Pauls Conclusion Pt.6 The Glorious Cross Pt.2

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 5 views
Notes
Transcript

Galatians 6:15

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:15. Kitabu hiki ni ajabu sana natumaini sana kukaa na kuingia sana kwa kila mstari imekusaidia na kusema ukweli natumaini sana imebadilsha maisha yako na tamaa zako kufuata Yesu zaidi.
Kwa wiki karibu tano tumeona Paulo kuanzisha vs.11 kutoa hitimisho lake, ni kujumlisha kila kitu ambacho amekuwa akisema kwa hii barua aliandika kwa makanisa wa region ya Galatia. Na unaweza kuona upendo wake kwanza kwa Bwana wake Yesu Kristo, na pia kwa ukweli wake na kwa wale watu ambao wanafuata Yesu. Lakini pia kama amesema ni kusaidia hata sisi kwa wakati wetu na hata baada ya sisi kwa watoto wetu na watoto wao ambao watasema Yesu kristo ni Bwana wa maisha yao. Hii ni muhimu hata wazazi, fundisha watoto wenu nyumbani vitu hivi. Keti na hawa na fungua neno la Mungu na inyesha hawa ukweli wake. Onyesha hawa kama sisi wakristo tunaishi na utakatifu wa maisha na kama inampendeza Mungu wetu. Hapa kanisani unafundishwa neno la Mungu, peleka hii mafundisho kila mahali unaenda. Weka maishani yako kwanza, halafu nyumbani halafu kila mahali miguu yako yanaenda. Kumbuka sababu sisi tunakuwa pamoja kial jumapili, kitu cha kwanza ni kuabudu Mungu wetu pamoja kama watoto wake na tunashikiriana pamoja hii siku katika Bwana wetu Yesu kristo ambaye ametuokoa kutoka dhambi zetu. Halafu kitu cha pili ni tunafika hapa kufundishwa neno la Bwana wetu. Angalia Waefeso 4:12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; Hii ni sababu Mungu alpea kanisa lake viongozi na mapsators na walimu, ili wanaweza kusikia, wanaweza kufundishwa na kutoka mahali hapa na wakotayari kuishi maisha ya mkristo mbele ya watu wengine na kufundisha hawa kama neno lake inasema. Ninyi unajua wengi wanaenda Bibla college kufundishwa neno la Mungu. Ninyi uko Bible collge kila jumapili, kila jumanne wanawake, Kial alhamisi kwa Mara Bible. Tunataka ninyi kujua bibilia sana, kazi yetu ni kuwakamilisha watakatifu, kwa ya huduma itendeke na mwili wa Kristo ujengwe. Fikiria maisha yako ya mwaka iliopita, miaka mbili iliopita, miaka saba, nane ilioptia ulikuwa naam na gani? na saa hii ukoaje? ni kwa sababu Bwana wetu Yesu kristo kwa njia ya kufundishwa neno lake anabadilisha maisha yako. Nafikiria ukiendelea kufika hapa, utakuwa wapi mwaka ujayo, baada y miaka tano.
Ukweli huu ni wa thamani sana, Shika, weka karibu, tumia. Sikia manneo ya Bwana wetu kuhusu ufalme wake Mathayo 13:44 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Ikiwa tumeona ukweli wa neno la Mungu na ufalme wake naam na hiyo, maisha yetu ingekuwa tofauti sana. Hii mstari inatuambia hakuna kitu kiingibe kama ufalme wa Mungu, hakuna kitu cha thamani inaweza kuwa kama ufalme wa Mungu, ni kila kitu na huwezi kuingia bila Yesu Kristo, bila msalaba wake. Tuliona Wagalatia 6:14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Wiki ilioptia tulianza kuangalia sababu tunajivunia msalaba wa Yesu pekee. Sababu ya kwanza tuliona ni kwa sababu hakuna kitu kiingine iko na uwezo kuleta uhuru kwa binadamu kutoka hii ulimwengu na nguvu yake. Paulo aliendelea kusema kwa vs.14 kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Ni msalaba wa Yesu tu. Leo tutaona sababu ya pili ni msalaba iko na nguvu kufanya kama mwili hawezi kufanya.
