The Cost of Follwoung Jesus

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 1 view
Notes
Transcript

Luke 14:28

Kwa wiki tatu tumeangalia sana kuhusu wokovu. Tumeona Habari mbaya. Habari mbaya ni kwamba sisi sote siku moja tutakufa na baada ya kufa tutaingia hukumu. Siku ile tutasimama mbele ya Mungu kutoa majibu kwa maisha haya na tulishi naam na gani. Kweli kweli hii ni habari mbaya kwa sababu siku ile tutasimama uko bila tumaini lo lote kwa sababu matendo yetu hayawezi kutimiza sheria ya Mungu na mahitaji yake. Tuliona wiki ya kwanza sisi binadamu tuko shida kubwa. Jumapili ya pili tuliangalia Habari njema. Na habari njema ni njema ukweli ni tamu kabisa wakati unashika habari mbaya. Habari njema ilitupea tuamaini kwa sababu Mungu alituma Mwanawe peke, yesu kristo, kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Ni yeye alituokoa na sasa tukiamini katika yeye na tunatubu kwa dhambi zetu na tunafuata yeye kwa njia ya kutii neno lake, siku ile hukumuni tunafunikwa na haki ya Yesu na si matendo yetu na ubaya wote tumefanya hapa kwa maisha haya na dhambi zetu zililipiwa na Yesu msalabani na kwa sababu ya Yesu sisi tutaingia mbinguni na tutakuwa na Yesu kwa milele. Jumapili ya tatu tuliangalia hii kitu inaitwa imani. Bila imani hii yote ni bure kabisa. Bila imani ya ulwei sisi hatuna tumaini lo lote. Ni watu wingi sana wanasema wako na imani lakini tumeona bibilia inasema utajua kwa matendo yao. Imani ukweli ni imani ambaye inabadilisha maisha ya watu kwa sababu wanajua vitu hivi ni ukweli na ni lazima wanishi maisha yao kwa njia tofauti, kwa njia ya kupendeza Bwana wao si kujipendeza. Tuliangalia sana Watu ambao bibiloia inatuonyesha walisihi maisha yao kwa imani, na pia tuliona bila imani huwezi kumpendeza Mungu.
Sasa leo nataka kuongea kuhusu kitu ambacho ni muhimu tena. Labda umekuwa Mkristo kwa muda na unajua hii na labda umesikia habari mbaya, umeona uko na shida na umesikia habari njema umetubu kwa dhambi zako na umeanza kufuata Yesu na imani yako katika yeye umeanza kuona inakuleta shida kidogo nje. Leo nataka ninyi kujua kufuata Yesu iko na bei yake. Na ni mzuri kujua hii bei kwa sababu itakugharimu kila kitu. Ni rahisi sana kusema na mdomo unapenda Yesu, nimeokoka, Bwana asifiwe na hii lugha ya kanisa yote lakini kumfuata yeye ni tofauti. Kusema ukweli inaonyesha ikiwa wewe ni Mkristo au wewe ni fake. Nataka ninyi kusikia kitu saa hii, Bei ya kufuata Yesu Kristo na Maisha yako ni kali. Bei ni juu. niseme tena Itakugharimu kila kitu. Ni mzuri sisi tunahesabu kujua ikiwa tunaweza kulipa.
Tusome mistari yetu ya leo. Kitabu cha Luka 14:27-30 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Hizi mistari zinatuonyesha kabla ya tunafanya kitu ni mzuri tunahesabu kuona ikiwa tunaweza kumaliza hii kitu tunataka kufanya, kwa sababu ukianza na huwezi kumaliza, itakuwa ayibu kubwa sana. Hii yote ni kusema ikiwa wewe unataka kufuata Yesu Kristo na hujahesabu bei yake na unaanza na kati kati unatoka, ni ayibu kubwa sana. Na watu watakuchekelea. Pia utaleta aibu kwa kwa ndugu na dada zako ambao ni wakristo na mbaya zaidi unaleta aibu kwa jina la Yesu. Ni kama unaingia hardware na unataka kujenga nyumba. Unaleta rafiki zako na wewe kubeba hii yote an unaingia na unaweka kila kitu unataka kwa lori, unaingia kulipa na mwenye duka anasema millioni mbili na wewe umekuja na elfu mia tatu. Hujahesabu vizuri sasa utafanya nini? Itakuwa aibu kubwa.
