The Church

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 5 views
Notes
Transcript

What should we be doing?

Kwa dunia yetu siku zetu unaweza kupata watu wengi wanasema hawa ni Wakristo na wanaenda kwa makanisa mingi tofauti. Kila kanisa liko na sheria yake na majina ya kanisa siku hizi ni mingi sana tofauti. Wakati sisi tunaangalia vitu hivi ingeleta huzuni kwetu wakristo kuona kama jina la Bwana wetu linatumiwa. Ni ngumu sana kwa sababu tuko na neno lake na kanisa ni lake, sisi wakristo ni wake, na anatuambia kama anataka watu wake kuishi na wakati tunakuja pamoja tufanye naam na gani. Ni mzuri ninyi unasikia ni njia moja kama Mungu anataka watu wake kumwaabudu yeye, ni ukweli moja. Tunaweza kufanya musiki tofauti, tunaweza kufanya ibada yetu tofauti lakini bado ni lazima kama tunafanya inaleta heshima kwa Mungu kama neno lake inalazimisha. Nafikiri mara mingu tunasahau tunaingia pamoja kuabudu Mungu wetu. Nimesoma hii wiki Yakobo 2:19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Ikiwa mapepo wanatetemeka na sisi? Mara ya mwisho umefikiria Mungu na umetetemeka ni lini? SIku zetu kwa makanisa mingi sana dunia nzima Mapastors hawahubiri neno la Mungu jinsi wanavyopaswa. Wanachafua sana na wanaruka vitu ambavyo inaweza kumkosea (offend) mtu. Wanaweka Mungu ya uongo kwa mawazo ya watu, Mungu wanahubiri siku hizi ni upendo tu, bila kuonyesha ako na ghadhabu pia, Ni neema na rehema bila utakatifu. Mungu kwa watu wengi ni mtu ambaye anaketi uko juu mbinguni na anatuongojea kuuliza kwa pesa au afya au zawadi fulani halafu labda ikiwa wewe ni mzuri utapata. Hii yote si Mungu wetu, si Mungu wa bibilia.
Nataka sisi kusoma sehemu ya maandiko ambaye ni mzuri sana. Paulo anaongea na Timtheo na anaongea na yeye kama mfanya kazi ya Mungu. Tunajua Timotheo alikuwa pastor ya kanisa la Efeso na Paulo alimaacha hapo kuhubiri injili ya Yesu. Paulo anaongea na yeye kama kiongozi lakini nafikiri hizi mistari ni mzuri kwetu sote kama Wakristo. Hii ni lemgo yangu kwa kila mtu ambaye anaketi hapa leo asabuhi na anasema yeye ni Mkristo. Tusome Waraka wa pili watimotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Hii ni nneo la Mungu wetu.
Tuombe:
Kama nimesema makanisa siku zetu wanafanya vitu vya ajabu na hata unaweza kujiuliza kwa nini wanafanya vitu hivi, haviko kwa neno la Mungu. Siku moja sisi sote tutasimama mbele ya Mungu, na kwangu nataka kusema nimefanya kama nimesoma kwa neno lako, nataka kusema nimejaribu na bidii kushughulikia ukweli wako na nimefundisha kundi lako kufanya hii pia.
Swali ni hii. Kama kanisa na kama tunasoma kwa neno la Mungu wetu, tuwe tunafanya nini kanisani? Nataka kutoa vitu sita kwetu leo asabuhi. Na sijapata vitu hivi kwa TikTok au kwa kitabu fulani ya program kusaidia maisha yangu, yote ni kwa bibilia. Ikiwa unatafuta kanisa ya kuwa mshariki ya kanisa lile hakikisha wanafanya vitu hivi .
