The Bad News

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Hebrews 9:27

Leo asabuhi nataka kuongea kuhusu kitu ambacho ni muhimu Zaidi, na polr kusema lakini ni kitu kibaya. Tunaweza kusema ni habari mbaya, si kama kawaida. Kama kawaida wakati mtu Fulani anahubiri atahuburi kuhusu Habari Njema. Ukitaka kusikia Habari Njema kuja jumapili ijayo. Lakini ni mzuri kujua huwezi kuwa na Habari njema bila Habari mbaya. Huwezi kushuka umuhimu ya habari njeema bila kujua habari mbaya na kusema ukweli habari mbaya leo ni mbaya zaidi ya kila kitu kwa hii dunia.
Ndugu na Dada zangu, tuko na shida kubwa sana. Shida ni hii, sisi sote tutakufa siku moja. Asabuhi moja mwili wako haitaamuka, siku moja itakuwa mwisho wako, utameza chakula ya mwisho, utakunywa soda ya mwisho, utawaamibia bibi ama bwana ama Watoto unawapenda mara ya mwisho, macho yako yataona jua kuenda chini jioni mara ya mwisho na maisha yako itaisha hapa kwa hii dunia. Maisha haya kwa hii dunia si kwa milele. Mimi na wewe na kila mtu tunajua, hii siku ya mwisho yetu inakuja, hata kusema ukweli tunasikia ndani yetu, tunaja siku moja tutakufa.
Hata watu wamehesabu na wamesema. Kila Sekunde watu 1.5 wanakufa. Kila dakika watu 107 wanakufa. kila saa watu 6,400 wanakufa, kila siku watu 150,000 wanakufa. Kwa ibada yetu leo zaidi ya watu 6,400 wa dunia watakufa. Hii ni watu wingi.
Leo idadi ya watu wa dunia mzima ni watu bilioni nane. Unaweza kufikiria hapo mwanzo mpaka leo watu wangapi wamekufa? Ni wingi sana. Billioni mia moja na nane. kumaanisha tangu mwanzo mpaka saa hii zaidi ya watu billioni mia moja wameshaa kufa.
Asabuhi hii nataka kuongea kuhusu maana ya kufa lakini si kukufa tu kukufa bila Yesu. Ni muhimu sana kwa sababu ninyi yote unajua mtu Fulani ambaye siku moja watakufa na hawana Yesu Kristo maishani yao. labda ni wewe. Hujui Yesu. Tafadhali sikiliza vizuri. Baada ya asabuhi hii utajua bila yesu maishani yako na baada ya utakufa nini itatendeka? Unasema waah nimekuja kanisa leo na nilitaka kusikia vizuri na sasa ni hii. Kwa dunia nzima ni watu wachache sana wanaweza kuongea kuhusu kifo na mauti bila kuogopa unajua ni nani? Ni wakristo, lakini hata wengi wa hawa hawapendi kuongea kuhusu hii. Labda hata ninyi saa hii huna raha kusikia hii, lakini ni lazima tunaongea kuhusu hii kwa sababu inakuja kwetu sote na ikiwa unakufa bila Yesu matokeo ni kubwa na ni mbaya. Labda Mke wako ama Bwana wako ama watoto wako ama Rafiki yako Hawajui Yesu na wakati unajua nini inawaongojea lazima utataka hawa kujua ukweli na kutoka hii shida na kujua Yesu kristo. Ikiwa ni wewe, tuko hapa kuongea na kueleza zaidi. Ni mzuri kila mtu ambaye ako hapa leo asabuhi umefika hapa si kwa baahati mbaya, lakini ilikuwa mpango ya Mungu utafika hapa na utasikia neno lake. Usitupe hii nafasi bure.
Kaabla ya tunaanza ni muhimu kufahamu kitu Fulani. Biblia ya sema ni watu wa namna mbili duniani. Mwenye haki, na Mwenye Uovu. Biblia ya sema Mtu bila Yesu ni Mwenye uovu. Hakuna kati kati. Labda wewe ama mtu Fulani unajua ni mtu mzuri wanafanya vitu vizuri lakini bila Yesu bado yeye ni Mwenye uovu. Bila Yesu huyu mtu ni giza na kila kitu chema anaweza kufanya ni taka taka. Kama ile wimbo tunaimba, Bila Yesu mimi ni mtu bure. Hatuwezi kufanya mema ya kutosha kutusiaida kwa macho ya Mungu bila Yesu.
