Restoration of a brother in sin Pt.3

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Galatians 6:3-5

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:3-5. Kwa wiki karibu nne tumeangalia hii jambo la kurejesha ndugu au dada ambaye ameanguka dhambini. Ni jambo la muhimu sana kwa sababu wengi wanachafua hii mafundisho ya bibilia na wanafanya kama wanataka au hawafanyi kitu cho chote. Nataka ninyi kujua kama tunafanya hii nidhamu ya kanisa au kurejesha mtu iko na matokeo mingi sana. Kitu cha kwanza inaonyesha ndugu yetu kama tunampenda yeye, hata wakati hataki kusikia kama tunasema, bado anajua tumefika na tunataka kusaidia yeye. Kitu cha pili inafanya ni kuonyesha wengine kanisani kwamba ukitenda dhambi mtu anakuja kwako kusiaida na kukuonya. Hata ikiwa ni viongozi wa kanisa ni lazima ikiwa wakodhambini tunakuja kwao na kuonyesha hawa makosa yao. Paulo alituonyesha kufanya hii kwa waraka wa kwanza watimotheo 5:19 Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Halafu anaendela kutuamboa sababu ya hii kwa vs. 20 Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
Kuanagalia hali ya kanisa la Yesu Kristo kwa dunia nzima ni ngumu kuona siku hizi lakini Yesu anataka watu wake kuwa safi na kuishi maisha ya utakatifu, na bila ndugu na dada zetu kutusaidia kusimama imara tutashindwa. Dunia inafundisha wakati wewe unafika miaka kumi na nane wewe unajitegemea sasa. Hata watu wanasema uwajibikaji si mzuri kwa sababu huyu ni mtu mzima sasa. Hii ni uongo zaidi. Waacha nitoe mifano kwenu na kukuuliza maswali. Kwa simu yako, unawajibika kwa nani? Nani anaweza kuangalia simu yako na kuona historia yake? Messages yake? SI simu tu, computer au tablet? Travis hii ni mbaya hii ni yangu na ni privacy yangu, Kweli kweli unaweza kujua huyu amefundishwa na dunia, na ikiwa hakuna shida watu wanaogopa nini? SIku zetu kusema ukweli simu zetu zinaleta watu kuanguka haraka zaidi ya kila kitu. Tunaweza kuchafua watu kwa status yetu tunaweza pigana na watu kwa messages, tunaweza uangalia pornography bila shida, tunaweza kutumia pesa zetu zote kwa vitu ambavyo watu hawawezi kuona kama Betika. Wewe umeshikwa na dhambi fulani na ni rahisi sana siku hizi kuendeela bila watu kujua kwa sababu ya faragha au privacy yako. Nataka ninyi kusikia maneno ya Yesu Kristo huyu mtu unasema ni Bwana wako na unamfuata. Angalia Mathayo 5:29-30 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Ni kali sana. Siku hizi kama nimesema tunaweza kuangalia vitu ambavyo ni ajabu kwa simu yetu, tamaa zetu zinaweza kujaa kabisa. Lakini Travis hata ikiwa ninaangalia pornography kwa simu yangu sikuumiza mtu mwingine, haina madhara. Nataka ninyi kujua hii uongo ya shetani. Angalia Mathayo 5:27-28 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Si mchezo. Nataka ninyi kujua Paulo alitoa orodha kwa Waraka wa kwanza wakorintho 6:9-10 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, Ngoja hii ni neno letu Yesu alisema hata kuangalia na kutamani mtu ni kufanya hii. wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi Hawataurithi ufalme wa Mungu. Na vitu hivi ni rahisi sana ni mbele yetu kuguza screen tu. Jicho lako likikukosesha, ling’oe na tupa mbali. Hata kwangu, computer, simu kila kitu mimi ninaweza kuangalia internet ziko na usalama au safety kwangu juu yao. Kila kitu mimi ninaagalia ni reporti inatumwa kwa Laura na rafiki ingine. Wakiona mimi nimeanaglia kitu ambacho si mzuri wanaweza kupigia simu yangu au kuuliza mimi , hii ni nini. Inasaidia mimi kuishi maisha safi, sitaki hata kukaribisha vitu vile vya chafu. Na wewe? Umeweka nini? Umekubali na nani? Travis wote wanafanya vitu hivi ya chafu siku hizi, simbaya sana. Nataka ninyi kusikia na wote watasiamama mbele ya Mungu kutoa majibu, hutaficha siku ile. Wakristo, hii si mchezo na ninajua tumejaza maisha yetu na chafu mingi siku hizi na tunafikiri bado tuko sawa kwa sababu watu hawajui, lakini mungu anajua na siku moja sisi sote tutajua.
Tusome mistari yetu kwa muktadha yao Wagalatia 6:1-5 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.
