Paul’s Conclusion
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
Galatians 6:11
Galatians 6:11
Leo tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:11. Kwa masomo yetu katika kitabu cha kitabu hiki tumeona mambo mingi sana. Natumaini imekusaidia kama imeniasidia. Kama tunafikiri kuhusu vitu, kama tunaishi maisha yetu na kama tunafanya vitu. Lakini zaidi ya yote natumaini sana umeona mandhari ya kitabu hiki na umuhuimu yake. Unakumbuka mandhari ni kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Unakumbuka shida ilikuwa walimu wa uongo waliingia kanisa la Galatia na waliaanza kufundishia uongo wao. Walisema ni lazima kufanya tohara ikiwa unataka kuokoka. Walifanya nini? Walirudisha wakristo wagalatia chini ya torati ya Musa. Walisema kupata wokovu ni kwa njia ya matendo yetu.
Nataka ninyi kusikia hii haiwezikani. Najua watu wengi hapa wanafundisha ni lazima unafanya hii ama hii ama hii kupata wokovu. Hata wengi wanasema lazima unapea pastor yako pesa, au wanyama, lazima unabeba yeye kwa mgongo wako, lazima unaenda kanisa, lazima unavaa nguo fulani, lazima unapakwa mafuta, lazima pastor yako anakuombea kupata wokovu, lazima unafanya hii sherehe au hii sherehe ya agano la kale au desturi la Wayahudi, Huwezi kula nyama, kunywa soda, kahawa hata chai. Kusema ukweli hakuna tofauti ya siku za Wagalatia, kusema ukweli siku zetu hata ni mbaya zaidi. Na kumbuka kama Paulo alisema Kwa Wagalatia 6:1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Ni kali sana, lakini ni ukweli, anasema ni kama umeruka akili, kama wako chini ya uchawi fulani. Alisema kwa wagalatia 1:6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Paulo ameshangaa walijua ukweli, walifuata ukweli na sasa wanafuata hii uongo kurudisha hawa chini ya sheria. Ukiona maneno yake hapa ni shida hata ya siku yetu ya leo, anasema kugeukia injili ya namna nyingine. Ni injili ya uongo, ni fake, si injili ya Yesu Kristo. Siku zetu tuko na watu ambao wanasema hawa ni balzi wa Yesu, wanasema wanafundisha neno lake lakini hawa ni uongo na wanafundisha injili ingine, wanafundisha Yesu mwengine. Wanafundisha watu wao kufanya vitu ambavyo Yesu hajasema kufanya, ni wakora. Kusema ukweli hawajali Injili ya Yesu, hawajali watu wa Mungu, hawa ni mbwa mwitu na wanakula watu wa Mungu, wanadangnaya hawa kuchukua pesa zao. Lakini lawama zote si panda yao peke yao. Watu wanataka vitu hivi wanauza na wanenda, wanapea hawa pesa zao, kwa sababu wantaka Baraka za afya, na pesa. Niambie kwa nini mtu mzima atakubali kupigwa na patsor kanisani? Kwa nini mtu mzima atakubali pastor fulani anatembea juu ya mgongo wake au ya bibi yake?
Nataka kuuliza kitu kwenu. ikiwa wewe unatembea kwa bara na unaona mtu anaruka na analala na anapiga kelele mingi sana, hata sauti yake ni kama ako na pepo. Utafanya nini? Huwezi karibisha huyu mtu, sivyo? Kusema ukweli utasema huyu mtu ameruka akili. Lakini tuweke huyu mtu kwa nyumba watu wanaita kanisa na tuweke jina la pastor kwake na watu wanakimbia uko kusikia. Natumaini sana umeona hii ni ujinga, uongo na mchezo ya shetani kuchafua neno la Mungu na kudanganya watu. Mimi ninasema Paulo nastaajabu kwa kuwa watu kutoka neema ya Yesu Kristi na uhuru ameleta kwetu na kugeuika injili ya namna nyingine.
Kanisa la Galatia ni mfano mzuri sana kwetu kwa siku zetu. Hawa walifundishwa na Paulo mwenyewe. Pia ni Paulo alianzisha kanisa la Wagalatia. Ni mzuri kujua Kanisa la Wagalatia haijakuwa kanisa moja, Galatia ilikuwa region na ilikuwa na kanisa saba ndani yake. Safari ya kwanza ya umishonari Paulo na Barnaba walitumwa kutoka kanisa la Antiokia na walianza makanisa kwa region ya Galatia. Unapata hii yote kwa kitabu cha Matendo 14. Unaweza kusoma hadithi mingi kuhusu mwanzo ya makanisa yale. Ilikuwa mwamka arobaini na mbili wakati walisafiri na Tunasoma Kwa matendo 14:1 Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wayunani wakaamini. Makanisa yale yamejaa na wyahudi na Wayunani, walikuwa waamini. Pia tunasoma Paulo aliponyesha mtu amabye alikuwa dhaifu wa miguu na baada ya hii walijaribu kusema Paulo Herme na Barnaba ni Zeu ay Zeus. Miungu ya uongo. Mambo mingi sana. Halafu tunaona Matendo 14:22-23 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini. Kumaanisha walianzisha kanisa.