Tusome mstari yetu ya leo kwa muktadha yake. Wagalatia 6:14-16 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.  Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Tunajua kitabu cha Galatia iliandikwa kwa sababu ya walimu wa uongo waliingia makanisa ya region ya Galatia na hawa walikuwa wapenda sheria na walianza kuongeza matendo kwa wokovu. Walijaribu kusema ni lazima kutayarishwa ikiwa unataka kufuata Mungu. Paulo tena hapa anasema hii ni ujinga. Kwa nini sisi binadamu tunajaribu kuongeza vitu kwa wokovu wetu. Sisi tumezaliwa katika dhambi zetu, sisi hatuna nguvu yo yote kuchukua Yesu, sisi tunasema tunapokea Yesu moyoni mwetu, naam na gani? Moyo wako ilikuwa jiwe kabla ya Yesu aliingia. Wewe ulikufa wafu na ni Mungu Alipulizia uhai ndani yako. Paulo hapa anasema kutahiriwa si kitu. Kwa wayahudi kusikia hii na kwa wale wapenda sheria kusikia hii walishangaa na bila shaka walikarsirika. Paulo alikuwa mnyahudi na alijaribu na nguvuyake yote kumpendeza Mungu, lakini ukikumbuka maisha ya Paulo hajaoendeza Mungu kwa sababu Alimtesa mwana wa Mungu. Unakumbuka wakati Paulo alikuwa kwa bara bara ya Damasko Yesu alikuja kwake na Paulo alishangaa kwa sababu ya nuru kutoka mbinguni ilikuwa kila mahali na tunaona kwa kitabu cha matendo 9:4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Halafu tunaona hii sauti ni ya nani vs.5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Paulo amefikiri anamoendeza Mungu kwa njia ya kufunga wakristo gerezani na kuua hawa kwa sababu alisema Wakristo wanamkufuru Mungu. Kwa nini? kwa sababu wanamfuata Yesu na wanasema Yeye ametimiza sheria na sasa wokovu haifiki kwa njia ya matendo yetu lakini kwa neema ya Yesu.
Hapa kwa Wagalatia kwa Paulo kusema kutahiriwa si kitu ni kubwa sana. Si kitu kwa mnyahudi . Kufuata sheria ilikuwa maisha yake. na aliendelea kusema na kwa Mataifa waka kutokutahiriwa. Na kutahiriwa hapa inawakilisha mifumo ya ulimwengu ya dini. Fikiria dunia yetu saa hii, ni ajabu kuona dini zote ambazo zimekuja. Saa hii ni zaidi ya 4,200. Zote ziko na imani yao. Unajua ni ngapi ya 4,200 wanasema wokovu inakuja kwa imani pekee kwa neema pekee? ni moja tu, na hii ni Ukristo. Lakini hata ukiangalia siku zetu uko na wakristo wa fake na mapastor wengi ambao ni fake na uko na makanisa mingi sana ni fake, si wakristo, mapastor na makanisa ya Bibilia. Yesu alisema kwa Mtahayo 7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, Yesu anasema wanakuja kama wakristo, wanaongea kama wakristo, utaona hawa ni kama moja wenu walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. na anasema kwa vs.16 Mtawatambua kwa matunda yao. Matunda gani? Kuongeza matendo kwa wokovu, kubadilisha neema ya Yesu kwa matendo ya binadamu. Siku zetu tuko na mbwa -mwitu wingi. Kial mtu ni pastor, kila mtu anaanzisha kanisa kwa sababu ni biashara mzuri sana. Ni watu wengi siku zetu wanafikiria unaweza kununua nafsi yako yako mbinguni na pesa. Ni wengine wameweka mchungaji wao mahali pa Yesu, Hata wanafikiri hawawezi kuokoka bila pastor wao kuwaombea. Wengine wanafikiri wanapata wokovu kwa njia ya mafuta, ubatizo, kufika kanisani, tumeweka kila kitu mbele ya Yesu kristo na neema yake. Nataka