Paul’s Conclusion Pt.2 (2)

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Galatians 6:13

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:13. Tumeangalia sana kitabu hiki cha wagalatia. Nafikiri utakubali na mimi imekuwa tamu sana. Tumekaa karibu mwaka moja kuangalia ukweli paulo aliwaambia Wakristo wale na bado iko na maana mingi hata kwetu leo kwa maisha yetu na kwa kanisa letu. Bado baada ya miaka elfu mbili vitu hivi vinafanyika. Kumbuka mandhari ya kitabu hiki ni kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Ukiangalia siku zetu kwa makanisa hii barua iko na maana zaidi. Kila kanisa unaenda siku hizi wanajaribu kuambia watu wao tendo fulani ni lazima wanafanya kuwa wakristo, hata wakoro wingi wameingia kanisa na wanajiita Pastor au bishop au prophet au apostle au oracle na wanakula kundi la Mungu kwa sababu hawa ni mbwa mwitu. Wanatumia jina la yesu vibaya sana na injili wanahubiri ni uongo. na iko kila mahali, si Kenya peke yake, kila mahali. Lakini usishangaa hata bibilia inasema hii itafanyika. Angalia Waraka wa pili Watimotheo 3:1-4 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; Hii ni rahisi sana kuona kila mahali tunaangalia. Kusema ukweli unaweza kufa moyo. Pualo anaendelea kusema vs.5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Hawa ni kama ni Man of God, wanatumia jina lake, anapata wanafunzi wake ambao wanafuata, lakini Paulo anasema kaa mbali na hawa watu.
Na wakati sisi tunakaa mbali na tunasimama imara ni mzuri unajua itakuwa ngumu sana, lakini kanisa ni lazima sisi tunasimama kwa ukweli, Angalia vs.12 na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. Tumeambiwa mapema hii itafanyika. Watu hawapendi ukweli na kwa sababu ya hii watatuleta shida mingi kwa sababu sisi tunaonyesha watu ukweli na kama hawa wengine ni uongo. Vs.13 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. Mpaka Yesu atarudi watu wale wataendelea kudanganya watu, na watu watafuata hawa, kazi yetu ni kama Paulo alimwambia Timotheo kufanya kwa vs.14 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, Kuwa mwaminifu, fuata kama umefundishwa na umeona, umehakikisha ni ukweli, umeona maishani yako na ya watu wengine. Siku hizi ni ngumu kudanganya ninyi. Ninyi umefundishwa ukweli wa neno la Mungu. Endelea, simama imara.
Tusome mstari yetu ya leo kwa kitabu cha Wagalatia kwa muktadha yake. Wagalatia 6:12-15 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kitu cha kwanza tunaona Kwa mstari yetu ya leo ni Paulo kuwaambia wakristo wagalatia hata hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria. Hii ni kusema hawa ni wanafiki. Kwa agano la kale tunajua kwa torati ya Musa zilikuwa sheria 613. Ni mingi na ni gumu sana kujaribu kufuata. Mafarisayo waliongeza zaidi ya sheria 1,500 kwa watu kufuata. Na hizi zilikuwa ya binadamu. Wakati unasoma Mambo ya walawi, Hesabu na Kumbu Kumbu la Torati unaweza kushangaa kuona kila kitu Mungu aliwaambia Musa kufanya. Ilikuwa kazi mingi sana kwa makuhani na kwa Waisraeli. Hii ni sababu mstari kama Wagalatia 5:1 iko na maana mingi zaidi Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Sisi tuko chini ya neema ya Yesu. Yesu alisema tukipenda Mungu na mioyo yetu yote, roho zetu zote na akili zetu zote na tunapenda jirani yetu kama nafsi yetu tumetimiza sheria yote. Ni ajabu sana, kusema ukweli kufanya vitu hivi mbili ni ngumu zaidi na sisi tunashindwa. Lakini wale wapenda sheria waliweka mzigo mingi juu ya watu na hawa wenyewe hawafanyi. Angalia kama Yesu alisema kwa Mafarisayo kwa kitabu cha Mathayo 23:2-5 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; Hii uzito mafarisayo waliweka juu ya watu ilikuwa uzito ya kuoata wokovu kwa njia ya matendo yao.
