Introduction to John
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
Leo asabuhi tunarudi kwa kitabu cha Yohana. Tumekaa sana bila kuingia kitabu hiki. Nilienda US mwaka iliopita na wale wengine waliingia kitabu cha Wagalatia na tumekaa kwa kitabu cha Wagalatia zaidi ya mwaka moja, lakini ilikuwa tamu kabisa. Kablya nilienda Amerikani mwaka iliopita tulifika mlango wa tatu ya Yohana, lakini kwa sababu imekuwa kitambo kidogo nilitaka kuanza tena na kuchukua jumapili tatu au nne kukumbusha sisi ya vitu amabvyo tumeshaa angalia kabala ya tunaingia tena pole pole. Nitajaribu kufupisha mlango wa kwanza na mlango wa pili. Lakini leo asabuhi nataka kufanya Utangulizi tena kwa kitabu cha Yohana. Ni mzuri sisi tunajua mandhari ya kitabu kitabu hiki au sababu Yohana aliandika kama ameandika na pia Yohana alikuwa nani, kwamba tutaka kujua kama anasema. SIjui tutakuwa kwa kitabu cha Yohana muda gani lakini labda itakuwa miaka mbili. Lengo yangu kuingia kitabu hiki ni kusaidia sisi kujua Bwana wetu Yesu Kristo hata zaidi na kufuata yeye. Lakini hata Yohana ako na mandhari yake na kila wakati tunaangalia mstari ya kitabu hiki au tunaingia kusoma sana mstari ya kitabu hiki tunajua sababu Yohana aliandika kama ameandika.
Ukisoma Mathayo, Marko na Luka utaona vitabu vile vinafanana sana, lakini Yohana ni tofauti. Kwa kitabu cha Yohana hutaona siku za mwisho, hakuna Yesu kutoa mapepo, hakuna majina ya wanafunzi kumi na wawili, na hakuna meza ya Bwana. Pia huwezi kuona kuzaliwa ya Yesu, Ubatizo wake, majaribio yake, kuteseka kwa Golgotha na huwezi kuona wakati Yesu alitoka dunia. Kitabu cha Yohana ni tofauti. Ni muhimu sana tunashika Yohana ni tofauti lakini hakuna kitu ndani yake inapigana na Mathayo, Marko na Luka. Hii ni uzuri na ajabu ya Bibilia. Bibilia yote inaenda Pamoja na imeandikwa na watu wengi tofauti kwa miaka mingi. Unajua ilichukua miaka 1,500 kuandika bibilia. Na bado yote inaenda Pamoja. Hii inatuonyesha ni neno la Mungu, ni Roho Mtakatifu alitumia binadamu kuandika lakini ni maneno yake, hii ni sababu yote iko Pamoja. Watu ni wingi lakini Mungu ni moja.
Kitabu cha Yohana inatuonyesha vitu viingine hatuwezi kupata kwa Mathayo,Marko na Luka. Unajua unaweza kufika mahali mtu amegongwa na uko na watu ukiongea na hawa unasema nini imefanyika hapa? Watasema mtu amegonga huyu. Hii ni Story yao. Unauliza wengine na wanasema huyu amesema hii, na huyu amesmea hii. Halafu huyu amegonga wengine na wengine amefanya hii. Wako na maelezo mingi sana. Yohana ni kama hii anaeleza Zaidi. Yohana aliandika kitabu hiki miaka mingi baada ya Mathayo na Marko na Luka na alijua watu wake walijua vitu Hawa wengine waliandika. Ni kama tuko na habari inaelezwa zaidi kwa kitabu hiki cha Yohana.
Kama Mathayo na Marko na Luka hata Yohana hasiemi nani aliandika. Mtu anaitwa Iraneus, Na aliishi baada ya Yoahana alikufa alisema ni Yoahana aliandika kitabu hiki. Iraneus alikuwa mwanafunzi ya mtu anaitwa Polycarp na Polycarp alikuwa mwanafunzi wa Yohana. Hata wasioamini walihakikisha Yohana aliandika kitabu cha Yohana.
Hata tuko na mwalimu moja alikuwa fundi ya historia na yeye alisema hii kuhusu kitabu cha Yohana. 1. Mwandishi alikuwa Myahudi. Mwandishi ya kitabu hiki alijua sana mambo ya desturi la wayahudi. Alijua kuhusu Masihi, alijua umuhimu ya mafunzo rasmi ya kidini. Mwandishi alijua sana uhusuiano ya wayahudi na wasamaria.
2. Mwandishi alikuwa Myahudi wa Mpalestina. Hii ni kama kusema wewe ni Maasai lakini ni Maasai ya Sekenani. Labda Maasai ya Mau hajui hapa hawezi kusema ukienda center utaona hii nyumba na baada ya hii ni duka la Fulani. Hata mwandishi wa Yohana aliandika kuhusu vitu ambavyo huwezi kujua bila kuishi uko. Anaongea kuhusu vitu kama Bwawa la Bethesda, unakumbuka kila mwaka malaika atakuja na ataguza ile maji na mtu wa kwanza kuguza maji ameponya ya ugonjwa wake.
