The rejected Messiah
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 3 viewsNotes
Transcript
John 1:9-11
John 1:9-11
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Yohana na tumefika mlango 1:9-11. Tangu tumeanza masomo yetu kwa kitabu hiki tumeona kila kitu ni kumhusu Yesu Kristo. Kumbuka sababu Yohana aliandika kitabu hiki anatuambia kwa 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Kila kitu Yohana anaadika ni kutuinyesha lengo yake ya kuonyesha watu Yesu ni Kristo. Wiki iliopita tuliona hata unabii wa agano la kale ulikuwa ukitumia. Kwa miaka mia nne hapakuwa na unabii kwa nchi ya Israeli na huyu Mtu anaitwa Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu, na sababu yake ilikuwa kama tumesoma kwa Kitabu cha Isaya 40:3 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Na wakati makuhani na walawi walitumwa na Mafarisayo kuuliza Yohana yeye ni nani kwa sababu alikoroga nchi ya Israeli na mafundisho yake alisema wazi kwa Yohana 1:20 Mimi siye Kristo. Na walisema halafu wewe ni nani? Alijibu vs.23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. unabii huu imeanza kutimizwa. Na tulisoma kwa Yohana 1:7 alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Bado Yohana hajasema jina la huyu mtu ambaye ni Neno, na Mungu na muumbaji ya kila kitu na nuru lakini sisi tunajua ni Yesu kristo.
Kitu cha ajabu sana ni zamani wakati tulikuwa na mifalme kwa hii dunia, wakati wo wote wataenda mahali, kabla ya watafika kwa ile mahali watatuma mtangazaji kusema mfalme anakuja, na huyu mtangazaji atatangaza ujumbe wa mfalme na atasema kwa wananchi, jiandae kwa ajili ya kuwasili kwa mfalme. Wote walitaka kusikia sauti ya mfalme wao na kujua atasema nini. Maisha itakuwa mzuri ama maisha itakuwa ngumu. Mfalme ameleta nini kwa wale watu ambao amekuja kuongea na hawa? Na sasa tuko na Mungu alituma Mtangazi wake kwa watu wake kutangaza Mfalme wao anakuja. Na kwa mistari yetu leo tutaona kama wananchi wamepokea mfalme wao.
Tusome mistari yetu ya leo. Yohana 1:9-11 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Hii ne neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Tulimaliza wiki iliopita kuona Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu kutangaza nuru amefika kwa hii dunia na tuliona vs.8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Halafu tunafika vs.9 na tunasoma Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Nuru halisi sisi tunajua ni Yesu kristo. Lakini hii dunia tangu mwanzo imejaribu hata mpaka saa hii kuweka nuru ya fake mbele ya watu. Shetani anataka watu kufuata nutu ya fake, hii ni sababu ameweka watu wake wingi kudanganya watu na kusema hawa ni ukweli, hawa wanafundisha ukweli hata wengine wanasema hawa wenyewe ni Yesu. Lakini wakati Yohana alisema nuru halisi anaonyesha kwamba hii dunia na watu ndani yake ni kipofu, kwa sababu ni mtu ambaye ni kipofu hawezi kuona nuru. Wasioamini ni vipofu wa kiroho. Ni mzuri kwako kujua ikiwa unaketi hapa leo asabuhi na wewe ni msioamini wewe ni kipofu kwa kiroho yako, hata Paulo alituambia kuhusu hii kwa Waraka wa Pili Wakorintho 4:4 mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Wasioamini wako kwa ufalme wa Bwana wao shetani na wanatembea gizani na hawawezi kuona nuru ya kweli, wanaona kama Bwana wao anaweka mbele ya hawa.