Unaona vs.5 Yesu alisema Walitenda matendo yao yote kuonekana na watu. Na anaendelea kusema matendo yao. Wakati tunasoma hii fikiria mapastors wa siku zetu. Vs.5 kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; Wako na nguo nzuri sana. Wanavaa ili kila mtu anaweza kuona. Kama siku zetu, Pastor anavaa suiti mzuri sana, ako na kalamu yake kwa hii mfuko hapa kwa shirti na labda hata hajui kuandika. Ni ajabu sana. na hata Watu wanajali nguo za mtu zaidi mioyo yao, zaidi ya kama wanaishi maisha yao. Anaendela vs.6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, Ni ajabu ama? Wanataka kuonekana na watu kama hawa ni wakubwa. Kwa sherehe wako wapi? Ni viti mbele kwa hawa. Hawa ni VIP. Wako na choo yao, wako na chumba chao wanakula na wenzao, hawa ni tofauti wametengwa na watu wa kawaida. Wanapenda sana wakati wa sherehe wanaitwa kusimama mbele ya watu wengine. Vs.7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Tena hii imeandikwa miaka elfu mbili iliopita lakini iko kwa wakati wetu. Wanapenda sana cheo chao. Reverened, Pastor. Kwa sababu unaweka hii jina kabla ya majina yao inaweka hawa kuwa kitu kubwa. Na wanafanya hii yote kwa jina la Yesu, wanatumia jina lake vibaya sana. Ikiwa wamejua kama Yesu alisema kuhuvu vitu hivi watu watakuwa toafuti sana. Angalia vs.11-12 Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa. Wangapi watataka hii kazi ya Pastor ikiwa walishi naam na hiyo? Mkubwa ni moja kwa kanisa nani Yesu kristo. Ni mzuri sisi sote tunakumbuka hii.
Kumbuka mstari yetu ya leo kwa Wagalatia 6:13 hata hao wenyewe waliotahiriwa hawashiki sheria. Hawafanyi kama wansema kufanya. SIku zetu ukiangalia Mapastors ni aibu sana. Hata hawa wanasema usikunywa pombe na unaoata hawa wanalewa. Wanaongea vibaya sana kuhusu malaya, kumbe hawa wanalala na malaya au wanaweka mimba kwa wanawake wingi kanisani yao. Hawa wanasema usitamani na ni hawa wanaiba pesa ya sadaka. Ni ajabu sana. Hii ni sababu wakati Mungu alitoa sifa za wanaume ambao wataongoza watu wake ilikuwa lazima wako na vitu hivi maishani yao. Vitu gani? Angalia Waraka wa kwanza Watimotheo 3:2-7 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. Ni ngumu kupata wanaume wale, kwa nini? Kwa sababu wale hawafanyi kazi ya Mungu kwa pesa, malmlaka, au kitu kiingine cho chote, ni kwa sababu wameitwa na Mungu na hawa ni watumwa wake.
Paulo anaendelea kwa Wagalatia 6:13 bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. Kwetu wakristo ubatizo ni ishara kwamba sisi tunafuata Yesu, lakini kwa wale Judiazers wakati hawa walipata watu kufuata hawa ilikuwa tohara. Na Paulo alisema wapate kuona fuhari katika miili yenu. Judaizers, hawajafanya kama sheria inasema lakini walifanya kazi na bidii kupata waongofu kwa sheria, ili waweze kujivunia watu waote ambao wanaongoza kufuata torati. Ni kama kukaa chini ya mti na kuongea kuhusu wanyama wako, uko na mbuzi ngapi, ngombe ngapi. Hawa ambao wanaongoza watu wengi kufuata sheria ni kama hawa wanaweza kuongea zaidi.
