John The Baptist
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 1 viewNotes
Transcript
John1:6-8
John1:6-8
Leo asabuhi tunendelea na masomo yetu katika ktabu cha Yohana na tumefika mlango wa kwanza mstari wa sita hadi nane. Kwa wiki mingi tuliangalia sana mstari wa kwanza hadi tano na tumeona zote ni kuhusu Yesu kristo. Ukisoma Yohana 1:1-5 na huwezi kutoka kujua Yesu Kristo ni kila kitu, ni Muumbaji wa kila kitu, Yeye ni Neno la Mungu, Yeye ni Nuru ya ulimwengu, kila kitu inashika pamoja kwa sababu ya yeye, kwa nini? Kwa sabab yeye ni Mungu. Ikiwa unasoma mistari yale tano na hujashika hii, sijui unasoma naam na gani au labda ni kwa sababu Roho Mtakatifu hatuko ndani yako na hajafungua macho yako kuona ukweli wa neno la Mungu. Lakini kusema ukweli wakati sisi oste tunasoma mitsrai yale ni lazima tunajibu Yesu Kristo ni nani.
Hata siku za Yesu kwa sababu ya maisha yake ya kusihi bila dhambi, kama ameongea na kama amesema yeye ni nani, Yesu alishika umakini wa watu na iliwalazimu kumwitikia. Na walifanya hii kwa njia tofauti. Ulikuwa na watu walisema Yesu ni mtu mzuri, wengine walisema yeye ni kiongozi mzuri wa dini, wengine walisema yeye ni nabii. Wakati Yesu alilisha watu elfu tano walijarubu kuweka Yesu kuwa mfalme wao kwa nguvu. Na inaonyesha kama watu wako, na ni mzuri hata sisi tujichunge sana. Wale watu wakati Yesu aliingia Yerusalemu angalia kama walisema Kitabu cha Mathayo 21:9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni. Hii ni mzuri sana, hii ni watu wale wote wameona Yesu kufanya mambo mingi sana, Kuponyesha watu, Kumfufua Lazaro kwa wafu, lisha watu wingi na mikate tano na samaki mbili, Mponye kipofu, mambo mingi wameona, hii ni sababu wanasema kama wanasema, Mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana. Na baada ya siku tano tu ni watu wale tunaona wanasema kitu tofauti sana kwa kitabu cha Yohana 19:15 wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari. Ni ajabu sana. Ni watu wangapi ni kama hii? Kanisani wanatoa sifa mingi kwa Yesu na wanaimba na jumatatu inakuja na wako kazini na unaweza kuona huyu mtu kukataa hata anajua Yesu ,labda kwa maneno yake anatumia au kwa maisha yake.
Uko na watu wengine walipenda sana kama Yesu alsiema na alifundisha na walitaka kumfuata lakini waliogopa, hata viongozi. Anaglia Yohana 12:42 hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Hata siku zetu tuko na watu kama hii. Wako juu, ni wakubwa, wanajua ukweli na wanaamini lakini kwa sababu ya msimamo wao au mkubwa wao hawawezi kusema kwa sababu wanaogopa kupoteza nafasi yao.
Uko na wengine ni kama tajiri kijana mtawala. Alishi maisha mzuri, aliita Yesu Mwalimu mzuri, alitaka uzima wa milele, alisema amefanya amri za Mungu tangu alikuwa mdogo, baad ya hii tunaona Yesu alisema Kwa Marko 10:21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Huyu tajiri ameshangaa lakini alitaka uzima wa milele na amepata jibu kutoka Yesu mwenyewe, atafanya nini? Vs.22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Wengi nikama huyu. Wanataka Yesu lakini hawataki kuweka yeye juu ya kiloa kitu maishani yao. Si kama Yesu alitaka huyu kuwa maskini, alitaka kuonyesha huyu anaoenda nini zaidi. Lazima kufuata Yesu tunamoenda zaidi ya kila kitu na kila mtu maishani yetu.
Kwa watu wengine walijibu Yesu ni nani na haijakuwa mzuri. Ulilkuwa na watu wanasema Yesu anaongoza watu vibaya, wengine wakati alikuwa mbele ya Pilato walisema amekata kulipa kodi, wengine walisema alikuwa na pepo. Kusema ukweli hii yote ni matokeo ya kutoamini. Kutoamini ni dhambi ambaye inawalaani wale wote wanomkataa Yesu. Bila kuamini Yesu ni Kristo na ni kwa yeye peke yake mtu anaweza kuokoka ni shida kubwa. Lakini kwa wale ambao wanaamini wanapokea baraka mingi. Baraka ya wokovu, uzima wa milele, msamaha wa dhambi zao na wanaitwa watoto wa Mungu. Ni ajabu sana. Halafu leo kwa mistari yetu tunaona mtu anaitwa Yohana na kama amekuja kufanya ni ajabu.
