Jesus Christ Pt.2

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

John 1:3

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yoahan na tumefika mlango wa kwanza mstari wa tatu. Kumbuka sababu Yohana aliandika kitabu chake. Alituambia wazi kabisa kwa Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Kwa sababu ya hii tunajua kila kitu tunasoma, lengo ya Yohana ni kuweka macho yetu kwa Yesu na kutuonyehsa kwamba alikuwa Masihi, Mungu na kwetu kuamini na kupata uzima kwa jina lake. Wiki iliopita tulianza kuangalia maajabu ya Bwana wetu yesu kristo. Hakuna mahali ingine bibiliani nzima ni wazi kama hapa kuhusu Yesu na Uungu wake. Yesu Kristo ni Mungu na ikiwa hujashika hii au hujaamini hii, bado wewe ni msioamini na uko na shida kubwa mbele yako. Tuliona Yohana kusema Yesu alikuwa neno kwa Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Hii ni Yesu. Na wiki iliopita Yohana alisema neno hili lilikuwa mwanzo hata ilikuwa na Mungu na ilikuwa Mungu, Yesu kristo ni wa milele, hana mwanzo, hana mwisho.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake. Kitabu cha Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Hii ni neno la Mungu wetu kuhusiana na Yesu.
Tuombe:
Nigependa sana ikiwa kila siku hii wiki ambaye iko mbele yetu ikiwa ninyi yote utasoma hizi mistari ya Yohana 1:1-5 kila siku, labda wakati unaamuka asabuhi au kabla ya unalala usiku. Kisha fikiri juu ya mambo yanayosemwa. Ni ajabu sana kufikiri ule mtu Yohana anaongea kuhusu ni Bwana wangu, ananiita rafiki. Unajua mara mingi nimesema hapa Kenya kila kitu inategemea watu ambao unajua, ni ngumu sana kufanya vitu bila kujua mtu. Sasa sisi tunajua Yesu kristo na yeye anatuita rafiki. Sisi hatujampea yeye kitu kidogo, au chai au kitu kiingine na yeye ni Mungu wa kila kitu. Angalia kama Yohana anasema kwa Yohana 15:14-15 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Bwana wa kila kitu anatuita rafiki zake. Huyu rafiki yetu si kama wengine. Yeye ni mfalme wa mifalme na Bwana wa mabwana na yeye si kama mtu kwa ofici ambaye leo ako na kesho ametoka, Yesu Kristo atatawala milele. Ikiwa Yesu kristo hajakuita rafiki wewe uko na shida.
Rafiki yetu, anamiliki kila kitu. Tunaweza kusema hii naam na gani? Kwa sababu ya mstari yetu ya leo. Yohana 1:3 Vyote vilifanyika kwa huyo; Hapa Yohana anaendela kueleza kuhusu Yesu. Yohana hapa anasema Yesu aliumba kila kitu. Nani ni umbaji wa kila kitu? Mungu, Tena Yohana anatuonyesha kwamba Yesu ni Mungu. Tunaona mistari mingi kwa bibilia inasema Mungu aliumba kila kitu. Mwanzo 1:1 inasema nini? Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Yeremiah 32:17 Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza; Ni mingi sana na tunajua ni Mungu aliumba kila kitu. Hapa Yohana anasema ni Yesu. Kumbuka kwa umbaji Tunaona Baba Mungu anaongea na mwengine angalia Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Anaogea na nani? Yesu na Roho Mtakatifu. Vs. 2 tumeshaa ona Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Hii ni Roho Mtakatifu, na Baba ni Roho pia huwezi ona roho, na ikiwa Mungu anasema tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu hii ni nani? Nani ako na sura kwa utatu? Ni Yesu.
Sasa ni ajabu sana kufikiria mtu ambaye anatuita rafiki Vyote vilifanyika kwake. Nimesikia kitambo mtu aliniambia una marafiki wenye nguvu, na hawa wanaongea kuhusu binadamu kwa ofici fulani, wanakuja na wanaenda. Lakini kweli kweli niko na rafiki ambaye ako na nguvu zaidi ya kila mtu na kila kitu, yeye ni mfalme wa kila kitu. Hata siku moja tumeambiwa kwa Wafilipi 2:10-11 kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. KWa nini hii itafanyika? Kwa sababu yeye ni umbaji wa kila kitu na kila mtu. Vyote vilifanyika kwa Yesu. Anastahili sifa zote.
