Sowing and Reaping Pt.1
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
Galatians 6:7
Galatians 6:7
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:7. Wiki iliopita tumeona Paulo kusema vs.6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. Tumeangalia sana maana ya hii na tulisema ya kwanza ni watu ambao wanaingia kusaidia mtu ambaye ameanguka dhambini halafu tuliangalia kama ni mzuri pastor analipwa mshahara na tumeangalia mistari mingi na tumesema pastor ambaye ni pastor ya ukweli na anafanya kazi ya ukweli ya kuhubiri na kufundisha, ndiyo ni mzuri alipwe mshahara.
Leo Paulo anaendelea kuwaambia wakristo wagalatia kitu cha umuhimu sana na hata ni mzuri sisi tunashika maneno ya Paulo. Kwa sababu anasema kila kitu tunatenda iko na matokeo yake.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake Wagalatia 6:7-10 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Tuombee:
Kitu cha kwanza tunaona kwa mstari yetu leo ni Msidanganyike. Siku zetu kwa vitu vya Mungu ni kama wamedanganywa sana na hata hawajali. Hata ukiangalia ukora amabye inafanyika kwa jina la Mungu unashangaa. Ni kama siku hizi kudanganywa ni lazima. Pastor na kanisa si kama zamani. Ukienda uko unajua uatapata tumaini utapata maneno ya uhai, unajua uko na uponyaji ya Roho yako. Siku hizi watu wanauza Yesu na injili yake, kanisa limekuwa biashara, tumaini linatoka uko ni fake na mananeo unapata ni ya mwalimu wa uongo. Watu wanataka uponyaji wa mwili si ya Roho. Watu wamedanganywa sana. Msidanganyike, Tunaona hii mara tano tu kwa bibilia nzima. Nataka sisi kuangalia mahali inatumiwa kwa sababu si mchezo. Mara ya kwanza tunaona ni Kumbu Kumbu la Torati 11:16 Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; Tunaona hapa ni mioyo ya watu yanaweza kudanganywa na ni kweli mara mingi sisi tunafuata vitu viingine na tunasahau Mungu, tunaabudu miungi miingine, miungu ya pesa, kazi, familia, shule, wanakuwa sanamu maishani yetu. Tunaona matokeo ya mioyo yetu kudanganywa kwa vs.17 hasira za Bwana zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana. Na hii ilifanyika. Watu wa Isareli walifuata miungu miingine na Mungu alifanya kama alisema.
Mahali ingine tunaona Yesu anaongea na wanafunzi wake kuhusu siku za mwisho ni Luka 21:8 Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao. Tunaona hapa Yesu anasema Mkadanganyika kwa imani yako. Tunaona kwa hii mstari ni kama siku zetu, tunaona watu wengi wanakuja kwa jina la Yesu lakini hawa ni uongo. Wanafundisha injili ingine, wanaongea kuhusu Yesu lakini si Yesu ya Bibilia. Anagalia Mathayo 24:23-25 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Hii ya mwisho Yesu anasema nimekwisha kuwaonya mbele. Ametuambia mapema ili hatuwezi kudanganywa na hii uongo na kwa imani yeti tutafuata Yesu wa uongo. Vs.26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Halafu anatuambia kama atarudi vs.27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Na sisi tunajua hii na bado watu watafuata wale wa uongo na Kristo wa uongo. Na matokeo ya hii nii hukumu na jehanamu. Wakati tunasikia Msidanganyike si mchezo.
Mahali Ingine ni Waraka wa kwanza wakorintho 6:9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Paulo anasema Msidanganyike kama unaishi. Kama unaishi iko na matokeo ya milele. Usifikiri wewe ni Mkristo na unafanya vitu hivi, ikiwa wewe unafikiri uko sawa na Yesu na vitu hivi ya hii orodha viko maishani yako umedanganywa. Matokeo ya kutenda vitu hivi ni huwezi kuingia mbinguni. Vs.11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu. Ikiwa unafanya vitu hivi msidanganyike hujaoshwa, hujatakaswa, hujahesaibiwa haki na hujui Yesu Kristo.
Mahali ingine ni Waraka wa kwanza wakoritnho 15:33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tena hii ni ukweli kabisa. Usifikiri unaweza kukaa na marafiki wako wabaya na kufikiri uko sawa. Ni kama kusema giza na nuru zinaweza kukaa mahali moja. Na umejidanganya kufikiri tabia yako itabaki kuwa mzuri wakati unaenda na watu wabaya. Hapa kwa kiswahili inasema Mazumgumzo lakini kutafsiri vizuri inasema watu amabo uko pamoja na hawa, ikiwa hawa ni wabaya, tabiia yako itaharibika pia. Sisi sote tumeona hii. Tuko na kijana au msichana mzuri sana na anaenda secondary na tabia yake wakati anarudi nyumbani ni tofauti sana. Kwa nini? Kwa sababu ya watu amabo amepata uko.