Tusome mstari yetu ya leo. Wahebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.
Tuombe:
Ni watu wingi sana hawataki kusikia hii mstari, kwa sababu inawakumbusha ya ukweli wa maisha haya, inatuambia siku moja sisi sote tutakufa. Mungu anajua siku ile Kwangu na Kwako. Hatuwezi kufanya kitu chochote kuhusu siku ile. Inakuja na Hatujui ni lini, lakini siku ile tutakufa kila mmoja imewekwa kabla msingi ya dunia ilikuwa. Tunaweza kusema imeshaa andikwa, mpango imekuwa. Mungu amejua njia tutakufa na siku, saa na dakika tangu dunia iliumbwa. Sasa ikiwa unaweza kuangalia mbele na unaona kesho utakufa saa sita na saa hii nis saa sita uko na maa saa ishirini na nne inabaki kwako, utafanya nini? Utaongea na nani? Utataka kuwa wapi Pamoja na nani? Utasema nini kwa hawa watu? ni ngumu lakini pia ni mzuri kufikiria vitu hivi. Kwa sababu hata hakuna mtu moja hapa ndani anajua mbele yake. Labda hata maa saa ishirini na nne ni mingi kwako, mtu yo yote anaweza kutoka mlango ya kanisa leo asabuhi na kabla ya unafika gate una mshtuko wa moyo na umeingia milele. Labda ulikuwa na mipango mingi sana ya kesho, wiki ijayo, hata mahali unaenda kula lunch baada ya kanisa, na yote imeisha.
Siku moja sisi sote tutakufa kwa sababu gani? Kwa sababu ya dhambi zetu. Warumi 6:23 inatuambia Mshara wa dhambi ni mauti. Wakati ulizaliwa ulikuwa mwenye dhambi, kusema ukweli ulizaliwa katika dhambi. Kwa sababu sisi sote tuko na damu ndani ya mwili wetu, damu yetu ni sawa sawa ya damu ya baba yetu, Adamu na kwa sababu Adamu alitenda dhambi Watoto wote wake walizaliwa na hii ugonjwa, tangu mwanzo na itakuwa mpaka mwisho na hakuna dawa yo yote hii dunia inaweza kuleta kusaidia. Tuko na madakatari, na hospitali na tuko na shukrani kwa wote, lakini bado kwa miaka elfu saba, tangu dunia imeumbwa mpaka saa hii, hakuna dawa ya kifo.
Kumbuka tunaongea kuhusu watu ambao hawajui yesu na watakufa bila yeye. Mstari yetu kwa wahebrania 9:27 inaendelea kusema Baada ya kifo halafu hukumu.
Hukumu ni nini? Hukumu ni siku ile wakati utasimama mbele ya Mungu na utatoa majibu kwa maisha yako. Ulifanya hii na hii na hii kwa sababu gani? Tunapata hii hukumu kwa kitabu cha Ufunuo 20:11-15 ni ngumu kusoma ikiwa huna Yesu maishani yako hii italeta hofu mingi inasema Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Sasa hii ni kila mtu ambaye ameshi tangu dunia ilikuwa mpaka mwisho billioni mia moja ama mia mbili na wote wako hapa na wanahukumiwa kwa matendo yao. Unajua nani wengine wako hapo? Mimi na wewe tuko hapo, Ndugu na dada zetu wako hapo, Baba na Mama wetu wako hapo, watoto wetu, wako hapo. Inaendelea kusema vs.14-15 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Bila Yesu Mungu Atapima maisha yako na sheria yake. Nani anaweza kusimama mbele ya sheria ya Mungu? Siku ile, utasema nini? Mungu atakuambia nini? Tafadhali fikiria vitu hivi. Bila Yesu Kristo hujafunikwa na damu yake na Mungu anaona dhambi zako tu. Wakati kila kitu umetenda maisha yako yote au kila fikirio umefikiri iko wazi mbele ya wote na ni lazima unajibi kwa nini umetenda au kwa nini umefikiri kama hii, utasema nini? Hii si mchezo, hi si dini la Mzungu, dini fulani na labda unaketi na unafikiri mimi sina shida niko sawa si amini vitu vile. Ukiamini au huamini si kusema si ukweli na haitafanyika.
