Mara Christian Chapel
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 4 viewsNotes
Transcript
Genesis 3:1-7
Genesis 3:1-7
Leo asabuhi tumefika kwa kitabu cha mwanzo 3. Kwa hii mlango tunaanza kuona shida kubwa inaingia kwa umbaji wa Mungu na kwetu binadamu. Ni mistari mingi kwa hivyo tunanza
Mwanzo 3:1-7 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Ni vitu vingi vinafanyika hapa kwa hizi mistari. Vs.1 tuko na nyoka anaingia. Nani anapenda nyoka? Wakati sisi tunaona nyoka tunafanya nini? Mara mingi ninajua ninyi unaua na mawe. Lakini hii nyoka ilikuwa tofauti. Tunaona huyu alikuwa mwerevu. Na sisi tunajua shetani aliingia hii nyoka. Lakini Adamu na Hawa hawajaogopa hii nyoka, kumbuka bado binadamu hawajaanguka dhambini na kila kitu ilikuwa chema. Bila shaka hii nyoka ilikuwa mara dati sana kwa sababu hajaanza kuwa nyoka kama sisi tunajua. Na pia Shetani si kama watu wanafikiri, lakini Bibilia inatuambia kwa Waraka wa pili Wakorintho 11:14 Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Hata siku ile bustani Shetani aliingia ile nyoka na alidanganya Hawa, alikuwa kama kitu kizuri. Halafu tunaona kitu cha ajabu. Hii nyoka inaanza kuongea. Na hutajaona Hawa kukimbia ama kuogopa lakini aliaanza kuongea na hii nyoka. Na kitu cha kwanza hii nyoka anfanya ni kujaribu kudanganya na kuchafua neno la Mungu. Anasema Hivyo Ndivyo alivyosema Mungu. Analeta shaka, anataka hawa kufikiria ikiwa amesikia kama Mungu amesema ukweli. Kumbuka Mungu aliwaambia Kwa Mwanzo 2:16-17 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Hii ni neno la Mungu na imekuwa kama Mungu amesema na sasa Nyoka anataka kugeuza neno la Mungu. Na tunaona jibu la Hawa na tunaona anasema kama Mungu alisema Vs.2-3 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Hawa alisema ukweli, ni kama Mungu alisema. Alijua atakufa akikula matunda ya mti kati kati ya bustani. Na sasa ni mzuri kujiuliza Kwa nini ni nyoka na Hawa wanaongea. Adamu ako wapi? Mungu alimwambia Adamu hii maneno yote, hata Hawa hajaumbwa bado wakati Mungu aliongea na Adamu kuhusu hii. Sasa tuko na Mwanamke anaongoza hii maneno yote. Wametoka mpango ya Mungu kwa Mwanamume kuongoza familia yake. Adamu ako, alikubali bibi yake anaongoza na hajalinda yeye kutoka hii nyoka na hatari yake.
Halafu vs.4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, Huyu ni mkora sana. Kwanza alichafua neno la Mungu na sasa anasema uongo. Yesu alisema Shetani alikuwa Mwongo na muuaji tangu mwanzo na ni hapa inaanza. Unajua bado shetani ako na bado anadanganya watu, ni mzuri kukumbuka wakati mungu anasema kitu kwa neno lake hatuwezi kubadilisha au kuwa na shaka. Na hata leo shetani na peop zake wako na lengo lao ni kuchafua neno la Mungu na kudanganya watu ili watatenda dhambi. Lakini fikiria Adamu na hawa, walikuwa na kila kitu uko na Mungu aliwapea kila miti na matunda yake kwa chakula lakini alisema ni moja tu huwezi kula na Adamu na Hawa wanajipata kwa ile mti na majaribio imeingia. Hii ni mfano ingie mzuri kwetu, kukaa mbali kwa majaribio, usikaribisha. Kaa mbali. Mungu kwa neno lake ametuonyesha njia za kufuata Yesu na njia za uongo na vitu vibaya. Si kama sisi hatujui. Ni mbaya kuiba? Tunajua naam na gani? Ni mbaya kusema uongo? Tunajua naam na gani? Waraka wa kwanza wakorintho 6:9-10 kwa hizi mistari tunaambiwa Msidanganyike, hii ni muhiu sana, ni kitu cha umuhimu sana Mungu anataka sisi kujua kutoka neno lake. Kama Wakati alimwambia Adamu usikule kwa ile mti sasa anatuambia watu ambao ikiwa wanafanya vitu hivi hawawezi kuingia ufalme wa mbunguni anasema. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Sisi tunaona hii yote lakini sisi tunakaribisha vitu hivi sana na tunajaribiwa kwa sababu mwili wetu inasema, kweli Mungu amesema? Hakika hamtakufa na utaingia mbinguni, usijali. Kumbuka neno la Mungu anasema Msidanganyike.