Hapa kwa mstari yetu kwa Wagalatia 6:7 Ni kama Paulo anaonya hawa ambao wamejidanganya. Unakumbuka Yeremiah alituambia kwa kitabu cha Yeremiah 17:9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Paulo anasema kwa sababu umeokoka usifikiri unaweza kutenda dhambi kama kawaida. Wewe umedanganywa kufikiri Mungu hawezi kudeal na watoto wake wakati wanaanguka dhambini. Na dhambi hawa waliingia ilikuwa uhalali, Legalism. Walifikiri wanaweza kuweka matendo yao juu ya neema ya Mungu.
halafu tunafika kwa mstari yetu ya leo ni hii ni mahali ya mwisho bibilia inatumia hii. Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; Sasa wakati ninasoma hii ninashangaa kabisa kwa sababu nani atakuwa mjinga ya kutosha kufikiri Mungu angedhihakiwa? Ikiwa ni kitu moja hutaki kufanya ni kumdhihaki Mungu. Tuko na agano la kale imejaa na watu wamejaribu kufanya hii na maisha yao iliisha mbaya sana. Ni mtu gani atamdhihaki Mungu? Zaburi 14:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Mpumbavu, mtu mjinga sana anamdhihaki Mungu. Hana akili, ni mtu amabye anaishi kama anataka anafikiri hakuna matokeo ya matendo. Wasiaomini Mungu au Atheists, ni watu ambao wanasema hakuna Mungu Hawa wanamdhihaki Mungu. Watu ambao wanasema mageuzi au evolution ni ukweli. Kama hii dunia na kila kitu ndani yake ilifanyika tu, na siku moja nyani ilitoka dimbwi la matope na baada ya miaka millioni mingi sisi tulitoka nyani, watu amabao wanasema hii ni watu ambao wanamdhihaki Mungu. Daktari ambaye anaua watoto tumboni la mama ni mtu ambaye anamdhihaki Mungu.
Nataka ninyi kusikia hadidhi chace ya watu ambao wamemdhihaki Mungu katika miaka mia moja iliyopita. Mtu anaitwa John Lenon alikuwa mwimbaji maarufu sana na bendi inayoitwa Beatles. Musiki yao imeuza zaidi ya yote kwa dunia nzima. Huyu John Lenon alisema Ukristo utaisha, alisema sihitaji kubishana kuhusu hilo nina uhakika. Hii ilikuwa mwaka 1966. Alisema Yesu alikuwa sawa lakini wanafunzi wake walikuwa rahisi na leo sisi ni maarufu kuliko Yesu. Baada ya kusema hii alipigwa rasasi mara sita na alikufa.
Mtu mwengine anaitwa Tancredo Neves alitaka kua Rais ya Brazil na wakati anazunguka kucampaign alisema akipata kura elfu mia tano kutoka chama chake hata Mungu mwenyewe hawezi kumtoa kutoka kwa uaria wake. Alipata kura yote lakini siku moja kabla ya kuweka kwa kiti cha rais alikuwa mgonjwa na alikufa.
Ni mtu aliyetengeneza meli kubwa kuliko zote, labda umesikia inaitwa Titanic. Ilikuwa meter 265 kwa urefu na meter 28 kwa upana na ilisimama meter 53 juu ya maji. ni kubwa zaidi. Wakati walimaliza kujenga mwtandishi wa habari alimwuliza meli iko salama kiasi gani? Huyu ambaye alijenga alisema haa Mungu mwenyewe hawezi kuizamisha. Ikiwa unajua hii story unajua The Titanic kwa safari ya kwanza baada ya siku nne iligonga mlima wa barafu kati kati ya bahari na watu elfu moja mia nne tisini na sita walikufa na mpaka leo the titanic inalala chini ya bahari.