Kusimama mbele ya Mungu siku ile Labda utaanza kutoa vitu vizuri umefanya. Labda ulisaidia Majirani yako, ama ulitoa pesa nyingi kusaidia wagonjwa, labda ulihubiri Neno la Mungu, ama ulikuja kanisa kila jumapili.
Fahamu hii, Wakati watu wanona vitu hivi tunaweza kusema ni vitu vizuri. Lakini Mungu wakati anaona vitu hivi anaonaje? Kitabu cha Isaya 64:6 ya sema. Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo Iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Tunaweza kusema bila Yesu vitu vyetu vizuri, Matendo mema yetu tumefanya ni chafu mbele ya Mungu. Bila Yesu kila tendo jema unaweza kufanya ni taka taka. Hakuna hata moja inaweza kukusaidia siku ile hukumuni. Ikiwa umeweka imani yako katika matendo yako, niseme mapea pole kwako.
Pia unakumbuka Mathayo 7:21-23 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbiguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba Yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina Lako, na kwa jina Lako kutoa upepo, na kwa jina Lako kufanya miujiza mingi. Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Kwa sababu Watu wale walitenda vitu vizuri wanafikiri wakosawa, lakini Hawajui Yesu, hawawezi kuingia Mbinguni. Wanajua Jina Lake, walifanya vitu vingi katika Jina Lake lakini hawajui Yesu moyoni mwao. Hawa na uhusiano na Yesu hawajaweka Imani yao katika yeye na hawajatii neno lake. Tunajua hii yote naam na gani? Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Wale hawajafika kwa Yesu, ikiwa umefika kwake hawezi kutupa nje. Watu wanaweka imani yao katika matendo yao na wanafikiri siku ile hukumuni watakuwa sawa na Mungu atasema sawa ingia mbinguni na watashangaa. Siku ile hukumuni hata ni ngumu sana kuketi hapa na kufikiria.
Bibilia ya sema Kila fikirio na kila siri yako. Siku moja itakuja nje, itakuwa wazi. Huwezi kuficha, Mungu anajua moyo wako. Luka 12:2-3 Lakini hakuna neno lilio sitirika ambalo halitafuniliwa, wala liliofichwa ambalo halitajulikana. Basi yo yote mliosema gizani yatasikiwa mwangani, na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatatangazwa juu ya dari. Hata mimi wakati ninafikiria siku ile sipendi. Lakini najua wakati imemaliza, Mungu ataona haki ya Yesu juu yangu si maisha yangu si dhambi zangu. Na hii ni tumaini langu. Na wewe je? Unaweka tumaini lako wapi? Ni nini itakuokoa siku ile? Wakati kila siri yako imeonekana, wakati kila fikiria yako imekuwa wazi mbele ya wote, ni nini ama ni nani, atakuokoa?
Baada ya hukumu halafu nini? Sasa tumekufa, tumehukumiwa. Sasa, bila Yesu ni lazima unalipia dhambi zako. Kifo si mwisho, kifo ni mwanzo wa milele. Ni Kuanza kuishi milele na milele ama kulipa kwa dhambi zako milele na milele. Ni pastor moja alisimama mbele ya kanisa lake na alikuwa na kamba mrefu sana, karibi meter mia mbili na alikiuwa na tape nyakundu kwa sehemu ndogo sana kama inchi tatu na alisema, hii kamba yote ni kama milele na inaendlea na endelea na endelea na hii tape nyakundu ni maisha haya hapa kwa hii dunia, labda miaka sabini, themanini na hii kamba yote inategemea kama umeishi kwa hii muda fupi. Ni ukweli kabisa.