ninyi kusikia nimesema mara mingi sana hapa mbele yenu. Matndo yako hayawezi kukuokoa lakini wakati mtu anaokoka kweli kweli ataukuwa na matendo mazuri maishani yake. Kumbuka maneno ya Paulo kwa kitabu cha Waefeso 2:8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; Hii ni wokovu wetu, kwa kila mtu ambaye anasema Yesu ni Bwana wake. Sijali kanisa lake ni gani, anasihi wapi, kabila yake, rangi yake ikiwa wewe ni Mkristo, ikiwa umeokoka ni naam na hiyo. Na wakato mapastor wanafundisha kitu kiingine nje ya hii, hawa ni walimu wa uongo. Na tunaona hata imani tuko nai, ni kipawa cha Mungu. Na vs.9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Usisahau hii. Hakuna matendo unaweza kufanya kupoata wokovu wako, kwa sababu ikiwa unaweza kutenda tendo fulani wewe utapata sifa, utajisifu, wewe utakuwa mwokozi wako, na hakuna maana kwa Yesu maishani yako. Kama tunaona siku hizi, watu wanasimama mbele ya watu kwa masaa, bila kusikia kuhusu Yesu, bila kusikia ukweli wake, bila kusikia njia yake anasema kupata wokovu wake. Ndiyo labda utasikia jina lake, KATIKA JINA LA YESU! BWANA ASIFIWE, lakini nipe pesa zako, Kuja mbele ongea lugha ya ujinga, umwagwe mafuta, Twende kwa mlima kuomba. Kwa nini? Nafikiri Mungu anaweza kukusikia kila mahali. Chinga sana!
Paulo kwa kitabu cha Wagalatia baada ya kusema hii matendo yote, kutahiriwa, kutokutahiriwa, anasema kwa Vs.15 kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Bali Kiumbe kipya. Kuwa kiumbe kipya ni kila kitu. Na huwezi kuwa hii nje ya msalaba wa Yesu. Ni lazima sisi tunazaliwa tena. Kumbuka kama Yesu alimwambia Nikodemo, na kumbuka Nikodemo alikuwa mfarisayo, mtu ambaye anaongoza Watu waisraeli kwa sheria ya Mungu, alikuwa mwalimu ya vitu vya Mungu angalia kwa kitabu cha Yohana 3:3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Lazima tunazaliwa tena, maisha yetu ya zamani imechafuliwa sana, hakuna kitu unaweza kufanya kusaidia huyu ya zamani, hakuna tumiani lo lote. Hii ni sababu program fulani kusaidia mtu kubadilisha maisha yake haiwezi kumsaidia yeye, kwa sababu ameharibika kabisa na kwetu sote ni kitu moja tu inaweza kubadilisha maisha yetu na ni kuzaliwa tena. Kuzaliwa tena maana yake ni kwa roho zetu kuzaliwa tena, sisi hatuwezi kurudi kwa tumbo la mama yetu. Miili yetu haina matumaini, lazima itakufa, lkaini roho zetu zitaendelea kwa milele, na ikiwa haijazaliwa tena itaishi kwa mahali inaitwa jehanum. Ni mahali ya kuteseka kwa milele na milele. Lakini Roho ambaye imezaliwa tena itaishi mbinguni pamoja na Yesu kwa milele na milele. Wakati Yesu anatuokoa na tunaweka imani yetu katika yeye na tunafuata yeye kwa njia ya kutii neno lake tunasoma kwa Waraka wa pili wakorintho 5:17 mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Hii ni ajabu sana! hii ni wakati Yesu amebadilsha moyo wako, mawazo yako, maisha yako. Ni kama amefungua macho yako kuona vitu amabvyo hujaona maisha yako yote. Umekuwa kipofu na sasa unaona. Ulikufa wafu na sasa ameweka uhai ndani yako, ni mabadiliko ya maisha yako yote. Ulikuwa kwa ufalme wa giza na sasa uko kwa ufalme wa nuru. Umekuwa kiumbe kipya vitu vya zamani, hii mtu ulikuwa zamani hayuko hapa umekuwa mtu mpya.