Hawa watu walimdhihaki Mungu na story ni mingi sana zaidi, ni kitu mbachi huwezi kufanya na kufikiri uko sawa. Unajua nani wengine wanamdhihaki Mungu? Ni watu ambao hawajaweka imani yako katika Yesu kristo kwa wokovu wao. Wanatembea kama hii yote si ukweli na hakuna milele inakuja. Mtu ambaye amekataa Yesu kristo na wokovu wake ni mtu ambaye anamdhihaki Mungu. Na kama hizi story ziingine mwisho yao ni mbaya sana. Ni mzuri sisi sote tunakumbuka Warumi 14:11 imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu. SIku moja hii ni kila mtu. Labda unafikiri sio kweli ama ni mbali si saa hii. Hata ikiwa wewe ni Mwaislamu, dhehebu la Buddha, Kihindu au Msioamini, siku moja kila goti litapigwa mbele za Mungu. Na ulimi utamkiri Mungu, Hii ulimi utasema nini? Angalia Wafilipi 2:10-11 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Hii itafanyika na niakuambia saa hii Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; angalia ni nani ameweka Yesu kuwa naam na hiyo vs.9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; Ni Mungu amweka Yesu kuwa na jina lile lipitalo kila jina. Chunga sana! Matokeo ya kama unafikiri na kama unaishi maisha yako kuamini au kutoamini iko na matokeo.
Baada ya hii Paulo anasema kwa Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Hii ni ukweli kabisa. Ikiwa tunapnada mti ya machungwa tutapata nini? Machungwa. Tukipanda mahindi tutapata nini? Mahindi. Katika Bibilia mzima tunaweza kuona mifano mingi ya hii na kutuambia kama unapanda unavuna. Hata kitabu cha Ayubu 4:8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo. Kwetu ambao ni wakristo na tuko na haki maishani yetu tunapanda kwa hii na tunavuna badaye. Angalia Mithali 1:31-33 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.
Hata kwa watoto wetu tunaweza kuona hii. Mtoto ambaye amefanya kama anataka na amepata kila kitu anataka. na hakuna nidhamu maishani yake atakuwa mtu mzima kama hii pia. Unajua vitu ambavyo unatenda kwa miaka kumi na tani hadi miaka ishirini ni kama utafanya maisha yako yote. Tabia ya maisha unapata kwa miaka hiyo inakaa na watu. Misingi unaweka mishani yako ikiwa ni mzuri ama mbaya ni kama inabaki nawe maisha yako yote. Hii ni sababu hatutashangaa wakati tunajua Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Na tunaona huyu mtoto anakuwa mtu mzima na anafuata Yesu na maisha yake. Wazazi wake wamepanda hizi mbegu ndani yake. Ikiwa wewe ni mlevi, na hujali bibi yako au watoto wako na hujui kutumia pesa na kupanga masiha yako, utafikiri watoto wako watakuwa toafuti? Wewe unapanda hii ndani ya hawa, na utavuna badaye.
Tuko na mistari mzuri sana zinatuambia wazi kuhusu hii. Kwa warumi mlango wa pili tunaona Mungu ni mwamuzi mwadilifu na Warumi 2:6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; Kila tendo tunafanya tunapanda kitu. Anendelea kwa vs.7 wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, Hii ni matendo yao wametumia maisha yao kupanda vitu hivi na ansema kwa hawa watavuna watapewa uzima wa milele; Hii ni watu ambao wamepanda kwa roho na wamefuata Mungu lakini tunaona vs.8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, Hawa wamepanda wapi? Kwa hii dunia na tamaa za mwili wao, na watavuna nini? hasira na ghadhabu; Vs.9 dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; Tena mtu ambaye amepanda kwa mwili wake anavuna hii. Na vs.10 bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; Ni mtu ambaye amepanda kwa Roho na anafuata Mungu. Kumbuka hii ni Mungu ambaye ni Mwamuzi mwadilifu na kama mstari yetu ya Wagalatia ilisema Mungu hadhihakiwi. Itafanyika na inakuja kwetu sote.
Najua tumesoma hii mara mingi lakini nataka kufunga na hii leo asabuhi. Ikiwa unafikiri matendo yetu na vitu ambavyo tunatenda kwa maisha haya hayana maana ni mzuri kusika Kitabu cha ufunuo 20:11-15 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Maihsa haya iko na maana mingi na kama tunaishi na kama tunatenda iko na matokeo na tutavuna kama tumepanda. Swali langu kwako leo asabuhi ni wewe unapanda nini? Maisha yako saa hii ikoaje? na Bibi yako, bwana wako, watoto wako, wazazi wako, boy friend, girl friend yako, kanisa lako, kazi yako, mafikirio yako, macho yako, maneno yako?
Nitaomba tafadhali, jipima, kwa sababu maisha haya si ya milele, lakini maisha ambaye inakuja ni ya milele na Mungu wetu hasemi uongo na cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Tubu kwa dhambi zako na fuata Yesu, pea yeye kila kitu, panda kwake. Ikiwa unataka kuongea zaidi kuhusu Yesu, wokovu, maisha yako, tafadhali kuja baada ya ibada yetu na ongea na mimi.
Asanteni sana. Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.