Doctrinal Statement Pt.5
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 3 viewsNotes
Transcript
The Holy Scriptures 8
The Holy Scriptures 8
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu ya kama sisi tunaamini hapa kwa AIC Sekenani na kwa mission yetu. Tumesema umhimu ya kujua kama unaamini kuhusu vitu vya bibilia ni kwa sababu kama unaamini unaishi maisha yako, na kama kanisa lako linaamini ni kama litafnya kazi yake. Kama wanahubiri, kama wanafanya ibada yao, kama wanapenda watu wao, yote inatoka kwa kama wanaamini kuhusu Neno la Mungu. Kwa wiki karibu tano sisi tumeangalia kama sisi tunaamini kuhusu Neno la Mungu. Hii kitu inaitwa bibilia ni nini exactly, iko na nini ndani yake. Na tumeona mambo mingi. Tumeona ndani ya neno la Mungu iko na kila kiti tunahitaji kuishi maisha ya Mkristo, iko na kila kitu tunahitaji kujua kuhusu Mungu, Yesu, Roho, Wanadamu, dhambi, wokovu, kifo, maisha ambaye inakuja, umbaji wa kila kia kitu, kama Mungu anataka ibada yetu, mafundisho yetu kila kitu na kama sisi tunaishi kumpendeza yeye. Si lazima tunatoka nje ya bibilia kupata vitu hivi. Na wiki iliopita tuliona Bibilia iko na vitu ambaye ni ngumu kushika na vitu rahisi lakini vitu kuhusu wokovu kila mtu anaweza kushika kamma bibilia inasema.
Leo tumefika namba 8. Tusome pamoja The Old Testament was written in Hebrew, the native language of the ancient people of God. The New Testament was written in Greek, which at the time it was written was most widely known to the nations. These Testaments were inspired directly by God and by his unique care and providence were kept pure down through the ages. They are therefore true and authoritative, so that in all religious controversies the church must make their ultimate appeal to them. All God’s people have a right to and a claim on the Scriptures and are commanded in the fear of God to read and search them. Not all of God’s people know these original languages, so the Scriptures are to be translated into the common language of every nation to which they come. In this way the Word of God may dwell richly in all, so that they may worship him in an acceptable manner and through patience and the comfort of the Scriptures may have hope.
Tena nataka kusema, kumbuka hii si neno la Mungu, hii ni kama tunaamini kuhusu neno la Mungu na inatusaidia kueleza watu wengine rahisi. Inajumlisha kama sisi tunaamini kuhusu mafundisho. Tunaona wakati agano la kale iliandikwa iliandikwa kwa kiebrania. hii ilikuwa lugha ya watu wa Mungu. Tunajua kuwa mnyahudi ilikuwa kitu kubwa sana, kabila yako ilikuwa kabila Mungu alichagua kuwa watu wake. Angalia Kumbu Kumbu la Torati 7:6-8 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Wayahudi walikuwa watu wa Mungu, bila shaka na kwa sababu ya hii tunasoma kwa Warumi 3:1-2 Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Ikiwa uko na Bibilia ya niingereza inasema wamekabidhiwa maneno ya mungu.
Tunaona agano jipya iliandikwa na Kigiriki. Wakati wa agano jipya Kigiriki ilikuwa lugha ambaye mataifa menfi walijua. Ni kama Kiingereza leo kwa wakati wetu, karibu kila nchi wanajua kiingereza. Agano jipya ilikamilika katika mwaka wa mia moja, hii ni zaidi ya miaka elfu mbili iliopita na kwa hizi moaka yote, Mungu Amelifihadhi neno lake mpaka saa hii. Amehakikisha itabaki kama imeandikwa na maana yake bado ni kama amesema. Haijabadilishwa kwa hizi moiaka yoyte na kama tunasoma leo asabuhi ni kama Yohana aliandika na waandishi wote. Agano la kale ni zaidi ya miaka elfu tatu mia nne, na kama tunasoma leo ni kama Mungu alisema. Kusema ukweli kitabu hiki ni hazina kubwa sana na hakuna kitabu kiingine ni kama hii. Hii ni sababu tunasoma kwa Doctrinal Statement kwa sababu ya hiyo ni halali, ili kwamba katika mijadala yote ya kidini, kanisa linapaswa kuyategemea. Neno la Mungu ni safi.
Sisi sote ambao ni watu wa Mungu ni haki yetu kujua neno la Mungu na kusoma katika hofu ya Mungu na kutafuta ukweli wake ndani ya maandiko. Lakini si watu wengi wanajua Kihebrania au kigiriki. Nani hapa ndani wanajua lugha hizi? Tutasoma neno la Mungu naam na gani? Hii ni sbaabu sisi tunaamini ni lazima neno la Mungu linapaswa kutafsiriwa katika kila lugha. Karibu miaka elfu moja watu wote walikuwa na Tafsiri moja na ilitwa Latin Vulgate na karibu watu wote hawajua lugha ya kilatini au Latin. hii ni sababu Wakatoliki na Maaskofu wao watasimama kila jumapili na watasoma kanisani kutoka Latin Vulgate na watu ambao wanaketi uko ndani hawajui inaema nini na huyu mtu askofu atasema Bibilia inasema hii na hii hata ikiwa ni uongo. Hii ni sababu wakatoliki walianza kulipa hii kitu inaitwa indulgence kwa familia yao ambao wamekufa na askofu atasema wanateseka purgatory na ni lazima ulipe kuleta faraja kidogo kwao. Na watasimama mbele ya watu na soma neno la Mungu na kusema Mungu amesema hii. Wewe umeona hii wakati unasoma bibilia? Mimi sijasoma hii, lakini kwa sababu ni ko na bibilia kwa lugha yangu ninaweza kusoma na kushika kama inasema. Zaidi ya miaka elfu moja wakristo waliishi naam na hiyo, kudanganywa, si kwa sababu hawajui kusoma, kwa sababu hakuna bibilia kwa lugha yao. Kuwa na shukrani sana uko na bibilia kwa lugha yako, hazina kubwa. Lakini siku zetu ukiona kama Mapastor wanadanganya watu na watu wanafuata hawa, utafikiri hatuna neno la Mungu kwa lugha yetu, kwa sababu wanafanya kama wale waaskofu wa zamani na wanasema Bibilia inasema hii na ni uongo na unaketi hapo na neno la Mungu kwa lugha yako na unaamini kila kitu wanasema, aibu kubwa sana. Kumbuka wale wa walishi kwa Berea fuata mfano yao Kitabu cha Matendo 17:10-11 Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
Tukisoma na tunajua na tunatumia neno la Mungu wetu kama hii inasema Neno la Mungu likikaakwa wingi ndani yenu, na iko na sababu, sisi tunaweza kumwaabudu Mungukatika namna inayokubalika , na kwa saburi na faraja ya maandiko tupate tumaini. Fikria miaka yote hiyo, watu hawajakuwa na hii nafasi kama sisi leo. Kusema ukweli tumeishi kwa wakati wazuri sana, tumebarikiwa kubeba hata neno la Mungu kwa simu yetu. Ikiwa unashika ni nini imefanyika ili tunaweza kuwa na hii kitabu kwa lugha yetu utashangaa. Labda siku ingine tutaangalia. Lakini wakristo, watu wa Mungu angalia Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Natumaini sana umeanza kuona sababu kama tunaamini kuhusu vitu kama neno la Mungu na kama tunajua ni muhimu sana.
Asanteni sana. Kuna maswali?