Creation Day 4

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Genesis 1:14-19

Karibuni Mara Christian Chapel Service. Natumaini sana hujaenda likizo na umesahau kila kitu umefunzwa kwa chapel service. Unakumbuka tunaongea kuhusu nini? Umbaji! Na tumefika siku gani ya umbaji? Siku ya nne. Tumeshaa ona siku ya kwanza Mungu aliziumba mbingu na nchi, Siku ya pili aliumba nuru. Mungu alitenga nuru na giza. Aliita nuru mchana na giza usiku. Halafu tukiona siku ya pili Mungu aliumba anga, siku ya tatu tulianza kuona uhai kuingia na Mungu aliumba nchi kavu, majani, miti, matunda. Leo ni Mwezi, jua na nyota.
Kabla ya tunaingia tuangalia mistari yetu nataka ninyi kujua, Mungu aliziumba vitu hivi vyote kwa sababu gani? Kwa utukufu wake. Suleamni alisema kwa Mithali 16:4 Bwana ameumba kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kusudi la umbaji ni kuleta utukufu kwake. Kitu cha ajabu sana ni Bwana wetu yesu kristo. Tunasoma kwa kitabu cha Yohana 1:1-3 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Halafu tunasoma kwa kitabu cha wakolosai 1:15-17 Yesu ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Hii yote tumesoma kuhusu umbaji ni ajabu kufikiria Bwana wetu Yesu kristo vyote hushiikana katika yeye. Wakati tunasoma vitu hivi vya umbaji tafadhali kumbuka hii, Yeye ni kila kitu ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.
Tusome Mwanzo 1:14-19 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;  tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.  Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.  Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi  na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.  Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
Tunaona vs.14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; Unakumbuka siku ya kwanza Mungu aliumba nuru na giza na sasa ameumba mianga kutenga mchana na usiku. Tunaona vs.16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana. Sasa tunajua hii ni jua yetu. Jua yetu ni ajabu sana. Kitu cha kwanza ni joto, ni kali sana. Joto yake ni millioni sita hadi muni na tano. Kitu cha pili ni kubwa sana. Radius au kupima panda moja hadi panda ingine ya dunia ni 6,371 KM ukipima jua pana moja hadi oanda ingine ni 695,700 KM! Kumanisha unaweza kuweka dunia millioni moja na mia tatu ndani ya jua. Ni kubwa. Na pia iko Kilometer millioni 149 kutoka sisi hapa kwa dunia. Ikiwa unaingia ndege kubwa itachukua miaka kumi na tisa. Ikiwa unaedesha gari itachukua miaka 177 kufika na ikiwa unatembea itachukua miaka 3536! ni mbali. Na Mungu wetu kwa neno lake ameumbwa jua yetu, na kila kitu Mungu aliziumba ilipangwa vizuri sana. Unakumbuka siku ya tatu Mungu aliumba nini? Majani, mitu, matunda, nyasi. Na vitu hivi vinahitaji nini kuishi? Jua! bila jua hii yote itakufa. Na ameweka dunia yetu mahali pazuri, kamili kusema ukweli kutoka dunia. Ikiwa tulikuwa karibu zaidi kwa jua kila kitu itachomeka, ikiwa tulikuwa mabali kidogo kila kitu kingeganda au itakuwa barafu. Hii ni sababu wakati tunasikia vitu kama Global warming au Climate change ni maneno watu wa dunia wanahjaribu kutumia kusema tuko na shida na sisi tunaweza kuokoa dii dunia yetu, tukifanya hii ama hii ama hii. Lakini Mungu wetu anatawala kila kitu, ni umbaji wake.
Tunaona mianga Mungu ameweka ya kwanza kubwa ni jua na tunaona Mwanzo 1:16 kuendelea kusema na ule mdogo utawale usiku; hii ni gani? Ni mwezi yetu. Mwezi wetu ukipima pande moja hadi ingine ni kilometer 1,734 unaona si kubwa kama jua ni kidogo na pia iko karibu dunia ni kilometer 384,000 kutoka sisi. Hata binadamu wamenda uko mara mingi. Wamesimama juu ya yake. Inachukua karibu siku nne kufika. Ni siku nne ya kuenda speed ya kilometer elfu tisini an hour.
Tunasoma kwa mwanzo 1:14 mwisho inasema nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; Unajua si lazima uko na saa kujua ni saa ngapi. Hata unaweza kujua ukijua mwezi na jua ziko wapi. Hata Majira yetu, kama rainy season na dry season ni kwa sababu ya mianga mbili Mungu aliumba. Hii ni sababu tuko na masiku na miezi na mwaka, yote ni kwa sababu ya jua na mwezi yetu.
Sasa siku moja au masaa ishirini na nne dunia yetu inazuka mara moja na inachukua mara 365 kuzuka jua yetu mara moja. na wakati imezunguka mara moja kwa jua yetu ni mwaka moja. Na ukiangalia juu usiku unaona mwezi, na leo mwezi ni kidogo sana na mara ingine ni nusu na mara ingine imejaa kabisa, tunajua wakati ni kidodgo mwezi inaanza na wakati imejaa ni mwisho ya mwezi. Hii yote haijafanyika tu, kwa lipuko kubwa au kitu kiingine. Mungu aliziumba hizi kwetu kuwa na saa, mwezi na miaka. Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu na ajabu. Kumbuka aliziumba nyota zote pia na anita hawa wote kwa jina lao. Kumbuka hata hatuwezi kuhesabu nyota kwa sababu ni mingi zaidi.
ggggMwanzo 1:17-18 ya sema Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi  na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Hii yote wakati tunaaglia juu ni ajabu sana. Na wakati tunana vitu hivi Zaburi 19:1 ya sema Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mungu wetu ni umbaji wa hii yote na ni rahisi kuona. Ni fungua macho yako na kuangalia, umbaji wake uko kila mahali.
Kama Mungu alitumia jua na mwezi kugawa nuru na giza hata sisi wakristo tumetengwa na ulimwengu. Bwana wetu yesu kristo ni alituokoa kutoka dhambi zetu na alitoa sisi kwa ufalme wa giza na amtuweka sisi kwa ufalme wake ya nuru. Yohana 8:12 Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Kwa sababu ya hii tunasoma kwa kitabu cha Waefeso 5:8 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru.
Mwisho ya Mwanzo 1:18 Mungu akaonavvvv na unaweza kuwaambia watu wengine kuhusu Mungu na Yesu kwa sababu ya vitu hivi. Ni mzuri kukumbuka Mungu wetu ni ajabu sana na sisi ambao tumeweka imani yetu katika Yesu ni watoto wake na anapenda watoto wake sana. Asanteni.
Related Media
See more
Related Sermons
See more