Ukiangalia dunia yetu saa hii huwezi fikiri ni kitu kizuri sana. Lakini ni mzuri unajua hii dunia tunaishi saa hii ni tofauti sana, si kama wakati Mungu aliumba mwanzo. Mwanzo 1:31 ya sema Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Halafu dhambi iliingia kwa njia ya Adamu na Hawa na iliharibu kila kitu hata umbaji. Siku moja Yesu atakomboa watu ambao wameweka Imani yao katika yeye, lakini pia atakomboa umbaji. Warumi 8:19-21 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Siki moja wakati laana ya hii dunia imeondolewa itakuwa tofauti sana. Nataka ninyi kusikiliza Isaya 11:6-8 anaongea kuhusu siku ile wakati Yesu atarekebisha kila kitu Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Halafu Isaya 65:25 Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.
Ni ajabu kufikiria siku ile lakini kama tumesoma ni siku ambaye Yesu amekuja na laana ya dhambi imetoka dunia na umbaji itakuwa kama amesema kwa Mwanzo, ni chema sana. Tena tunaona Yohana anatuonyesha Yesu kristo ni Mungu. Yesu Kristo, Neno la milele, aliumba kila kitu ambaye imekuwa. Angalia Wakolosai 1:16-17 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Bwana wetu ni ajbau. Yesu ni Mungu. Katika yeye vitu vyote, hii ni kila kitu, hakuna kitu ambacho iko, imeumbwa nje ya Yesu. Hata vitu amabvyo hatuwezi kuona. Hata mifalme, rais, falme, mamlaka, hii yote imeumbwa katika Yesu na ukiona vs.17 vyote hushikana katika yeye. Ni kwa sababu ya yeye hata vitu hivi vinaweza kuendelea. Ukitoa Yesu hata kwa sekunde moja kila kitu itakuwa machafuko. Haitaendelea. Na ni ajabu kwetu huyu ni mwokozi wetu, ni Bwana wetu na anatuita rafiki. nani atakataa rafiki kama hii? Na kila siku zaidi ya watu bilioni sita wanaishi maisha yao kinyume na Kristo. Wanakataa hata yeye ni ukweli. Ni Neema kubwa sisi tumepokea kujua Yesu, Ni baraka kubwa Yesu alifungua macho na masikio yetu kuona na kusikia ukweli wake, alibadilisha mioyo yetu na alitutoa kwa ufalme wa hii dunia ya giza na ametuleta kwa ufalme wake. Rehema yake ni ajabu.
Lengo yangu ni kama lengo ya Yohana. Nataka ninyi kuona nje ya Yesu Kristo na kukaa hapo ni bure kabisa. Yesu ni sababu ya maisha haya. Kwa familia yako, kwa ndoa yako, kwa kazi yako, kwa watoto wako. Ikiwa Yesu ni Bwana ya hii yote utashangaa. Familia yako watakuwa tofauti, Ndoa yako itakuwa kitu ambacho wengine hawawezi kuamini. Unajua wewe na bibi au bwana wako ni wenye dhambi wa wili na sasa umekuwa pamoja, lakini ikiwa kumpendeza Yesu ni lengo yengu ninyi wa wili, itakuwa kitu chema zaidi. Ni mzuri kabla hujafunga ndoa na mtu unaketi na unakubaliana malengo ya ndoa yako na ikiwa Yesu si kati kati ya kila kitu, toka hii haraka na pata mtu ambaye ataweka Yesu kwanza. Bwana wewe si kwanza kwa ndoa yako, Yesu ni kwanza, Bibi, wewe si kwanza kwa ndoa yako, Yesu ni kwanza. Watoto wenu si kwanza kwa maisha yenu, Yesu ni kwanza. Kwa kazi yako ikiwa Yesu ni kwanza utashangaa. Lengo yangu na si rahisi kwa sababu bado tunadeal na wasioamini wingi ni kwa Ten 31 kuwa kama jina lake inamaanisha. Waraka wa kwanza wakorintho 10:31 mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. Yesu Kristo ni kwanza kwa kazi yetu, hii ni lengo yangu. Hata kwako, lengo ya kazi yako ni nini? Ni kwako kuwa na vitu vingi, au ni kutumia kama uko nai kuleta utukfu kwa Bwana wako? Kila kitu ni yake. Tumeshaasoma katika yeye vitu vyote viliumbwa, kila shilingi, kila dola, hata nguvu yako uko nai ni zawadi kutoka yeye. Tumia hata nguvu yako kwa utukufu wake.
