Jesus Christ
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 11 viewsNotes
Transcript
John 1:1-2
John 1:1-2
Leo tunaingia masomo yetu ya kitabu cha Yohana. Wiki ilioptia tuliangalia utangulizi ya kitabu hiki natumaini sana unakumbuka lakini Zaidi nataka ninyi kukumbuka sababu au lengo ya Yohana kuandika Hii, ilikuwa kwa Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Kwa hii mafundisho yote ya kitabu cha Yohana jaribu kukumbuka hii. Kila mstari tutaona hii ilikuwa lengo ya Yohana kwa wwasomaji wake kufahamu.
Wiki iliopita nilisema tutachukua jumapili tatu ama nne kutukumbusha ya mlango wa kwanza na ya pili halafu tutarudi mahali tulikuwa kablya nilitoka kuenda Amerikani. Pole sana kwa sababu wakati niliketi kusoma mlango wa kwanza na ya pili tena nimesema ni mzuri tuanze mpya. Kila mstari imejaa na ukweli wingio sana na mimi sitaki sisi kukosa hata kitu kidogo. Lengo yangu ni kwamba tutajua Mwokozi wetu zaidi sana na kuangalia vitu hivi vizuri itasukuma sisi kutembea karibu sana na yeye. Ni ajabu sana kufikiri, mimi na wewe tunaweza kuwa na uhusiano na Muumba ya kila kitu, hata zaid kwamba atatuita ndugu na dada kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu ikiwa tumeweka imani yateu katika Yesu kristo.
Kufungua kitabu chake Yohana anatumbia ukweli wazi kabisa na anasema vizuri sana hata mtoto anaweza kushika, lakini wengine wako smart kabisa na hawawezi kushika, hii ukweli ni hii, Mungu alikuwa bindamu na alifanya hii katika Yesu Kristo. Hii ukweli ni manthari ya kitabu cha Yohana na tunaona hii kwa Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, hii ni Yesu Kristo.
Yesu alikuwa Mungu ni ukweli moja ya Imani ya ukristo ambaye hakuna shaka. Ikiwa huamini hii wewe si Mkristo. Tunaweza kuona mistari mingi sana ambaye yanatuonyesha Yesu alisema yeye na Mungu ni mmoja. Lakini Yesu Kristo ni Mungu. Ikiwa hajakuwa Mungu alikufa bure msalabani, ikiwa yeye si Mungu hajafufuka kweli kweli, na ikiwa yeye si Mungu Maisha yake hapa kwa hii dunia ni bure, ikiwa Yesu si Mungu yeye si mwokozi wetu na sisi hatunatumaini lo lote kwa maisha haya na maisha ambaye inakuja. Kwa sababu sadaka kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alitaka ilikuwa kondoo kamili asiye na doa. Yesu Kristo alikuwa hii, alikuwa kamilifu bila dhambi yo yote. Alikuwa binadamu kabisa na alikuwa Mungu kabisa.
Unajua siku zetu unaweza kusema karibu kitu cho chote kuhusu Yesu, lakini huwezi kusema yeye ni Mungu. Watu wa siku zetu kama siku za Yesu wanasema kusema Yesu ni Mungu ni kukasirisha hawa. Ikiwa mtu anaamini Yesu ni Mungu halafu ni lazima kama anasema ni ukweli. Ukiamini Yesu ni Mungu halafu unahakikisha dini nyingine zote ni uongo na Ukristo ni ukweli peke yake. Hii ni kama Yohana anafundisha kuanzisha kitabu chake. Wengi wanasema hizi mistari tano ya kwanza ni ajabu na vya kupendeza katika bibilia nzima. Hakuna mistari ziingine zinatuonyesha uungu na ukuu wa Yesu Kristo kama hizi mistari tano.