Tuombee:
Tumeona sisi ambao ni ya Roho turejesha ndugu au dada yetu na tumeona kufanya naam na gani, Tumeona sisi wakristo tunabeba mizigo, hii uzito ya ndugu na dada zetu lakini kwa nini wengi hawataki kufanya hii. Tunaona kwa vs.3 mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Kumbuka vs.1 tumeona sisi ambao ni ya Roho tunarejesha mtu kwa roho ya upole. Shida yetu ya binadamu ni sisi tunajiangalia kama sisi ni kitu, na sisi hatuwezi saidia huyu mtu ambaye ameanghuka ni kama tutapata chafu yake. Sisi tunajiweka juu, tutaimba kanisani, tutafundisha sunday school hata tutahubiri lakini wakati mtu ako ameanguka dhambini hatunatime kwa hii. Na kama Paulo alisema unajidanganya nafsi yako. Watu wengi siku hizi ni kama mafarisayo, hawajali haki ya ukweli ambaye inakuja kwa njia ya unyenyekevu lakini wanajali kujihesabia haki na kusema ukweli hii, huwezi kupata kwa ufalme wa Mungu. Watu kama hii hawawezi kusaida, kurejesha ndugu yao lakini wanamhukumu. Unaweza kusikia vitu kama amejiweka kwa hii shida waacha ajitoe. Hii sii mawazo ya Mkristo. unakumbuka ile orodha ya vitu Mungu anachukia kwa kitabu cha Mithali, unakumbuka kitu cha kwanza? Angalia Mithali 6:16-17 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi. Hii ni nini? Hii ni majivuno. Ni kama sisi tunajiweka kuwa kitu kwa macho yetu na tunaangalia wengine kama wako chini. Ni mzuri kwetu kukumbuka sisi ni wenye dhambi, hakuna mtu moja anaweza kujiokoa na bila neema na rehema ya Mungu maishani yetu tutakuwa kama huyu ambaye ameanguka, labda ni yeye leo lakini labda ni wewe kesho, kuwa na unyenyekevu. Ni rahisi sana kwetu kufikiri sisi ni kitu. Kusema ukweli hii ni sababu tunalalamika na hali yetu, kwa sababu unajiweka juu kwa macho yako unasema mimi ninstahili kuwa hapo kama huyu mwengine, si mahali hapa niko saa hii. Kila mtu anajiweka dhamani yake juu kabisa. Lakini kama Paulo alisema tunajidanganya nafsi yetu. Ikiwa huwezi kukubali wewe mwenyewe uko na dhambi mingi na majaribio mingi, utasidia wengine naam na gani? Kama Yesu alisema ni lazima tutoe ile boriti katika jicho letu kwanza halafu tunaweza kusidia ndugu yetu kutoa kile kibanzi kutoka jicho lake.
Kwa sababu ya hii Paulo anaendelea kwa kitabu cha Galatia 6:4 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Hii ni mzuri sana na kama nimesema mara mingi sana, hakuna mtu anakujua kama wewe. Wewe unajijua zaidi. Wewe unaua mawazo yako, moyo wako, matendo yako wakati uko peke yako. Ni rahisi kusimama kanisani na kuimba kutoa ushuhuru hata kufundisha na kaa kama mtu ambaye anaenda na Roho lakini wakati uko peke yako au kwa biashara yako uko naam na gani? Paulo anasema pima kazi yako. Hakikisha kwamba wewe unaishi maisha ambaye inampendeza Mungu. Kwa macho ya Mungu maisha yako iko safi? Kwa sababu ikiwa si naam na hiyo huwezi kusaidia wengine. Baada ya kufanya hii ikiwa umejipima kweli kweli anasema utakuwana sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu.
Sisi tunajua kujisifu kaiwezi kumpendeza Bwana wetu, sababu Paulo anasema hii ni nini? Kwa sababu ikiwa wewe ni Mkristo wa kweli wakati unajipima utajua hakuna kitu kizuri ndani yako ya wewe mwenyewe na kitu ambacho ni mzuri ndani yetu ni Yesu tu, na kazi yake, hakuna kitu kiingine. Sababu sisi tunweza kujisifu au kufurahi ni kwa sababu ya kazi Yesu amefanya ndani yetu. SI kwa sababu ya mimi na si kwa sababu ya wewe. Kusema ukweli tukiweza tutafuata tamaa zetu za hii mwili saa hii lakini kwa sababu ya Yesu na kazi amefanya mioyo yetu hatupendi dhambi zetu kusema ukweli zaidi na ziadi tunachukia dhambi zetu. Mimi si mwaminifu kwa sababu ya mimi, mimi si mtu ya kutii kwa sababu ya mimi , lakini kwa sababu ya Mungu na kazi yake amefanya ndani yangu. Wakati tunashika ukweli wa hii halafu tunaweza kusaidia ndugu au dada yetu wakati wameanguka dhambini.
