Restoration of a brother in Sin Pt.2

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript

Galatians 6:2

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika mlango wa 6:2. Wiki iliopita tuliangalia Paulo kuwaambia hawa wakristo wagalatia kwa vs.1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Tuliona ni kazi yetu ya sisi wakristo kusaidia ndugu na dada zetu wakati wanaanguka dhambini, lakini lazima kabla ya sisi tunafanya hii, toho yetu ikuwe safi. Kwa sababu sisi tukiingia kusaidia mwenzetu na moyo yetu iko na chafu ahata sisi tunaweza kuanguka dhambini.
jambi hili ya kurejesha ndugu au dada ambaye ameanguka dhambini ni muhimu sana na ni lazima tunajua kufanya naam na gani. Sisi tunaishi kwa dunia ambaye imejaa na chafu na dhambi, kumbuka tuko vitani, kila siku ya maisha yetu. Roho yetu na mwili wetu wanapigana na mara mingi Mkristo, mwili na tamaa zake wanamshinda na anaanguka. Ni mzuri kujiangalia sana na kusiaida bila majivuno kwa sababu hata sisi ni binadamu na kesho inaweza kuwa sisi ambaye tumeanguka. Lengo yetu ya Mkristo ni kumpendeza Bwana wetu Yesu Kristo na kila kitu. Kila kitu cha maisha haya. Waraka wa kwanza wapetro 1:15-16 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Tunaweza kusihi kama hii hata kusema ukweli ni lazima tunajaribu kila siku ya maisha haya kuishi kama hii mstari inasema. Nataka ninyi kusikia Waefeso 5:3-4 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Utaona kama vs.3 ya sema kama iwastahilivyo watakatifu. Ni njia ambaye Wakristo wanastahili kuishi, lazima ndani ya maisha yako uako na utakatifu, bila hii hujui Yesu Kristo. Mara kwa mara tunapoteza njia yetu na tuanaanguka lakini Mungu kwa neno lake amtupea njia kwa wenzetu kuturejesha. Tunaweza kusema asante sana Mungu.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake Kitabu cha Wagalatia 6:1-5 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombee:
Baada ya kusema kurjesha ndugu au dada yako tunaona Paulo kusema Mchukuliane mizigo na kutimiza hivyo sheria ya Kristo. Nataka ninyi kujua Paulo anawaambia Wakristo wagalatia vitu ambavyo tunaita maisha ya kikirsito ya kila siku. Anainyesha hawa na sisi tabisa ya wakristo. Tuko na hii usemi kwa kiingereza inasema ikiwa anatembea kama bata na kuzungumza kama bata lazima inakuwa bata. Kwetu wakristo ikiwa tunasema sisi ni wakristo na tunatumia maneno ya wakristo ni lazima tunatenda kama wakristo. Wakaati sisi tumerejesha ndugu au dada yetu na anasimama tnea baada ya kuanguka lazima tunaendela na yeye. Haitoshi kumwmambia mtu kuhusu dhambi zake. Kusema ukweli mara mingi wakti mtu ameanguka na ameanza kufuata njia ya kweli tena ni wakati Shetani anazidi kumshambulia huyu mtu.
Wakati tunaona neno hili mchukuliane maana yake ni kubeba mzigo. Ni kuvumilia na mtu, uko pamoja na anajua wakati ako na shida anaweza kukuita. Wakati ninafikiria hii ninafikiria Musa na Haruni na Huri. Waamaleki wakapigana na Waisraeli na Musa alimwambia Yoshua kuchagulia watu kuenda na kupigana na Waamaleki. Na Musa alimwambia Yoshua atasimama juu ya mlima na atakuwa na fimbo ya Mungu mikononi Mwake. Na tunaweza kuona hii kwa kitabu cha Kutoka 17:10-13 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. Ni ajabu sana, wakati Musa atanunua mkono yake Israeli wanashinda lakini mkono ya Musa ilikuwa mzito. Bila shaka ukiweka mkono yako juu kwa muda inachoka, sivyo? Na wakati mkono yake inaenda chini Amaleki walishinda. Tunaona ndugu ya Musa na rafiki yake waliingia kusaidia na Haruni na Huri walishika mikono ya Musa kusaidia yeye kubeba uzito wao na tunasoma Yoshua na Israeli walishinda kwa sababu ya hii.
Ni mmfano mzuri kwetu kushika mikono ya ndugu au dada yetu na kusaidia hawa kubeba uzito wao. Wakati tunafanya hii tunaweza kusaidia hawa kushinda. Kwa kitabu cha Galatia wakati tunasoma hii neno mzigo, Ni vitu vile ambao ni mzito na nguumu kubeba. Hapa ni kama Paulo anasema hii mzigo ni ile jaribu kurudi kwa ile dhambi waliingia na wametoka. Lakini bado majaribio yako kurudi na kutenda tena, Sisi sote ambao ni wakristo tunajua bila shaka wakati tuko na dhambi maishani yetu na tunatubu na tunatoka, majaribio ni kila mahali na ni kama mitego mingi imewekwa kwetu kuanguka tena. Tunaanza kusema, hii dhambi simbaya sana, ni maisha yangu haileti shida kwa mwengine, nijaribu kidogo tu sitaingia sana. Hivi ndivyo vishawishi vinayotuharibia. Bila ndugu au dada kutembea na sisi na kusema, hapana, huwezi, hii ni mbaya, weka macho yako kwa Yesu, tusome bibilia pamoja, bila huyu maishani yako kusaidia wewe kubeba hii mzigo utaanguka tena. Unajua labda tumepata