Jesus Christ Pt.4

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

John 1:5

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Yohana na tumefika 1:5. Karibu wiki nne tumeangalia vs.1-4 na tumeona Yesu Kristo, Bwana wetu ni ajabu sana. Ni Mungu bila shaka. Hakuna mistari zimngine zinatuonyesha Uungu wa Yesu kristo kama hizi mistari tano. Pia tumeona lengo ya Yohana kuandika kitabu hiki kwa Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Tunataka kukumbuka hii wakati tunasoma kitabu cha Yohana. Kwa hizi mistari tano tumeona Yesu ni Neno la Mungu, Yesu ni Muumbaji ya kila kitu Yeye anashikilia kila kitu pamoja. Tumeona alikuwa na Mungu mwanzo na hata alikuwa Mungu. Pia tumeona Yesu ni uzma na nuru ya watu. Hatuwezi kusoma vitu hivi na kusema Yesu ni kitu kiingine, Yesu ni Mungu, Yesu ni Masihi na tukiamini hii tutakuwa na uzima kwa jina lake.
Hakuna kitu kiingine kwa Mkristo anapenda zaidi ya Yesu Kristo, hakuna kitu kiingine tunaoenda kuongea kuhusu kuliko Yesu kristo. Wakati tunasoma hizi istari tano ingefurahisha roho zetu kujua, huyu mtu, Yesu ni Bwana wetu, ni mfalme wetu, ni mwokozi wetu. Dunia inajaribu kusema hii yote ni uongo, Shetani anajaribu anageuza na kugeuza Neno la Mungu na ako na makanisa mingi na mapastor wengi sana ambaye wanahubiri Yesu mwengine, injili ingine, wanabeba neno la Mungu tunaona ni bibilia kwa mkono wao lakini wanachafua sana. lakini wakati unashika Yesu Kristo ni nani hakuna shukrani ya kutosha, hakuna sifa za kutosha sisi tunaweza kumpea. Na anatuita ndugu na dada, anatuita rafiki. Ajabu, na tumaini sana wakati unafikiria vitu hivi na wakati unasoma mistari kama hizi unashangaa. Yesu anastahili kila kitu tunaweza kumpea, anastahili sifa zote, Tunampaswa kutoa maisha yetu kwa utumishi wake. Ikiwa wakristo wanaweza kushika kabisa maana ya Matendo 17:28 ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kila kitu itakuwa tofauti. Maisha yetu, Familia yetu, kanisa letu, community yetu hata nchi yetu itakuwa tofauti sana. Lakini i mzuri kwetu kushika tunaishi kwa hii dunia na ni giza. Shetani ni Mungu ya mfumo ya hii dunia na sisi tuko hapa. Haitakuwa rahisi, hata kusema ukweli itakuwa ngumu sana.
Tusome mtsrai yetu ya leo kwa muktadha yake. Kitabu cha Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Hii ni neno la Mungu wetu kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo.
Tuombe:
kwa vs.4 tulisoma Ndani ya Yesu ulimokuwa uzima nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Tuliangalia hii sana wiki iliopita. Tuliona Yesu ni kila kitu, tuliona alishinda ufalme wa giza na alileta uhai kwa sisi ambao tulikuwa wafu katika dhambi zetu. Ni mzuri sisi sote tunashika kwamba hii dunia na mfumo yake ni giza. Tunasoma kwa Waraka wa pili wakorintho 4:4 mungu wa dunia hii. Mungu wa dunia hii ni shetani na wakati tunasoma hii ni mzuri tunajua Paulo anaongea kuhusu mfumo wa hii dunia. Shetani ana ushawishi katika mambo haya yote na huwaongoza watu wasiomcha Mungu kufanya kazi yake. Na ni mzuri unajua kazi yake si kama watu wanafikiri lakini kazi ya sheatni ni kudanganya watu ili hawajui ukweli wa neno la Mungu. Anataka kuchafua sana neno la Mungu, anataka watu kufikiri kutoa mapepo ni ukweli, anataka watu kuamini kuponyesha watu kwa huyu Pastor fulani ni ukweli, anataka watu kuamini kumwanga mafuta juu ya watu italeta Roho Mataatifu, anataka watu kuamini wakati unaongea maneno ya ujinga unaongea na ulimi wa malaika, anataka watu kutoa meno yao na sasa wanafikiri ni hawa peke yao watafika mbinguni, si kwa sababu ya imani yao katika Yesu na wanafuata neno lake lakini kwa sababu ya kitu kama kutoa meno, anataka watu kuamini huyu “Man of God” ako na mamlaka fulani na watu wanamfuata na inatoa macho yao kutoka Yesu na neno lake. Anataka watu kuamini hii uongo wote tunaona watu wanasema ni ya kanisa na Yesu kwa siku zetu. anataka watu keweka imani yao katika maji mtakatifu, au kitu kiingie mapastor wanauza na siku hizi shetani anacheka sana kwa sababu watu wamekuwa rahisi sana kudanganya na wanafuata kitu cho chote.