Halafu Paulo anasema kwa Wagalatia 6:5 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. Hapa ni kama inapigana na vs.2 wakati Paulo anasema Mchukuliane mizigo. Lakini kama tunaona hata kwa kiswahili ni neno tofuati hapa. Paulo anasema kila mtu atabeba furushi lae mwenyewe. Paulo hapa anaongea kuhusu njia ambaye tumeishi maisha yetu. Siku moja sisi sote tutasimama mbele ya mwenyezi Mungu. Wakati tunafikiria siku ile ingesiaida sisi kuishi maihsa mtakatifu hapa kwa hii dunia. Wakati tunafanya hii tutakuwa na uwezi kusaidia wenzetu. Shida ni watu wingi wanaishi maisha yao bila kufikiria kesho, kesho kutwa au kwa milele ambao iko mbele ya sisi sote. Watu wanaishi maiosha ya kwa leo peke yake. Hawajui kama wanaishi iko na matokeo. Nitoe mifano kwetu. Mtu amekkunywa pombe mpaka amelewa kabisa na ameingia gari na aliaanza kuendesha lakini amelewa, mawazo yako ni fujo na anaginga mtoto kwa bara bara. Wakati alianza kunywa alifurahi sana, hajafikiria matokeo ya hii na sasa amejipata kwa gereza kesho. Mwanamume analala na mwanamke ambaye si bibi yake na baada ya wiki tano sita mwanamke anapata ako na mimba. Siku ile walijifurahisha lakini hawajafikiria baada ya wiki tano sita itakuwaaje. Na pia labda mwanamume alikuwa na HIV na hujajua kwa mwaka mzima. Sisi tunaishi kwa saa hii na ni hatari sana. ni mifano mingi lakini nafikiri umeshika kama ninasema.
Paulo hapa anasema siku moja sisi sotes tutasimama kutoa majibu kwa maisha yetu. Na siku ile haitakuwa kama saa hii wakati tunaweza kusaidiana na kubeba mizigo ya ndugu au dada, ni sisi peke yetu, bila wazazi wetu, bila walimu wetu, bila rafiki zetu bila pastor yetu, ni sisi na Mungu na kila mtu ambaye wameishi watakuwa kusikia. Kitabu cha Mhubiri 12:14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. Hii siki inakujakwetu sote. Lazima tuangalia mbele na kufikiria siku ile ili tusihi maisha ya leo tofauti. Ni Sulemani aliandika kitabu hiki cha Mhubiri, Mungu alimprea maarifa zaidi ya kila mtu ambaye aliishi na alifanya mema na pia mwisho yake alifanya mabaya. Hadi leo hakuna mtu mwengine amukuwa tajiri kama Sulemani. Tunajua alikuwa na mashamba, manyumba mingi sana, Wake wingi zaidi, hata wamaasai hawawezi kuwa na wake kama Sulemani, unakumbuka alikuwa wake mia saba na masuria mia tatu, amejua upendo wa wanawake, alikuwa na kila kitu moyo ya mtu anaweza kutaka na angalia ushauri wake kwa mwisho ya maisha yake vs.13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kusema ukweli hakuna kitu kiingine iko na maana kuliko hii. Ikiwa wewe ni maskini na huna kitu cho chote au wewe ni tajiri na uko na kila kitu, hii ni jumla ya maisha. Kwa sababu ya siku ile ambaye inakuja na hii maneno yote ingine ni taka taka lakini kama umeishi maisha yako katika Yesu Kristo ni kila kitu. Angalia Warumi 2:5-8 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; Luka anasema kila kitu umesema kwa siri ndani ya nyumba yako itatangazwa juu ya paa. Kila fikirio umekuwa nai itakuwa wazi kwa kila mtu kuona.
Halafu tunafika kitabu cha ufunuo na tunaona hii yote inafanyika kama tumesoma kwa agano la kale na agano jipya Ufunuo 20:11-15 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Ikiwa unaishi kwa leo peke yake na unafikiri matendo yako hayana maana, wewe uko na shida kubwa sana. Mimi ninaomba sana wakristo, ishi maisha ya utakatifu, kumpendeza Mungu, Mcha yeye na fuata kama amesema kwa neno lake. Siku moja hii vitu vyote unaishi maisha yako kupata, haitakuwa na maana yo yote.
Ni kweli siku moja sisi tuatsimama mbele ya Mungu kutoa majibu lakini kwetu ambao Yesu Kristo ametuokoa na tumemfuata yeye kwa maisha haya, atakuwa hapo nasi. Hukumuni Mungu ataona haki ya mwana wake kufunika sisi. Lakini bila Yesu hunatumaini.
Leo asabuhi ikiwa wewe hunatumaini kwa maisha haya au maisha ambao inakuja nitaomba sana, tubu kwa dhambi zako, fuata Yesu, amini yeye na weka imani yako katika yeye. Ukitaka kufanya hii, karibu mbele kuongea na sisi baada ya ibada yetu, tunaweza kueleza zaidi kwako.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe, na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more