Baada ya miaka sita ama saba ilipita na hawa walimu wa uongo waliingia na walianza kufundisha uongo wa tohara kupata wokovu na Paulo aliandika kitbu cha Wagalatia kwa maknisa yale. Sisi tumeona karibu mwaka mzima ama Paulo aliwaambia na leo tumefika 6:11.
Tusome Wagalatia 6:11 Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!
Tuombe:
Tumeona Paulo alianzisha hizi makanisa. Kwa kiroho watu wale ni watoto wake. Ni uchungu sana kuona kitu ambacho umeanzisha kuenda njia ingine au kufanya tofauti ya kama moango yako ilikuwa. Bila shaka ilikuwa ngumu kwa Paulo kusikia viongozi wa kanisa wamekubali kwa hawa walimu wa uongo kuingia. Hata alikarsirika na wale walimu wa uongo unakumbuka Wagalatia 5:12 Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao! Kusema ukweli wakati moja wetu hapa kwa kanisa hili au mission yetu wanapost kitu cha uongo au wananza kufuata kitu cha uongo hata mimi ninakufa moyo, mara kwa mara hata ninakasirika kwa sababu umefundishwa vizuri hapa, wewe unajua ukweli wa neno la Mungu na bado unafuata hii uongo au kusema ukwelu Yesu haitoshi kwako na unafuata mtu ambaye anasema ukifanya hii utapata hii, ukinunua hii maji ya Israeli itafanya hii kwako, ukipea pesa yako hapa utapata baraka, ukikunywa hii maji ya mizizi ya mti huu mtaponywa. ninyi unakumbuka loliondo tanzania bila shaka.
Paulo alijua watu wale na ilikuwa uchungu kwake kusikia hii habari kama pastor yo yote ambaye watu wake wanafuata uongo. Tunafika vs.11 na ni tofauti kidogo. Kitu cha kwanza tunaona ni Tazama! Sasa imagine Makanisa ya Galatia waliitwa pamoja kuskia barua imeandikwa kwa hawa na Paulo. Wanaketi uko na wanasikia kila kitu sisi tumesoma kwa mlango wa kwanza hadi hapa kwa Mlango wa sita mstari wa kumi na moja. Ni mzuri pia kujua wakati bibilia iliandikwa hakuna milango na mistari. milango na mistari yaliongezwa miaka mia nne sitini na saba iliopita, kabla ya hii hakuna. Lakini msomaji wa hii barua alifika hapa na maandiko ilianza kuwa tofauti. Tazama! Ikiwa ulianza kulala kidogo na mtu alisema TAZAMA bila shaka utaanza kuangalia. Na Paulo anasema ni kwa herufi gani kubwa nimeandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe. Hii iko na maana mingi sana.
Kitu cha kwanza tunona ni kwa herufi gani kubwa nimeandikia. Kama kawaida kwa Paulo alikuwa na maandishi ambaye ataandika kama anasema. Hatujui kwa nini, lakini watu wanasema Paulo, macho yake yalikuwa mbaya. Alikuwa mzee, hata nilisoma mahali ingine labda macho yake yalikuwa mbaya kwa sababu wakati yesu alikuja kwake kwa bara bara ya Dameski tunaomsa Kwa kitabu cha Matendo 9:3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Hii nuru kutoka mbinguni lazima ilikuwa kali sana kwa sababu tunaona vs.8-9 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi. Halafu tunasoma Bwana alimwambia mtu anaitwa Anania kuenda na kupata Paulo na kurudisha macho yake tunasoma Matendo 9:18 Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona. Labda macho ya Paulo yalikuwa na shida kwa sababu ya hii hatujui kabisa. Hata wengine wanasema wakati Paulo aliongea kuhusu mwiba katika mwili yake, alisema ni mjumbe wa shetani ili anipige, uko na na watu wanasema hata hii ilikuwa macho mabaya yake. Lakini wengine wansema ni walimu wa uongo. Hatujui. Lakini ukikumbuka Wagalatia 4:13-14 Lakini mwajua ya kuwa naliwahubiri Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili; na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu. Paulo alikuwa na ugonjwa fulani na hatujui hii ugonjwa ilikuwa gani lakini tunasoma mwisho ya 4:15 Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling'oa macho yenu, mkanipa mimi. Hii itaongoza sisi kufikiri ugonjwa wake ilikuwa shida ya macho.