uhuru kutoka dhambi fulani lakini hatujapata uhuru kutoka majaribu yake. Mimi ninajua watu ambao walikuwa walevi kitambo na hawajakuwanya miaka thelathini. Wameokoka wanapenda Yesu ana wanamfuata lakini wanasema mara kwa mara wanatamani kuonja pombe tena. Hii mzigo ya dhambi zetu ya zamani iko ndani ya sisi sote. Bila ndugu na dada zetu itakuwa ngumu sana. Unajua tunaambiwa na Petro vitu vizuri sana kwetu kujua na kuchunga na pia kutia mioyo yetu. Angalia Waraka wa kwanza wa petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Tunajua hii inafanyika. Tunajua tukianguka dhambini shetani anafurahi sana. Lakini angalia vs.9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Tunajua kila mahali ndugu zetu wanashinda na wanasimama imara kila mahali na kujua hii inasaidia sisi pia, si kama tuko peke yetu. Na wakati ndugu au dada yetu ameanguka enda, ongea na yeye, inua yeye na kitu cha umuhimu sana kumwombea na kuomba naye. Hakuna kitu kama maombi katika vita hivi.
Pia nataka ninyi kusikia ikiwa umeanguka dhambini ni wajibu wako kuruhusu ndugu na dada yako kukusaidia. Kitabu ya Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Mungu anatumia sisi kusaidia wenzetu. Tuko na mfano mzuri kwa agano jipya ya hii. Mtume Paulo mwenyewe alisema alikuwa chini sana. Angalia Waraka wa pili wakorintho 7:5-7 Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito. Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi. Ni muhimu sana kwetu kufika na kubeba mizigo ya wakristo wengine, na si sisi peke yetu lakini kanisa letu pia. Ni mzuri kukumbuka sisi wakristo ni kanisa la Yesu, si hii nyumba ya mawe. Sisi ni mwili moja na wakati jicho au mkono iko na shida sisi sote tunasikia hii uchungu pamoja na tunataka hii sehemu ya mwili iponywe.
Wakati wakristo wanabeba mizigo ya mwengine Paulo kwa mstari yetu katika Wagalatia 6:2 anasema tunatimiza hivyo sheria ya Kristo. Sheria ya Kristo ni nini? Angalia Kitabu cha Yohana 13:34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hii ni sheria ya Kristo. Upendo, Upendo kwa wengine. Sisi wakristo tuko chini ya sheria tofauti ya hii dunia. Hii dunia na sheria yake ni kujiangalia kwanza, kila kitu ni kuhusu mimi. lakini wakati unaingia ufalme wa Yesu unaingia chini ya sheria tofauti. Kila nchi iko na sheria tofauti hata kwa Yesu na mfalme wake. Kama kawaida unajua wananchi na tabia yao kulingana na nchi wametoka. Yesu anaendelea kusema kwa Yohana 13:35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Tutajua naam na gani mtu ni mwanafunzi wa Yesu? Wakati unapendana. Usisema wewe ni Mkristo na uko na chuki kwa ndugu au dada yako. Usisema wewe ni Mkristo na unachafua jina la ndugu au dada yako. Hii si kupendana. Wewe umejitoa chini ya sheria ya Kristo.
Hata Paulo kwa kitabu cha Wagalatia tuliona alituambia sheria ya Kristo inaonekana naam na gani. Hata alisema sisi tuko na uhuru kwa ufalme wa Yesu, sisi ni raia ambao tuko na uhuru. Angalia Wagalatia 5:13 ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Hii inaonekana naam na nagani? Vs.14 torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Wakati Yesu anadika sheria yake kwa moyo wa mtu utaona hii maishani yake. Utapenda jirani yako kama nafsi yako. Wakati unapenda naam na hiyo utabeba mizigo ya mwenzako. Utajua ako chini utajua ameanguka na ameanza kusimama tena, utashika mkono yake, ataweka mkono yake juu yako na utasaidia yeye kubeba mzito ya hii mizigo.
Wagalatia 6:2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Ni kitu ambacho hii dunia haiwezi shika, haiwezi kufahamu. Hakuna maneno hii dunia iko nai kueleza mwengine sababu wakristo wanafanya hii. Kumbuka vs.1 Paulo alisema hii ninyi mlio wa Roho. Kumbuka hii dunia hajui roho. Labda watu watasema wewe ni mjinga, waachana na huyu, waacha apate matokeo ya dhambi zake na ni kweli baada ya muda ikiwa huyu anakataa atapata matokeo ya dhambi zake lakini sisi wakristo tunapenda wakristo wengine zaidi na sisi hatutaki kuona hawa wanapata hii matokeo tunataka kutoa hawa kwa hii shiada na kurejesha hawa haraka.
Mfalme wa mifalme, Bwana wa mabwana ni kiongozi wetu na yeye alisema fuata sheria yangu na saidia watoto wake wengine. Si rahisi, na ni lazima tunajichunga kwa sababu ya mwili wetu na tamaa zake lakini ni lazima. Wiki ijayo Mungu akipenda tutaangalia sababu wakritso wengi hawafanyi hii, na ni mzuri sisi sote tujichunge kwa sababu hatutaki kuwa kama Paulo anaendelea kusema. Karibui sana wiki ijayo kusikia neno la Mungu. Nataka sisi kushika vitu hivi sana kwa sababu ni muhimu.
Asanteni sana, Bwaa wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more