Tusome mistari yetu ya leo, Kitabu cha Yohana 1:6-8 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kwa vs.6 tunasoma Palitokea mtu, ametumwa kutoka Mungu, jinal lake Yohana. Ni ajabu sana baada ya kuongea kuhusu Yesu Kristo kwa mtari ya kwanza hadi tano sasa Yohana alianza kuandika kuhusu mtu. Lakini kumbuka ni Mtume Yohana anaandika kitabu hiki na Hapa kwa hii mstari anaongea kuhusu Yoahan Mbatizaji. Mtume Yohana alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji na bila shaka hata Yohana Mbatizaji aliongoza Mtume Yohana kujua Yesu na kufundisha yeye Yesu alikuwa Masihi Wao. Mtume Yohana alijua sana Yohana Mbatizaji na kama aliandika unaweza kuona kwa sababu alieleza hata nguo ya Yohana Mbatizaji zilikuwa naam na gani, kama alihubiri, tabia ya maisha yake. Tunaona kwa Kitabi cha Yohana 1:35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Tunajua moja alikuwa Andrew na watu wanasema huyu ya pili alikuwa Mtume Yohana.
Kitu cha kwanza anasema ni Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu. Alitumwa kufanya nini? NA ni mzuri kujua wakati tunaangalia mtu kama Yohana Mbatizaji, alikuwa na wafuasi, walifuata yeye, lakini tutaona kitu kubwa kwa Yohana na watu leo. Mungu alimtuma Yohana kuwa mtangazaji. Kitu cha kwanza alitumwa kutimiza unabii wa agano la kale. Tuliambiwa ni mtu atatumwa kuja mbele ya Masihi. Angalia Isaya 40:3 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Tunaona hii ilikuwa Yohana Mbatizaji angalia Mathayo 3:1-3 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Kairbu miaka mia saba kabla Mathayo iliandikwa watu hawajajua ni nani atakuja kufanya hii kazi, lakini sisi tunaona ilikuwa Yohana Mbatizaji. Na tunasoma hii kwa kitabu cha Mtahyo, Marko na Luka na hawa wote wanakubali ilikuwa Yohana Mbatizaji. Ikiwa ilikuwa myahudi na uliishi kwa hii wakati ungeshangaa kuona unabii huu wote wa agano la kale kutimizwa kwa wakati wako.
Kitu kiingine kuona Yohana alitumwa na Mungu ni kuzaliwa kwake, ilikuwa muujiza. Wazazi wake walikuwa wazee na hawajakuwa na watoto. Luka 1:7 Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Hii ni mama ya Yohana Mbatizaji na tunajua Ni Mungu alifungua tumbo la Elizabeti ili aweze kuzaa.
Kitu kiingine tunaona kwa Yohana alitumwa na Mungu ni Malaika wa Bwana alitumwa kuwaambia Zakaria na Elisabeti kwamba huyu mtoto wao atatangaza kwamba Masihi ya Mungu amekuja. Angalia Luka 1:11-17 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. Hii ni Yohana Mbatizaji.
Kitu kiingine ni Mungu alituma Yohana Mbatizaji kwa wakati uliowekwa na Mungu kufika na kuanza kazi yake. Luka 1:80 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. Ni Mungu alipanga siku hii. Hakuna shaka yo yote Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu, hata Yesu mwenyewe alisema kwa Mathayo 11:11 nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.
Karibu miaka mia nne kwa nchi wa Israeli hakuna manabii na Yohana Mbatizaji aliingia na alianza kutoa unabii. mahubiri yake yalikuwa na nguvu sana. Tunasoma kwa Marko 1:4-5 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Kazi yake ilikuwa kutayarisha mioyo ya watu kwa masihi yao. Hata alimkabili Mfalme Herode kwa sababu alikuwa na mke wa ndugu yake. Hata mfalme Herode alikuwa mbaya sana na bado alipenda kusikia Yohana kuhubiri. Angalia Marko 6:20 Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha. Lakini kwa sababu ya kusema Herode alivunja sheria kuwa na mke wa ndugu yake alifunga Yohana gerezani na tunajua badaye Alitoa kichwa cha Yohana. Tuafika uko labda mwako ujayo.