Kitu cha kwanza ni Usomaji wa Maandiko hadharani (Public). Ni lazima tunasoma bibilia wakati tuko pamoja kanisani. Wakati Paulo aliandika Timotheo Barua yake alisema kwa Waraka wa kwanza Watimotheo 3:15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Sasa hii ni mzuri sana kwa sababu Mtume Paulo mmwenyewe alisema anataka kumwambia Timotheo iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, halafu ikiwa hii haijakuwa wazi anasema iliyo kanisa la Mungu. Wakati tunasoma kitu kama hii, kumbuka hii ni neno la Mungu, ni Mungu mwenyewe anatuambia kama anataka wakati tunakuja pamoja kumwaabudu. Halafu Tunaona anaeleza kwa mlango wa nne anaanza kuisema nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, watadanganywa na mafundisho ya mashetani, halafu tunasoma 4:3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, sisi hatutaki kufanya hii, ni uongo. Halafu anasema vs.6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata. Neno la Mungu ni kila kitu kwetu wakristo, ni chakula chetu cha roho zetu. Inaweka mawazo yetu na macho yetu kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Halafu tunafika vs.13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma. Kwa kiingereza inasema Until I come, give attention to the public reading of Scripture, Hata nitakapokuja, angalieni usomaji wa Maandiko hadharani. Hakikisha wakati unatafuta kanisa au ikiwa unaenda kanisa fulani wanasoma hadharani maandiko. Si wakati wanahubiri peke yake. Hii ni sababu kila jumapili utaona sisi kuanza na maombi halafu Jonathan anasimama mbele yetu na anasoma neno la Mungu, wakati huu tunasoma zaburi. Ni muhimu sana sisi tunasikia neno la Mungu. tuko hapa leo asabuhi kwa sababu ya neno la Mungu, inatuambia kila kitu kuhusu Mungu, yesu, Roho, Binadamu, Umbaji, sababu sisi tuko hapa, shida yetu ya dhambi, wokovu, kila kitu. Inatuambia kuhusu kanisa, na wakati tunakuja pamoja, viongozi wa kanisa. Ikiwa unaenda kanisa ambalo hawafungui neno la Mungu, kimbia haraka kwa sababu si kanisa la kweli.
Tunaona Paulo anaendelea kwa Waraka wa kwanza Watimotheo 4:13 kusema baada ya ufanye bidii kusoma na na kuonya na kufundisha. Kitu cha pili kwetu kufanya kanisani ni Lihubiri neno. Waraka wa pili watimotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Ni lazima sisi viongozi wa kanisa tunahubiri neno. Ikiwa unaenda kanisa ambalo wanashika bibilia na mkono yao lakini hata hawawezi kufungua, ni mzuri unakimbia. Siku hizi makanisa mingi wanahubiri maneno ya binadamu, wanakula kundi la Mungu na hawa ni fake kabisa, Hawana kitu cha kusema kuleta faraja, tumaini, kutia moyo ya mtu, hakuna maneno ya uzima wa milele. Wale wanajali programs na wanataka kuhakikisha viti vimejaa kanisani, wanataka kupendeza watu hata ikiwa hawa ni wasioamini. Paulo anamwambia Timotheo Lihubiri neno na uwe tayari, wakati ukufaao na usiokufaa. Ni kwetu kujua neno sana zaidi hata ikiwa mtu anataka kuongea sisi tukotayari, ikiwa mtu ako na swali, tuko tayari kutoa majibu kutoka neno la Mungu. Lazima ikiwa tutakuwa naam na hiyo, sisi tuatkuwa watu ambao tunaishi ndani ya neno la Mungu, Tunaomsa, tunafikiria, tunatenda kama inasema, halafu tutakuwa tayari kutoa majibu. Nataka ninyi kusikia, ikiwa unafikiri unaweza kufika hapa kwa masaa mbili kila wiki na kuketi hapa kwa kiti na kusikia mafundisho ya jumapili peke yake na kutoka hapa na kuwa tayari hii ni uongo. Lazima wewe mwenyewe uko ndani, unasoma, unaweka kwa mawazo yako na unatenda kama inasema, halafu utakuwa tayari. Na tuko naam na hiyo ili tunaweza kukaripia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu na mafundisho.
Kanisa hii ni lazima kwa masiha yetu kama kanisa la Yesu kristo, na ukiendelea kusoma utaona sababu sisi tunafanya kama hii, angalia Waraka wa pili watimotheo 4:3-4 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Lihubiri neno ni lazima. Kanisani ndiyo ni walimu na pastor lakini hii ni kwetu sote, kila siku ya maisha yetu, nje ya hii nyumba. Ikiwa kanisa lako halihubiri neno, wewe pia hutalihubiri neno.