3. Mwandishi ya Yohana alikuwa shahidi wa macho. Aliona kila kitu aliandika kwa macho yake. Mwandishi ya kitabu cha Yohana alikuwa na maelezo mingi sana, Zaidi, kama mtu ambaye alikuwa uko, hajasikia hii story kutoka mwengine, alikuwa, ameona, amesika, ameguza. Vitu kama jina la baba ya Yuda Iskarioti, pia muda Lazaro alilala kwa kaburi, alikuwa na hesabu kamili. Pia huyu mwandishi aliandika mikate ule kijana alikuwa nai wakati Yesu alilisha watu elfu tanio ilikuwa mikate mi tano ya shayiri. Mathayo, Marko na Luka hawajaandika ilikuwa ya shayiri. Huyu alikuwa na maelezo sana. Pia alisema baada ya Mariamu aliweka nardo safi yenye thamani nyingi kwa miguu ya Yesu nyumba ikajaa harufu marhamu. Hakuna mwengie anandika hii. Huyu alikuwa hapo na akasikia harumu yeye mwenyewe.
4. Mwandishi ya kitabu hiki alikuwa mtume. Unaweza kuona wakati anaandika alijua na alisikia kama mitume kumi na wawili.
5. Mwandishi alikuwa mtume Yohana. Kwa kitabu cha Mathayo na Marko na Luka Unaweza kuona jina la Yohana Zaidi ya mara ishirini, na huwezi kuona hata mara moja kwa kitabu cha Yohana. Lakini kwa Yohana 21:20 Mwandishi anasema kitabu hiki iliandikawa na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu. Huyu Ni nani? Tunaweza kuona kwa chakula cha jioni ya Yesu Pamoja na wanafunzi kumi na wawili wake. Yohana 13:23 inasema Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda. Tunajua hii ni Yohana. Hata alikuwa Pamoja na Petro sana hawa walikuwa karibu. Hii ni sababu Petro aliuliza Yesu baada ya Yesu alimwambia yeye atateseka kwa jina lake alisema na huyu? Anaongea kuhusu Yohana. Kwa miaka elfu moja mia tisa hakuna shaka kwamba Mtume Yohana aliandika hii kitabu. Pia ni mzuri kujua Yohana Mbatizaji na mtume Yohana ni watu tofauti. Mara mingi wakatoi tunasikia Yohana tunaweka hawa wa waili pamoja na ni watu tofauti. Yohana Mbatizaji alikuwa binamu au cousin ya Yesu. Yesu alipenda sana pia Yohana Mbatizaji. Yesu alisema kumhusu Yohana Mbatizaji kwa kitabu cha Mathayo 11:11 nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; Hata tutaona Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu mbele ya Yesu Kristo na tunaona kwa Yohana 1:7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Yohana ambaye aliandika kitabu hiki ni Mtume wa Yesu na si familia wa Yesu. Mtume Yohana wanasema alikuwa mdogo wa mitume, alikuwa na ndugu anaitwa Yakobo, si Yakobo ambaye aliandika kitabu cha Yakobo. Lakini Yohana na Yakobo, Yesu aliita hawa jina liingine tunaona kwa kitabu cha Marko 3:17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; Hii ni maanisha Yohana na ndugu yake Yakobo walikuwa nguvu mingi sana. Wakati waliongea watu walisikia. Hawajaogopa kusema ulweli na tunaona hii wakati tunasoma Waraka wa kwanza, wa pili na watatu ya Yohana. Yohana alikuwa kali na ukweli alisema hajacheza naye. Kwa mfano unakumbuka Waraka wa kwanza wa Yohana 3:7-10 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, Hawajaogopa kusema ukweli, hajacheza na maneno yake. Na siku zile kama siku zetu watu hawataki kusikia hii ukweli. Sisi tunahitaji watu kama Yohana siku zetu, tunahitaji Mapastor kuongea kama yeye.
Steve Lawson ni mhubiri moja mimi ninapenda sana, na yeye alisema tunahitaji wanaume wanaohubiri neno la mungu, wanaume ambao wanapokuja kwenye mimbari hawajishindi na skirti yao, wanaume ambao wasioogopa kusema ukweli wa Kristo. Yohana alikuwa mfano mzuri ya hii. Na Yohana alikuwa naa m na hiyo kwa sababu alisikia na aliona Bwana wake kufanya hii. Kumbuka Yohana aliandika kuhusu Yesu kuongea na wayahudi ambao walitaka kumshika na kumwua yeye kwa Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. Hata sisi tuko na neno la Bwana wetu, sisi pia tunaweza kuwa na hii uwezo kuongea kama amesema.
