Introduction to Creation
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 6 viewsNotes
Transcript
Genesis 1:1
Genesis 1:1
Leo tunaanza masomo ya kitu ambacho ni muhimu sana, UMBAJI! Tunapata kuhusu umbaji wa kila kitu kwa kitabu cha Mwanzo. Na kama tunafikiria mlango wa kwanza hadi kumi na moja ya Mwanzo ni muhimu sana, kwa sababu ni misingi ya kila kitu. Ikiwa misingi yako ni mbaya nyumba nzima ni mbaya. Siku zetu kila mahali watu wanajaribu kutuambia mahali umbaji ilitoka. Kwa shule, kwa seri kali kwa makanisa na wengi hawataki kujua Bibilia inasema nini kuhusu hii, kwa sababu hawataki kujua kwamba ni Mungu ameumba kila kitu. Siku hizi ni mafundisho mingi sana na ni uongo zaidi kwa sababu wanajaribu kutoa Mungu kwa umbaji wake. Wanasema hii yote ilifanyika tu na sisi tulitokana na nyani! Watu wanasema huyu ni babu wetu. Na kwa masomo yetu tutaona Mungu alituumba kwa sura wake.
Kwa wiki mingi tutaangalia kila chapel service, siku moja ya umbaji na Mungu aliumba nini siku ile. Tunajua Mungu Aliumba kila kitu kwa siku sita halafu alipumzika siku ya saba na baada ya siku ya sita tunasoma kwa kitabu cha Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Kila kitu kilikuwa kamilifu hata Wanadamu.
Leo nataka sisi kuangalia mstari ya kwanza. Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Hii mstari moja imejaa na vitu vingi sana, kusema ukweli muda hautoshi leo asabuhi kuongea kuhusu yote. Lakini kitu cha kwanza tunaona ni hapo mwanzo. hapo ni wapi? ni kama inasema hapo mwanzo, mwanzo ya kila kitu, hakuna kitu ilikuwa isipokuwa Mungu. Mungu ni wa milele hana mwanzo hana mwisho. Wengi wanasema alikuwa peke yake alikuwa upweke, lakini kumbuka Yesu alikuwa na Roho Mtakatifu alikuwa, na ndani ya hawa tatu wana ushirika mkamilifu pamoja. Hawahitaji chochote nje ya hayo.
Hapo Mwanzo, hakuna kitu cho chite kilikuwa na tunasoma, Mungu. Hii ni muhimu sana. Kwa sababu siku zetu watu wengi wanajaribu kutuambia Hii yote ilifanyika tu. na wanasema kitu inaitwa Big Bang, mlipuko mkubwa kilitokea na kwa sababu ya hii tuko na sayari, planets na kila kitu ambacho tunaona, miti, mawe, milima, maji. Lakini Neno la Mungu linatuambia Mungu alikuwa, na Mungu Aliziumba mbingu na nchi. Bila kuamini hii hatuwezi kusema tunaamini Mungu ni Mkuu, ana nguvu zote na Anajua kila kitu. Ikiwa Mungu si Muumbaji ya kila kitu yeye si Mungu. Lakini tuko na mistari mingi kutuambia kuhusu Mungu na umbaji wake. Angalia Isaya 40:21-22 Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia? Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; Ukiendelea kusoma tunaona vs. 25-26 Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi, hizi ni nyota; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake. Hii ni ajabu sana. nani ameangalia juu usiku na umeona nyota mingi sana? hii mstari inatuambia Ni Mungu aliumba nyota zote na hata anaita hawa kwa majina yao. Mungu wetu ni ajabu!