Kusema ukweli tangu mwanzo binadamu wanatumia dini kujaribu kufunika dhambi zao, na kama Judiazers au wapenda sheria wanatuonyesha, unaweza kufanya kazi mingi kanisani, unaweza kuimba kila jumapili, unaweza kufundisha Sunday school, unaweza kusafisha kanisa kila jumamozi hata unaweza kuwa pastor na bado umepotoka kimaadili na kiroho. Unajua mara mingi sisi tunafikiri hatari itatoka nje ya kanisa kwetu wakristo, lakini hatari kwa mkristo wa kweli inatoka ndani ya kanisa. Kwa sababu ya unafiki kanisani na hawa ambao ni wanafiki na ni viongzi na wanatumia jina la yesu na kanisa na watu wa Mungu kufanya biashara si Wakriso , so watoto wa Mungu si watu amabo Mungu amweka kuongoza watu wake, hawa ni fake na wameingia kwa siri. Angalia kitabu cha Yuda. Kiatbu hiki ni mzuri sana kwa vitu hivi, ni mlango moja lakini tunaweza kukaa hapa kwa mwaka mzima lakini anagalia kama anasema Yuda vs.4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Unaona kama hawa wameingia kwa siri, ni watu ndani, tutasema ni moja wetu na wanaanza kuongoza watu vibaya na wanaweka neema ya Mungu vibaya na wanaanza kuongeza vitu kwa tamaa zao wenyewe na wanamkana Bwana wetu pekee, Yesu kristo. Ukisoma kitabu cha Yuda unaona mara mingi yeye kusema Watu hawa, watu hawa, ni hawa watu ambao wanakula sana watu wa Mungu. Angalia vs.12-13 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa; ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele. Si ngumu kupata watu wale siku zetu, ni kuingia kanisa lo lote. Kial mwaka ni kitu tofauti, wanaongoza watu kama wanataka, siku zetu ni mafuta. Ilianza kuleta Roho Mtakatifu kwa watu wanasema, sasa hii fresh fry ya suku zetu unaweza kupika chips, mboga, leta roho mtakatifu lakini wameongeza hata unaweza kumwaga kwa lami na kutoa mapepo ya kuendesha vibaya, unweza kuweka kwa viatu vya watu hata kwa manyumba yao. Ni ajabu, kwa nini watu hawataki kufundisha neno la Mungu? Ni hii peke yake iko na majibu kwa maisha yetu ya wakristo, ni hii peke yake iko na manneo ya uhai ndani yake. Watu wanajaribu kuweka neema ya Mungu kwa kitu kama freash fry au mafuta. Lakini hii mafuta imetoka Israeli. Nchi ya Israeli hawapendi Yesu. Israeli iko na idai ya watu millioni kumi, wamehesabu wakristi ni Elfu mia moja hamsini. Hii ni asimilia moja na nusu. Ni wachache sana. Dini ya kwanza ni karibu asimilia sabini na tano ni dini la mnyahudi, hii ni kusema hawa ni watu wa sheria, wanasema bado Masihi hajafika. Yesu hajakuwa mwokozi wao, wamemkataa Yesu! Sasa unataka kuleta mafuta kutoka nchi ambaye wamekataa yesu na unaleta hapa kufanya nini na hii mafuta kwa kanisa la Yesu kristo?
Angalia Yuda vs.16 Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida. Ni watu wa kiburi na tunaona sababu yao na kwa nini wanafanya vitu hivi, si kwa sababu wanapenda Mungu, SI kwa sababu ya watoto wa Mungu lakini kwa ajili ya faida. Ikiwa huoni hii, fungua macho yako, saidia wengine kufungua macho yao. Uko na watu wa siku zetu ni kama Wagalatia 6:13 wanweka hii maneno yote juu ya watu ili kusema angalia mimi, anaglia wafuasi wangu ni wingi, angalia kanisa langu ni kubwa, angalia pesa niko nai. Kwa watu ambao wanafuata Yesu ukweli, wanapenda ukweli wa neno la Mungu na tumaini sana vitu hivi vyote vinakukasirisha. Ninaomba sana ninyi ambao unajua ukweli saidia hawa wengine kuona ukweli wa neno la Mungu. Angalia Yuda vs.18-19 Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Watu wale wako hapa. watu wa dunia hii tu, na wasio na Roho, lakini wanasimama kila jumapili mbele ya watu wa Mungu. Chunga sana. Tufanyaje? Angalia Yuda 20-23 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,  jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele. Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine. Tunavumilia. Tunakuwa waminifu, tujilindeni katika upendo wa Mungu, kwa hawa ambao wako na shaka, tunoyesha hawa ukweli, tunonyesha rehema. Lazima tunasimama na kusema ukweli, lazima tunafungua neno la Mungu na tunafundisha watu imani inakuja kwa njia ya kusikia neno la Kristo na wakati tunafanya hii tunawanyakua katika moto.
Ninaomba sana uskifuata wale ambao wanakutumia kuonyesha wengine wewe ni mfuasi wao. Chunga sana watu ambao wanatoa neema ya Yesu na waneweka uzito wa matendo yetu kupata wokovu. Wiki ijayo Mungu akipenda tutaona mfano mzuri ya kiongozi na ni watu kama hii tunataka kusikia na kufuata, kwa sababu ni hawa wanafuata Yesu kristo.
Leo asabuhi ikiwa uko hapa na hujui Yesu naomba sana weka imani yako katika yeye, hakuna tumaini lingine kwa maisha haya au maisha ambaye inakuja. Ikiwa uko hapa na umedanganywa na unafuata walimu wa uongo au unafikiri wewe ni mkristo kwa sababu ya tendo fulani unatenda, naomba, tubu na weka imani yako katika Yesu Kristo pekee. Ikiwa unataka kuongea au unataka kuokoka, karubu mbeke baada ya ibada yetu na ongea na mimi.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more