Restoration of a brother in sin

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

Galatians 6:1

Leo tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa sita mstari ya kwanza. Kweli kweli nimefikiri wakati nimerudi kutoka US mwezi wa kumi na moja mimi ninarudi kwa kitabu cha Yohana na hawa wemeshaa maliza kitabu hiki, lakini kumaliza kitabu hiki kimekuwa tamu sana. Sisi tumeona mambo mingi sana, na bado kwa hii mlango ya mwisho tutaona mambo mingi. Natumaini sana vitu hivi tumeona vimkusaidia kwanza kujua ikiwa wewe ni mkristo wa kweli na ya pili ikiwa wewe ni mkristi vitu hivi vimetia moyo wako kuvumilia na kufuata Yesu na neno lake.
Kwa mlango wa sita tutaona vitu vingi tena ya kusaidia maisha yetu kuwa Mkristo na vitu ambavyo lazima tutaona kwa maishani ya Mkristo. Leo Paulo anatuonyesha jinsi ya kurejesha ndugu au dada aliyeanguka dhambini. Tunajua walimu wa uongo wameingia na wamegawa watu na mafundishi wa uongo wao. Bila shaka watu walifuata hawa na ilileta fujo na fitina mingi kanisani na kati kati ya watu. Ikiwa ni naam na hiyo lazima tunataka kujua kurudisha hawa watu naam na gani kwa ukweli. Siku zetu hata ni ngumu kupata makanisa wanafanya hii na ikiwa mtu ako dhambini , watu wananyamaza. Pole hatuwezi kunyamaza. Na leo lengo yangu ni tutaona kurejesha au kurduisha mtu naam na gani kama Bibilia inasema.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake. Wagalatia 6:1-5  Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombee:
Kitu cha kwanza tunaona kwa mstari yetu ya leo mstari ya kwanza ni ndugu zangu. Hakuna shaka yo yote Paulo anaongea na nani hapa, ni wakristo wa kweli, kama tutasoma leo si kwa wasioamini, hawawezi kufanya kama tutasoma leo. Anaendelea kusema mtu akighafilika katika kosa lo lote. hii ni kusema nini? Ikiwa mtu ametenda dhambi yo yote na sasa huyu mtu anaishi dhambini. Kumbuka tumekuwa kwa wiki mingi sana kuongea kuhusu matendo ya mwili. Ikiwa mtu ako na dhambi ya (Gal. 5:20-21 for dominic) uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo. Hii yote ni dhambi na natumaini sana sisi hapa hatuna shaka ya kujua dhambi ni nini? Paulo anasema watu ambao ni wakristo wakipata mtu anaishi kwa dhambi, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo. Hapa ansema ninyi mlio wa Roho. Kwa kiingereza anasema ninyi ambao ni Spiritual. Nataka ninyi kujua kitu cha kwanza ikiwa mtu ameanguka ni mzuri tusaide huyu mtu kusimama tena. Anahitaji kusimamam teba si kubaki chini, ikiwa mtu ameanguka na analala chini ako hatarini. Hatujui ikiwa amevunjika kitu au ameumwa wapi, kazi yetu ni kusaidia huyu kusimamam tena. Hawa watu wameanguka dhambini wanahitaji sisi ambao ni wa Roho. Mungu akipenda wiki ijayo tutaangalia sana njia ya kufanya nidhambu ya kanisa au Church discipline. Lakini huyu mtu ambaye ameanguka anahitaji sisi kusaidia yeye, si kupiga yeye wakayti ako chini, si kuongeza vitu viingine kwa shida yake.
Lakini baada ya kusiadie yeye kusimama bado anahitaji kukemewa, kurudisha miguu yake kwa njia ya kweli. Jukumu la watu ambao wangemrejesha mtu kama huyo iko juu yetu ya kanisa, watu ambao wanatii neno la Mungu na unaona maishani yao. Utajua hawa watu naam na gani? Tumeongea wiki tatu kuhusu hawa, ni watu ambao wako na matunda ya roho na tunaona ndnai ya hawa kwa sababu wanafanya. (Gal.5:22-23 for Dominic) upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; Hawa ambao wako na vitu hivi na ni dhairi ni watu kusaidie ndugu na dada kusimama tena.
