Paul’s conclusion Pt.3
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
Galatians 6:14
Galatians 6:14
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:14. Tumekaa sana kwa kitabu hiki, karibu mwaka moja, ama nafikiri labda tumepita mwaka moja. Unajua lengo yangu kwa kanisa hili ni wakati tumeingia neno la Mungu unajua kama inasema, huwezi kusema, hii inamaanisha nini, au sijui inasema nini, au kuwa na udhuru maishani yako kusema Bibilia ni ngumu kufahamu kwa sababu ya hii, sisomi? Pia ni kutia moyo yako na kwako kujua Bibilia ni neno la Mungu na ndani yake tunapata ukweli kuhusu kila kitu cha maisha haya, uzima wa milele, kifo, tumaini, neema, rehema, jehanamu, mbinguni, Yesu, Mungu, Wokovu. Hii ni sbabau wakati tumemaliza na masomo yetu ya kiatbu fulani utajua maana yake, sababu iliandikwa na iko na maana gani kwetu kwa siku zetu. Kitabu cha Wagalatia ni tamu sana kwa sababu inatuonyesha kwamba baada ya miaka elfu mbili, tangu kanisa la Yesu ilianza, bado tuko na watu wanajaribu kupata wokovu kwa njia ya uwezo wao, kwa matendo yao kwa mfumo fulani ya biandamu na kitabu hiki kumbuka mandhari yake ni kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Yote ni Yesu na neema yake. Uhai ni wake, wokovu ni zawadi yake anapea watu wake, tumaini ni lake, na sisi tunaoata hii yote kwa njia ya kuamini na weka imani yetu katika Yesu, maisha yake, alikuwa mkamilifu, Masihi ya Mungu, Kifo chake, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, na ufufuo wake. alishinda kifo na mauti na hii ni tumaini letu. Leo anaishi na huwezi kufika kwake kwa tendo lo lote unaweza kutenda, ni kuamini, ni kutubu kwa dhambi zako, na kufuata neno lake kama anasema. Lakini ni mzuri kwetu kujua hata imani yetu ni zawadi anatupea. Waefeso 2:8 mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Tumeona Judiazers, Wapenda sheria waliingia makanisa ya area ya galatia, yalikuwa kanisa saba ama nane Paulo alianzisha. Na walianza kufundisha ni lazima ukitaka kuwa mkristo uwe umetahiriwa. Tena hii ni tendo binadamu waliweka juu ya watu ambaye haiwezi kusaidia. Hata watu wambao wanajaribu kufuata sheria ya agano la kale na ni wengi hata siku zetu, ni mzuri wanajua huwezi na wokovu haiwezi kufika kwa njia ya sheria, huwezi kuwa na mema ya kutosha, huwezi kufanya vitu vya kutosha. Kumbuka mlnago wa tatu ya kitabi hiki cha galatia Paulo aliongea sana kuhusu torati na imani. Angalia tena Wagalatia 3:23 kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. Tumefungwa, hii ni kama ulikuwa gerezani, ilikuwa uzito na hakuna mtu anaweza kufanya kama inataka. lakini imani ilikuja. Vs.24 Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. Torati ilikuwa kiongozi, au kwa kiingereza ni kama mwalimu kuonyesha sisi Kristo. Torati haiwezi kuhesabia haki mtu, ni imani peke yake, imani katika Kristo na hii ni Yesu. Vs.25 Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. Ni wazi kabisa, tumetoka chini ya matendo yetu kumpedeza Mungu, sasa ni imani katika Kristo na wakati tunafanya hii hata matendo yetu yanampendeza Mungu kwa sababu tuko ndani ya Yesu. Nje ya Yesu matendo yetu ni chafu kwa macho ya Mungu. Kwa sababu ya hii vs.26 ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Sisi ni wana wa Mungu naam na gani? kwa matendo yetu? Kwa sababu tuafuata torati au sheria fulani? Kwa sababu ya kanisa letu, pastor yetu, mama ama baba yetu? naam na gani? Kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Warumi 8:3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; Marafiki yangu, Hii ni habari njema ukweli, hakuna matendo mazuri ya kutosha unaweza kufanya, si juu yako, Yesu Kristi ameshaa fanya na sasa ni kwako kuamini, weka imani yako katika yeye. Usisikiliza wale walimu wa uongo, Kristo Yesu alileta uhuru kwetu.
