Those who believed
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
John 1:11-12
John 1:11-12
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu katika kitabu cha Yohana na tumefika 1:11-12. Tangu tumeanza kitabu hiki nafikiri umeona kila kitu Yohana anaandika ni kumhusu Yesu Kristo. Mstai ya kwanza hadi kumi tumeona Yesu ni Neno, Yesu ni Mungu, Yesu ni Muumbaji, Yesu anashikilia kila kitu pamoja, Nadni yake ni uzima, Yesu ni Nuru, Tumeona alikuwa hii yote na alifika hapa kwa hii dunia kwa mwili na hii dunia ilimkataa na si dunia peke yake lakini hata watu watu wake wayahudi.
Hakuna kitu kiingine kwa hii dunia ni muhimu zaid ya kile unachofikiri kumhusu Yesu Kristo. Hii ni sababu Yohnaa aliandika kitabu hiki, hii ni sababu ni muhimu tunaangalia sana kama watu ambao walikuwa pamoja na Yesu wanasema. Tunafika mwisho ya kitabu hiki na Yohana anasema kwa Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Yohana hajakuwa na shaka yo yote kuhusu Yesu na yeye ni nani. Wakati Yesu aliuliza wanafuzi wake kwa kitabu cha Mathayo Watu hunena Mwana wa Adamu ni nani? Tunaona jibu la Petro kwa Mathayo 16:16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Petro hajakuwa na shaka yo yote kuhusu Yesu na yeye ni nani. Kwa kitabu cha Wakolosai Tunaona kama Paulo aliandika kuhusu yesu. Wakolosai 1:15-20 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. Paulo hajakuwa na shaka yo yote kuhusu Yesu na yeye ni nani. Na wewe? Uko na shaka yo yote kuhusu Yesu na Yeye ni nani? Ikiwa uko na shaka nitaomba sana keti na sisi na uliza maswali yako na tuangalia Bibilani kuona Yesu ni nani na tutoe shaka yako, kwa sababu ni muhimu sana.
Tusome mistari yetu ya leo. Kitabu hca Yohana 1:12-13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Neno la kwanza tunaona ni bali, au inaweza kuwa lakini. Na hii bali ni muhimu sana. Tunaweza kusoma vs.10-11 na tunaweza kufa moyo kwa sababu tunaona Yohnaa kusema hii yote kuhusu Yesu na kama yeye ni nani na amefika hapa kwetu. Kumbuka ilitabiriwa karibu miaka mia saba kabla ya Yesu alizaliwa kuhusu yeye. Kitabu cha Isaya 7:14 Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Tukienda kwa kitabu cha Mathayo 1:23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Mungu alikuwa hapa, Alitembea nasi. Yohana anasema hii kwa hizi mistari na watu walimkataa.
Halafu tunafika kwa vs.12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; Kwa sababu hii dunia na watu wake walimkataa Yesu si kumaanisha wote walimkataa. Si kama watu wa hii dunia walichafua mpango wa Mungu. Tutaona kwa Yohana 1:14 Yohana alisema Tukauona utukufu wake. Bado ni watu ambao watampokea Yesu kwa Masihi yao. NA itakuwa watu ambao Mungu alichagua kabla ya misingi ya dunia yamewekwa. Tunasoma hii kwa kitabu cha Waefeso 1:4 alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Tunasoma Yesu kusema kwa kitabu cha Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Ikiwa wewe ni mkristo leo asabuhi ni kwa sababu Mungu kwa mapenzi yake kabla ya dunia hata iliumbwa alikuchagua, so kwa sababu ya matedno yako au wema wako lakini kwa sababu ya neema yake. Hii ni sbabau wewe ni Mkritso leo asabuhi. Ikiwa ni wewe unajaribu kupata Yesu au ni wewe umechagua Yesu na wewe umepokea yesu halafu uko na shida. Hii yote ni kusema ni wewe umebadilisha maisha yako lakini sisi tlikuwa wafu katika dhambi zetu, mtu ambaye ni wafu hawezi kufanya kitu. Ni mzuri tuwache wokovu kwa mahali yake, kwa mwenyewe, mwenye wokovu ni Mungu nani zawadi yake anawapea watu ambao anataka. Ikiwa wokovu ni ya Mungu na ni yeye amekuokoa, halafu wokovu wako iko sawa kabisa, huwezi kupoteza, kwa sababu nani anaweza kutoa sisi kwa mikono ya Mungu? Hakuna mtu.