Mara mingi watu wanaenda na wanaongea na fulani ambaye amekosa na huyu ambaye ako dhambini anasema nini? Wewe ni nani kuniambia hii na wewe unafanya hii na hii na hii. Labda hii sababu watu haoa haendi kuongea na mtu ambaye ameanguka kwa sababu maisha yake mwenyewe si safi? Lakini pole kusema ikiwa wewe ni mtu ambaye unaongozwa na Roho, watu ambao wako dhambini ni shida yako.
Sisi tulio na nguvu kiroho na kiadili tuna daraka au jukumu la kuwalea walio dhaifu kiroho na kiadili. Ni ngumu sana na hii kazi haitaisha, usichoke. Paulo alisema kwa Warumi 15:1 imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. Halafu Waraka wa kwanza wathesalonike 5:14 Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. Ni kazi yetu. Pole usichoke, haitaisha, lakini siku moja tutapumzika mbinguni.
Tuko na mfano wa Bwana wetu Yesu kristo wakati aliongea na mwanamke amabye ameshikwa dhambini ya Uasherati. Hii ni ajabu sana, na tunaona watu ambao wanasema hawa watu wa Mungu lakini hawa hawajakuwa na Roho. Ni Mafarisayo na waandishi. Watu wa sheria ya Mungu. Angalia kitabu cha Yohana 8:3-4 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? Unajua kwa hii hadithi huyu Mwanamke ameshikwa wakati hii uzinzi inafanyika, lakini huoni wameketa mwanamume ambaye anafanya hii pia. Kwa sheria huyu Mwanamke anastahili kufa kwa njia ya kupigwa na mawe mebel ya watu wote. na vs.6 tunaona wanapima Yesu Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Walitaka Yesu kuvunja sheria ya Musa ili wanaweza kusema yeye ni mbaya. Lakini tunaona Yesu anafanya kitu cha ajabu. Vs.6 inaendelea kusema Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Sisi hatujui ameandika nini katika nchi lakini watu wengi wanafikiri labda ameanza kuandika dhambi za Waandishi na Mafarisayo. Vs.7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Hii ni ajabu sana. Yesu alijua sisi sote tumezaliwa katika dhambi, na kwetu kuhukumu mwengine kwa dhambi ni ngumu kwa sababu sisi sote ni wenye dhambi. Wakati wamesikia hii vs.9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. Vs. 10 -11 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena. Hii ni mfano yetu wakati tunarejesha mtu, wakati tunapata mtu dhambini, kurudisha hawa, kusaidia hawa. Yesu hajataka kuharibu huyu mwanamke lakini kusaidia yeye.
Nimesema si kazi yetu kuhukumu mwengine na ni kweli. Lakini ni mahali ingine Yesu aliongea na watu wanatumia hii mstari mbaya sana na nje ya muktadha yake. Angalia Mathayo 7:1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Watu wengi wanapenda kutumia hii, Bibilia inasema usinihukumu. Hata unaenda kuongea na mtu kuhusu kosa wametenda Usinihukumu. Lakini tukiangalia vs.3-4 tunapata muktadha ya hii mstari. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Yesu anaongea kumhusu mtu ambaye ako na uadilifu binafsi, ni mtu ambao anafikiri yeye ni hakimu, na anatoa hukumu kwa wengine, anaona yeye ni mzuri tu na wengine, wote ni wabaya. Huyu mtu ambao ni naam na hiyo si muzri anahukuma mwengine. Lakini wakati mtu anatubu kwa dhambi zake na anaishi maisha safi na kufuata neno la Mungu Tunoana vs.5 Yesu alisema Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. Huyu mtu ni lazima anasaidia ndugu yake kutoka dhambi zake. Kwa sababu atakuwa kama hyu mtu Paulo anasema atakuwa mtu ambaye mlio Roho. Na lazima tunamrejesha upya mtu ambaye ameanguka dhambini.
Kazi yetu ni kusaidia watu kuona makosa yao. mara mingi wakati watu wanaanguka dhambini hawawezi kuona wametenda makosa, hata watu ambao wanajua ukweli. Na sisi ambao ni ya Roho na tunafuata Yesu ni lazima tunafanya hii kwa kila mtu ambaye wanasema mimi ninafuata Mungu au mimi ni Mkristo. Mara mingi sisi ni kipofu kwa dhambi zetu, lakini kama Yesu alisema tunaona dhambi za watu wengine haraka. Ni mahali ingine bibliani mfalme Daudi alianguka dhambini. Labda unakumbuka aliona Bathsehaba wakati anaoga juu ya dari na tunasoma huyu alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Daudi alichukua yeye alilala na yeye na hata alijua ako na Bwana, hata huyu Bwana wake aliitwa Uria, Mhiti a bado Daudi aliingia na alilala na yeye na akapata mimba. Uria alikuwa mshujaa ya Daudi walikuwa thelathini na saba na walikuwa marafiki sana na Daudi, walimpenda Daudi. Na bado Daudi alifanya hii kwa bibi ya Uria. Halafu baad aya hii tunasoma Daudi alijaribu kufunika au kuficha hii dhambi na aliita Uria nyumbani ku kaa na bibi yake Bathsheba. Uria alikataa na alilala kwa mlango ya Daudi usiku mzima. Tunasoma kwa Kitabu cha pili cha Samweli 11: 14-15 Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria. Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe. ni ajabu sana.