Kwa kitabu cha Yohana 1:1-5 Yohana anaweka misingi ya kitabu chake kwamba Yesu kristo alikuwa Mungu. Watu wengi kwa dunia yetu wanakataa kabisa kama hizi mistari tano yanasema. Lakini kwetu wakristo ni imani muhimu zaidi ya imani yetu. Bila kuamini hii wewe si Mkristo. Na leo tutaanglaia vizuri mstari ya kwanza na ya pili. Tusome kwa muktadha yao. Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kitu cha kwanza tunaona Yohana kusema ni vs.1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno,. Yohana anasema hapo mwanzo. Mwanzo ni wapo? Ni kma tunasoma kwa kitabu cha Mwanzo 1:1 Hapo Manzo. Na yahona naasema Kulikuwako Neno. Hapa Yohana anaongea kuhusu nani? Angalia Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Ananongea kuhusu Yesu kristo. Ni ajabu sana kuona. Yesu Kristo alikuwa hapo mwanzo, alikuwa kabla ya kila kitu imekuwa. Neno hajaanza wakati. wakati ulianza, si kitu ambacho iliundwa na Yesu si mtu ambaye ako na muumbaji. Neno Alikuwa kabala ya wakati, Neno Alikuwa umilele uliopita. Na wakati tunasoma Yesu Kristo alikuwa neno inatuonyesha yeye ni Mungu kwa sababu ni mtu moja ni wa milele na ni Mungu. Watu wengi wanasema Yesu alizaliwa na hii ni wakati alianza lakini hii ni uongo sana. Mungu alizaliwa na mwanamke ili anaweza kuwa kama mimi na wewe, kwa mwili, alikuwa na ngozi na alizaliwa kwa hii dunia kama sisi lakini hajatenda dhambi hata mara moja. Labda unakumbuka wakati malaika aliongea na Mariamu na alimwambia yeye ataita mtoto wake Immanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Ni Yesu alichagua hatua hiyo na wakati katika historia na kwa njia ya mwanamke gani atazaliwa. Si kama mimi na wewe, mimi sijachagua mama na baba yangu au nchi nitazaliwa. Yesu alichagua, Ilipangwa kabla ya misingi ya dunia. Yesu alikuwa mpango ya Mungu, Alikuwa njia Mungu alipanga kuokoa watu watu wke kutoka dhambi zao. Na ilikuwa kwa njia ya kifo chake, kwa msalaba. Hii ni sababu Yesu alizaliwa wakati waroma na kama waliua watu. Kwa kitabu cha Ufunuo tunaona watu walianza kuabudu Yesu wa uongo na tunaona kitu cha jabu sana, Anglia Kitabu cha Ufunuo 13:8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Umeona ile ya mwisho? Aliyechinjwa tangu lini? Tangu Waroma walimshika? Kabla ya Makuhani walimweka kwa majeshi ya Waroma, Kabla ya Yuda alimsaliti? Tangu kuwekwa msingi ya dunia. Ilikuwa mpango kabla ya mwanzo.
Tumeshaa sema Yesu alikuwa Neno. Tunaona Yohana anaendelea kusema kwa Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, Walikuwa pamoja. Sasa tunaanza kuona mafundisho ya utatau. Mungu moja lakini ni tatu tofauti, na sisi tunajua hii ni Baba, Yesu na Roho Mtakatifu. Kumbuka kama tulisema, hakuna kitu ni ya umilele ili Mungu. Unakumbuka kwa umbaji wakati tunasoma Mungu aliumba binadamu kwa kitabu cha Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; Mungu anaongea na nani hapa? Yesu na Roho. Ni mzuri kukumbuka Bibilia inatuambia Mungu ni Roho, hana mwili, huwezi kuona Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu na ni Roho, hana mwili, huwezi kuona yeye. Yesu Kristo ni Mungu na ni mwili na tumeumbwa kwa sura yake. Lakini Neno alikuwako na Mungu ni zaidi ya kama tunashika hapa. Yesu alikuwa pamoja na Baba na walikuwa na Usharika kamili, upendo kamili, walikuwa uso kwa uso, walikuwa sawa bila sisi, bila hii dunia, bila kitu cho chote nje. Furaha kabisa ilikuwa. Na ni ajabu kufikiri Yesu alitoka mahali yake na Mungu, alijitoa na hii yote na tunasoma wafilipi 2:7-8 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa nini? Kwa ajili ya dhambi zetu na wakati tunapokataa hili tunamtemea Mungu mate usoni na tnampiga makofi usoni. Natumaini sana unaona sababu wakati sisi tunakataza Yesu kristo kuwa Bwana wa maisha yetu ni mbaya sana, wakati watu wanachafua wokovu wa Yesu ni mbaya sana.
Yohana anaendelea kusema kwa kitabu cha Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Ikiwa umekuwa na shaka yo yote, Yoahan anatoa hapa, anasema Naye Neno, na neno ni nani? Ni Yesu, Naye neno alikuwa Mungu. Kwa madini yote ya hii dunia wako na shida zaidi na hii wakati sisi wakristo tunasema Yesu alikuwa Mungu. Hawataki kusikia hii, hawataki kuamini hii, hata wayahudi saa hii, ukienda na unasema Yesu ni Mungu, alikuwa Masihi, watakasirika sana. Waisalmu, hawana shida na Mungu lakini ukisema Yesu alikuwa Mungu, shida mingi inaingia. Lakini Yohana aliona na alisema Yesu Alikuwa Mungu, Neno Alikuwa Mungu na naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, hii mwili ilikuwa mwili wa Yesu.
Uko na wengine wanasema Yesu alifika kwa hii dunia wakati alizaliwa, kweli? Tuangalia kidogo kuhakikisha ikiwa hii ni ukweli. Wakati tunasoma agano la kale na tunaona Watu wanaongea na Mungu,wanaongea na nani? Kumbuka Mungu Baba ni Roho. Labda unakumbuka wakati Musa alikuwa jangwani na anachunga mbuzi na kondoo na tunasoma kwa kitabu cha Kutoka 3:2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Halafu vs.4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! NA Musa na Mungu wana mazungumzo. Ni ajabu sana! Halafu tunafika vs.13 na Musa anasema Unanituma kwa wana waisraeli kama Mungu wao na Musa anasema wakati wananiuliza jina lako nitasema nani? Vs.14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu. Tunaona Mungu anasema waambia MIMI NIKO, hii ni jina lake. Na hii ni miaka 1350 kabla ya Yesu alizaliwa.
