Commandment of God vs. the Tradition of Men
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 1 viewNotes
Transcript
Matthew 15:7-9
Matthew 15:7-9
Kabla ya tunaingia masomo yetu katika kitabu cha Yohana nilitaka kuongea kuhusu nafikiri watu wengi wanasema na inaleta mkanganyiko kwa wale wanosikia. Ni hii kitu watu wansema wakati unaongea kuhusu bibilia na kama inasema na hawa wanasema kitu tofauti. wansema lakini Mungu ni moja. au sisitunaabudu Mungu moja. Kama mimi nimeanza kusikia watu kuongea kama wanaamini ninaweza kusema wazi, Mungu hawa wanaabudu si Mungu wa biblia, na ikiwa si Mungu wa bibilia si Mungu wangu na sisi tunaabudu Mungu tofauti. Mungu kwa neno lake ni wazi kama anastahili kuabudiwa na ni mzuri tu chunge sana kwa sababu watu wengi wanasema wanaabudu mungu wa biblia na ni Mungu wameumba na desturi lao. kutumia lugha ya agano la kale watu wale wakatoa moto ya kigeni mbele ya Bwana.
Tuko na hizi mistari kwa agano la kale unashangaa kidogo kusoma ni Mambo ya walawi. Kabla ya tunaosma ni mzuri unashika kwamba
tuko na wana wa Haruni hapa na Haruni ndugu ya Musa alikuwa kuhani mkuu Mungu mwneyewe alichagua. Na sasa wana wake wanaingia kuwa makuhani ya Mungu pia. Wameona baba yao maisha yao yote walijua mahitaji Mungu ameweka kwa makuhani yake. Sasa tunafika hii mahali mbapo watu walikuwa pamoja na makuhani wanatoa sadaka yao kwa watu waisraeli na Mungu aliandika kama ni lazima watu wanafanya hii na tunasoma wa Mambo ya Walawi 10:1-2 Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza. Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana. Sisi tunasoma hii na tunashangaa kidogo, shida ilikuwa nini? Shida ilikuwa hawa wawili hawajafanya kama Mungu alitaka , tunaaona wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, hii ni moto ambaye haijapendeza Mungu. Pia nataka sisi kukumbuka mstari ya umuhimu sana Wahebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Yesu Kristo ni Mungu. Na hii mstari inasema Habadiliki. Bado Mungu wetu ya leo ni Mungu ambaye aliua wale makuhani kwa sababu hawajafanya kama alisema. Kama sisi tunaabudu Mungu na kama tunafundisha neno lake ni muhimu zaidi.
Tusome mistari yetu ya leo Marko 7:1-9 Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake, wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba. Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
Tuombe:
Kwa hii sehemu ya maandiko tunaweza kuona Mafarisayo na waandishi. Hawa walikuwa viongozi wa wayahudi kwa mambo ya Mungu na hawa walipenda sana kuongeza sheria kwa watu, sheria ambayo Mungu hajasema. Yesu alieleza Mafarisayo na Waandishi ni nani ukweli kwa wanafunzi wake kwa kitabu cha Mathayo 23:4-7 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Ukiendelea kusoma Mathayo 23 Yesu anaonyesha hawa ni nani vizuri sana. lakini Tuliona vs.4 wanapenda sana kuweka mizigo mizito juu ya watu na wanafundisha vitu hivi vimetoka Mungu na wanajali vitu ya nje ya mtu kuliko mioyo yao na kama imebadilishwa. Yesu alisema walikuwa wana wa Jehanum. Kumaanisha wale watu wa dini, wale wanaongoza watu wa Mungu kwa sheria zake walikuwa wasioamini. Na leo nafikriri ninyi unajua kwa sababu ni rahisi kuona, hata kwa siku zetu tuko na mafarisayo na waandishi wingi.
Rudi kwa Marko 7. Ni mistari ya mwisho ya mistari yetu leo nataka sisi kuangalia. Mwisho ya vs.7 anasema kama Isaya alitabiri Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Halafu vs.8 Yesu anasema Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Kama nimesema wakati tulianza leo watu wengi wanasema Mungu ni moja. Nataka sisi kujua tofauti ya dini nyingine na tuko na hawa watu hata hapa leo asabuhi. Sitaki mtu kufikiri ninchapa mtu au kiti kama hii lakini nataka kuonyesha kama wanaamini na ikiwa ni kutoka neno la Mungu au ni desturi lao wanafundisha kama ni neno la Mungu.