Wengine wanasema herufi kubwa Paulo alitumia kwa wale wakristo wagalatia ilikuwa kama anafundisha hawa kama watoto. Kama anasema sawa, hujashika vizuri waacha niandike herufi kubwa ili unaweza kuona na kushika kama ninasema. Hushiki sawa waacha ni chore picha labda utashika kama ninasema. Ama labda ametumia herufi kubwa kwa sababu anasema kitu cha umuhimu sasa na anataka hawa kushika. kama wakati sisi tunaandika kitu kwa ALL CAPs au tunaweka BOLD print kwa sababu iko na maana na mtu akisoma ataangalia sana hii sehemu. Labda umeweka line chini ya maneno yako kwa sababu mtu akisoma macho yao yataenda hapo haraka. Ni kama unasema maneno haya ni muhimu sana. Tutaona maneno haya wiki ijayo na umuhimu wao.
Pia tunaona Paulo kusema kwa mkono yangu mwenyewe. Paulo anataka hawa kujua si maandishi anandika vitu hivi, si kama Paulo amesema kitu na labda mwandishi ameongeza kitu, ni Paulo mwenyewe, ni ule mtu amabye ulisema ukotyari hata kutoa macho yenu kwake, ni mimi. Na mimi ninaadnika hii Paulo anasema na mkono yangu. Paulo alipenda hawa, alitaka hawa kujua hii barua wametumwa ni muhimu sana na kama alianza kusikia kuhusu walimu wa uongo kuingia na kuharibu imani yao katika Yesu kristo hawezi kubali. Kwa Paaulo kusema nimeandikia kwa mkono yangu ni kwake kusema hii ni muhuri yangu kwa kila kitu umesoma. Tunaona hii ilikuwa desturi ya paulo kufanya kama hii wakati aliandika barua kwea kanisa. Waraka wa kwanza wakorintho 16:21 Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. Wakolosai 4:18 Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Waraka wa pili wathesalonike 3:17 Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ni muhimu sana kwa sababu walimu wa uongo ni uongo, wanaweza kuandika kitu hata kwa jina la Paulo na watu wataamini ni Paulo alisema hii. Bila shaka hii Paulo anaadnika kwa mwisho ya barua zake ilikuwa kama muhuri.
Ninyi unajua hata siku zetu uko na watu wanapiga simu au wanatuma sms na wanasema hii ni princial ya shule na mtoto wako ni mgonjwa tuma pesa kwa hii numba. Hata watu walituma sms kwa simu ya Michelle siku ingine na walisema hii ni Travis na niko kwa mkutano na ninatumia number ingine, usipigie simu yangu tuma pesa tu kwa hii number. Wakora hawajaanza juzi tu, walianza kitambo na bila shaka hata siku za Paulo watu walitaka kuharibu makanisa ya Yesu na ukweli wamefundishwa. Unakumbuka hata tunaona walifanya hii. Wapenda sheria walisema wanaongea kwa mitume, kama walitumwa na mitume wa Yesu na walijarubu kudanganya watu. Angalia Matendo 15:1 Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Baada ya hii mitume walikuwa pamoja na Petro alisimama mbele ya watu wengi pamoja na Mafarisayo na alisema kwa vs.11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. Bila Petro kusimama na kusema ukweli hawa watu wangeendelea kudanganya watu. Wakati mtu anasimama kwa ukweli neno lake ni muhimu sana. Na bila watu watu watajaribu kuchafua jina lake, watu watajaribu kusema amefanya vitu vibaya na yeye si mzuri. Hii ni sababu ni muhimu sana sisi wakristo tuishi maisha yetu safi na wazi. Ikiwa Paulo alikuwa mbaya au wakati alikuwa na Mafarisayo alisema kitu moja na wwakati alikuwa kanisani alisema kitu kiingine watu watasema anaongea panda mbili ya mdomo, hatuwezi kuwa naam na hiyo. Kumbuka kama Mithali 22:1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Hii ni kumaanisha wewe ni mwaminifu, unasema ukweli, Ndiyo ni ndiyo na la ni la. watu wanajua wakati unaongea si uongo.
Paulo alikuwa na hii jina. na alisema kwa mwisho baada ya kusema na mkono wangu nimeandika vitu hivi, mimi mwenyewe. Hakuna mtu amelazimisha Paulo kuandika vitu hivi, ni yeye na ameongozwa na Roho Mtakatifu. Kumbuka ni Paulo anandika lakini ni neno la Mungu. Tena PAulo alitaka hawa kujua aliwapenda, waliaamini kama alisema safari ya kwanza na bado maneno yake hayakubadilika. Kama tumesoma kwa kitabu cha Wagalatia bila shaka ni vitu kama amewaambia wakati walikuwa pamoja mara ya kwanza. Na wiki ijayo Mungu akipenda tutaanza kuona vitu hivi Pauo anataka kuwaambia ya mwisho na ni mzuri sana.
Leo asabuhi ikiwa hujaweka imani yako katika Yesu Kristo nitaomba tafadhali fikiria maisha yako, jipima. Mimi mwenyewe nitakuambia saa hii kusimamam mbele yako, Wokovu iko, na ni neema ya Mungu tukipata, lakini ni kwako kutubu na kuamini. Hakuna tendo fulani unaweza kutenda kupata hii zawadi ya Mungu. Ukitaka kujua zaidi kuhusu hii ongea na sisi baada ya ibada yetu.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.