Tuendelea na kitabu cha Mwanzo. Nyoka aliendelea, Mwanzo 3:5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Nyoka anadanganya Hawa sana. Ni kama anafanya kwetu leo kusema ukifanya hii utakuwa kama Mungu, wewe utakuwa Mungu ya maisha yako. Dhambi ni furaha, dhambi ni kuoata uhuru na kufanya kama unataka, hii ni ukora wa shetani, na anataka sisi kufikri Bibilia, neno la Mungu ni shida, na ukifuata kama inasema huwezi jifurahisha. Utajua bila kujaribu naam na gani? Jaribu kidogo tu, haiwezi kuleta shida. Hii ni uongo wa hii dunia na shetani na watu wengi sana wako jehanmu saa hii kwa sababu ya kufikiri naam na hiyo.
Vs.6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. Baada ya hi yote, alijuaneno la Mungu, hata alitumia neno la Mungu na majaribio ilingia na nguvu na aliweka neno la Mungu kando na alichukua ile matuda. Unaona hii mstari inasema ilipendeza macho. Kama dhambi, inapendeza macho yetu sana, hata wakati tunajua ukweli. Na kama Hawa tunachukua ile kitu na tunafikiri iko sawa. Na Hawa alikula. na Akampa Adamu na yeye alikula. Tena kwa nini Adamu anasimama hapo wakati hii nyoka inadanganya bibi yake? Kwa nini sasa anafuata bibi yake kukula hii matunda Mungu alimwambia yeye asikule. Mpango ya Mungu kwa familia imeharibika. Na hata leo wakati tunakubali kufuata dunia na mpango yake kwa familia yetu, kwa wanawake na wanaume, inaleta shida kubwa sana.
Sasa dhambi imeingia umbaji wa Mungu na kwa sababu ya hii kitu moja imeingia kweti sote. Sisi site tumetoka Adamu na Hawa. Wale wawili ni wazazi wetu na kwa sababu ya hii kosa moja ya kutotii Mungu imeleta sisi sote kuzaliwa na dhambi. hii ni sababu tunakwa mgonjwa, hii ni sababu tunakufa na hii ni sababu tunahitaji kuokolewa. Na ni Yesu peke yake anaweza kutuokoa.
Vs.7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Walipata kama walitaka. Macho yalifumbuliwa, walijua mema na mabaya. Walikuwa na aibu kwa sababu walikuwa uchi. Kabla ya hii hakuna aibu kwa sababu hakuna dhambi. Dhambi ni hatari sana, inaharibu kila kitu. Hatuwezi kucheza na dhambi, Mungu anachukia dhambi, ni giza kabisa. Na sisi sote kila siku tunatenda dhambi au tunajaribiwa kutenda dhambi. Kila mtu ambaye amezaliwa ni mtumwa wa dhambi na ni Yesu tu anaweza kutuleta huruna kutupea nguvi ya kupinga dhambi na kuwa nuru. Ni yeye anaweza kurudisha sisi kuwa na uhusiano na Mungu. Tutaona wiki ijayo, hii dhambi walitenda iliharibi uhusiano wa Adamu na Hawa na Umbaji wao. Sisi sote tunahutaji Yesu kristo, na ikiwa hujui Yeye, ni mzuri unaiongea na mtu ambaye anaweza kueleza zaidi.
Asanteni sana.