Kwanza ni Wakatholiki. Na siwezi kwa jumapili moja kueleza kila kitu wanaamini so nitajaribu kuongea kuhusu vitu vichache tu. Kitu cha kwanza ni wanaweka pope na mabaraza ya kanisa kuwa sawa sawa na Bibilia. Hii ni sababu Wakatholiki wingi hawasomi bibilia. Wanategemea kama kanisa watawaambia. Pia wako na vitabu viingine wanaweka sawa sawa na Bibilia moja inaitwa Apocrypha. Hii ni sababu moja tulikuwa na matengenezo au Reformation zaidi ya miaka mia tano iliopita. Kila jumapili mkuhani fulani atasimama mbele ya watu wake na watu hawajakuwa na bibilia kwa lugh ayao, na huyu mkuhani atasimama na ataanza kusoma bibilia kwa lugha ya Kilatini (latin) hakuna mtu anafahamu hii lugha ni mkuhani peke yake. Baada ya kusoma ataeleza maneno alisoma lakini shida anadanganya watu na alisema vitu ambavyo Mungu hajasema. Hii ni sababu ilikuwa muhimu sana kila mtu alikuwa na bibilia kwa lugha yake, ili yeye mwenyewe anaweza kusoma na kuona kama inasema. Wale ambao walitafsiri bibilia kwa lugha za watu, wengi waliuuawa na kanisa la Katholiki kwa sababu Wakatholiki walijua ikiwa watu wanasweza kusoma bibilia peke yao hawawezi kudanganya hawa. Lakini hata leo asabuhi tuko na watu wataamini kama Pope ama Makuhani yao watasema kuliko Bibilia na tutaona mafundisho mabaya hii imeleta.
Kitu cha pili ni Mariamu. Kama Wakatholiki wanaweka Mariamu ni hatari sana. Wanaweka yeye kati kati ya watu na Yesu. Huwezi kupata hii bibliani. Bibilia ni wazi kabisa kuhusu hii. Angalia Waraka wa kwanza watimotheo 2:5 Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; Si Mariamu, MAriamu alikufa na aliwekwa kaburini na hajafufuka. Hata Mariamu aliaamini katika Yesu Kristo kupata wokovu. Bila kuamini hakuna wokovu kwa mtu yo yote. Hii mambo ya Mariamu ni desturi tena ya kanisa la Katholiki. Na kama wanaweka yeye na watu wanamwomba ni mbaya sana. Sisi tunaomba Mungu pekee. Sasa yeye ni mungu, yeye ni mungu mdogo? Wakati wanafanya hii wanaweka Mariamnu kuwa sanamu. Nitakuambia wazi saa hii, Mariamnu hawezi kukusaidia. Tena fuata Maandiko si desturi.
Kitu cha tatu ni kuzaliwa upya kwa ubatizo (Baptisimal Regenration). Wanasema wakati Mkuhani anaweka hii maji juu ya kichwa ya mtoto inaleta wokovu. Ni hii maji inatumiwa kwa sababu ya mkuhani na kazi yake kuweka hii maji inatoa dhambi za huyu mtoto na inaleta hawa kuzaliwa mpya. Shida ya hii ni wakatholiki wingi sana wanaweka tumani lao kwa hii kusema wameokoka. Hawa na uhusiani na Yesu, hawa na imani katika Yeye, hawampendi Yesu lakini kwa sababu ya hii kitu imefanyika kwao wakati walikuwa mtoto, wanajua wanaenda Mbinguni. Sasa hii ni kuweka imani yao katika matendo yao, kusema ukweli hata si matendo yao, ilifanyinka wakati walikuwa wadogo, ni katika imani ya desturi lao na maji na mkuhani. Ni mzuri unajua Dini la Katoliki ni dini la Matendo, si kama Paulo aliwaambia kanisa la Wagalatia ni imani katika Kristo pekee. Na pia ni mzuri sisi sote tunakumbuka kama mtume Petro alisema Kitabu cha Matendo 4:12 hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Ikiwa hujui hii ni nani anasema kwa vs.10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Hakuna tendo fulani hakuna mtu fulani ni Yesu kristo peke yake.