Hii mstari ya waraka wa pili wakorintho inaendelea kusema mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini. Na wakati tunaona hii maneno yote tunaona ni ukweli kabisa na hata hawa watu wanajiita wakristo, wanasema wanafuata Yesu lakini Yesu wanafuata ni Yesu shetani ameumba, ni injili ya uongo. Si injili ya Bibilia na si Yesu tunapata kwa neno la Mungu. Mstari inaendelea kusema isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Shetani anataka watu kuishi kwa giza, kwa ujinga, kuendelea kuwa wafu, hataki hawa kuona nuru ya injili ya utukufu wake kristo.
Angalia mstari yetu ya leo kitabu cha Yohana 1:5a. Nayo nuru yang'aa gizani. Nayo nuru ni Yesu. na alikuja hapa kwa hii dunia na Mungu wa mfumo wa hii dunia alikuwa na shida. Ufalme wake wa giza inaonekana. Kudanganya watu sasa si rahisi kwa sababu wakati nuru iko watu wanaweza kuona kila kitu, na Yesu aliweka kila kitu wazi kabisa. hata Yesu mwenyewe alisema kwa kitabu cha Yohana 8:12 Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Kumanisha dhambi haiwezi tawala tena juu ya waufuasi wa Yesu. Sasa tunaona, Yesu ametoa upofu wa shetani na sasa sisi tunaona wazi. Labda unakumbuka wakati ulikuwa msioamini ilifikiria vitu tofauti. Labda kabla ya Yesu, kusikiliza musiki mbaya na inatumia lugha mbaya ilikuwa sawa, lakini sasa wakati unasikia unasema siwezi sikiliza hii, labda hata ni uchungu kidogo wakati unasikia, hii ni sbabau ulikuwa gizani na hujajua tofauti, sasa Yesu ameleta nuru na ameuonyesha ni dhambi. Labda kabla ya yesu ulikunywa pombe mpaka unalewa, au ulilalal na boyfriend au girlfriend yako, lakini sasa hata huwezi kufikiria vitu hivi kwa sababu Yesu amefungua macho yako kujua ukweli ya dhambi na mahali uliishi ilikuwa gizani. Kitu cho chote umetenda kabla ya Yesu alifungua macho yako bila shaka sasa unaona tofauti, kwa sababu nuru imeingia na unaona kila kitu wazi kabisa.