Kitabu hiki kiliandikwa kati ya mwaka themanini ku tisini. Karibu miaka hamsini baada ya Yesu alikufa na karibu miaka ishirini baada ya Petro alikufa. Na aliandika hii kitabu wakati aliishi kwa Kijiji ya Efeso. Kumbuka mitume yote walikuwa tayari wameuawa. Ni Yohana peke yake alibaki. Kwa historia watu wanasema Yohana alikuwa kiongozi wa kanisa la Waefeso hata tunsaoma kwa waraka wa tatu wa Yohana 1:1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Hajajiita Mtume au Apostle alijiita mzee. Mzee hapa ni kama alikuwa pastor au kiongozi wa kanisa. Imagine mtu ambaye ni Apostle wa kweli wa Yesu amefanya miujiza ya kweli na hajajiita Apostle. Ni mzuri hawa wa wakati wetu wasome hii. Lakini kumbuka kama Yesu aliita Yohana na ndugu yake Yakobo Boanerge, wana wa ngurumo. Bila shaka Yohana alihubiri uwkeli wa Yesu na nguvu sana na viongozi wa Roma hawajapenda kama anasema. Tunaweza kusoma kwa waandishi wengine walijaribu kumwua Yohana walimtupa katika mafuta yanayochemka halafu walijaribu na sumu lakini hajakufa. Baada ya hii Yohana alipelekwa uhamishoni kewenye kisiwa kiitwacho Patmo. Patmo ilikuwa mahali walituma watu wabaya, wahalifu. Na ilikuwa hapo aliandika kitabu cha Ufunuo.
Maana ya kitabu cha Yohana. Ni mzuri wakati tunasoma barua au kitabu tunajua sababu mwandishi aliandika. Kwa vitabu vyote vimeandikwa kwa bibilia kitabu cha Yohana alisema wazi sababu ya kitabu chake. Angalia Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Wakati sisi tunasoma kitabu cha Yohana ni mzuri kukumbuka hii kila jumapili. Lengo yake ya kuandika hii ilikuwa kwetu kuamini kwamba huyu mtu anaitwa Yesu, alikuwa Kristo, Masihi na alikuwa Mwana wa Mungu mwenyewe, na tukiamini hii tutakuwa na uzima kwa jina lake. Hata Yohana alitumia neno kuamini Zaidi ya mara mia moja kwa kitabu hiki. Hii ni sababu mara mingi wakati uko na mtu na anataka kujua Zaidi kuhusu Yesu au wokovu tunamwambia hawa enda na soma kitabu cha Yohana. Yohana anasema kwa watu ambao wanaamini watapokea uzima wa milele.
Kwa sababu Yohana alitaka watu ambao watasoma kitabu chake kuamini Yesu alijaribu sana kutuonyesha kwamba Yesu ni Mungu, Masihi, na Mwokozi wa uliwengu. Hii ni sababu kwa kitabu hiki tunaona Yohana kuandika sana kuhusu miujiza ya Yesu. Hata tutaona miujiza nane amefanya na hii ni Zaidi ya Mathayo, Marko na Luka. Tutaona Yesu kugeuza maji kuwa divia, kupona mwana wa maafisa wa kifalme, akiponya kiwete katika ziwa la Bethesda, kulisha watu elfu tano, alitembea juu ya maji, aliponyesha mtu ambaye alizaliwa kipofu, kufufua Lazaro, na pia kuvuta Samaki ambaye ilikuwa miujiza. Na Zaidi ya hizi miujiza yote ni ufufuo wa yesu mwenyewe. Yohana aliandika vitu hivi na hajakuwa na shaka yo yote kwamba Yesu alikuwa Kristo, alikuwa Mungu. Yohana aliona hii yote na macho yake. Angalia kama Yohana alisema kwa Waraka wa kwanza wa Yohana 1:1-3 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; Hii yote kusema Yohana alikuwa. Hii habara si habari amesikia, aliona, aliguza, alisikia. Kwa habari ya neno la uzima. Hii ni nini au nani? Ni Yesu Kristo. Angalia Kitabu cha Yohana 1:1-4 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Hii ni Yesu kristo.
Tutaona Yohana kusema Yesu ni neno la milele, Masihi na mwana wa Mungu na kwa njia ya kifo na ufufuo wake ameleta wokovu kwa binadamu, watu hujibu hii yote kupokea au kukataa hii wokovu ambaye inakuja kuamini yeye. Kitabu hiki wakati tunamaliza na labda itachukua muda lakini utajua kama Yohana amesema kuhusu Yesu kristo.
Sasa, lazima niulize, wewe uko wapi na hii yote? Wewe unakataa Yesu au umeamini? Hakuna njia ingine ya kuokolewa ni kuweka Imani yako katika Yesu kristo na Maisha yake aliishi na kazi yake alitenda na kuamini alifufuka. Hakuna swali liingine unaweza kujiuliza ni muhuimu zaidi ya hii. Lakini inabidi sisi sote tujiuliza tunaamini nini kuhusu huyu mtu anaitwa Yesu. Ikiwa hujafanya hii na unataka kuongea Zaidi tafadhali ongea na sisi baada ya ibada leo.
Kwangu mimi niko na furaha kuingia kitabu hiki na kuona itabadilisha Maisha yako naam na gani, maisha yangu naam na gani na maisha yetu kama kanisa naam na gani. Haitakuwa fupi, lakini najua baadaye sisi tutakuwa karibu na mwokozi wetu Zaidi. Baada ya hii tunaweza kueleza kwa wenzetu na Jirani yetu Zaidi. Karibuni sana wiki ijayo natutaingia mlango wa kwanza.
Asanteni sana na Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe.