Jesus Christ Pt.3

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 5 views
Notes
Transcript

John 1:4

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumwfika vs.4 ya mlango wa kwanza. Kusema ukweli kwa wiki mbili tunaweza kusema ni masomo yetu kuhusu Yesu Kristo. Hakuna Mtu au kitu kiingine ni tamu zaidi kufundisha kuhusu kuliko Bwana wetu Yesu kristo na kumbuka Kitabu hiki ya Yohana na lengo yake alitueleza vizuri sana. Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Ninaweza kusema tutakuwa kwa kitabu hiki kwa miaka mingi lakini Lengo yangu ni kama Yohana alisema tutajua Yesu Kristo.
Kwa siku zetu tuko na watu wengi wanafundisha uongo wingi zaidi kuhusu Bwana wetu, wingi wanadannga kumhusu yeye, wengine wanatumia jina lake kupata pesa, mamlaka na mambo mingi. Kanisa la yesu Kristo limekuwa biashara na kwetu watoto wake, Marafiki yake Tunataka kujua yeye kama neno lake linasema. Hakuna utafiti ni muhimu zaidi ya kujua Yesu kristo ni nani na neno lake linasema nini kumhusu yeye. Watu wanatumia maisha yao yote kutafuta majibu kuhusu vitu vya hii dunia, na mimi niko na shukrani kwa watu wale kama madaktari, na wengine ambao wanasaidia ubora wa maisha yetu. Lakini hakuna mtu anaweza kuongeza masiku kwa maisha yetu kupita kama Mungu amepanga. Milele iko mbele ya kila mtu ambaye wanaishi saa hii, wengine kabala ya sisi ambao wameshaa enda, wameingia milele tayari, hatuwezi kusaidia hawa lakini kwa wale amabo wako saa hii bado tumaini liko. Hii ni sababu kwetu Wakristo ni muhimu sana tunajua kila kitu tunaweza kujua kuhusu huyu mtu anaitwa Yesu. Sisi wakristo tuko na jukumu juu yetu kueleza kuhusu Yesu kwa kila mtu tunajua. Familia yetu, marafiki yetu, jirani yetu kila mtu. Tunapata habari yake bibliani na zaidi kwa injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Kwa vitabu hivi nne tunapata kuhusu wakati ametembea hapa na binadamu, na vitu ambavyo alisema na alitenda.
Unajua ni kitu moja kila mtu dunaini nzima wanatafuta, unajua ni nini? Uhai. Watu wanataka kuishi, na watu wanatafuta hii mahali mingi sana, labda hata wewe saa hii unatafuta uhai, au unajaribu kupata majibu kwa swali kubwa ya watu wengi na ni maana ya maisha haya ni nini. Wengi wako na majibu, wengine wamekuwa watajiri kuuza majibu lakini jibu la kweli ni moja tu, maana ya maisha haya ni Yesu Kristo na huwezi kupata ukweli nje yake.
Tusome mstari yetu ya leo kwa muktadha yake, na hizi mistari tano kwa bibilia yote hakuna zingine zinaongea kuhusu Uungu wa Yesu kama hizi. Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Hii ni neno la Mungu wetu kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo.
Tuombe.
Hapa Yohana tena ako wazi kabisa. Na anatuonyesha Yesu mwenyewe ni uhai na ndani yake ni uhai, na alikuwa nuru ya mbinguni na aliingia hii dunia na alikuwa pamoja na binadamu. Ni muhimu sana kushika kwamba Kitabu cha Wakolosai 1:17 ya sema Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Yesu ni kila kitu na vitu vyote hushikana katika yeye. Kila pumzi yako ni kwa sababu ya yeye, kila mpigo wa moyo wako ni kwa sababu ya yeye. Wakati tunaanza kushika hii, upendo upendop wetu kwa Bwana wetu itakuwa zaidi ya kila kitu.
Kwetu Wakristo hii ni muhimu ana hii ukweli wa Yesu kwamba hana mwanzo ni kubwa sana. Yesu ni wa milele. Na kwa sababu yeye ni wa milele yeye ni chanzo cha uhai. Kama tumesoma Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu alziumba mbingu na nchi. Ni kitu hapa kwa maneno haya ni muhimu Zaidi ya ukweli wote. Kwamba Yesu alikuwa na Yesu hana mwanzo na hana mwisho. Hii ni sababu wasioamini wanajaribu kutoa hii mambo yote ya umbaji. Ukitoa umbaji halafu hakuna muumba, na watu wanaweza kuishi kama wanataka bila hukumu kwa sababu wakati tunakufa, ni mwisho. Pole kwa hawa, wamejidanganya. Angalia Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Ikiwa Yesu si kila kitu kwako basi yeye si kitu kwako. Kama nimesema mara mingi wokovu si Yesu na, Maisha haya si Yesu na, yeye ni kila kitu. Hii mstari ni ukweli kabisa na inatuonyesha ukweli kuhusu Yesu Kristo, Yeye ni uhai. Na ndani yake tunaishi, tunakwenda na tunapata uhai wetu. Unajua watu bila Yesu kristo ni wafu. Wanatembea kwa Maisha haya kama wamefunga macho yao. Wanamuka kila asabuhi wanafanya kama wanafanta na wanarudi kulala, siku yao haina maana, hakuna lengo ya milele, ni lengo ya saa hii, ya leo.
Yesu ni uhai, Yesu ni muumba ya kila kitu, Yohana anasema Yesu ni neno. Kusema Yesu ni uhai ni kusema ni yeye anatupea uzima wa milele kwa watu ambao wanaamini.
Yohana anasema Yesu ni nuru. Wakati unafikiria nuru, unafikiriaje? Nuru ni ukweli na utakatifu na inonyesha giza na dhambi na uongo wa watu. Yohana 8:12 anasema Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Sisi wafuate wa Yesu hatuwezi kuishi gizani kwa sababu Yesu anaishi ndani yetu na yeye ni nuru. Ikiwa wewe unaishi gizani, ikiwa wewe uko na Maisha ingine nje ya kanisa ikiwa wewe ni mtu tofauti hapa na nje wewe ni mwengine ni mzuri kuhakikisha unamjua Yesu kweli kweli. Sisi tunajua mahali ya nuru hakuna giza, ukiwaka torch yako usiku, giza inatoka, inatoka kila mahali nuru inaangalia. Unasema wewe ni Mkristo, nuru ya Mungu inaishi ndani yako na unaishi gizani naam na gani? Hawezikani. Usijidanganya.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.