Kitu cha nne Indulgences. Kwa kiswahili ni Msamaha. Waacha nitumie indulgence. Sasa Indulgence ni kitu moja kitambo wale makuhani watasimama mbele ya watu wao na watasoma Bibilia na hakuna mtu anajua anasema nini kwa sababu ya lugha na mkuhani atasema Mungu amesema lazima watu wanalipa hii kitu inaitwa indulgence ili roho za wale watu ambao wameshaa kufa kama marafiki au famili wanaweza kupata nafuu (relief) kwa sababu wanateseka toharani (Purgatory). Toharani ni mahali mbapo roho za watu zinaenda kuendelea kulipa kwa dhambi zao kwa muda, na wakati wamemaliza kulipa wanaweza kuenda mbinguni. Lakini ikiwa wewe uko hapa bado na unalipa hii indulgence, halafu huyu mtu wa familia yako atapata pumziko la mateso kwa muda fupi. Unasikia vitu hivi unashangaa, mtu anaweza kuuliza ikiwa bado tunaongea kuhusu Mungu na Bibilia na Yesu. Lakini unaweza kuona sababu kanisa la Katoliki wako na pesa mingi sana. Kwa sababu hakuna mtu anataka familia yake kuteseka toharani, Kwa hivyo wanalipa na ukilipa zaidi, huyu mtu ambaye anateseka atapumzika zaidi. Unajua si mimi ninasema vitu hivi ni mafundisho ya kanisa la katoliki. Nimeenda kwa website ya kanisa moja yao na ni hii wamesema : “Kusamehewa ni ondoleo la adhabu ya muda mbele ya Mungu kwa ajili ya dhambi ambazo hatia yake tayari imesamehewa, ambayo Mkristo mwaminifu ambaye ameadhimishwa ipasavyo huipata chini ya masharti fulani yaliyoamriwa kupitia tendo la Kanisa ambalo, kama mhudumu wa ukombozi, hulitoa. na hutumika kwa mamlaka hazina ya ridhiki za Kristo na watakatifu.” Hii ina maana kwamba mtu tayari ameshaadhimisha sakramenti ya Kuungama na Upatanisho, ameungama dhambi zake, amepokea ondoleo, na amekamilisha kitubio. Kwa hivyo, msamaha sio mbadala wa Sakramenti. Ni ziada ya kisakramenti na inahusisha dhana ya haki ya kimungu. Hata baada ya dhambi zetu kusamehewa, haki inayodaiwa na Mungu - ikimaanisha malipo ambayo tunaweza kuwa na deni kwa Mungu kwa ajili ya dhambi ambazo tumetenda -, Sasa na tumaini sana ninyi unaona shida na kama wanasema, bado tuko na deni kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zetu? Ni jabu sana. Wanaendelea kusema: bado ni sehemu kubwa ya maisha yetu. Tunazungumza juu ya hili mara nyingi kuhusiana na Purgatory, kuwepo kwa nafsi baada ya kifo ambapo adhabu ya muda (maana ya adhabu ya asili fulani yenye mipaka) kwa ajili ya dhambi inakamilika. Sadaka ni zawadi kwetu kutoka kwa Mungu kwa njia ya Kanisa ambayo kwayo sisi katika maisha haya tunaweza kutimiza hitaji lolote la haki ya kimungu ambalo tunawiwa na Mungu kwa kushiriki ipasavyo katika kazi ambayo Kanisa limetupa ili kupokea neema ya Mungu. anasa. Hii si mimi ninasema kama wanaimni ni hawa. Kusema ukweli tunaweza kukaa hapa kwa muda kwa sababu ni uongo sana, lakini kwa sababu ya Muda tuangalia Kitabu cha Wahebrania 10:10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Sitaki ninyi kukosa kama nimesoma, umeona sisi wakristo, watu ambao tumeokolewa, tumeokolewa tumetakaswa kwa yesu kristo, na ni muhimu sana unaona hii ya mwisho mara moja tu. Wakati Yesu alikuwa mslabani na amesema imekwisha, amemaanisha, imekwisha, dhambi zimelipia kwa watu wake. Anglia Wahebrania 10:11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Sasa ikiwa hata makuhani wanasimama na wanatoa dhabihu mara mingi kwa dhambi na kama mstari inasema haiwezi kabisa kuondoa dhambi, halafu wewe utafanya nini. Wakatoliki wanasema bado tuko na deni na Mungu, angalia vs.12 Lakini huyu, huyu ni nani? Yesu Kristo, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; Yesu alitoa dhabihi moja kwa ajili ya dhambi halafu aliketi, waqkati aliketi ni kumaanisha imekwisha. Hatuwezi kuongeza kwa dhabihu yake. Halafu vs.14 kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Mkristo, huna deni na Mungu, Yesu Kristo ameshaa lipa. Tunaweza kukaa hapa sana, kwa sababu hii ni mbaya zaidi, hii mafundisho yao inaweka kifo cha Yesu kuwa kitu kidogo kama haina nguvu ya kutosha.