Tusome mstari yetu ya leo kwa muktadha yake. Kitabui cha Wagalatia 6:12-15 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu. Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kumbuka wiki iliopita tuliangalia sana kama wale Judiazers, Wapenda sheria, walitaka watu kufuata mafundisho yao ili wanaweza kusema angalia wafuasi yangu, angalia mimi. Kama siku zetu Walimu wa uongo, Mapastor wingi na watu amabo wanatumia jina la Yesu kristo wanataka watu kuangalia hawa, wanatoa macho ya watu kwa Yesu na wanataka watu kufuata hawa wenyewe, Wanajaribu kuweka imani ya watu katika vitu kama mafuta, kaji mtakatifu, hawa mwenyewe, hata nyumba ya kanisa, na wanawacha Yesu nje. Na hii yote ili wapate kuona fahari katika miili ya wafuasi wao. Wanapenda sifa za watu, na kumbuka Yesu alisema kwa Mathayo 23:15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. Na hii ni sababu tunaona wakati watu wanafuata watu wale hawa si wakristo wa kweli hata ikiwa wanatumia jina la Yesu, hata wakienda kansia. Kwa sababu Ikiwa Mtu ni Mkristo kweli kweli ako na Roho Mtakatifu anaishi ndani yake na anaweza kudanganywa, sisi sote tunaweza kudanganywa lakini huwezi kaa hapo. Ikiwa wewe unasoma neno la Munguna Roho anaishi ndani yako, atafundisha macho yako kuona ukweli wake. Na wale wa uongo wanajua hii pia hata Yesu alisema kwa vs. 13 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie. Ni dini tu, si Yesu, si Mungu.
Halafu tuko na mstari yetu ya leo, na unaweza kuona tofauti kubwa kwa moyo wa Paulo na hii ingekuwa mioyo yetu pia. Angalia Wagalatia 6:14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote. Kitu cha kwanza tunaona hapa ni watu wa Yesu si watu kujisifu. Sisi tunamsifu moja tu na ni Yesu Kristo. Sisi hatutaki sifa za watu, sisi hatutaki macho ya watu kuangalia sisi, sisi tunaweka macho ya watu kwa Yesu, yeye ni mfalme wetu, yeye ni Bwana wetu. Paulo alitumia neno kali sana hapa anasema Hasha! ni kusema hata huwezi kufikiria kufanya kitu kama hii. Na anasema juu ya kitu cho chote. Paulo alikuwa mtume wa Yesu kristo, alitoa mapepo, aliponyesha watu, Hata leso au nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo ikiwa mtu anaguza aliponyeshwa. Ni ajabu sana, nyoka mwenye sumu ilishika mkono yake na aliitikisa tu na alendelea na watu waliona hii walijua atakufa, Paulo alifanya kwa ukweli kama hawa wa uongo wanasema wanafanya leo na bado anasema nisione fahari juu ya kitu cho chote. Na ikiwa Paulo anasema hii, sasa sisi tutasema nini? Nanoi hapa amefanya muujiza? Nani hapa ameponyesha mtu? Lakini badi tunajaribu kujisifu kwa watu. Na sisi hatuna kitu cho chote kuleta mbele ya Mungu na kusema angalia hii nimefanya kwako.