Halafu tuko na Ibrahimu unakumbuka wakati Mungu alikuja kwa Abrahamu kumwambia yeye ataharibu Sodoma na Gomorrah? Tunaona kwa kitabu cha Mwanzo 18. na kwa vs. 1-2 Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, Halafu ukiendelea kusoma hii mlango unaona mara mingi inasema Bwana, akamwambia, si malaika alisema. Bwana, hapa ni jina la Mungu Yahweh. Abrahamu anaongea na Mungu lakini kumbuka Mungu ni Roho, hii Mungu ambaye ako na mwili ni nani?
Angalia Yohana 8:56-59 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Ukotayari? MIMI NIKO! Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. Kwa nini walitaka kupiga Yesu na mawe? Kwa sababu alisema Mimi Niko, I AM. Hii ni jina la nani? Ni jina la Mungu alijita kwa agano la kale, lakini tunaona hapa Ni kama Yesu na Abrahamu walijuana na hata kama wayahudi walisema Yesu hajakuwa miaka hamsini na alijua Abrahamu naam na gani? Abrahamu aliishi miaka elfu mbili kabla ya yesu alizaliwa. Na Bibilia ni wazi kabisa kwamba Mungu ni Roho, na huwezi kuona Mungu, Yesu ni Mungu. Huwezi kupata ikuwe wazi zaidi ya kama Yohana alisema kwa Yohana 1:1. Yesu hajakuwa Mungu mwengine, alikuwa Mungu.
Yohana anarudi kuhakikisha tena kama ameshaa sema kwa Yohana 1:2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Huyo, Yesu, nilitembea naye, nimesikia suati yake, nimeona na macho yangu miujiza alifanya, huyo rafiki yangu, niliketi naye, nilikula naye nilicheka naye, alikuwa Mungu, alikuwa mwanzo kwa Mungu. Hana mwanzo hana Mwisho na alitembea nasi hapa. Alisema kwa Yohana 10:30 Mimi na Baba tu umoja. Ajabu! Angalia vs.31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. Kwa nini? Kwa sababu kusema hii ni kusema Yesu ni Mungu. Yeye na Baba yake ni Mmoja.
Hii mafundisho ya Yesu alikuwa Mungu ni muhimu sana na kwetu wakristo hakuna shaka hakuna kati kati kwa hii. Hata waraka wa pili wa Yohana 1:10 anasema Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, mafudisho hayo ni nini? Ni mafundisho ukweli kuhusu Yesu na kwamba amekuja na yeye ni nani, Ikiwa uko na watu kama hii tufanyaje? Hata msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Mafundisho kuhusu Yesu na yeye ni nani si mchezo na ni msingi ya Imani ya Mkristo. Ikiwa uko na shaka kuhusu hii, au hujui, halafu Yesu yako hana nguvu kukuleta wokovu, kwa sababu siku ile Yesu Kristo alikufa mslabani, ikiwa hajakuwa Mungu wakati alikuwa hapa nasi na hajakuwa binadamu halafu Yesu Kristo na kifo chake haiwezi kusaidia sisi. Alikuwa binadamu kabisa na Mungu kabisa. Alikuwa pamoja na Mungu walikuwa moja na alitoka mbinguni kuwa kama sisi. Mwokozi wetu si kama miungu miingine, anajua sisi kwa sababu alikuwa kama sisi lakini bila dhambi.
Wakati ninaketi na ninafikiria hizi mistari ya Yohana 1:1-5 ninashangaa. Mungu, Yesu, Ameniokoa, Alinichagua kuwa mtoto wake, alinitoa kutoka ufalme wa giza na amenileta kuingia ufalme wake wa nuru. Alifanya hii kwa njia ya kifo chake, kifo cha uchungu mslabani. Ikiwa mtu alikuwa na shaka yo yote kwmba Yesu alikuwa Mungu, baada ya siku tatu alitoa shaka yote wakati alishinda kifo na mauti na alitoka ile kaburi. Wakati ninasoma hizi mistari ninshangaa kwa sababu Huyu Yesu ya hizi mistari ni Bwana wangu, na kwa sababu ya neema na rehema yake ninafuata yeye.
Wewe unaweza kusema hii? Leo asabuhi, wewe unajua huyu Yesu? Natumaini sana hujui Yesu ya hii dunia na walimu wa uongo lakini unajua Yesu ya Bibilia, Yesu kama Yohana alijua na aliandika. Ikiwa hujui yeye, tafadhali baada ya ibada yetu karibu hapa mbele au keti kwa kiti chako na tutaongea na wewe. Ikiwa uko na maswali tafadhali uliza, ikiwa ukodhambini, tafadhali tubu na rudi kufuata Bwana wako.
Asanteni Sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
