzima yamejaa na watu kama hii. Hii ni sababu Paulo alitoa hii orodha na aisema kwa Waraka wa pili wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. Ni mzuri sisi sote tunafanya hii.
Nataka sisi kusoma mstari yetu kwa muktadha yake Kitabu cha Wagalatia 5:16-24 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tuombe:
Tulisoma Paulo kusema kwa Wakorintho Jijaribuni mwenyewe, Swali nzuri ni tujipime naam na gani? Iko kwa mstari yetu ya leo. Unakumbuka Kwa wiki mbili tuliona kwa maisha ya Mkristo tuko vitani. Kila dakika ya maisha haya, Kwa mwili wetu na Roho yetu. Paulo anatuambia kwa mstari yetu ya leo kwa lugha kali kuua hii mwili na tamaa zake.
Ananza na vs.24 kusema na hao walio wa Kristo Yesu. Hii ni kumanisha watu ambao wameokoka kweli kweli. Watu ambao Mungu ameita kwa neema yake kuwa watoto wake. Ni wale watu ambao utaona matunda ya Roho na wanajaribu kfuata Yesu na neno lake. Tuko na watu ambao wanajiita Mkristo, tunaona hawa kila siku, wanaenda kanisa, labda ni mapastor lakini hawa hawajabadilishwa na Yesu Kristo, ni watu ambao wanatumia hii jina kusika vizuri, kwa biashara au kitu kiingine. Lakini hawa ndani ni corrupt na uovu. Ni watu wa deni si watu wa Yesu. Unajua ukisoma agano jipya utaona yesu na wenye siasa na utaona Yesu na watu wa deni. Kwa wenye siasa Yeye si kali sana, kwa sababu anajua hawa ni ya hii dunia na hawa hawasemi hawa ni ya Mungu, lakini ukiona yeye kuongea na watu wa deni, Mafarisayo yeye ni kali sana. Kwa nini? Kwa sababu wanatumia jina la Mungu vibaya. Angalia kama anasema kwa mafarisayo Kitabu cha Mathayo 23:15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. Kumbuka anaongea na Mapastor ya siku zile. Angalia vs. 25 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. VS.27 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. VS.33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Na ni hawa watu, watu wa deni, mapastors, viongozi wa kanisa anasema hawataingia ufalme wake. Angalia Mathayo 7:21-23 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Ni mzuri kujua hawa watu bado ni wasioamini, hawana tumaini kwa maisha haya na maisha ambao inakuja na wanapata thawabu yao hapa kwa hii dunia.
Ni muhimu sana kujua Paulo anasema hao walio wa Kristo Yesu, hii ni watoto wake, hii ni kondoo wake, wanasikia sauti yake na wanamfuata. Ni hawa watu amnao wameamini kwa kazi yote ya Yesu, maisha yake, kifo chake na ufufuo wake, wamezaliwa tena na wamekuwa viumbe vipya. Ni wale watu Yohana 1:12 ya sema Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; Ni sisi ambao tunaishi toafuti, tunajua hii dunia si nyumbani yetu lakini tunajua uraia wetu uko mbinguni. Tumebadilishwa, mawazo, moyo, maisha kila kitu ni tofauti sasa. Hii ni hao walio wa Kristo. na Paulo anaendelea kusema Kwa Wagalatia 5:24 hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ikiwa wewe ni Mkristo unafanya hii. Unaua kabisa hii mwili.
Wakati Paulo aliandika hii anatumia lugha kali. Kusulibisha mtu ilikuwa kifo mbaya sana. Watu wa kwazna kutumia hii njia ya kuua watu walikuwa Watu wa Uajemi au Persians. Walizanza hii karibu miaka mia nne kabla ya Yesu Alizaliwa. Wanasema kusulubishwa ni njia chungu zaidi na mbaya zaidi za kufa. Kwa sababu unakufa pole pole, unakosa hewa, umewekwa msalabani na kila pumzi ni kujiinua kwa mikono na miguu yako na mikono na miguu yako yameshikwa kwa miti na misumari. Kufa naam na hiyo ilikuwa kwa wahalifu wabaya zaidi na watu waovu zaidi. Paulo anasema mwili wetu ni kama hii, imechafuliwa na dhambi zetu, Wakati sisi tunakuwa wakristo hii mwili ni adui yetu ya kwanza. Si shetani, si mtu mwengine ni sisi mwenyewe. Na Paulo anasema sulubisha hii adui yako.
Related Media
See more
Related Sermons
See more