Tunaona Kwa Mwanzo 1:1 Mungu Aliziumba mbingu na nchi. Hii ni kila kitu. Kila kitu tunaweza kuona na kila kitu hatuwezi ona. Mungu Aliziumba. Hata Bacteria na Vijidudu, Germs. Huwezi kuona lakini Mungu aliziumba. Nataka nyinyi kuona vitu ambavyo ni ajabu sana Mungu wetu Alziumba. Dunia. Earth. Hii ni mahali tunaishi. Jua yetu, The Sun. Jua yetu ni kubwa sana, ukijaza jua na dunia itachukua dunia millioni moja na mia tatu. Ni kubwa sana! Sayari, Planets. Nyota, Stars. Galaxies. Galaxies zinaweza kuwa na nyota millioni moja au trillioni kumi. Hii ni Galaxy yetu, inaitwa Milky way galaxy. Galaxy yetu iko na zaidi ya nyota bilioni mia moja. Dunia yetu iko hapa. Lakini ni kidogo kuliko punje moja ya mchanga. Kwa sababu ya Technologia na kitu inaitwa darubuni au Telescope sisi binadamu tunaweza kuangalia na kuona mbali sana siku hizi. Telescope inaingia anga ya nje na inapiga picture na inatuma hapa kwetu. Inaweza kuchukua siku kumi na moja kwa picture moja kurudi hapa dunia kutoka darubini au telescope. Ni ajabu vitu ambavyo tumeona, tumeona uliwengu Mungu wetu aliumba. Ni picture moja ilipigwa na tunaweza kuona Galaxy elfu kumi na tano. Hii ni ajabu na kumbuka bado hatujaona nyuma ya hii camera. Kweli kweli Mungu wetu ni ajabu sana.
Pia tuko na vitu ya mara dari mingi na ajabu na zinaonyesha utukufu wa Mungu wetu. Ni kitu inaitwa nebula na nebula ni nyota ambaye inkufa na wakati inakufa inalipuka na inatupa vumbi na gesi. Lakini ni mara dari sana. hii ni Eagle Nebula. Hii ingine ni Ant Nebula. Helix Nebula. Orien Nebula. Na ni mingi sana zaidi. Ikiwa unaingia computer na unagoogle vitu hivi utashangaa. Na Mungu aliziumba vitu hivi vyote naam na gani? Angalia kiatbu cha Zaburi 33:6 Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Mungu alisema na ikawa. Hii ni nguvu ya Mungu wetu. Kwa sababu ya neno la Mungu sisi tunajua hii yote, na wakati tunamini inaleta imani na kitabu cha Wahebrania 11:3 ya sema Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Hata tutaona kwa masomo yetu ya umbaji Mungu aliumba sisi pia, Adamu na Hawa ni wazazi wetu lakini walikosa na hawajatii neno la Mungu na walitenda dhambi na hii iliharibu uhusiano wa binadamu na Mungu. Hii ni sababu Mungu alituma Yesu kristo, kufa kwa ajili ya makosa yetu na kurudisha sisi kwake. Kwa sababu ya Yesu tunaweza kuwa na uhusiano na Umbaji wetu tena. Bila Yesu hatuwezi. Kifo cha Yesu msalabani ilikuwa lazima kulipa kwa dhambi zetu na wakati tunaweka imani yetu katika Yesu na kifo chake na tunaamini hii yote, Bibilia inasema tumeokolewa na tunarudishwa kuwa sawa na Mungu.
Ni kitu kiingine ni ajabu sana ya umabaji wa Mungu. Karibu kati kati ya Uliwengu au Universe wamepata Galaxy na inaitwa M51 spiral Galaxy na wameshangaa kupata kati kati ya hii galaxy ni kitu kubwa inaonekana kwa picha ambaye ilirudi. Ni hii: Msalaba. Na wamepima hii na ni kubwa wanasema ni Light year elfu moja mia moja. Light year ni kasi ya mwanga. Ni kusafiri kilometer elfu mia tatu kwa sekunde moja. Kumaanisha itachukua miaka elfu moja mia moja ya kusafiri kilometer elfu mia tatu kila sekunde kusafiri panda moja hadi panda ingine.
Mungu wetu ni ajabu, Yesu Kristo ni ajabu, tunataka kuwapea sifa zetu. Asanteni sana.