Doctrinal Statement Pt.3
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
The Holy Scriptures 6-
The Holy Scriptures 6-
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa dcotine yetu au vitu ambavyo sisi hapa kwa AIC Sekenani tunaamini. Hii ni jumapili ya tatu na tumeona Maandiko au Bibilia ni kila kitu. Inatuonyesha kila kitu kuhusu Mungu, Yesu, Roho Mtakatifu, Dhambi, kifo, Ufufuo, inatuonyehsa kuishi maisha haya naam na gani. Hii ni sababu iko kitu cha kwanza wakati tunaongea kuhusu uamini wetu. Kama tunaamini kuhusu Bibilia ni kila kitu, kama tunasoma bibilia ni muhimu sana. Ikiwa unasoma vibaya, Doctrine yako itakuwa mbaya ma labda kama unaishi maisha yako itakuwa mbaya. Kumbuka sisi sote tunaihsi maisha yetu kama tunaamini. Yesu alisema kwa Mathayo 6:22-23 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! Hata sisi tunataka mawazo na ufhamu wetu kuwa safi kuhusu Neno la Mungu. Ikiwa si safi halafu italeta shida mingi sana kwetu na maisha yetu. kusema ukweli tungetamani sana kujua bibilia zaidi, tungetaka ufahau wetu ikuwe juu kabisa, kwa sababu ni kumhusu Bwana wetu, Mungu wetu na kila kitu cha maisha haya.
Tumeshaa ona Maandiko iko na kila kitu cha kutuonyesha imani, maarifa na kutii. Hakuna kitu kiingine inaweza kufanya hii, ni Bibilia peke yake. Hii ni sababu Mungu aliandika kwetu na kwa watoto wa watoto wa watoto wetu na kwa kila kizazi mpaka atarudi siku moja. Na tumeona bibilia ni vitau sitini na sita ndano ya kitabu moja. Kitabu hiki unashika kwa mkono yako ni Neno la Mungu, inaanza na Mwanzo na inaisha na ufunuo. Kitabu cho chote nje ya hii si neno la Mungu.
Tuombe:
Tutaanza na 1:6 leo na tutaona tufike wapi. Inasema The whole counsel of God concerning everything essential for his own glory and man’s salvation, faith, and life is either explicitly stated or by necessary inference contained in the Holy Scriptures. Nothing is ever to be added to the Scriptures, either by new revelation of the Spirit or by human traditions.9
Nevertheless, we acknowledge that the inward illumination of the Spirit of God is necessary for a saving understanding of what is revealed in the Word. We recognize that some circumstances concerning the worship of God and government of the church are common to human actions and organizations and are to be ordered by the light of nature and Christian wisdom, following the general rules of the Word, which must always be observed.
Nataka kuendelea kwa hii point ingine 1:7 Inasema Some things in Scripture are clearer than others, and some people understand the teachings more clearly than others. However, the things that must be known, believed, and obeyed for salvation are so clearly set forth and explained in one part of Scripture or another that both the educated and uneducated may achieve a sufficient understanding of them by properly using ordinary measures.
Hii ni ukweli kabisa. Nafikiri unakubali? Uko na vitu ambavyo ni wazi sana na uko na vitu ambavyo ni ngumu. Halafu uko na watu ambao wanashika hii vitu vigumu na ni rahisi kwao kufahamu na watu wengine wanastruggle kidogo na wanhitaji mtu kwaeleza zaidi. Hii ni sababu Mapastor wa siku zetu wanajifunaisha (take advantage) na watu. Hata hawa wenyewe hawajui inasema nini ukweli na wanachafua ukweli wa neno la Mungu. Na wanaongoza watu vibaya kwa njia ambaye Mungu hajasema. Hii ni sababu lengo yangu ni kwa kila mtu kujua ukweli wa neno la Mungu. Sitaki ninyi kunitegemea na kila kitu, nataka wewe mwenyewe kuketi na kufungua Bibilia yako na kujua kama inasema, wewe unaweza kuwa na uhakika kwa vitu mabavyo umesoma si kwa mtu mabye anasimama mbele yako na anasema Bibilia inasema. Hata Petro aliongea kuhusu hii. Angalia Waraka wa pili wapetro 3:15-16 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe. Wale watu walitumia vibaya kama Paulo alisema na unaona matokeo? Uvunjifu, hii kumanisha ilileta uharibifu juu yao.
Tuko na mfano ingine kwa bibilia na ni mzuri sana na ni mzuri unakumbuka watu hawa. Tunawapata kwa kitabu cha Matendo 17:10-11 Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Hapa uko na Paulo na Sila. Paulo na mtume wa Yesu kristo na anafundisha kwa sinagogi na ulikuwa na watu kutoka mahali inaitwa Beroya, sisi tunaita hawa Bereans na unaona kama walifanya? Walipokea neno Paulo na Sila walileta lakini hawajapokea kama kila kitu ni ukweli, walifanya nini? Wakayachunguza maandiko kila siku, kwa nini watafanya hii? Waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Walihakikisha hawa wenyewe kuona kama wamefundishwa ni ukweli. Lazima sisi tunafanya vivyo hivyo.
Lakini pia tunaona kwa kitabu chetu 1:7 inasema ni vitu vigumu na vitu rahisi lakini vitu vya wokovu ni wazi kabisa, si ngumu. Watu ambao wamesoma na watu amabo hawajasoma wanaweza kushika kama inasema. Vitu ambavyo ni lazima tunajua, tunaamini na kama tunatii ni wazi. Bibilia ni wazi kabisa, ni lazima mtu anatubu kwa dhambi zake. yesu mwenyewe alisema Luka 13:3 msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Na ni lazima tunaamini Paulo alisema kwa kitabu cha Warumi 10:9 ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Na lazima ikiwa umeamini na umetubu utakuwa na matunda ya kuonyesha maisha tofauti. Yohana aliwaambia mafarisayo na wengine ambao wlaikuwa wanafiki kwa Mathayo 3:8 Basi zaeni matunda yapasayo toba; Hii ni matunda ya maisha yako na ni lazima kuonyesha ikiwa toba yako ilikuwa ukweli. Neno la Mungu ni wazi kuhusu vitu hivi kwa kila mtu. Zaburi 119:130 Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Ni kufungua na kusoma kama inasema.