Yohana Mbatizaji alifundisha na nguvu na hajaogopa hata kidogo na Israeli nzima ilianza kuwa fujo kwa sababu ya mahubiri ya Yohana. Rudi kwa mistari yetu ya Leo. Yohana 1:7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Yohana Mbatizaji kazi yake na sababu alitumwa ni aishuhudie ile nuru, na kwa wote kuamini kwa Yesu. Hii ingekuwa lengo ya kila Mkristo. Sisi tunataka wote kuamini, hata maadui yetu. Sisi tunajua nini inaongojea watu wale wakati wanakufa, ni hukumu, watasimama mbele ya Mungu ambye ni mtakatifu na watatoa majibu kwa miasha yao na baada ya hii yote watatupwa kwa ziwa la moto. Sisi tunataka wote kuona nuru na kutoka giza. Ikiwa uko na lengo ingine kwa maisha haya na hii si juu ya yote ni mzuri unahaikisha Yesu ni Bwana wako. Yohana Mbatizaji hajapoteza lengo yake na kazi yake kutangaza Masihi amefika, wokovu iko. Paulo alisema kwa Waraka wa pili wakorintho 4:6 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Hii ni sisi pia, Aliyeng’aa mioyoni mwetu, sisi tumefundishwa tuko na elimu ya utukufu wa Mungu, tunajua kila kitu cha maisha haya ni kumhusu Yesu. Hata wakati maisha inakuwa ngumu sana hatuwezi sahau lengo ya maisha yetu na ni Yesu na kutii yeye na kutangaza habari yake, angalia vs.8-9 Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; Mkristo akotayari kuteseka kutimiza lengo yake, huwezi kutuambia kitu tofauti, huwezi kumzuia mkristo. Vs.10 siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. natumini sana hii ni moyo wako, kwa sababu ikiwa kanisa letu linaweza kuwa na moyo kama hii, tutabadilsiha hii area kabisa. Usiketi hapa maisha yako yote kwa kanisa hili au kanisa lingine na kuwa mtu ambaye ameketi tu, ikiwa unafanya hii hakikisha unamjua Yesu kweli kweli. Mkristo, unajua umeitwa kufanya nini, tuko na mifano mingi sana bibliani kwa wafuasi wa Yesu. Labda hutakuwa Yohana Mbatizaji lakini sisisote tunaweza kuleta mabadiliko kwa watoto wetu, familia yetu, boma yetu.
Yohana Mbatizaji Alichochea mkoa mzima na mahubiri yake. Alikuwa na wafuasi wingi sana, lakini tuangalia kama alisema Yohana 1:8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Alijua yeye si Kristo, hajajaribu kuchukua nafasi ya Yesu. Kama walimu wa uongo wote siku zetu wanaingia nafasi ya Yesu, wanataka watu kuwaabudu, Kusema ukweli wanataka kutoa yesu ili watu watafuata hawa kama hawa wenyewe ni Mungu. Yohana Mbatizaji alisema kwa Kitabu cha Yohana 1:20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Kitu cha kwanza tunaona ni Yohana kusema yeye si Kristo, hakataka watu kufikiri yeye ni kitu. Alikuwa na umaarufu, alikuwa na wafuasi wingi sana, hata walijiita wanafunzi wa Yohana, lakini hajasahau sabau alitumwa. Angalia Luka 3:16 Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; Alijua yeye mwenyewe si kitu, na Yesu ni kila kitu ni Mungu. Sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake, kusema hii ni kusema uko chini zaidi. FIkiria watu leo, watasema hii ukweli?
Yohana Mbatizaji alikuwa mtu muhimu sana tumeshaa angalia lakini moyo wake ni nyenyekevu sana. Yeye alitangaza Masihi amefika na alikuwa ya kwanza, ni ajabu. Kama mstari ya nane inasema hakuwa nuru, bali alikuja ili aishuhudie nuru. Wakakti ninasoma maneno haya ninatamani sana kwamba sisi sote tunaweza kuwa na hii moyo wa Yohana Mbatizaji, kwa sababu sisi sote, wakristo tumetumwa na Bwana wetu. Kila mwanafunzi wa Yesu tuko na mission kwa mfalme wetu. Angalia Mathayo 28:18-20 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Kumaanisha kama tunaenda kial siku ya maisha yetu, kwa kazi, kwa familia, kwa marafiki yetu, tukisafiri, kila mahali tuanenda tunabeba na sisi habari kuhusu nuru ambaye ameingia hii ulimwengu, tunabeba na sisi kifo chake, ufufuo wake, tumaini lake, tunataka wengine kutubu na kufuata Yesu, na sisi tunaweza kuwa na hawa kufundisha hawa ukweli tuko nai katika neno la Mungu. Kweli ni pendeleo la ajabu tuko nai.
Leo asabuhi ikiwa uko hapa na hujui Yesu Kristo, hujaweka imani yako katika Yeye, usichelewa, wakati wako ni saa hii. Msamaha iko, maisha mpya iko, tumaini la uzima wa milele iko, ni kutubu kwa dhambi zako na kuamini Yesu Kristo na kazi yake msalabani na amekufa kwa ajili ya dhambi zako. Weka imani yako katika yeye. Ukitaka kuongea zaidi niko hapa kueleza zaidi na kuomba nawe. Karibu baada ya ibada yetu na tutaketu pamoja.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.