Nimesoma hadithi ya mtu ambaye alikuwa mstuni na ilianza kuonyesha na ilikuwa usiku. Hajakuwa na torch na hawezi kuona vizuri, alipata shimo kubwa kwa mawe na aliingina na alilala usiku mzima kwa hii shimo. Asabuhi aliamuka kupata mahali alilala ilikuwa nyumba ya nyoka mingi sana. walikuwa kila upande wake. Sasa tofauti ni nini? Aliingia bila kuona kwa sababu ya giza, lakini wakati nuru ya asabuhi ilikuwa imeweka kila kitu kuonekana. Maisha ya Mkristo ni naam na hiyo. Sisi ni wajinga tunajaribu kutembea kwa maisha haya gizani lakini wakati nuru ya Yesu inaingia maisha yetu, macho yetu yanafaunguliwa kuona kila kitu kama iko. Shetani na watu wa hii dunia hawapendi hii nuru. Tunasoma kwa kitabu cha Yohana 3:19-20 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Hii ni shida kubwa kwa watu, tunaona wanapenda giza kuliko nuru, kwa nini? Kwa sababu matendo ya ni ni maovu, na wakikuja kwa nuru kila kitu wanatenda itaonekana. Hii ni Yesu yetu, anatuonyesha sisi ni nani? Watu hawataki kujua hawa ni nani, watu wanapenda kufikiri hawa ni wazuri, hawa wako sawa, lakini Yesu anatuonyesha ndani yetu kwa moyo wetu na mawazo yetu sisi ni nani. Ikiwa Yesu unayemfuata hafanyi hii maishani yako, unafuata Yesu ya uongo. Ikiwa unafikiri unaweza kusihi maisha yako ya chafu na kujioendeza na fuata Yesu, unafuata Yesu ya uongo. Yesu ni nuru, watu wake ni nuru, dhambi ni giza. Huwezi kuishi gizani na sema wewe ni Mkristo. Kanisla la Korintho walikuwa na vitu vingi sana, watu walitoka chafu mingi ya hii dunia na walianza kufuata Yesu, lakini bado wengi walijaribu luishoi kwa maisha ya zamani na walifikiri wanaweza kufuata Yesu Paulo alisema kwa hawa Waraka wa pili wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. ikiwa unaishi maisha yako kujipendeza na vitu vya zamani anasema Jijaribuni, Jithibitisheni, hakikisha Yesu ako ndani yako kweli kweli, ama labda utapata unaanguka mtihani na hayuko. Yesu wetu ni nuru. Ni mzuri kukumbuka Waraka wa kwanza wa Yohana 1:5-6 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; Usiseme wewe ni Mkristo na unaishi kama msioamini. Wkaati unafanya hii Bibilia ni wazi kabisa, wewe ni mwongo na hujui ukweli.
Ukirudi kwa mstari yetu ya leo kwa kitabu cha Yohana 1:5 unaona Nayo nuru yang'aa gizani, lakini anaendelea kusema wala giza halikuiweza. Hii ni muhimu sana. Watu wengi wanafikiri Mungu na shetani wakovitani na hatujui nani atashinda na nani atashindwa, wema dhidi ya uovu na sisi tuko kati kati ya hii yote. Hii ni uongo sana. Ni ukweli shetani amejaribu sana mara mingi kumshinda Yesu lakini kila wakati ameshindwa. Kumbuka Mwanzo 3:15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Hii ni kumaanisha kwamba Yesu kristo atamshinda shetani. Ndiyo hii mstari inasema shetani atamponda Yesu kwa kisingino, lakini kugonga mtu kwa kisingino ni uchungu lakini haiwezi ua mtu. Kuginga mtu kwa kichwa yake umemshinda. Lakini hii mstari inatuonyesha ya kwamba giza itajaribu kushinda nuru. Ni mzuri kukumbuka shetani anajua neno la Mungu, yeye ni fundi ya neno la Mungu na anajua ameshaashindwa anajua mwisho yake ni nini. Shetani anajua kama Mathayo 25:41 Yesu alisema mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; Anajua Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. Watu wamefundishwa vibaya sana. Wanafikiri Jehanamu ni mahali shetani anaishi na yeye ni kitu mbaya sana hata kuangalia yeye ako na pembe na mkia wenye ncha na yeye ni nyakundu. Hii ni uongo sana. Paulo anasema kwa Waraka wa pili wakorintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Yeye ni madadari sana. Na kwa hii sehemu ya maandiko Paulo anaongea kuhusu Walimu wa uongo, mitume ya uongo na anasema usishangaa wale walimu wa uongo wanafuata baba yao na yeye anajifanya kama ni malaika wa nuru vs.15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. Shetani anajua atatupwa kwa ziwa la moto, hataki kuenda uko, lakini ni mwisho yake na ako na wakati fupi kudangaya watu na anajua hii.
