What we believe about Creation and Evolution

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Various

· Wiki iliopita tulisherekea Pasaka natumaini sana umeshika sababu ya siku ile na umuhimu wake. Leo asabuhi kablaya tunarudi kwa kitabu cha Yohana nilitaka kuongea kuhusu kitu cha umuhimu sana. Ni umbaji na Evolution. Wiki chache iliopita nilisema kitu kuhusu hii kwa kanisa na tangu siku ile ni mambo mingi sana imetoka. Mimi nilianza kujua hata hii taka taka inafundishwa kwa mashule hata hapa Mara Christia Academy. Usikuwa na wasi wasi, sisi tumeketi Pamoja na walimu wote na hawa wako sawa kabisa, n ahata tulifanya chapel service moaja na wanafunzi na nilieleza kama sisi wakristo tunaamini. Lakini leo asabuhi nilitaka sisi kama kanisa na wazazi kujua na kuongea kuhusu vitu hivi na matokeo yao. Matokeo yao ni tofauti sana na ina madhara makubwa kwa Watoto wetu na hata kwa jamii yetu. Shida ni watu wingi wazazi wingi hawajui waoto wao wanafunishwa nini shuleni, na labda hata wakijua hawajui shida ni nini.
Tuombe:
· Nataka kuanza na Evolution. Evolution ni mchakato ambao spishi hubadilika kwa wakati kulingana na mabadilika ya mzingira yao na inakuwa kitu tofauti. Ukigoogle evolution utapata hii definition. Wakati unaendelea kuuliza maswali kama binadamu walitoka wapi au walianza wapi utapata majibu kama hii. Wanadamu waliibuka kwa mara ya kwanza barani Africa karibu miaka million ishirini iliopita. Na Baba na mama ya sisi sote ni sokwe au tumbili, Chimpanzee. Nyani ni ndugu na dada yetu. Hata wakati unaanza kuuliza dunia ilianza naam na gani utapata majibu mingi tofauti lakini mingi wanakubali kwa kitu inaitwa natharia ya mlipuko mkubwa, Big Bang Theory. Ukigoogle hii itakuambia maana ya hii ni uliwengu iliumbwa miaka billioni mingi iliopita kwa sababu ya mlipuko mkubwa. Kila kitu cha Evolution ni mfumo wa mtu, hii ni sababu huwezi kujua ukweli, hii ni sababu kila mtu anaweza kusema kitu tofauti ndani yake au miaka tofauti ya kila kitu. Hii mfumo inategemea binadamu kusema nini ni ukweli, kupima terehe ya kitu inategemea mfumo ya mtu ambaye hata yeye menyewe hajui. Hata hii mafundisho ya Evolution ilianza miaka mia mbili sabini na tano iliopita, Kablaya hii hakuna mtu amesikia kuhusu hii. Na ikiwa kitu ni miaka mia mbili sabini na tano, hawa watu wako na Ushahidi au utaratibu gani kufuata kusema kitu ni miaka biliono au milioni?
· Kusema ukweli Evolution ni dini ambalo watu wameanza kutumia kueleza kila kitu kuhusu wanadamu na umbaji na uliwengu bila Mungu. Ni dini kwa sababu inataka Imani mingi sana kuamini vitu vile.
· Sasa sisi Wakristo, watu ambao wameweka Imani yao katika Yesu kristo na kazi yake msalabani na neno lake tunaamini kitu tofauti kubwa sana. Sisi tunaamini Mungu anaitwa Yahweh, Elohim aliumba kila kitu na alituambia hii na alifanya naam na gani kwa neno lake kitabu cha mwanzo. Hii si mfumo ya binadamu, ni ya Mungu. Haijabadlika tangu imeandika mpaka saa hii, miaka elfu 3,500 iliopita. Musa aliandika kitabu cha Mwanzo. Adamu hadi Musa ilikuwa miaka 2,500. Hakuna kitu ni tofauti kusema ukweli kwa sababu ya Technology inahakikisha kila kitu ambacho imeandikwa kwa kitabu cha Mwanzo. Tusome Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Hii inatuambia nani aliumba kila kitu, ni Mungu halafu tunaona kwa hii mlango mzima anasema ameumba nini na nini. Siku ya kwanza ya umbaji tunaona vs.3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Aliumba nuru na giza. Lakini hii inatuambia njia ya Mungu kuumba kila kitu unaona? Mungu akasema. Mungu alinena na ilikuwa. Hajatumia kitu ambacho ilikuwa kujenga au kutengeneza alinena na ilikuwa. Pia tunaona vs.5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. Mwisho hapa tunaona ikawa jioni ikawa asabuhi, siku moja. Ni mzuri kujua ni watu wengine wanajaribu kusema Mungu aliumba nuru na giza halafu aliongoja miaka elfu moja kabla ya alianza na vitu viingine. Lakini sisi wakati tunasoma hii mstari tunaona nini? Ni siku moja, na hata leo tutakuwa na asabuhi na jioni na itakuwa siku moja, ni ukweli? Siku moja ni siku moja. Halafu siku ya pili aliumba anga, siku ya tatu aliumba nchi kavu, Bahari, majani na miti. Siku ya nne aliumba jua, mwezi na nyota. Siku ya tano tunaona vs.21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Siku ya sita aliumba wanyama wote wa nchi kavu halafu kwa mwisho tunaona vs.26-27 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Tunaona Mungu aliumba kila kitu kwa siku sita na kwa mwisho alituumba. Unaona ni tofauti sana ya Evolution. Na kila kitu Mungu aliumba ilikuwa kwa utaratibu si fujo. Evolution hata haiwezi kutuambia miaka ngapi iliopita hii yote ilifanyika na wakati ilifanyika ilikuwa ni mlipuko, na hata hayo mambo yalipogongana yalitoka wapi?