Kitu cha kwanza ni mzuri unajua na labda ni kitu cha ngumu sana kwa watu kusikia ni bei ya kufuata yesu itakugharimu ni lazima unajifia mwenyewe (die to yourself). Kila kitu wewe unataka kufanya imeisha, mataminio yako yote sasa yameenda. Maisha yako sasa si kuhusu wewe, si kujipendeza, si kjufurahisa. Umeshika kama tumesoma kwa kitabu cha Luka? Angna Luka 14:27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake. Nafikirri sisi sote tunajua msalaba ni nini. Ni kitu cha kuteseka na kitu cha kifo. Msalaba ni mahali watu wanakufa. Wakati wewe unsema “mimi ni Mkirsto” “ Mimi nina fuata yesu” ni mzuri kujua kama unasema. Kwa sababu hapa Yesu anasema ikiwa wewe hauko tayari kubeba mslaba wako, kumanisha ikiwa wewe hauko tayari kufa kwa ajili ye Yesu anaendelea kusema huwezi kuwa mwanafunzi wangu. Huwezi kuwa Mkristo, huwezi kuwa na wokovu bila kuwa tayari kuweka kial kitu kando maishani yako na kusema yote ni bure nikilinganisha na Yesu. Mipango yako ya maisha yako ulikuwa nai, sababu ya maisha yako, lengo ya maisha yako, wakati unfuata Yesu na unabeba mslaba yako sasa ni tofauti. Wakati Yesu kristo anabadilsiha mawazo yako na moyo wako huyu mtu ulikuwa ameenda na ameenda na kila kitu. Hii ni sababu Paulo aliwaambia kanisa la Efeso kwa kitabu cha Waefeso 4:22-24 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Sasa wewe ikiwa wewe ni Mkristo wakweli ni mtu tofauti kabisa. Unaweza kuona bei ya hii ni kali sana. Kwa sababu huyuu ya zamani alikuwa na marafiki, kazi, familia, tamaa, mipango na sasa umeokoka na unaingia kubeba msalaba wako na kufuata yesu. Hii yote ya zamani itakuwa shida.
Kwa rafiki zako na wale ambao ulienda na hawa kabla ya uliokoka angalia Waraka wa kwanza wapetro 4:3-4 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. Alikuwa best friend yako kwa miaka mingi sana, ninyi ulikuwa pamoja kila mahali na sasa umeanza kubeba msalaba wako na huwezi kufanya kama zamani na huyu mtu ambaye alikuwa karibu na wewe anakutukana. Uko tayari kulipa hii bei? Unajua shida ya siku zetu si kama zamani. Kuwa mkristo siku hizi ni cool, ni kitu ambacho tunasema tu, bila kufikiria maana yake. Unaenda kanisa? Ndiyo na huyu mtu hata hajui maana ya kanisa, hajui Yesu, hata hawezi kueleza injili ya yesu. Zamani kusema wewe ni Mkristo ni kumanisha utapoteza kila kitu hata labda maisha yako. Leo asabuhi tuko na ndugu na dada katika Yesu na wanakutana kwa mahali ambapo iko chini ya ardhi, na kila jumapili inaweza kuwa mahali tofauti kwa sababu huwezi kwa wakristo na kutana kama kanisani kwa China. Huwezi kuwa na bibilia. Wakipata unakutana au hata uko na bibilia unaweza kufungwa gerezani. Hii ni sababu ukitaka kuingia kanisa China, kabla ya unaingia unaulizwa maswali mingi na moja ni. umeingia gerezani mara ngapi kwa ajili Yesu. Ikiwa hujaingia labda huwezi ingia.
