Church Discipline

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 5 views
Notes
Transcript

Matthew 18

Tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika Mlango wa sita mstari wa kwanza. Wiki ilioptia tuliangalia vs.1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Tuliangalia hii sana kuhusu mtu ambaye ni wa Roho. Tumeona lazima sisi tunakuwa safi na tunatembea na Yesu na kutii neno lake ikiwa tunataka kusaidia ndugu au dada yetu. Leo nataka kuangalia huyu mtu mwengine ambaye ameanguka dhambini. Bila shaka kwa sababu ya walimu wa uongo waliingia kanisa la wagalatia wengine wameingia dhambi wameanguka kwa sababu wamefundishwa vibaya, Paulo alitaka hawa wengine ambao hawajaanguka kurejesha hawa, kurudisha hawa kwa njia ya kweli. Hata Bwana wetu Yesu Kristo alituambia kufanya hii naam na gani na tunaoata hii yote kwa kitabu cha Mathayo 18.
Nimeulizwa mara mingi kuhusu hii kitu inaitwa nidhamu ya kanisa au church discipline. na kusema ukweli ni meshangaa kusikia kama watu wanafanya na mapastor wengi wamechafua mafundisho ya hii. Sisi tunajua kanisa ni ya Mungu ni kwa Yesu si yetu na ni lazima tujue yeye anasemaje kuhusu watu wae ambao wameanguka dhambini. Ni kama mafundisho ya hii siku hizi watu wanafanya kama wanataka. Nimesikia kanisa moja waliweka mshariki moja wao kwa nidhamu ya kanisa kwa sababu aliingia jumapili moja na hajasalimia pastor. Pole sana lakini hii ni mbaya sana, na ni uongo na ikiwa mapastor wanakubali na hii, hawajui neno la Mungu na wanataka watu kuwaabudu hawa, na wanajiweka kuwa kitu kwa kanisa la Mungu ambaye Mungu mwenyewe hajasema kufanya. Fikiria hii. Wewe unapata mfanya kazi tuseme ni mchungaji ya kuchunga kondoo yako. Labda uko na kondoo mia tatu. Umekubali huyu mtu kuingia na kufanya hii kazi, halafu baada ya muda unapata huyu mtu kwa soko na kumbe anauza kondoo mbii na ni yako, hata anawaambia watu hii kundi la kondoo ni yake, wewe utafanyaje? Ni mzuri ninyi unajua mapastor wengi sana wanafanya naam na hiyo kwa kundi la Mungu. Hii ni hatari sana na mtu ambaye atafanya hii ni mzuri ako na hofu maishani yake.
Kitu cha kwanza nataka sisi kuangalia ni nidhamu ya kanisa ni nini, au iko kwa sababu gani na ni kwa nani. Watu wa Mungu au wakristo sisi tumeitwa kuwa watakatifu. Waraka wa kwanza wapetro 1:16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Bwana wetu anataka watu wake kuwa nuru kwa hii dunia na kwa watu ambao hawamjui yeye. Angalia Mathayo 5:16 nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Yesu Kristo alilipa deni letu msalabani na alitoa sisi kwa ufalme wa giza na ametuleta kwa ufalme wake wa nuru. Yesu alinunua sisi Waraka wa kwanza wakorintho 6:20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. Hata anaita sisi chumvi ya hii dunia. Tunaogeza ladha kila mahali tuko kwa sababu sisi ni tofauti na sisi ni watoto wa Mungu wetu na mfalme wetu ni Yesu kristo.