Tunaona Shetani alijaribu kumfanya Yesu Aanguke. Alijaribu kushinda nuru na giza yake na alitumia neno la Mungu. Kwa kitabu cha Mathayo 4 na Luka 4 tunapata hii yote. Yesu hajakula siku arobaini na alikuwa na njaa. Na Ibilisi amemjaribu Mathayo 4:3 mwisho tunasoma Ibilisi alisema amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Halafu tunaona alijaribu kupima imani yake kwa Mungu alimwambia Yesu kuruka kutoka juu ya kinara cha hekalu na Mungu atamwokoa na Yesu alisema vs.7 Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. ya mwisho alijaribia Yesu na tamaa za mwili ya sisi binadamu. Ibilisi alionyesha Yesu milki zote za ulimwengu na vs.9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Shetani alijaribu sana na alishindwa. Ni mzuri kujua kwamba Shetani kama walimu wa uongo wanatumia neno la Mungu vibaya, wanachafua na dawa ya hii yote ni kama Yesu alifanya, ni kutumia neno la Mungu ukweli kama imeandikwa. Lakini ni ajabu sana. Halafu tunaona kwa mwisho alijaribu kushinda nuru ya hii dunia wakati Aliingia yuda kusaliti Yesu. Angalia Luka 22:3-4 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. Hii ni wakati Yuda alimsailiti Yesu, unaona Shetani aliingia na alijua kama watafanya. na tunajua kama ilifanyika. Yuda alimsaliti Yesu, makuhani walimshika na walimleta mbele ya wakuu halafu kwa Roma. Walimpiga Yesu sana halafu alibeba msalaba wake kwa mlima na walimweka msalabani. Uchungu kama sisi hatuwezi fikiria na baada ya maasaa Yesu ako karibu kufa na tunasoma kwa Mathayo 27:45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Ni mzuri kujua hii ni kati kati ya siku na giza imekuwa kila mahali. Nuru ya hii dunia ako karibu kutoka. na baada ya hii tunasoma Yesu alikufa. Wafuasi wake walikimbia na walijificha, Bwana wao alikufa. Bila shaka hawa wamesikia hii giza na ilikuwa mzito.
Kumbuka mstari yetu ya leo Yohana 1:5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Wala giza haijashinda Bwana wetu Yesu kristo. Baada ya siku tatu Yesu Alitoka kaburi, alishinda kifo na mauti na dhambi na mipango ya shetani. Nuru ilirudi kwa hii dunia na nguvu na hii ni Bwana wetu. Shetani hana tumaini lo lote watu wake hawana tumaini na wafuasi wa Yesu tunabeba Yeye kila mahali tunaenda na sisi, anasema ako pamoja nasi kila mahali hata Mathayo 5 Yesu anasema sisi ni chumvi ya hii dunia halafu anasema sisi ni nuru ya hii dunia Mathayo 5:16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Kwa sababu ya Yesu hata sisi hatuwezi kushindwa na giza. Shetani hana mamlaka juu yetu. Hata Kitabu cha Yakobo 4:7 ya sema Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Ajabu sana.
Lakini bila Yesu kama ile wimbo inasema, mimi ni mtu bure. Yeye ni chanzo cha kila kitu kwetu na ikiwa hujaweka imani yako katika yeye bado wewe ni giza na unasihi chini ya Bwana mwengine. Ni njia moja kuwa Mfuasi wa Yesu na hii ni kutubu kwa dhambi zako na kuamini, kuamini kila kitu kwa neno lake ni ukweli na kuweka imani yako katika Yeye kwa kila kitu, maisha haya, wokovu, tumaini na maisha ambao inakuja baadaye. Ikiwa hujafanya hii na unataka kuongea zaidi karibu hapa mbele baada ya ibada yetu. Tunataka kuongea na wewe.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more