Ni mzuri kwetu kushika kwamba kuna aina mbili za watu katika ulimwengu huu. Ni waamini na wasioamini, na watu wale ni nuru au giza, Mtumwa wa Yesu au Mtumwa wa Shetani, raia ya ufalme wa nuru au raia ya ufalme wa giza. Yesu alikuwa Nuru halisi amtiaye nuru kila mtu. akija katika ulimwengu. Ulimwengu huu ilikuwa giza kwa miaka elfu mingi na wakati Yesu aliingia hii yote ilibadilika. Yohana anasema amitaye kila mtu. Watu wako bila udhuru. Nuru ambaye Yesu Kristo ameleta kwa hii dunia imewacha watu bila udhuru, sasa wameona ukweli, ukweli iko mbele ya hawa na bado ni watu watakataa. Yohana 3:19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Nuru ya Yesu inatoa giza ya dhambi na kutoamini na inaweka wazi ili kila mtu anaweza kuona ukweli wa dhambi na matokeo yake. Lakini kama Yohana amesema watu bado wanapenda giza kwa sababu bado wanaweza kuficha dhambi zao ambazo wanapenda. Kwa sababu Yesu amekuja na yeye ni nuru halisi na watu wameona sasa hata watu ambao hawatakuwa watoto wa Mungu, Hawataamini Yesu kristo ni mwokozi, hawatafuata yeye kwa njia ya imani yao, hata wao wanawajibika kwa maarifa ya Mungu na nru yake iliyofunuliwa katika Yesu kristo. Tunaona Paulo kuongea kuhusu wasioamini na jinsi wanavyowajibika kwa warumi 2:14-15 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; Umeona hata wasioamini wako na torati imeandikwa kwa dhamiri zao na wanaweza kuona Mungu kila mahali kwa sababu ya umbaji wake, wako bila udhuru. Yesu alisema kwa Yohana 8:12 Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Yohana 1:10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, Ni ajabu sana! Mungu wa kila kitu, Muumbaji ya kila kitu alikuja hapa na alitembea nasi. Alikuwa moja kama sisi. Ni ajabu sana kufikiria mtu ambaye anaanzisha kampuni fulani na inaanza kidogo sana na baada ya muda inakuwa kitu kubwa sana. unafikiri mwenye kampuni ikiwa anaingia watu hawajui yeye? Kila mtu atajua yeye ni nani. Sasa uko na muumbaji ya kila kitu hata ya binadamu na sasa ameingia na hawa, alisema Yeye ni Mungu na hawajajua yrye, kusema ukweli walimkataa. Alikuwa Muumba wao na hata alikuwa mwokozi wao, kwa njia yake watu wanaweza kuwa na uzima wa milele, lakini walimkataa. Lakini siku moja wote watalazimika kumkiri Yesu. Angalia Wafilipi 2:9-11 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Hii siku inakuja. Na ni watu ambao wameshaa fanya hii wakati wako na uhai na tunaita hawa wakristo, ni sisi, na ni watu ambao hawajafanya hii na ni wasiaomini, lakini siku moja watafanya hii lakini haiwezi kuwaokoa, wameshaapoteza nafasi yao na wataenda jehanamu kwa milele na milele na watakuwa na mawazo yao kufikiria kila nafasi walikuwa nai kuweka imani yao katika Yesu, Watu ambao walienda kanisa kila jumapili na walisikia ukweli wa neno la Mungu na hawajaamini, na wako na milele kufikiria vitu hivi wakati wanatseka motoni. Unasema hii ni kali sana Travis, ni kweli, ni kali zaidi, na bila kukuambia kuhusu siku ile, ningeshindwa kwa kazi yangu kuwa pastor yenu. Ni muhimu sana ninyi unashika kwamba kial mtu unajua, angalia jirani yako, salimia yeye, yeye siku moja ataingia hukumu, ikiwa uko na mtoto hata ikiwa ni mdogo angalia yeye, siku moja ataingia hukumu, Familia wako ambao wako nyumbani saa hii au wameneda kuchunga wanyama wako leo asabuhi, siku moja wataingia hukumu, watasimama mbele ya Mungu. Watahukumiwa na kitu cha umuhimu zaidi ni, ikiwa wamejua Yesu kristo. Kwa sababu alikuwa Nuru halisi, alikuwa Mwokozi na ikiwa hawajamjua yeye, hawataingia uzima wa milele, wataingia katika giza la milele na mateso na tumaini lote limepotea kwao. Tafadhali ikiwa unajua mtu ambae hajaokoka leo wakati unatoka kanisa na unaenda kuona hawa, waambia hawa kuhusu Yesu Kristo na kwamba amekuja kwa hii ulimwengu na alikuwa nuru ya ulimwengu na alikufa kwa ajili ya dhambi zao.