Shida ni hii, bado tuko na hii mwili. Ni ukweli roho zetu zimezaliwa upya lakini hii mwili inaoza kila siku na bado iko chini ya laana ya dhambi na iko na tamaa mingi sana. Kama tumeangalia sana angalia Wagalatia 5:16-17 Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Hii ni kumaanisha kwamba mara kwa mara ndugu au dada yetu wanaweza kuanguka dhambini, na sisi tunajua dhambi ni giza, na huwezi kuishi gizani na kusema wewe ni Mkristo. Waraka wa kwanza wa Yohana 1:5-6 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; Nidhambu ya kanisa iko kusaidia kanisa la Mungu kurejesha au kurudisha mkristo ambaye ameanguka dhambini au anaanza kucheza na dhambi. Ni kitu ambacho Mungu anatumia kusafisha kanisa lake ili ikae safi. Kwa sababu tena giza haiwezi kuisha nuruni, chafu haiwezi kuwa safi. Natumaini sana umeanza kuona ni kitu kubwa zaidi ya kukataa kusalimia pastor yako, si kuhusu pastor yako ni kumhusu Mungu na watu wake. Hii ni sababu Yesu kristo mwenyewe alitoa malekezo kwetu kwa mambo ya nidhamu ya kanisa.
Tunapata hii kwa kitabu cha Mathayo 18:15-18 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Hii ni neno la Bwana wetu Yesu Kristo.
Tuombee:
Tunaona kwa vs.15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. Kitu cha kwanza tunaona hapa ni ikiwa ndugu yako akikukosa. Ni kusema ikiwa ndugu yako ameingia dhambi na kwa sababu ya hii dhambi imekukosea. Sasa hapa si pastor yako, si kanisa lako au marafiki yako lakini jukumu ni juu yako kuenda na kuongea na ndugu au dada yako. Na inasema ndugu, na ndugu atakuwa mtu ambaye ni Mkristo ni mtu ambaye ameweka imani yake katika Yesu. Lakini hata hii ni mfano mzuri kufanya kwa mtu yo yote maishani yako. Sasa Hii shida saa hii ni kidogo na ni kati kati ya wewe na huyu mtu. Na unaenda na unaogea na yeye, sasa unaongea na yeye kuhusu hii makosa au dhambi ambaye imefanyika. Na hii ni kwa kila Mkirsto, ikiwa ni mimi pastor yako au mwengine, lazima tunadeal na dhambi kama ni ugonjwa mbaya. Kwa sababu kusema ukweli dhambi ni ugonjwa mbaya sana na ikibaki bila kutibiwa itakuwa mbaya zaidi badaye. Na wakati ndugu au dada yetu wanatukosea ni mzuri kuenda haraka, si kuchelewa. Kwa sababu kitu ambacho inaendelea, inakuwa kubwa zaidi. Mungu ameita watoto wake kwa waefeso 4:32 kuwa naam na hiyo, iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Unajua kanisa inajileta shida kubwa wakati haiwezi fanya hii vizuri. Hii ni sababu makanisa mingi sana wako na wakora, wizi, walevi, na watu amabo wanaishi dhambini na unasikia watu kusema, siwezi enda kanisa lile kwa sababu limejaa na watu wabaya sana. Kila dhambi, kila moja wenu unafanya nje ya kanisa hili inachafua sisi sote ndani ya washiriki wetu. Ikiwa unadanganya mtu kwa gate na unauza kitu bei kali watu wanasema huyu ni mkora na anaenda AIC Sekenani. Ikiwa uko na duka na mtu anataka kitu na unauza vibaya wanasema na huyu anaenda AIC Sekenani. Hata tumedeal na watoto wa shule ambao wamekosa na mimi nafikiri tumefanya vizuri na hawa na bado utasikia mzazi kusema na hii ni shule ya kanisa. Dunia inaongojea nafasi kuongea vibaya kuhusu kanisa ya Yesu. Ni mzuri unajua kila kitu unafanya nje unaleta sifa au unaleta aibu kwetu sote, kwa mwili wa Yesu.