Paulo anaendelea kusema kwa vs.14 hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Kwisha maneno. Nataka ninyi kuona na kushika kwa maisha haya na maisha ambao inakuja, kila kitu ni Yesu Kristo. Kitabu cha Matendo 17:28 ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Maisha yyetu yote lengu letu ingekuwa kuishi maisha hawa kwa Bwana wetu Yesu kristo kama amesema kwa neno lake na kuonyesha wengine kama Yeye ni ukweli, na watu wanaona yeye ni ukweli wakati watoto wake wanaishi kama alisema na kuonyesha hawa msalaba ya Yesu. Paulo alisema Sifa zote ni ya Bwana wetu Yesu kristo na kazi yake msalabani. Ni kwa sababu ya hii sisi tuko na wakovu, ni kwa sababu ya hii kanisa liko, ni kwa sababu ya hii tunahuburi, ni kwa sababu ya hii binadamu wanakabiliwa na wao ni nani kweli kweli. Msalaba inatukumbusha kwamaba dhambi iko na dhambi iko na bei yake. Na kuokoa watu kutoka dahmbi zao lazima mtu alipe, lakini haiwezi kuwa mtu ya kawaida, mtu ya kawaida akikufa msalabani haisadii kitu cho chote, lakini lazima inakuwa mtu kamilifu, bila dhambi yo yote. Tutapata mtu kama huyu wapi? Ni moja tu, tangu mwanzo wa dunia hadi saa hii na ni Yesu, mwana wa Mungu. Na mtu kamilifu hastahili kufa kwa sabbabu hajakosa, hajavunja sheria kama sisi, inastahili sisi sote kila moja akufe kwa ajili ya dhambi zake na bado haiwezi kutuokoa. Lakini tunasoma kwa kitabu cha Wafilipi 2:7-8 bali, Yesu alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Ni ajabu, hivi ndivyo tunavyojivunia si matendo yetu mema, Bwana wetu alibeba hii yote kwetu, uzito wa dhambi zangu ya dhambi za watu wake. Mslaba, kama kawaida ni kitu kibaya sana, chombo cha mateso, lakini kwetu ni kitu cha kutoa sifa. Waraka wa kwanza wapetro 2:17 Yesu mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Umeona kupigwa kwake uliponywa. Ikiwa ulikuwa na ugonjwa mbaya sana na hapakuwa na tiba kwa hii ugonjwa wako na mtu alikuja na alisema nimepata dawa yaa hii ugonjwa wako na ulimeza na uliponyeshwa utanyamaza? Huwezi kuenda kila mahali na kutoa sifa kwa hii dawa? Nataka wewe kujua hii ni mara kadha, Roho yako ililaaniwa, kuteska jehanamu kwa milele na milele na milele kwa sababu ya dhambi zako, na kwa sababu ya dhambi zako Mungu na wewe hakuna uhusiano hata huwezi kujua Mungu kwa sababu Mungu anachukia dhambi na wewe ni mwenye dhambi, na Yesu alikufa mslabani kwa ajili ya dhambi zako na alirudisha wewe kuwa na uhusiano na Mungu. Msalaba kwetu wakristo ni kitu cha sifa kabisa.
Unakumbuka Kwa vs.13 Paulo alisema wale walimu wa uongo wanataka watu kufuata hawa ili wanjivuna katika mwili. Kusema angalia mimi. Na si kama Paulo alikuwa mtu ambaye hanakitu kwa maisha haya na ni mtu ya kawaida. Angalia Wafilipi 3:4-6 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Paulo alikuwa kitu hata alikuwa juu ya Jiudiazers wengi, ikiwa angeendelea hata labda angekuwa mkubwa wao lakini anaendelea kusema kwa vs.7-10 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; Hii ni moyo wa Mkristo. Hii maneno yote ya dunia hajali, sisi tujataka kujua Yesu kristo, sisi tunataka kufuata yeye, ni tamaa za mioyo yetu kuwa kama yeye zaidi na zaidi kila siku.
Na Paulo anaendela kusema Kwa Wagalatia 6:14 nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Mungu akipenda tutaanza wiki ijayo kuangalia hii zaidi. Lakini nataka ninyi kuenda hii wiki nakufikiria wakati unasoma hii ya mwisho, inamaanisha nini kwako? Mimi niko na wiki tatu inabaki kwangu kwa kitabu hiki cha Wagalatia na mimi nataka kutumia wiki tatu hizi, kutuonyesha sababu sisi wakristo tunajisifu tu katika mslaba wa Kristo. Iko na nguvu mingi sana. Lakini fikiria hii mstari wiki huu nisome tena nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
Ikiwa uko hapa leo asabuhi na hujaweka imani yako katika Yesu Kristo kwa wokovu nitasema tafadhali tubu kwa dhambi zako na amini. Amini kwamba Yesu ni Mungu na alikufa msalabani kuleta wokovu kwa watu wake. Umeshika kwamba hakuna kitu cho chote kwa uwezo wako unaweza kutenda kujiokoa au kuopata wokovu ni neema Ya yesu kristo, na ukiamini hii Bibilia inasema utakuwa kiumbe kipya, vitu vya zamani zilipita, na tazama vitu vipya vimekuja. Ukitaka kuongea zaidi tafadfhali kuja mbele baada ya ibada yetu na ongea na sisi, tuko hapa kueleza zaidi.
Asanteni Sana, Bwana wetu Yesu kristi Asifiwe na karibuni wiki ijayo.