Ni missionari moja aliingia China na alikutana na Pastor wa wili na waliweka yeye kwa gari lakini ilikuwa kwa back seat na hata si kwa kitu nyuma walilazimisha yeye kulala kwa sakafu ya gari maa saa kumi na tisa, hawajataka watu kuona yeye. Walinena yeye mbali sana, tunaweza kusema ni bush ya China na wakati walifika, missionari alitoka kwa sakafu na aliona Mapstor wingi sana ya China na wote wlikuja pamoja kwa sababu alileta Bibilia chache kwao. Wakati aliwapea bibilia walianza kurarua kila bibilia sana. Missionari alisema alishangaa wanaharibu bibilia naam na hiyi an aliuliza pastor moja wanafanya nini? Pastor alisema kwa sababu hakuna bibilia na sisi ni wingi kila pastor anachukua kitabu moja ya bibilia na watahubiri hii kitabu moja kwa mwaka moja mpaka wote watarudi hapa mwaka ujao na watabadilisha na mwengine. Fikiria hii, mwaka mzima mtu atakuwa na kitabu cha Philemoni at Waraka wa tatu wa Yohana. Na sisi tunaketi hapa na Bibilia nzima na hata wengi watatoka hapa leo asabuhi na itarudisha kwa shelf bila kufungua mpaka julapili iajayo. Kila jumapili unatoa vumbi kwa bibila yako. Kweli unajua bibilia ni nini? Na muhimu zaidi unajua ni kumhusu nani? Umehesabu bei kusema wewe ni moja yake na unamfuata? Labda siku moja utapimwa halafu utajua.
Si kwa rafiki zako peke yake itakuwa shida. Hata kwa kazi yako. Labda mahali ulikuwa umefanya mambo mingi na sasa unabeba msalaba wako umekuwa Mkirsto. Utrafanya nini. Ikiwa campuni wamekutegemea kupika vitu kufanya vitu chini ya meza au siku zetu wanasema kiswahili imeingia na wewe unaongea vizuri, sasa utafanya nini? Kitu cha kwanza nataka ninyi kujua ni Corruption ni dhambi, ni giza na hakuna udhuru kutenda hii. Sikiliza Mithali 17:23 Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu. Rushwa hapa ni nini? Ni Bribe, ni corruption na bibilia inasema huyu mtu Asiye haki, ni mtu mbaya. Unajua wakati Corruption iko, iko na matokeo. Angalia Kitabu cha kutoka 23:8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. Bei ya kufanya haki si rahisi. Kusema ukweli mimi ni Mzungu haoa Kenya, unafikiri imekuwa rahisi kwangu kufanya hii yote? Ninyi unajua. lakini ni lazima. Ni mzuri unahesabu hii bei ya kufuta Yesu.
Sasa hii ni ngumu lakini si rafiki zetu si kazi yetu peke yake lakini itakuwa shida kwa familia yetu pia. Sasa hii ni mahali mbapo wingi wanashindwa kwa dunia nzima. Lakini hapa kusema ukweli ni desturi lenu. Na madestrui yote ya dunia yameumbwa na nani? Na binadamu, na kama kawaida desturi inatoa Mungu kabiosa kwa sababu ni kwa wanaume kujipendeza na karibu desturi lote linaweka wanawake chini. Nisema wazi kabisa na hii ni kwa kila desturi langu pia, huwezi kufuata desturi na Yesu pamoja. Pia nataka kusema si kila desturi ni mbaya lakini ikipigana na bibilia au inatuambia kufanya kitu tofuati ya Bibilia huwezi kufuata. Kabla ya mistari yetu ya leo kwa kitabu cha Luka Yesu alisema kitu ambacho imeshangaza watu wingi angalia Luka 14:26 mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Hii ni ngumu sana. Karibu kila desturi kwa dunia nzima hakuna mtu utapenda zaidi ya familia yako, mama, baba, ndugu, dada hata anasema mke hapa. Lakini Yesu hasemi kuchukia hawa watu. Tuko na mistari mingi sana ya bibilia kusema kupenda na kuheshimu hawa. lakini sababu anasema kitu kama hii ni kuonyesha lazima yeye akuwe namba one maishani yako. Lazima Yesu akuwe juu ya kila kitu na kila mtu maishani yako. Baba na mama lazima tunaonyesha heshima kwa hawa lakini ikiwa hawa wanasema kufanya kitu ambacho bibilia inasema huwezi kufanya, unaoenda nani zaidi? Yesu anasema huwezi kuwa mwanafunzi wake ikiwa unapenda familia yako zaidi ya yeye.