· Mungu wetu kwa neno lake anatueleza kila kitu na ilikuwa na mpango. Halafu baada ya kila kitu tunaona Mwanzo 2:1-2 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Baada ya kuumba kila kitu Mungu aliona kila kitu aliumba na alipumzika siku ya saba. Hii ni sababu tuko na siku saba kwa wiki yetu. Hii ni sababu jua inatoka asabuhi na mwezi inatoka usiku na tunajua siku moja imeenda. Kila kitu, kwa sababu Mungu aliumba iko nautaratibu. Waraka wa kwanza wakoritnho 14:33 ya sema Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani;
· Kwa mafundisho ya evolution uko na mafundisho mingi sana lakini mbili ingine ni Global Warming and Climate change. Global warming na Climate Change inafundisha kwamba tuko kwa dharura ya kimataifa, Global Emergency. Inasema joto la dunia inapanda kwa sababu ya sisi wanadamu, na wanasema ni kwa sababu sisi tunatumia diesel, gas, mafuta yo yote na pia kwa sababu ya kilimo au watu kulima. Pia wanasema kwa sababu tunakata misitu, transportation na hii ya mwisho ni mzuri sana, wanasema Carbon Dioxide au CO2 inaharibu dunia yetu. Ninyi unajua CO2 ni nini? Kila wakati unapumua ndani Oxygen inaingia halafu wakati unapotoa pumzi CO2 inatoka. Kwa sababu ya sisi wanadamu kupumua tunaaribu dunia yetu. Sisi sote kwa hii dunia tukohatarini kwa sababu ya mabadailiko ya tabianchi, Climate Change lakini shida ni sisi wanadamu tunapumua. Ni ajabu kusema ukweli . Unaona ujinga wa hii yote wakati unaanza kutoa Mungu kwa kila kitu.
· Global warming, Climate change and mafundisho yote ya Evolution lengo yao ni kutoa Mungu kwa kila kitu cha umbaji wake. Kusema ukweli wamefaulu. Amerikani huwezi kuomba shuleni, huwezi ongea kuhusu Yesu, huwezi vaa t shrit inasema kitu kuhusu Mungu. Hata ikiwa wewe ni mwalimu na unapatikana kuomba kabla ya darasa au baada ya mchezo utakuwa sacked. Ni ajabu sana lakini yote imetoka kwa hii mafundisho. Amerikani hata watu hawajui ikiwa hawa ni Mwanamke au Mwanamume. Mahali mingi mwalimu haiwezi kuingia darsa lake na kusema boys na girls kwa sababu labda anajitambulisha kama yeye ni paka leo na ukiuliza yeye swali anajibi na meow! Hata hivi karibuni nilisoma kijana miaka tatu alisema yeye ni msichana, alianza kuvaa dresses kucheza na vitu ya wasichana, sasa yeye amefika miaka saba na Baba amekataa huyu ni msichana lakini mama anasema yeye ndiye kama anajitambulisha, msichana. Mama na baba waliwachana na walienda kortini na hakimu alikubali msichana kukaa na mama yake. Mama alisema wakati mtoto wakea akotayri wataenda kwa daktari atatoa sehemu zake za siri, na watanza dawa ya kuleta vitu vya mwanamke.
· Hii inaanza kuwa kawaida kwetu Amerikani. Unashangaa! Kwa sababu ni ujinga kubwa. Amerikani tunaanza kuona zaidi na zaidi machoo. Kama kawaida uko na picha na mwanamume kwa mlango na unajua hii ni choo ya wanamume, au mwanamke na hii choo ni ya wanawake. Siku hizi uko na picha na ni ya mtu, panda moja ni mwanamume na panada ingine ni mwanamke. Lakini ni picha ya mtu moja. Kuonyesha choo ni ya kila jinsia. Unaweza kuwa na wanaume kuinga na wasichana kwa sababu wanaume wanasema hawa ni wanawake. Tukiendelea kuongea kuhusu hii nafikriri kichwa yangu italipuka, lakini hii yote inaanza kwa mafundisho mabaya, kwanza nyumbani hakuna mtu kufudisha hawa watoto halafu wanaenda shule na wanafundishwa hii uongo. Wazazi nataka ninyi kujua kitu cha umuhimu sana, mtoto wako atafundishwa, na itakuwa wewe nyumbani kufundisha hawa vitu vya bibilia na Mungu na Yesu au hii dunia itafundisha hawa. Lakini wakati unaanza kutoa Mungu kwa picha na neno lake unapoteza kila kitu hata wakati Mungu alisema baada ya Umbaji kwa mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Bila hii unaweza kuwa kitu cho chote, hata mbwa.