Tuliangalia sana Wagalatia mlango wa tano na kwa sababu sisi tumekuwa kiumbe kipya tuko vitani. Roho zetu na miili yetu yanapigana. Huyu ya zamani anataka kurudi na kushinda huyu mtu mpya, mtu mpya anataka kushinda ule mtu wa zamani. Lakini ni mzuri wewe unajua ikiwa hii vita iko ndani yako hii ni mzuri, ni kumaanisha umeokoka. Ikiwa huna vita maishani yako, wewe hujakuwa kiumbe kipya.
Kiumbe kipya ni kubadilishwa ndani na neno tunatumia kwa hii kwa kiingerza ni Regeneration au Kuzaliwa upya. Matendo yetu hayawezi kufanya hii, ni Roho Mtakatifu ndani ya mwaamini na anamfanya kuwa kiumbe kipya katika Yesu. Lakini kuzaliwa upya ni mwanzo tu. Kazi ya Roho mtakatifu anaongoza sisi kwa toba na imani na hii itaonekana kwa kila siku ya maisha yetu kuua dhambi na tamaa zetu na kukua daima katika utakatifu na tunakuwa zaidi na ziadi kama Yesu kristo. Kuwa kiumbe kipya ni kumaanisha tuko na tabia mpya pia, mfumo yetu ya kama tumeishi ni tofauti, tuko na mfumo mpya, mapenzi na tabia yetu imekuwa tofauti kwa sababu ya kazi Roho Mtakatifu anafanya ndani yetu. Kusema ukweli wakati tunaongea kuhusu wokovu au tunasema mtu ameokoka kitu moja tu iko na maana na ni ikiwa hii nimesema saa hii imefanyika na bado inaendelea kila siku kufanyika. Paulo alijua hii na hii sababu anasema kama wewe ni Myahudi aliyetahiriwa au Myunani haijalishi, haina maana. Cha muhimu zaidi ni ikiwa huyo ni Mkristo aliyezaliwa upya. Na ikiwa wewe hujapata ROho Matakatifu anafanya kazi ndani yako ni mzuri unaongea na Mungu na uliza yeye kubadlisha wewe, kubadilisha moyo wako na mawazo yako, kwa sababu mabadiliko inaanza ndani halafu inatoka nje.
Ni mzuri kukumbuka, milele iko mbele ya sisi sote. Labda ni leo, labda ni kesho au labda ni baada ya miaka mingi. Bila shaka wale watu walibebwa na maji kwa mafuriko wiki chache ilopita walikuwa na mipango, bila shaka walikuwa na mipango kusafiri kesho na kukutana na fulani wiki ijayo na dakika moja tu walibebwa na wanasimama mbele ya Mungu na Yesu, macho yao yameona ukweli. Mimi nafikiri uongo kuu wa shetani ni kudanganya watu kwamba wana muda, si lazima leo, waacha nifanye wiki ijayo, mwezi ijayo. Mimi ninaomba saa hii, jipime, fikiria masiha yako na maisha ambaye inakuja, usichelewa. Najua wakenya wanachelewa kwa kila kitu, lakini kwa hii usichelewe na pia usiweke tumaini lako kwa matendo yako, hayawezi kukusaidia.
Ikiwa uko hapa leo asabuhi na wewe unategemea matendo yako mema kukuokoa tafadhali tubu, hii ni dhambi na weka imani yako katika Yesu na matendo yake. Ikiwa hujui Yesu na hujaweka imani ytako katika yeye, nitaomba, tubu weka imani yako katika yeye na amini, fuata yeye na maisha yako.Ukitaka kuongea na mimi karibu baada ya ibada yetu. Niko hapa na nitapenda sana kuongea.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo, wiki ijayo mimi ninamaliza wakati wangu kwa kitabu cha Wagalatia.
Related Media
See more
Related Sermons
See more