Pauls Conclusion Pt.7 The Glorious Cross Pt.3

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Galatians 6:16

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika 6:16. Hii ni mwisho kwangu kufundisha kwa kitabu hiki. Nimeshangaa kusema ukweli, tumeanzisha kitabu hiki Mwezi wa sita terehe kumi na moja mwaka iliopita. Mimi na Jonathan na Dominic na Gilbert tuliketu na tulisema ni kitabu gani tunaweza kuhubiri wakati mimi nilikuwa US. Tuliona kitabu cha Wagalatia na itakuwa kama jumapili 21. Mimi nilirudi mwezi wa kumi na moja na nilianza mlango wa tano vs.7. Kumbe, bado tuko hapa baada ya jumapili thelathini na nne. Lakini natumaini sana ninyi unajua kitabu hiki na hazina zote tumeona. Zaidi ya yote natumaini sana umeona mandhari ya kitabu hiki ni kuhesabiwa haki kwa imani pekee katika Kristo pekee. Natumaini sana Yesu kristo amebadilsha maisha yako na unatembea na yeye na ikiwa wewe ni Mkristo natumaini mafundisho haya ya kitabu hiki yameleta wewe kuwa Mkristo mwenye nguvu zaidi.
Kwa wiki sita sisi tumeona kuanza vs.11 hitimisho la Paulo kwa makanisa ya region ya Galatia. Amefupisha kila kitu ameandika kwa hawa kushika. Na kama ameanzisha kitabu hiki ana maliza na Yesu. Kumbuka Wagalatia 1:1-5 Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia; Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. Utukufu una yeye milele na milele, Amina. Yesu alibadilsha maisha ya Paulo na lengo ya maisha yake. Kila kitu kwa Paulo ilikuwa Yesu Kristo. Lengi yake ilikuwa kwa watu wote kujua Yesu na neema yake kuokoa wenye dhambi kutoka dhambi zao. Alisafiri sana, alihubiri Yesu kristo na kifo chake na ufufuo wake. Paulo alianzisha makanisa kwa regions na miji, Tunajua kanisa kumi na nne alianzisha kwa Galatia, Filipi, Thesalonike, Korinthi na efeso. Maisha yake ilikuwa ngumu sana, lakini alisema kwa vs.1 hajatumwa na wanadamu, alitumwa na Yesu kristo na Mungu Baba. Na alisema kwa vs.4 ni huyu Yesu Kristo alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu. Na alifanya hii kwa kifo chake msalabani.
Kwa wiki mbili tumeone hitimisho la Paulo ilikuwa kuongea kuhusu hii msalaba na nguvu yake hii ni sababu alisema kwa Wagalatia 6:14 hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Na tuliona wiki ya kwanza msalaba wa yesu iko na nguvu kuleta uhuru kwa binadamu, uhuru kutoka utumwa wa ulimwengu huu. Hakuna kitu kiingine inaweza kufanya hii. Wengi wamejaribu kupata kitu kiingine na bado wanajaribu lakini wote wameshindwa na watendelea kushindwa. Kitu cha pili tuliona ni msalaba wa Yesu iko na nguvu ya kufanya kama mwili wetu haiwezi. Hakuna tendo tunaweza kufanya au matendo mema ya kutosha kujioka. Na leo tutaona msalaba wa Yesu iko na nguvu kuleta wokovu.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake. Kitabu cha Wagalatia 6:14-16 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Wiki iliopita tuliangalia sana wakati Paulo alisema kutahiriwa si kitu wala kutokutahiriwa. Hii yote ilikuwa matendo ya watu kujaribu kupata wokovu. Lakini tuliona Paulo aliendelea kusema kitu cha maana sana ni kwamba mtu ni kiumbe kipya. Na leo vs.16 anasema Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo. Kanuni gani? Kwamaba matendo hayawezi kuokoa mtu na kuwa kiumbe kipya ni ya maana zaidi. Kumbuka kama Paulo alisema kwa Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kanuni hiyo ni kama hii mstari imesema. Wokovu ni kipawa cha Mungu. Si kwa njia ya matendo yetu. Hapa kwa mstari yetu wale walimu wa uongo bila shaka walikuwa wakati hii ilisomwa kwa watu kusikia. Hata hii ni mwaliko kwao na kwa wemgine ambaye hawajui Yesu Kristo kama mwokozi wao. Si lazima wanakaa kama wasioamini ambaye wamepoteza njia , lakini kwa imani katika Yesu kristio na kazi yake wanaweza kuenenda kwa kanuni hiyo ya injili ya Yesu Kristo. Hi ni kwa kila mtu, hata ikiwa unaketi hapa leo asabuhi na hujui Yesu, hujaweka imani yako katika yeye au labda umedanganywa na unafikiri wewe ni mkristo kwa sababu ya kitu fulani umetenda, bado uko na uhai na unaweza kutubu na kuweka imani yako katika Yesu na kumfuata yeye. Nafikiri kila mtu