Tuko na vitu ambavyo tunaamini kuhusu Bibilia na sisi tunaamini ni kama Mungu anasema kwa neno lake. Sisi tunajali neno la Mungu na tunaiweka juu sana. Tuko na taarifa ya mafundisho sisi tunaamini na moja sisi tunaamini na tunakubaliana naye inaitwa 1689 London Baptist Confession of Faith. Kwa mlango wa kumi ya hii inasema kitu kuhusu wokovu na ni tamu sana inasema : Hao ambao Mungu amewachagulia uzima, anapendezwa kwa wakati wake teule na uliokubalika, kuwaita kikweli, kwa neno lake na Roho, kutoka kwa hali ya dhambi na kifo ambamo wako kiasili, hadi neema na wokovu kwa Yesu Kristo, akiwaangaza akili zao kiroho na kwa wokovu kupata kuelewa mambo ya Mungu, akiwaondoa roho yao ya mawe, na kuwapa roho ya nyama, aikfanya upya nia zao, na kwa uwezo wake mkuu akiwashuhudia kile kilichochema, akiwavuta kikweli kumfika Yesu kristo, hivi kwamba wanakuja kwa hiari, wakishafajujjnywa watake kwa neema yake. Mwito huu uzaao matunda ni wa neema huru na maalum ya Mungu pekee, haitokani na cho chote kile kilchoonekana kimbele kwa mwanadamu, wala kutokana na uwezo ama uwakala uwao ndani ya kiumbe, akiwa mle hana cha kufanya, amekufa katika dhambi na makosa, hadi pale anapohuishwa na kufanywa upyana Roho Mtakatifu, pale anawezeshwa kuitikia mwito huu, na kuikumbatia neema inayopeanwa na kuwakilishwa mle, na hilo linafanyikwa kwa uwezo usiopungua ule uliomfufua Kristo kutoka wafu. Hii ni kama tunaamini na kama tunafundisha. Watu wale watampokea Yesu. Tunaona kwa mstari yetu ya leo kwa Yohana 1:12 wakati tunasoma waliompokea ni kumanisha wameshika, na ni zaidi ya kushika kama Yesu anasema anaendelea kusema kwa hii vs.12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; Waliamini. Tutaona kuamini ni kitu kubwa kwa Yohana wakati anaandika kituabu hiki. Hata anatumia neno hili kuamini karibu mara tisini na nane. Kuamini ni kitu kubwa sana. Lakini watu wale wanaamini nini? Jina lake. Yesu. Wanaamini kwamba kila kitu tumesoma kwa hizi mistari ya kwanza hadi hapa ni ukweli, wakati wanasikia jina la Yesu ni kila kitu, Wanajua yeye ni Mungu, yeye ni muumbaji, yeye ni Masihi, mwokozi, yeye ni alfa na omega, hana mwanzo na hana mwisho, habadiliki watu ambao wanaamini wanashika kabisa maana ya Paulo wakati alisema kwa kitabu cha Matendo 17:28 ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Imani ambaye ni ukweli na inaweza kuokoa mtu ni imani ambaye inapokea Yesu kama Maandiko inasema kumhusu yeye.
Kwa wale watu ambao wanafanya hii Yohana anasema kwa vs.12 Aliwapa uwezo kufanyika watoto wa Mungu. Aliwapa uwezo ni kubwa hapa. Ni Yesu, si sisi, ametupea hii uwezo kufanyika watoto wa Mungu. Watu hawawezi kuokoka mpaka wanapokea na wanaamini katika yesu kristo, lakini wokovu ni kazi kuu ya Mungu ambaye anafanya kwa mtu ambaye ni wafu na kusema ukweli ni kipofu. Na haknuna mtu kwa historia nzima mabye amekuwa kipofu amerudisha macho yae mwenyewe. Ni mtu moja tu anaweza kufanya hii na ni Yesu. inapaswa kutunyenyekezakusikia maneno haya. Aliwapa uwezo kwetu kuaamini na kuwa watoto wa Mungu. Ikiwa bado unaamini sisi binadamu tuko na uwezo ndano yetu ya kufanya jambo fulani kuhusiana na wokovu wetu Nataka sisi kuangalia kitabu cha Waefeso 2. na hapa ni mananeo ambaye watu hawataki kusikia lakini Paulo ni wazi kabisa kuhusu sisi binadamu. Nataka sisi kuangalia vizuri vs.8-9 lakini tuangalia muktadha ya hizi mistari, Vs. tunasoma Tulikuwa wafu kwa sababu ya makosa na ya dhambi zetu. Vs.2 tunaona maisha yetu ilikuwa kutembea kulingana na ulimwengu huu na mfalme wa uwezo wa anga, hii ni shetani alikuwa bwana wetu. Vs. 3 tunaona tabia yetu ilikuwa kujipendeza kwa tamaa za miili yetu na hata tunaona tulikuwa watoto wa hasira, kumaanisha tulikuwa chini ya ghadhabu ya Mungu.
Sasa kwa hizi mistari nne tunaona sisi tuko na shida, hatuataki kitu cho chote na mambo ya Mungu, kusema ukweli yeye ni adui yetu. Halafu tunaona vs.4 Mungu anakuja ndani. Tunasoma Waefeso 2:4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; Aliyotupenda ni sisi ambao tulisoma kwa mlango wa kwanza mstari wa nne alisema alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuweka msingi ya ulimwengu. Mungu aliyotupenda hata Waefeso 2:5 wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; Natumaini sana unaweza kuona sisi na kama tulikuwa na sasa Mungu ameingia na anafanya kazi yake, tena anasema tulikuwa wafu na Mungu alituhuisha pmaoja na Kristo. Si sisi, si mimi ninatafuta Yesu, mimi ninajipendeza kwa tamaa zangu, mimi ninaendelea kufuata Mungu ya hii dunia, shetani mimi ninafikiri nikosawa na mbele yangu ni ghadhabu inaniongojea, lakini Mungu. na tunasoma vs.6 Ni yeye Akatufufua pamoja naye, Ni yeye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, na alifanya hii yote , katika Kristo Yesu; vs.7 Paulo anasema nema ya Mungu ilikuwa wingi sana, ilikuwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu. Ikiwa baada ya kusikia hii yote hunashukrani kwa Mungu wewe uko na moyo ngumu sana. Ikiwa majivuno yako haijaenda mbali wewe uko na shida kubwa sana.