Tukipata moja wetu amefanya vitu hivi enda peke yako kwanza. Baada ya ukamwonye akikusikia, pongezi sana umepata nduguyo. Ni kumanisha ametubu, amekubali ametenda dhambi na ametubu aliomba msamaha kwanza ya Mungu na ya pili kwako. Ni mzuri kushika kwamba mtu anaanguka dhambini mtu wa kwanza alikosea ni Mungu mwenyewe na hii uhusiano wake na Mungu imeharibika, lazima hii kwanza itengenezwe halafu atengenezwe uhusiano wake na ndugu au dada yake. Lakini baada ya hii jambo limeisha. Hakuna mwengine kujua, hakuna kurudi tena na kusema kitu kiingine, imeisha. Lakini ikiwa huyu mtu alikukosa anakata kusikia na hawezi kubali ako dhambini Yesu anaendelea kwa vs. 16 kusema La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Sasa hasikii, hii kosa haiwezi kutatuliwa wewe na yeye unaleta ndugu zaidi. Hapa inasema moja ama wawili wengine. Kitu kiingine tunaanza kuona ni kufanya nidhamu ya kanisa ni kazi, inachukua wakaati wako na wengine lakini unafanya hii yote kwa sababu unapenda ndugu au dada yako na unataka hawa kutubu na kurudi kutembea pamoja na Bwana. Sasa kwa nini Yesu anasema kupeleka moja ama wawili? Ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Sasa hii shida au dhambi huyu ameingia ilikuwa wewe na yeye na bila shaka ikiwa amekataa kusikia wewe peke yako anakataa amekukosa au ako dhambini. Sasa huyu moja ama wawili wengine watakuwa mashahidi kwa kila kitu ambacho ninyi unasema. Wakati wanasikia hata hawa wataomba huyu kutubu kwa dhambi yake. Wataona pia si wewe unasema kitu ambacho ni uongo kuhusu mwengine. Hata Musa aliandika hii kwa sheria ya agano la kale kwa kumbu kumbu la torati 19:15 Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote, katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu. Halafu ninapenda sana ukiendelea kusoma hizi mistari, ningependa sana ikiwa bado tulifanya hii hata society yetu ingekuwa tofauti sana na hakuna mtu atasema uongo kuhusu mwengine, fikiria hizi mistari vs.16-20 Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu ye yote na kushuhudia juu yake ya upotoe; ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za Bwana, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. Hii ni mzuri sana ikiwa imepatikana kwamba mtu amesema uongo kuhusu mwengine itafanyika kwake, kwa huyu mkora kama yeye alitaka kufanya kwa huyu ambaye ni bila hatia. Fukuzu yeye, toka hapa, sasa ni wewe kutoka hapa, ni wewe kufukuzwa ikiwa unasema uongo. Kwa nini? Vs.20 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. Tafadhali usikuwe shahidi wa uongo, ni mabaya sana hata hapa inasema huyu ni uovu.
Turudi kwa Mathayo 18. Sasa watu waili watatu wamenda wameongea na huyu ambaye ako dhambini bila shaka ataona kosa lake, ama? Hii ni tumaini letu, lakini dhambi ni mzito na watu wanajipenda sana na chuki iko na nguvu. Labda amekataa hata hawa, tufanyaje? Yesu anaendelea kusema kwa vs. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; Umefuata kila kitu Yesu alisema kufanya na bado huyu anakataa unapeleka kwa kanisa. Hii ni mwili wa Yesu ambaye wewe unashiriki. Kama hapa utaleta kwa AIC Sekenani. Kwanza ni mzuri kuongea na viongozi wa kanisa na wataongoza njia ya kuleta kwa wote kanisani. Mimi nitasimama hapa na kusema kila kitu halafu kuuliza wewe na mashidi wako kuhakikisha ikiwa ni ukweli. Kwa nini tunafanya hii wazi kwa kila mtu ya kanisa? Kwa sababu yesu alisema kufanya hii na pia Waraka wa kwanza watimotheo 5:20 Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Halafu itakuwa kazi ya kila mshariki wa kanisa hili kuenda na kuongea na huyu mtu, moja kwa moja ama wawili kwa wawili kama umepanga. Kuketi na kuomba sana warudi na watengeneze uhusiano wao na Mungu na huyu mtu ambaye alikosa. Kazi ya watu wa kanisa si ku kuwa mwamuzi lakini kuwaambia hawa wako dhambini na kutubu. Baada ya mwezi moja mbili na kila mtu amepata nafasi kuongea na huyu mtu, na kumbuka huyu mtu ni ndugu ama dada yako, anasema yeye ni mkristo. Baada ya hii muda inaweza kuwa fupi ama mrefu inategemea dhambi yake. Ikiwa amesika halafu tumepata nduguyo. Lakini inawezikana mtu anakataa kila mtu kuongea na kuomba yeye kutubu na kuonyesha yeye kosa lake? Ndiyo, watu wangu dhambi ni giza na wakati unaingia ni ngumu kuona njia ya kutoka.