Kumbuka lengo ya Yohana na sababu aliandika kitabu hiki kuamini Yesu ndiye Kristo na kaumani utakuwa na uzima. Bila kuamini hii hunatumaini lo lote, kwa maisha haya na maisha ambaye inakuja. Bila kuamini Yesu kristo si rafiki yako, si mwokozi wako na utasimama mbele yake siku moja hukumuni, na huwezi kuweka imani yako katika yeye siku ile, italzaimishwa kuamini lakini umeshaa chelewa. Ukiweza kufikiria mtu mbaya sana unajua saa hii? Huyu mtu ni mbaya zaidi, labda maisha yake ni chafu sana, hata yeye siku moja atapiga magoti mbele ya Yesu atamkiri kwamba yeye ni Bwana. Fikiria mtu ambaye ni mtajiri, hana shida yo yote kwa maisha haya, hata yeye siku moja atafanya hii pia. Yesu ni Bwana wa kila kitu na kila kitu ambaye iko imekuja kwa njia yake.
Yohana anaendelea kusema kwa Yohana 1:3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. tena Yohana anasema nini hapa? Yesu ni Mungu. Yesu ni mtu ya pili kwa utatu. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Wote wako sawa sawa, hakuna moja ako juu ya mwengine. Najua watu hapa wanafikiri lazima kwa sababu ni Baba yeye ni mkubwa, hapana. Ikiwa moja ni juu ya mwengine halafu uko na miungu mi tatu na Mungu wetu ni moja na hata kuabudu Mungu mwengine inavunja amri zake. Yesu ni Mungu na ametuonyesha Baba yake kwa mwili alisema. Anagalia Yohana 10:30 Mimi na Baba tu umoja. Huwezi kuwa moja na baba na kuwa chini yake. Wewe ni moja, sawa sawa na kila kitu lakini kazi tofauti. Mungu Baba ni muumbaji, lakini Yesu an Roho walikuwa pia. Yesu ni Mkombozi, lakini Baba na Roho walikuwa pia. Roho ni Masaidizi, Mwenye kutakasa, lakini Baba na Yesu wako pia. Tunaweza kuongea zaidi siku ingine kuhusu vitu hivi lakini ni muhimu sisi tunashika kwamba Yesu ni 100% God. Hii ni vita tunayopigana hapa duniani. Watu hawataki kubali kwamba yesu ni Mungu. Wakikubali Yesu ni Mungu halafu kila kitu alisema kwa neno lake ni ukweli na watu wako na shida kubwa na hii. Kwa sababu kama wanasihi maisha yao na kama wanaamini iko na matokeo kubwa. Hukumu iko mbele yao na bila kuamini na kuweka imani yao katika Yesu watasimama kuhukumiwa mbele ya Mungu.
Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Kusema hii iko na nguvu sana. Yesu ni mwenye mamlaka, yeye anatawala juu ya kila kitu, kila mtu, ni yeye anastahili ibada yetu, na ibada yetu ni kumpea maisha yetu kwa ajli ya utumishi wake, kwa ajili ya kazi yake, kwa makusudi yake. Lazima ninauliza, nje ya Yesu, utaenda wapi? Utaenda kwa nani? Utaweka imani katika nini? Nani au nini inaweza kukuokoa kutoka dhambi zako na hukumu ambaye inakuongojea?
Leo asabuhi Ikiwa hujui Yesu, hujui Mungu, na hunatumaini kwa maisha haya au maisha ambaye inakuja, lakini leo uko na nafasi kuamini na kujua Yesu Kristo, kuitwa rafiki yake. Ikiwa unataka kuongea zaidi tafadhali baada ya ibada yetu kuja mbele au keti kwa kiti chako na wakati watu wametoka tutaongea. Ikiwa uko na maswali au unatako kuongea tu tuko hapa.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more