Tunajua hii mahali kulipa kwa dhambi zetu, inaitwa ZIWA LA MOTO ama JEHANUM. Hapa ni mahali mbaya sana. Biblia inatuambia kuhusu Jehanum. Mathayo 13:40-42 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Unajua wakati una pika chai ama chakula na unachoma vidole vyako, inaleta uchungu sana, fikiria mwili wako wote motoni milele na milele hakuna mwisho. Ni giza tu, na mafikirio yako, huwezi kutoka, huwezi kufa. Mahali ingine bibilia inasema ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Ni mahali mabaya sana.
Saa hii sisi sote tunajua watu wamekufa bila Yesu, Ni ukweli ama uongo? wako wapi? Hatupendi kufikiria hii, lakini tunajua wako wapi. Hadithi ingine Bibliani tunapata kwa Luka 16:19-31. Inaongea kuhusu mtajiri moja na masakini moja anaitwa Lazaro. Na walikufa. Na moja alienda kifuani ya Abrahamu, tunasema hii ni peponi. Na mwengine alienda Jehanamu. Luka 16:23-24 ya sema kule kuzimu aliyainua macho yake alipokuwa katika mateso. Akalia, akasema Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu, kwa sababu ninateswa katika moto huu. Sasa hii hadithi ni ukweli, si kama hadithi Fulani ambaye haijakuwa ukweli. Yesu anaongea kuhusu watu waili ambao waliishi hapa kwa hii dunia kama mimi na wewe na siki moja walikufa. Watu wengi waliuliza nini inafanyika wakati mtu anakufa. Hii hadithi inatuonyesha vizuri sana. Lakini ni lazima kuuliza Hawa watu wako wapi leo? Bado moja Ako kule kuzimu. Bado hata leo anateseka sana na Atakuwa kuzimuni milele na milele, hawezi kutoka. Na mwengine ako Pamoja na Mungu.
Kusema ukweli watu hawapendi kufikiria vitu hivi, ni ngumu, hata Labda unaogopa sasa. Pole sana lakini ni mzuri. Unahitadji kufikiria vitu hivi. Labda unajua Yesu ukweli na ukosawa. Wewe unajua utaenda kuwa na Yesu mbinguni siku moja na huna hofu, Lakini watoto wako, bibi yako ama bwana wako, Majirani yako, Rafiki zako, wanajua Yesu? Watakuwa Pamoja naye siku moja ama ni kama ile hadithi Yesu alituambia na siku moja kuteseka inaongojea hawa. Labda wanasema wanajua Yesu, lakini matunda yao ni nini? Ni matunda ya Mkristo? Ni matunda ya bibilia maishani yao? Tunaweza kujua miti naam na gani? Kwa matunda ambayo inatoa. Ni muhimu sana unaweza kuwaambia hawa kuhusu Yesu, na siku moja anarudi tena, na bila yeye watasimama mbele ya Mungu bila tumaini. Hakuna nafasi ingine kuishi, ni maisha haya tu. Na siku moja wakiamini au wanakataa kuamini bado siku moja Bibilia inatuambia kwa wafilipi 2:10-11 kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Unaweza kufanya wakati nafasi iko na utakuwa na Yesu kwa milele au unaweza kukataa na baada ya unakufa utafanya hii lakini umechelewa na utaenda kuteseka kwa milele jehanamu.
Taphadhali Mkuje tena jumapili ijiao na utasikia Habari Njema na njia ya kurekebisha maisha yako. Lakini si lazima unaongojea wiki ijiao. Hata leo unaweza kujua Yesu, unaweza kuweka Imani yako katika yeye na kazi yake msalabani. Leo unaweza kutoka kanisa hili kiumbe kipya. Unaweza kuwa na uhakika, kwamba ukikufa utakuwa Pamoja na Yesu mbinguni, Leo unaweza kupata msamaha. Tafadhali ongea na sisi Baada ya ibada yetu ukitaka kutubu kwa dhambi zako ukitaka kuokoka na unataka kujua Yesu ukweli.
Asanteni sana Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na tafadhali, Karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more