Ikiwa anakataa hata kanisa vs. 17 na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Maana ya hii ni huyu hata kuwa ndugu ama dada yako, atakuwa kama Mataifa na mtoza ushuru, maana ya hi nini? Atakuwa kama msioamini kwako na kwa kanisa. Kwa wakati wa Yesu mataifa na mtoza ushuru hawatashiriki pamoja kusema ukweli hatakuongea hawawezi. Ni lazima mtu ambaye ako dhambini haiwezi kufanya pamoja na wakristo, hawezi kufanya meza ya Bwana haiwezi kuwa sehemu ya vitu hivi vyote ya kanisa letu, na wakati ametolewa tumaini bado ni kwamba atataka kurudi siku moja na Mungu atatumia hii kuwekwa nje ya kila kitu kupinga moyo wake. Hata badaye ikiwa unaona ndugu au dada yako kwa center au mahali ingine bdao tunajaribu kuwaambia hawa kutubu na kurudi kwa Ushiriki wetu. Lakini ni mzuri kukumbuka lengo ya hii yote si kutoa mtu hatupendi kwa kanisa letu lakini ni kumrejesha mtu huyo.
Mchakato huu si rahisi, inaweza kuchukua siku moja ama mbili au hata miaka, na inataka maombi mingi sana, na watu ambao wanapenda usafi wa kanisa la yesu. Inaleta maumivu ya moyo, inaleta marafiki au famili ya huyu mtu ambaye ako dhambini kukasirika hata labda hawa watatoka kanisa pia, ni uchungu sana na mara mingi ni uchungu zaidi kwa viongozi wa kanisa, lakini ni lazima. Sasa natumaini sana umeona nidhamu ya kanisa ya ukweli ya Bibilia na kama Yesu anasema kufanya. Si kama watu wanafanya hapa. Na pia ikiwa ndugu ama dada yako amekukosa uko na njia ya kurekebisha. Kwa mwisho ya hii yote uko na mistari mbili hapa na watu wanatumia hizi mbaya sana, hata labda ni picha kwa ukuta wako au imeshonywa kwa pillow nyumbani na watu wanatoa hii mstari kwa muktadha yake ni vs.19-20 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. Muktadha hapa ni muhimu sana, Yesu anaongea kuhusu nidhamu ya kanisa si kitu kiingine. Ikiwa wewe unweka mtu chini ya nidhamu ya kanisa na wawili u watatu wamekusanyika kwa jina la Yesu ako pamoja na hawa.
Leo asabuhi ikiwa uko dhambini na unataka kutubu au ikiwa hujui Yesu Kristo na unataka kuweka imani yako katika yeye. Ikiwa wewe uko na shida na ndugu ama dada yako na umemkosa hawa tuko na mistari mingine na ni mzuri tunajua ni Mathayo 5:23-24 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Yesu anasema hata ikiwa unakuja kanisa kuleta sifa zako kwake na uko na shida na ndugiu ama dada yako, waacha hii sifa hapo na enda kutengeneza hii shida yenu kwanza halafu rudi kutoa sifa kwake. Yesu hataki sifa ya mtu ambaye ako na chafu kwa moyo wake.
Ikiwa unataka kuongea zaidi au uko na maswali yo yote tafadhali kuja mbele baada ya ibada yetu na ongea na sisi.
Asanteni sana, Bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more