Mara Christian welcome back 2024

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

· Karibuni wote. Karibuni kwa shule tena na kwenu ambao umeingia mwaka huu. Kwa chapel service leo nataka kukaribisha ninyi na lengo yangu ni kwenu kujua lengo yetu ya Mara Christian.
· Kiti cha kwanza ni muhumu sana ninyi unajua Mara Christian si kama shule nyingine. Hapa ni tofauti sana. Nataka nyinyi kujua tunakupenda, na tunapenda roho yako. Ni kweli utasoma vizuri sana hapa, kila kitu unahitaji iko na masomo itakuwa juu lakini kwangu hii si lengo yangu ya kwanza.
· Lengo yangu kwenu ni hii: Kujua Mungu Yuko. Huwezi kumjua Mungu mpaka ujue Mungu Yuko. Wahebrania 11:6 ya sema Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Hii ni kitu cha kwanza, Mungu yuko, si kama sisi tunaishi hapa kwa hii dunia kwa bahati mbaya. Mungu ni Umbaji na aliumba kila kitu hata mimi na wewe na yeye ni Mtakatifu na uhusiano wetu imeharibika kwa sababu ya Mama na baba ya sisi sote, Adamu na Hawa, walitenda dhambi.
· Ikiwa Mungu yuko na uhusiano wetu imeharibika na yeye tufanyaje? Tunataka kurudi kwake na kuwa na yeye. Bibilia inatuambia ni njia moja, ni Yesu kristo. Sisi hatuwezi kufika kwa Baba bila Yesu Yohana 14:6 Yesu alisema Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Ni Yesu tu, hakuna Miungu miingine au nabii, au mtu mwengine anaweza kutuleta kwa Baba ni Yesu. Sasa ikiwa Mungu yuko na njia kufika yeye ni Yesu, lazima tufanyaje? Kuamini katika Yesu Kristo. Tunamini naam na gani? Wakati tunasikia neno lake. Kitabu cha Warumi 10:17 ya sema imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Chanzo cha Imani yetu ni kusikia neno la Mungu. Bila kusikia neno la Mungu hakuna wokovu, hakuna kujua Yesu wa kweli. Labda unaketi hapa saa hii na unafikiri umeokoka, ikiwa chanzo cha Imani yako haijatoka kusikia neno la Mungu, Imani yako ni fake, si ukweli. Hapa kufundisha neno la Mungu kwako ni muhimu sana kwetu, hii ni sababu tunafanya boys clubs, girls clubs, chapel, Mara Bible, Ucahmbuzi wa bibilia jumapili asabuhi, kanisa. Ni muhimu sana kwa sababu bila hii hakuna imani na hakuna kuamini Yesu Kristo.
· Wakati mtu anaamini katika Yesu kristo daika ile dhambi zake zimesemehewa. Umesafishwa na damu ya Yesu Kristo iliyomwagwa msalabani. Bibilia inatuambia Yesu Alikuwa Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Baada ya hii sisi tunaweza kujua tunaamani na Mungu na kwa sababu ya Yesu Kristo na wokovu wake tuko na uzima wa milele. Mtume Yohana alisema kwa waraka wa kwanza wa Yohana 5:13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Wakati mtu anaamini katika Yesu kristo anakuwa kondoo yake na anasikia sauti yake na anamfuata. Sisi tunataka ninyi kufuata Yesu Kristo na akuwe Bwana wenu. Tunataka ninyi kujua hakuna kitu wewe mwenyewe unaweza kufanya kufika Mungu, hakuna matendo mazuri ya kutosha unaweza kutenda, yote ni kwa Yesu, maisha haya ni kwa Yesu.
· Kitabu cha Matendo 17:28 inatuambia ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Wakati unatoka Mara Christian lengo yangu ni utasema hii ni lengo yako ya maisha yako.
· Kwa sababu ya hii yote, hapa tunaheshimiana, Tunaheshimu walimu na walimu wanaheshimu wanafunzi. Tunaishi Pamoja kwa amani, Hatupigani sisi kwa sisi. Vijana tunachunga wasichana, tunaweka hawa mbele kwa line, tunafungua mlango kwao. Walimu na wanafunzi hapa wanacheza Pamoja, tunakuwa Rafiki ya wanafunzi lakini bado wanafunzi lazima heshima ikuwe na hata wewe utapata heshima. Ikiwa uko na shida tafadhali ongea na sisi, tuko hapa kusaidia. Ikiwa ni mambo ya shule au nyumbani au uhusiano wako na mwengine, ongea na mimi ama Laura ama Mwalimu. Unaweza kuenda kuongea na Miriam kwa ofici yake. Tuko hapa kwako, kwa sababu ya lengo yetu ya kwanza.
· Hata hii shule iko na sheria yake, kuwa hapa sio haki yako lakini ni upendeleo wako au privilege. Ikiwa huwezi kufuata sheria ya shule, hutakuwa hapa. Unaweza kupima kuona na pole sana utaona.
· Karibuni sana tena, tumefurahi umefika hapa.
Kitu kiingine nilitaka kusema ni umeona wakati umeingia mission ilikuwa mara dari, hakuna taka taka inalala chini, mimi ninaomba unaheshimu hapa pia. Ikiwa unaona taka taka weka kwa bin, ikiwa unapata kitu ambacho si yako peleka kwa ofici na pea head teacher ama principle, hata ikiwa ni pesa. Kumbuka macho ya Mungu ni kila mahali na anaona kila kitu. Ikiwa huwezi kufanya kama tunasema hutaenda snackchack kununua sweets. Wakati unafungua kitu weka kartasi yake kwa taka taka. Sawa? Asante.
Related Media
See more
Related Sermons
See more