Nani atamrejesha Mfalme wa Israeli? Tusome kwa kitabu cha pili cha Samweli 12:1-6 Ndipo Bwana akamtuma Nathani aende kwa Daudi. Naye akamwendea, akamwambia, Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wa pili maskini. Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng'ombe wengi sana; bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana kondoo mmoja, mdogo, ambaye amemnunua na kumlea; naye akakua pamoja naye, na pamoja na wanawe; hula sehemu ya posho lake, na kukinywea kikombe chake, na kulala kifuani mwake, akawa kwake kama binti. Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia. Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo Bwana, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa; naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Hii hadithi Nathani alimwambia mfalme Daudi ilikuwa ngumu sana na Daudi alikasirika kama mtu anaweza kufanya kitu kama hii kwa mwengine. Sasa fikiria Nathani anasimama mbele ya mfalme wa Israeli, bila shaka si rahisi na tunasoma vs.7 Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Kusimamam mbele ya Mfalme na kumwambia yeye huyu mtu ni wewe, ni wewe umeteda dhambi na tunasoma votu viingine amemwambia yeye vs.9-11 Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni. Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Nathani alikua maisha yake ilikuwa mikononi ya Daudi, angesema ua huyu mtu, Bila shaka wajeshi wa daudi wangetoa kichwa cha Nathani. Lakini tunasoma vs. 13 Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Hii ni lengo ya sisi sote ambao tutamrejesha ndugu yetu. Daudi aliona makosa yake na alitubu kwa hii dhambi. Hata ni baada ya hii Daudi aliandika Zaburi 51. Sikia moyo wa Daudi kwa Zaburi 51:1-4 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Halafu vs. 7-14 ‌Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na damu za watu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako. Hii ingekuwa mioyo ya kila mtu wakati wameanguka dhambini na wametubu kweli kweli. Baada ya Nathani kuleta hii kwa Daudi aliandika hii na amerejeshwa. Hii ni lengo yetu.
Sisi tunataka kuona watu wamerejeshwa na Mungu. Kurejesha mtu maana yake ni kutengeneza kitu. Ilikuwa kama mtu alivunjika mkono yake na wakati anaenda Daktari, huyu Daktari anarudisha mfupa ikuwe mzuri ili inaweza kupona na kurudi katika hali ya kawaida. Na sisi tunafanya hii kwa njia ya kuonyesha watu makosa na kuwaambia hawa kutubu kwa sababu uhusiano wao na Mungu imeharibika. Wakati dhambi iko kmaishani yako, uhusiani wako na Mungu si mzuri, kwa sababu Mungu anachukia dhambi.
Tunafanya hii na ndugu na dada zetu kwa roho ya upole kama mstari yetu ya Wagalatia inasema. Kwa sababu tukihukumu huyu au tunakuwa mbaya kwake hata sisi wenyewe tunaweza kuanguka dhambini. Ni mzuri kukumbuka sisi sote ni wenye dhambi na leo tunaweza kuona mtu kutenda dhambi ya ajabu sana na bila kujichuna hata kesho ni sisi kufanya kama huyu. Kuongea na ndugu au dada kuhusu dhambi si kitu cha majivuno lakini ni kitu cha unyenyekevu na kusema ukweli huzuni. Wakati tunaona Mkristo mwengine anaanguka dhambini ingevunja mioyo yetu. zdawa ya hii yote ni kukaa karibu na Yesu na kutii neno lake. Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, Tukifanya hii tutakuwa watu wa roho, tutajichunga na tutasaidia wengine ambao wameanguka dhambini. Wiki ijayo Mungu akipenda tuaingia nidhamu ya kanisa. Tutaona kama Mungu kwa neno lake anasema kufanya hii na si kama watu wanafanya hapa.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more