Kitu cha tatu ni lazima sisi tunafanya kanisani ni maombezi (intercessions). Waraka wa kwanza watimotheo 2:1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; Lazima sisi wakristo wakati tunakuja pamoja tunaomba, tunaongea na Mungu wetu si kwetu peke yetu lakini kama anasema kwa watu wote. Tunaomba kwamba Mungu atafungua mawazo yao na mioyo yao kusikia ukweli wake na wataamini katika Yesu Kristo. Makanisa mingi siku hizi wakati wanaomba hata huwezi kujua wanasema nini, katika jina la Yesu ni maneno yao zaidi ya nusu ya maneno yote wanasema. Lakini kwetu tunajua hii si kama Mungu anataka. Mathayo 6:7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Sisi tunataka kuomba na moyo safi na tunataka kukumbuka washiriki wetu na wagonjwa wetu, Wasioamini kwa community yetu halafu hata ni ngumu najua lakini Paulo anaendelea kwa Waraka wa kwanza watimotheo 2:2 kusema kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hata kwa viongozi wetu, rais yetu, watu ambao wanaongoza nchi na county. Tunaomba kwa watu wale kwamba wataongoza kwa njia ambaye itampendeza Mungu. Wakati tunaomba na Mungu anajibu inajenga imani yetu hata zaidi na Mungu wetu. Hakikisha kanisa unaenda wanafanya hii.
Kitu cha nne ni lazima sisi tunafanya kanisani ni kuimba. Waefeso 5:19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; Kuimba ni muhimu sana, inaweza kutia mioyo yetu wakati tunaimba. Lakini ikiwa unaangalia hii mstari inatuambia jinsi tunapaswa kuimba. Na ukiona si kama makanisa mingi sana siku hizi wanaimba. Anasema zaburi, tenzi na nyimbo za rohoni. Hii yote imetoka neno la Mungu. SIku hizi uko nyimbo mingi zaidi na labda suati yake ni mzuri lakini ukisikia maneno yake unashangaa, hata si mzuri, huwezi kujua ikiwa mtu anaongea na Boyfriend au girlfriend yake ama anaongea na Yesu. Nyimbo zingine zinafundisha mafundisho mabaya kuhusu Mungu na ni uongo. Tunataka kuhakikihsa nyimbo zetu zinaongea kuhusu Bwana wetu na wanampea sifa si kusifa binadamu. Ukitaka kujua mambo ya nyimbo zetu angalia Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Kitu cha kwanza unaona ni neno la Kristo likae wingi ndani yenu. Wakati unajua neno la Mungu na unajali neno la Mungu zaidi na utakuwa na hekima yote na unaweza kujua ukweli na uongo. Utajua sababu ya kuimba pamoja na zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, na anasema Mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Hii ni lengo yetu wakati tunaimba, ni mzuri tunakumbuka hii.
Kitu cha tano ni Ubatizo. Ni muhimu sana kwa kanisa tunabaptiza watu ambao wanaweka imani yao katika Yesu kristo. Yesu mwenyewe alisema kwa Mathayo 28:19-20 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Wakati tunafanya ubatizo ni kumaanisha sisi, watu wa Yesu tukawafanye mataifa kuwa wanafunzi, sisi watu wa Mungu kama raia wazuri, tunaongea na wengine kuhusu ufalme tumeingia na mfalme wa ufalme tumeingina na ni Yesu, hawa wanaamini na wanatoka ufalme wa giza na wanaingia ufalme wa nuru. Njia moja ya kuonyesha wanafuata mfalme mpya ni ubatizo. Ni mzuri tunafahamu ubatizo haiwezi kuleta wokovu. Ni wingi nimeongea na hawa na hawajashika maana ya ubatizo vizuri au labda wamefundishwa vibaya. Wokovu inakuja kwa njia ya kumkiri Yesu na kinywa chako ya kuwa yeye ni Bwana na kuamini Mungu alimfufua katika wafu na umetubu kwa dhambi zako, ni hii. Ubatizo ni ishara kwamba sasa unafuata Yesu na maisha yako na unataka watu wote wa hii dunia kujua Yesu ni Bwana wako na alisema kufanya ubatizo kuonyesha hii. Si kama inasafisha dhambi zako, ni damu ya Yesu imefanya hii, si lazima mtu amebatiza kuingia mbinguni, ikiwa hii ni ukweli, halafu mwizi alisulibishwa pamoja na Yesu ako na shida. Yesu alisema leo utakuwa peponi nami. SI kama wajeshi waroma walisema, huyu ameamini tutoe yeye kwa msalaba tumbatize halafu turudishe yeye kwa msalaba. Waroma hawajajali vitu kama hii. Tena ubatizo ni ishara tu, kwako kuonyesha wasioaminin a waamini pamoja kwamba wewe unafuata Yesu na maisha yako. Hii maji unaingia si kitu tofauti ya maji unakunywa au maji unatumia kufua nguo zako.