Kitu cha tano na ni kama inaendelea kwa hii ya nne. Lakini mafundisho yao kuhusu kuhesabiwa haki. Wakatoliki wanaamini unaweza kuwa na imani lakini kuhesabiwa haki lazima inakuja kwa njia ya matendo yako, wanasema unaweza kupoteza wokovu wako. Nimepata hii kwa webiste ya kanisa la Katoliki inasema: mwamini anaweza kuanguka kutoka kwa imani, inafuata kwamba mwamini anaweza kupoteza uzima wa milele ambao anao sasa. Kwa hali hii, umiliki wa sasa wa uzima wa milele kupitia imani haimaanishi kuwa mwamini hatahukumiwa kamwe. Sasa mingi inategemea matendo yako na kama unaungama dhambi zako, si kwa Mungu lakini kwa mkuhani yako. Hawa wanasema unapata imani wakati unafanya sakramenti ya katoliki. Tena wakristo natumani sana unaona shida kubwa sana na hii. Angalia Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, Halafu angalia Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kumbuka kama tumesoma kwa Wahebrania hii imefanika mara moja tu, si kwetu kuendelea kujaribu kuogeza matendo yetu kwa kazi ya Yesu. Sasa ni kwetu kufuata neno lake na kuitii, lakini wokovu na kuhesabiwa haki inakuja kwa njia ya imani katika Kristo na kazi yake si kazi yetu.
Kitu cha sita. ni meza ya Bwana. Wakotoliki wanasema wakati wanafanya meza ya Bwana, mikate inakuwa mwili wa Yesu kweli kweli na divai wakati wanakunywa inakuwa damu ya Yesu kweli kweli. Ni mbaya sana kwa sababu wanafikiri wakati tunafanya meza ya Bwana Mwili na damu ya Yesu inaingia ndani yetu. Wingi wamedanganywa kufikiri wanaokolewa wakati wanafanya meza ya Bwana. Hii ni sababu watu wengi waliuawa kwa sababu walisema meza ya Bwana haijakuwa mwili na damu ukweli wa Yesu. Lakini ni kutukumbusha kama Bwana wetu yesu kristo alifanya kwetu. Angalia Waraka wa kwanza wakorintho 11:24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Unaona sababu> Yesu mwenyewe alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu. Vs.25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Tena kwa ukumbusho wangu. Halafu tunaona wakati tunafanya hii inafanya nini. Vs.26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Kama unafikiri kuhusu meza ya Bwana ni muhimu sana.
Kitu cha saba ni Toharani au purgatory. Sasa hii wanasema ni baada ya mtu amekufa anaweza kuenda kwa mahali hapa na kuteseka kwa muda kulipa kwa dhambi zake, na baada ya amelipa ya kutosha atapewa nafasi ya pili na anaweza kuingia mbinguni. Hii ni uongo zaidi. Ukikufa na wewe ni msioamini, hujaweka imani yako katika Yesu kristo, Bibilia ni wazi sana, na hakuna mahali bibliani nzima inaitwa Toharani. Tena hii ni walimu wa uongo walianza kuleta hii mafundisho ya uongo kuchukua pesa za watu, kumbuka ukilipa indulgences inasaidia wale ambao wamekufa na wanateseka Toharani. kama unalipa ni kama watapumzika kidogo. Ni kama wanauza wokovu, wameweka bei kwa watu kuingia mbinguni. Lakini Bibilia ni wazi, ni mstari mingi sana kutuonyesha ukikufa bila Yesu unaingia jehanamu na ni kwa milele, hakuna nafasi ya pili. Wahebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Kifo na hukumu, kwa watu ambao hawajajua Yesu kuteseka kwa milele na kwa wale amabo Yesu ni mwokozi wao, uzima wa milele.
Tumeenda sana na tumefika moja tu, ya Katoliki. Na bado ni mambo mingi sana Wakatoliki wanaamini hatujaongea. Kama Shanga za Rosari, Hii msalaba Wakatoliki wanavaa na bado Yesu ako msalabani. Ni mzuri ninyi unashika kwamba Yesu wetu wa bibilia ametoka msalba na amefufuka na ameshinda kifo na mauti. Kurudisha yeye kwa msalaba si mzuri. Lakini natumaini sana unaweza kuona kama Yesu alisema kwa Viongozi wa wayahudi, Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. Na bado watu wanafanya hii leo sana kama tumeona kwa Wakotoliki.
Ikiwa leo asabuhi umeaamini vitu hivi nitasema tafadhali tubu kwa dhambi zako na weka imani yako katika Yesu kristo na yeye peke yake, kwa sababu nje yake, hakuna tumaini. Ikiwa unataka kuongea na sisi, tutapenda sana kuketi na kueleza zaidi. Karibu baada ya ibada yetu.
Asanteni Sana, Bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo, tutaongea kuhusu Seventh Day.