najua hapa Kenya nimeona tuko na shida kubwa kwa ndoa. Hapa desturi linasema Baba ni kichwa hata wakati msichana na kijana wanaowana bado baba ni mkubwa. Hata baada ya dowry imelipwa, bado baba ni mkubwa. Na bado unajiweka chini ya baba. Pia nimesikia Bwana anaweza kurudisha bibi yake kwa baba ikiwa ni shida mingi na pesa zake zinaweza kurudishwa? Hii ni ajabu sana. Sasa Bibilia inasema? Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Angalia Waefeso 5:31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Hata Yesu Mwenyewe alisema nini? Angalia Mathayo 19:5-6 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Bibilia ni wazi kabisa, Bwana na mke wakati wanaowana wanatoka wazazi wao, sasa hawa ni mmoja, Bwana ni kichwa ya jamii yake sasa, hakuna mwengine, si baba si mama, si mtu mwengine. Huyu Bwana anajibu kwa Mungu kama anaongoza familia yake. Bado tunaheshimu wazazi wetu lakini hawa na kitu kusema kwa ndoa yetu. Ndiyo ikiwa hawa ni wakristo na uko na shida na unataka kuuliza advice yao ni sawa hata ni mzuri lakini hawawezi kuingia ndoa yako kama hawa ni wakubwa. Tena nataka kusema, huwezi kufuata desturi na Yesu. Utafuata gani?
Labda unasema Travis tukifanya hii italeta shida mingi, ndiyo, kumbuka tunaangalia leo gharama ya kumfuata Yesu ni juu na ni lazima unahesabu vizuri kabla ya unajiita Mkritso. Kufuata Yesu na mambo ya familia ni ngumu, Baba yako, mama yako. Kumbuka kufuata Yesu itakugharimu kila kitu. Hata kwa mambo ya familia Yesu alisema kwa Mathayo 10:34-37 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Kwa nini adui ya mtu ni nyumbani mwake? Kwa sababu Mkristo ukweli ni nuru na wasioamini ni giza. Hakuna kati kati. Na wewe utatumikia Yesu na hawa hawawezi kufahamu. Sasa swali ni, utafuata gani? Desturi ama Yesu? Huwezi kufuata Pamoja. Bwana na Bibi utafuata kama Bibilia na Yesu wanasema? Bwana ni kichwa cha familia yako si baba yako, si mama yako au utafuata desturi lako? Wanaume, utafuata Bibilia na Yesu kupenda bibi yako na kuweka yeye juu na kuheshimu yeye? Au utafuata desturi lako?
Labda gharama kufuata yesu kwa familia ni mama yako na baba yako na dada zako na ndugu zako watalalamika na hata labda watafukuza wewe kwa familia ikiwa unafuata yesu. nani akotayari kusema nitafuata yesu hata ikiwa hii yote inafanyika? Kwa sababu ikiwa hujahesabu na hujakuwa tayari, wewe si Mkristo kweli kweli, usiendelea kujidanganya. Utafuata nani? Mungu ama binadamu? Angalia Matendo 5:29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Hii ni makuhani wanawaambia hawa hawawezi kuendelea kufundisha kuhusu yesu kristo na wanachapa hawa mbele ya watu wengi, na wamesema nini? Imetupasa kumtii mungu kuliko wanadamu. Wewe uko tayari kusema hii, hata mbele ya baba yako? mbele ya dunia na watu wote? Ikiwa wewe ni Mkristo ukweli, utafanya.
· Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.