Halafu Paulo anafika vs.8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema. Sioni tendo lo lote hapa sisi binadamu tumetenda. ni neema ya Mungu hata moja yetu ameokoka. na inafanuika kwa njia ya imani. Lazima tunaamini, lazima tunatubu kwa dhambi zetu na tunafuata Yesu kristo na tunatii neno lake. Bila imani hakuna wokovu. Warumi 10:17 ya sema imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Wahebrania 11:6 ya sema pasipo imani haiwezekani kumpendeza; Kumpedeza nani? Mungu. Lakini Paulo anasema kwa Waefeso 2:8 hata hii imani chanzo chake si ndani yetu, haitokani na nafsi zetu ni kipawa cha Mungu. Halafu tunaona Waefeso 2:9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Wokovu si kwa matendo yetu, si kitu sisi tunafanya. Kwa sababu ikiwa tunaweza kufanya kitu kupata wokovu wetu nitakuambia saa hii sisi tutajisifu. Sisi binadamu tunapenda sana kusema angalia kama nimefanya. Wakati Yesu aliingia hii ni sababu watu wake walimkataa. Walikuwa na mfumo yao ya matendo kufuata torati ili wanaweza kusema matendo yao yamewaokoa. Yesu aliingia na alisema matendo yako, kufuata toarati haiwezi kuleta wokovu, wokovu ni kipawa changu na ni kwa neema yangu. Wakati unafikiri ni matendo yako na unajisifu unafikiri hakuna hitaji kwa Yesu. Kila kitu ni juu yako na kama unafanya.
Nilitaka kuangalia hii sehemu ya Waefeso kabla ya tunasoma Yohana 1:13. Wakati mtu atasoma Yohana 1:12 wanaweza kufikiri binadamu ako na nguvu mingi kwa wokovu wake. Kwa sababu tunasoma walimpokea na waliaminio jina lake ni kama Mungu anaketi uko na anaongojea sisi kufanya kitu. Ni mzuri kujua, ni lazima tunaamini, ni lazima tunamkiri Yesu na kinywa chetu na tunaamini Mungu alimfufua katika wafu na moyo wetu, lazima tunatubu kwa dhambi zetu na tunafuata Yesu kwa njia ya kutii neno lake lakini lazima tunaamini hatuwezi kufanya vitu hivi bila Mungu kufungua macho yetu, bila Mungu kubadilisha mioyo yetu. na wakati anafanya hii tunaamini, tunampokea Yesu na wakati hii inafanyika Yohana 1:13 waliozaliwa, Tumezaliwa tena, tumekuwa kiumbe kipya, na anaendelea kusema si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, Mara ya kwanza tulizaliwa ilikuwa kwa sababu ya mama na baba yetu. Labda walipanga au labda hawajapanga lakini ilikuwa kwa sababu ya hawa. Lakini kama sisi wakristo tumezaliwa ni kwa sababu ya binadamu na mpango yao si kwa sababu ya mapenzi yao lakini sisi tumezaliwa kama anasema, bali kwa Mungu. Mungu ni baba yetu, Mungu alituchagulia kuwa watoto wake, ni yeye ametutoa kwa ufalme wa giza na ametuleta kwa ufamle wake wa nuru. Kusema ukweli tunaweza kuwa na shukrani kwamba wokovu ni ya Mungu, kwa sababu ikiwa ni sisi, tutapoteza haraka sana, lakini ni ya Yesu na Yesu hawezi kupoteza hata moja ambaye Baba aliyempea.
Labda uko hapa leo asabuhi na unajiuliza, mimi ni mmoja wa wateule? Mimi nitajibu, umeamini? Umetubu kwa dhambi zako? Unafuata Yesu kwa njia ya kutii neno lake? Ikiwa unajibu ndiyo, halafu jibu ni ndiyo. Ikiwa unasema hapana, nitaomba, tafadhali, weka imani yako katika Yesu Kristo na amini, tubu kwa dhambi zako, kuwa kiumbe kipya kwa nguvu ya bwana wetu. Mimi sijui ni nani Mungu amechagua, kazi yangu ni kuhubiri ukweli wa neno lake, ili anaweza kutumia kufungua mawazo na macho na mioyo ya watu ambao watasikia. Ikiwa leo unataka kuongea zaidi, niko hapa. Kuja baada ya ibada yetu na tutaketi pamoja na unaweza kuongea zaidi ukitaka.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.