hata wasioamini wengi wanajua maneno matamu ya Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maneno haya si bure, maneno haya si kitu kizuri kuweka kwa ukuta na kushona kwa shuka, maneno haya na kama tunafikiria mananeo haya iko na matakeo kwa milele yetu. Lakini Yohana anaendelea kusema kwa vs.17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Sisi tunaokolewa naam na gani katika Yesu, hakuna njia ingine, ni matendo yake si matendo yetu, ni maisha yake na kifo chake na ufufuo wake. Bila kuamini katika Yesu Kristo ni hukumu. Angalia vs.18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Kuamini maana yake ni umeweka imani yako katika yeye. Nataka ninyi kusikia bila kufanya hii hakuna wokovu, wokovu ni sharti la wokovu. Na ni hali ambayo kila mtu anaweza kufanya. Wokovu unapatikana kwa wote bila ubaguzi. Waraka wa pili wapetro 3:9 maana Mungu hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. Hakuna mipaka kwa nguvu za msalaba. Waraka wa pili wakorintho 5:15 alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
Wanadamu hawawezi kubadilisha masharti ya wokovu. Tunajaribu sana. Unaona mahubiri wengi wanaweka vitu ambavyo Yesu mwenyewe hajasema. Kama walimu wa uongo waGalatia. Kama Mungu alivyosema katika neno lake ndivyo ilivyo. Lakini binadamu wanaweza kukataa masharti kama yalivyoandikwa na Mungu. Na tunaona hii kila siku ya maisha yetu, tunaona kila jumapili wakati watu wanakuja kanisa na ni wasioamini na wanasikia neno la Mungu na wanatoka kama waliingia. Watu ambao wanafanya hii hukumu yao itakuwa mbaya zaidi, kusema ukweli ingekuwa vizuri ikiwa hajasikia kitu cho chote. Angalia Wahebrania 10:29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? SI mchezo, na siku moja wakati unasimama mbele ya Mungu utasema nini? Ulikuwa na nafasi mingi sana na ulimkataa. Hata labda utasema lakini nilienda kanisa kila jumapili, niliimba kwa choir fulani, nilisaidia jirani yangu. Na Mungu atasema lakini hujaamini katika Mwana mwangu. Hujaweka imani yako kwake umeweka kwa kila kitu wewe umetenda. Hii ni kanuni Paulo anasema hapa kwa mstari yetu ya Wagalatia 6:16. Ni kukubali injili ya utimilifu wa Yesu kristo na dhabihu yake msalabani na kutembea kwa imani katika nguvu ya Roho Mtakatifu, Badaka ya nguvu na matendo yako. Ikiwa unafuata hii kanuni, wakati unasimama mbele ya Mungu siku moja utasikia maneno matamu kuliko maneno yote yaliyowahi kusema. Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Sisi sote tunataka kusikia hii siku ile lakini ni njia moja peke yake na ni Yesu kristo.
Paulo anaendelea kusema Kwa Wagalatia 6:16 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Tunaona vitu mbili kwa hii mstari kwa mtu ambaye anaishi kwa kanuni ya Mslaba wa Yesu kristo inaleta wokovu na si matendo yetu. Kitu cha kwanza ni Amani. Kial mtu ambaye anaishi kwa hii dunia anatafuta amani. Hii ni sababu unaona watu kutumia maisha yao yote kupata pesa, wanafikiri ikiwa wako na pesa kila kitu itakuwa sawa. Watu hata wengi hawawezi kulala usiku kwa sababu hawa na amani. Na ikiwa huna amani uko na nini? Wasi wasi. Na kwa sababu ya wasi wasi watu wanajaribu kujitoa kwa wasi wasi wao na wanaanza kunywa pombe au tumia dawa ya ulewi, wakati wanalewa wasi wasi inaenda, lakini shida ni baada ya masaa inarudi. Wanajaribu kujifurahisa na wanawake au wanaume lakini shida baada ya muda fupi wako na hatia tu na si hatia tu, labda ugonjwa au mimba. Bado hii wasi wasi inabaki na kila mahali unaenda iko pamoja nawe. Lakini kwetu ambao tumetubu kwa dhambi zetu na tumeweka imani yetu katika Yesu Kristo na ametupea wokovu wake ni tofauti sana. Angalia Wafilipi 4:6-7 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Amani ya Mungu haiwezi kununuliwa, haiwezi kupatwa kwa kanisa fulani, hawezi kupatwa na Pastor au prophet au Apostle au Reverned au mzungu fulani. Tunaona kwanza ni amani ya Mungu, ni yake na tunapata katika Yesu kristo na ni amani ambaye haiwezi toka kwa sababu ni ya Mungu. Kwa shida yo yote ninaweza kuwa na amani. Ukitaka amani kama hii, iko mbele yako, ni kutubu kwa dhambi zako na kufuata Yesu kristo.
Kitu cha pili tunaona kwa Wagalatia 6:16 kwa watu ambao wanaishi kwa hii kanuni ya Msalaba wa Yesu Kristo na si matendo yetu ni, iwe kwao na rehema. Ni kwa sababu ya rehema ya Mungu sisi tunaweza kuwa na amani, Ni mzuri sisi tushike kama tulikuwa na rehema ambaye Mungu ametupea. Angalia Waraka wa kwanza wakorintho 6:9-10 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,  wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Hii vitu ni mbaya sana, hakuna mtu anafanya vitu hivi anaweza kuingia ufalme wa Mungu. Angalia Wakolosai 3:5-6 vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. Hatuwezi kuingia ufalme waMungu na sasa tunaona tuko chini ya ghadhabu ya Mungu. Hii ni hukumu yake juu ya dhambi na hasira yake itakuja kwao ambao wanaishi kama hizi mistari yanasema. Mtu akiketi na anasoma vitu hivi na anajua nini inakuja kwake, angetetemeka na kusema Mungu nihurumie mimi mwenye dhambi. Hakuna tumaini lo lote kwetu wenye dhambi, mwisho wetu ni kuteseka chini ya ghadhabu ya Mungu kwa milele na milele na tunasoma waefeso 2:4-6 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, Hapa ni neno letu, rehema na hapa ni mahali mzuri kusema Bwana asifiwe kwa sababu ni ukweli, rehema yake ni mwingi. kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; Mungu kwa sababu ya rehema yake alituhuisha, akapumua pumzi ya uhai ndani yetu, pamoja na Kristo. Ajabu sana. Rudi kwa wakolosai 3. Baada ya hii orodha yote kusema ghadhabu ya Mungu inakuja kwa wana wa kuasi na vs.7 ya sema Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. Lakini kwa sababu ya rehema ya Mungu ametubadilisha na sasa vs.10 ya sema mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. Rudi kwa Waraka wa kwanza wakorintho 6. Baada ya hii orodha yote na watu ambao wanafanya vitu hivi hawawezi kuingia ufalme wa Mungu tunasoma kwa vs. 11. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; Mlikuwa ni kitu ya zamani, ilikuwa sisi zamani lakini si saa hii. Rehema ya Mungu ameleta kwetu ni ajabu na tunaona rehema ya Munngu inafanya nini kwetu lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
Hii rehema yote kwetu ililetwa kwa njia ya Msalaba, na Mungu alituma Mwanamwe peke, Yesu kristo, kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Sisi hatujastahili rehema yake na aneema yake na amani yake lakini hii yote ilikuja kwa njia ya Msalaba wa Yesu, si kwa matendo yetu. Lazima sisi wakristo tunaenenda kwa kanuni hiyo na tutajua tumepata rehema na hii italeta amani kwetu. Na pia kwa mwisho ya hii mstari yetu ya leo wagalatia 6:16 Paulo anasema Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Hii kwa Israeli wa Mungu ni wayahudi ambao wameweka imani yao katika Yesu kristo kwa wokovu na si sheria yao na matendo yao. Hawa ni wayahudi wa kweli, Israeli wa kweli wa imani kwa Masihi yao. Hakuna tofauti kwa mnyahudi au myunani . Lazima tunatubu kwa dhambi zetu na tuweke imani yetu katika Yesu Kristo kwa wokovu wetu na tufuate kama yeye amesema kwa neno lake.
Natumiani sana kitabu hiki cha Wagalatia imeguza maisha yako kama imeguza yangu. Imenileta kujiangalia sana, na kujipime maisha yangu na kutamani sana kufuata Yesu kristio na nguvu yangu yote. Ikiwa ukohapa leo asabuhi na hujui Yesu kristo na hujatubu kwa dhambi zako nitaomba tafadhali kuja mbele baada ya ibada yetu au kaa kwa kiti chako na wakati watu wote wanaenda nje ongea na mimi, nitapenda sana kuongea na wewe na kueleza zaidi kuhusu hii yote.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more