· Na wakati tunatoa Mungu tunanza kuona kitabu cha Warumi mlango wa kwanza kuwa kweli mbele ya macho yetu. Angalia Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Hapa tuko na watu ambao wanajaribu kutoa ukweli na waipingao kweli kwa uovu. Hawa watu ni nani? Anaendelea kusema vs.19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Ni watu ambao wamekataa Mungu Yuko. Lakini anasema ni rahisi sana kuona Mungu yuko kwa sababu Mungu amewaonyesha. Vs.20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; Mungu kwa umbaji wake ameonyesha wato wato yuko kila mtu wasiwe na udhuru. Lakini hawa watu wanaendelea kukataa hata macho yao na kila kitu wanaona na vs.21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Hawa watu walipotea katika uzushi wao na mioyo yao yenye ujinga wapi, ikatiwa giza. Sasa walianza kupata njia za kutoa Mungu kwa kila kitu, Na kwa sababu ya hii vs.22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; Hawa ambao wanasema wako na majibu ya hii yote, umbaji mwanzo ya wanadamu, hawa watu ambao dunia wanasema hawa ni smart, wamesoma wanajua, walipumbazika, walikuwa Wajinga. Na kwa sababu ya hii vs.23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Walitoa Mungu na walianza kuabudu miungu tofauti, vitu ya hii dunia, mafundisho ya binadamu, wanyama, ndege. Unajua saa hii Amerikani unaweza kuua mtoto tumboni la mama yake hata dakika moja kama anazaliwa. Daktari anaingia na mkasi na anakata uti wa mgongo, mtoto anakufa na iko sawa. Lakini ukiharibu au hata kuguza yai ya eagle, ndege unalipa faini ya shillingi milioni kumi na mwaka moja gerezani. Unaona tuko na shida, tukaubadili utukufu wa Mungu. Kwa sababu ya hii yote vs.24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Wakati unatoa Mungu halafu madesturi ya dunia yanaingia. Mungu anasema Waraka wa kwanza wakorintho 3:16-17 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. Ni mzuri sisi tunakumbuka hii. Mungu mwenyewe anaishi ndani yetu ya sisi ambaye ameokoa. Ni mzuri sisi tunachunga hii mwili na tunatumia kutoa sifa kwa Mungu wetu.
· Rudi kwa Warumi 1. Hii inaendelea kutuonyesha shida wakati tunatoa Mungu. Vs. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hii mstari inatuambia kabisa kuhusu mafundisho ya Evolution na climate change. Kila mtu anaweza kuangalia umbaji peke yake na kusema lazima iko na muumba lakini watu walichukia mungu zaidi mpaka waliibadili kweli wake kuwa uongo na walianza kuabudu kiumbe, hii dunia na vitu ndani yake na walitoa Muumba yake.
· Matokeo ya hii ni vs.26-27 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; Wakati unatoa Mungu na unaabudu kiumbe kuliko muumba ni hii. Hata si tamaa za kawaida lakini ni tamaa za aibu na hii ni wanawake wanaanza kutamani wanawake wengine na kulala na hawa vs.27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Hii yote ni matokeo kufundisha mafundisho ambaye inatoa Mungu kwa maisha ya watu. Lakini iko kwa mtihani, lazima inafundishwa. Unaona shida. Ni sababu dunia yetu iko kwa shida kubwa saa hii. Hata watu hawajui ikiwa hawa ni mwanamke au mwanamume lakini hii iko kwa mtihani. Na kwa sababu walitoa Mungu kwa kila kitu vs.28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Hii ni nini? Akili zao zisizofaa, vs.29-31 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
· Si kitu kidogo na sisi hatuwezi kukubali kwa sababu iko kwa mtihani fulani. Ndiyo tutafundisha, hata ni mzuri sisi na wanafunzi wanajua imani ya madini yengine ili wanaweza kupinga na neno la Mungu lakini haitafundishwa hapa kama ni ukweli. Wazazi tafadhali saidia watoto wako kujua ukweli au mtu mwengine atasiadia hawa kujua ukweli wao. Na wakati wewe umeshindwa kufundisha hawa usiketi na kushangaa kwa tabia ya watoto wako.
· Natumaini sana hii imesaidia ninyi kujua sisi tuko wapi na hii mambo yote kwa kanisa letu. Ikiwa uko na maswali tafadhali uliza.
· Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more