Tumeangalia vitu hivi ni lazima sisi wakristo tumefanye kanisani, Usomaji wa maandiko hadharani, lihubiri neno, maombezi, kuimba na ubatizo. Kitu cha sita ni meza ya Bwana. Hii ni kitu ambacho watu wamechafua sana, na ni kitu ambacho ni muhimu zaidi kwetu wakristo kufanya kanisani. Ni kitu ambacho Paulo alipokea kutoka Yesu mwenyewe. Angalia Waraka wa kwanza wakorintho 11:23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, Halafu anaendelea kusema wakati Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi wake na wanakula pamoja, ni usiku ile Yuda alimsaliti Yesu na Paulo anatoa Utaratibu ya kufanya meza ya Bwana. Tuko na mikate na kikombe. Mikate ni kukumbusha sisi ya mwili wa Yesu ambaye ilivunjikwa kwa ajili yetu, halafu kikombe, bila shaka ilikuwa na divai ndani yake ilikuwa kukumbusha sisi ya damu ya Yesu ambaye ilimwagwa kwa ajili ya dhambi zetu na ilileta sisi kusimama haki mbele ya Mungu. na sababu tunafanya meza ya Bwana Paulo anasema kwa Waraka wa kwanza wakorintho 11:26 kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Ni mzuri kwetu wakristo kukumbuka hii yote Yesu amefanya kwetu na pia kutangaza mauti ya Bwana wetu na sababu yake. Hii si kwa wasioamini hata kwa watu ambao ni wakristo lakini wanaishi dhambini. Ikiwa unaishi dhambini kabla ya unafanya meza ya Bwana ni mzuri kutubu kwa dhambi zako . Paulo alisema wingi wanafanya vibaya, isivyostahili na watu ambao wanafanya hii Paulo alisema ni dhaifu, wagonjwa na wengine wamekufa. Si mchezo na inaleta watu wa Mungu kuwa safi moyoni mwao.
Vitu hivi ni muhimu sana, kama nimesema ikiwa unatafuat kanisa ya kuingia na kuwa sehemu yao, hakikisha wanafanya vitu hivi na wanafanya vitu hivi kama neno la Mungu inasema kufanya. Tuko na neno la Mungu wetu na iko na kila kitu ndani yake kwetu wakristo. Paulo anaongea kuhusu Maandiko na alimwambia Timotheo kwa waraka wa pili watimotheo 3:17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. Natumaini sana hii itakuwa sisi hapa kwa AIC Sekenani.
Labda leo asabuhi wewe uko hapa na wewe hujaweka imani yako katika Yesu kristo, leo ni siku yako. Ni kuamini katika yeye na maisha yake na kazi yake na kifo chake. ALikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na baada ya siku tatu alifufuka na hii ni tumaini letu. Ukitaka kuongea zaidi karibu mbele baada ya ibada yetu. Labda uko hapa leo na huna kanisa, wewe si member au mshariki ya kanisa na unataka kujua zaidi kuhusu kanisa letu, karibu kuongea na sisi kuhusu hii pia.
Asanteni sana, Bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.