Yohana anasema Yesu alikuja ulimwenguni na hawajajua yeye halafu tunaona kitu hata mbaya zaidi kwa Yohana 1:11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Yesu Alikuja si kwa uilmwengu peke yake na watu wake lakini alikuja kwa watu wake, wayahudi, na walimkataa. Wakati tunasoma maneno haya, Alikuja Kwake ni kama alikuja nyumbani, lakini watu wa nyumba yake walimkataa. Sasa hii ni mbaya zaidi kwa sababu wayahudi walikuwa na kila kitu, maisha yao yote tangu walianza walikuwa watu wa Mungu. Ikiwa Mataifa hawajapokea Yesu ni mbaya lakini Wayahudi, kumkataza Yesu ni ajabu. Hata utafikiri watakaribisha Masihi yao. Fikiria Hekalu yao na kazi yake yote, Torati yao, Manabii wao, Historia yao, hata maisha yao ya kila siku kama walisihi, hii yote ilikuwa kwa sababu ya Mungu wao, hii yote ilikumbusha hawa ya kwamba Mungu Akakaa kati yao na angekuja kwake. Bila shaka mtu atafikiri ikiwa ulimwengu wote ilimkataa Yesu, bila shaka milango ya hekalu, nyumba yake, itafunguliwa kwake, hii ni sabbu hekalu ilikuwa, sivyo? Ilikuwa nyumba ya Mungu. Labda utasema hawajajua Yesu alikuwa Masihi yao, hii ni sababu walimkataa. Walijua, Wayahudi, desturi lao, kila kitu walifanya ilikuwa kwa sababu ya Mungu, walijua agano la kale sana, walijua wakati Masihi anakuja kama atafanya. Wayahudi hawajamkatza Yesu kwa sababu hawajamjua yeye lakini kwa sababu walimjua. Hata Yesu Mwenyewe alisema hii wakati aliwaambia hawa hadithi ya wakulima wa mizabibu. Unakumbuka hii? Angalia kitabu cha Luka 20:9-15 Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu. Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu. Akatuma na mtumwa mwingine. Wakampiga huyu naye, wakamwaibisha wakamfukuza mikono mitupu. Akamtuma na wa tatu; huyu naye wakamtia jeraha, wakamtupa nje. Basi, bwana wa shamba la mizabibu alisema, Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu, mpendwa wangu; yamkini watamheshimu yeye. Lakini, wale wakulima walipomwona, walishauriana wao kwa wao, wakisema, Huyu ndiye mrithi; haya, na tumwue, ili urithi uwe wetu. Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Yesu aliwaambia hii mfano kuonyesha wayahudi wanafanya hii na yeye. Alitumwa na Mungu na walimkataa hata ukikumbuka walifanya kama alisema Wakati Pilato alileta Yesu mbele ya wayahudi angalia kama walisema kwa Mathayo 27:22-23 Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe. Halafu vs.25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.
Wale watu walikuwa na Yesu, waliona kila kitu amefanya kwa miaka tatu. Na bado walisema hii. Tutaona Kwa kitabu cha Yohana kama watu walimkataa yesu kuwa Masihi yao. Tutaona Miujiza ya Yesu na tutaona wivu miujiza yake yalileta. Tutaona kama Yesu alifundisha na mamlaka na upinzani ulioleta. Tutaona wakati alipofunua asili yake ya kimungu, rehema yake, nguvu yake kupea mtu uhai, hukumu yake, unyenyekevu yake ya kujitoa na tutaona kila wakati watu walikuwa hapo kuchafua na kujaribu kuleta shida. Tutaona viongozi wa Wayahudi kuleta mitego kwa Yesu na mafundisho yake, hata walichukua mawe na walitaka kumpiga Yesu, tutaona kama walipanga kumwua yesu na tutaona walifaulu kumsulubisha. Alikuja kwake na wake walimkataa. Ni ajabu ukiona mahubiri ya kwanza ya Mtume Petro aliwaambia wayahudi wazi kabisa. Angalia Kitabu cha Matendo 2:22-23 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; Tunaona Petro kuhubiri kama hii mahali mingi sana kwa kitabu cha Matendo. Angalia Matendo 3:14-15 Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji; mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. Watu wake walimkataa. Nitaomba sana usimkataa. Petro tena anaongea na viongozi wa wayahudi na Ukiangalia Matendo 4:11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Na Petro hapa anaendelea kusema kitu cha umuhimu sana na ni muhimu zaidi hata kwetu leo asabuhi, Vs.12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Ni Yesu! Labda unasema sijamkataza yesu, kuendelea na kutokuamini ni kukataa. Leo asabuhi ikiwa hujui Yesu kristo, ikiwa hujaweka imani yako katika Yeye na kuamini hii yote ni ukweli, nitaomba, tafadhali kuyasalimisha maisha yako kwa Yesu. Fuata Yeye kwa sababu yeye ni mkombozi wa watu wake. Ikiwa hujui maana ya hii na unataka kujua zaidi, kuja mbele baada ya ibada yetu na tutaongea sana, ikiwa uko na maswali tutapata majibu kwa neno la yesu.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijyao.