The Word became Flesh
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
John 1:14
John 1:14
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 1:14. Tumeona mambo mingi mpaka hapa kwa kitabu hiki na kusema ukweli ni ajabu. Yohana ameadnika vizuri sana na alikuwa wazi kabisa kuhusu Yesu Kristo na yeye ni nani. Na yeye anasema Yesu ni Mungu. Kumbuka sababu Yohana aliandika vitu hivi, anatuambia kwa 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Hata wakati sisi tunaongea na watu ni mzuri tunakumbuka hii na tungetumia neno la Mungu kuonyesha watu Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na kumaini mwe uzima kwa jina lake.
Yohana ametueleza kwa vs.1-13 kuhusu huyu mtu anaita Yesu kristo. Anasema alikuwa Neno na alikuwa tangu mwanzo, alisema Neno ilikuwa Mungu na Yesu Kristo ni neno, ni lazima sisi tunasema Yesu ni Mungu. Alituonyesha kila kitu ambaye iko vilifanyika kwa Yesu, tumeona Yesu ni uhai na yeye ni nuru ya watu. Na hii nuru ilikuwa na nguvu sana na giza haiwezi kushinda. Halafu Yohana alieleza kuhusu Yohana Mbatizaji na kama alifika kutangaza kuhusu Yesu na yeye ni nani. Hata Yohana Mbatizaji alisema dunia iliumbwa kwa njia ya Yesu na pia tuliona Yesu, Mungu alikuja kwa watu wake na walimkataa. Lakini kwa watu ambao watampokea aliweka hawa kuwa watoto wa Mungu ikiwa wataamini katika jina lake.
na leo kwa mstari yetu Yohana atatueleza kitu cha ajabu tena. Tusome mstari yetu ya leo Kitabu cha Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. hii ni neno la Mungu wetu kuhusu Bwana wetu Yesu kristo.
Tuombe:
Hii mstari tumesoma saa hii ni fupi lakini imejaa na vitu vingi sana kuhusu Yesu na Mungu. Kusema ukweli hii mstari yetu ya leo ni moja ya aya muhimu zaidi katika Bibilia. Kuonyesha umuhimu ya hii mstari nikuambia, kwa maneno haya machache ikiwa huamini kama inasema huwezi kuwa Mkristo, hakuna wokovu kwako. hii mstari Inatuambia kuhusu Umwilisho wa Mungu au kwa kiingereza ni Incarnation, inamaanisha wakati Mungu alikuwa na mwili. Tunasoma Naye Neno Alifanyika mwili. Tumeona Yohana kueleza kwa Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Anaongea kuhusu Yesu kristo. Yesu kristo alikuwa Neno la Mungu. Na sasa Yohana anaeleza Mungu alivaa mwili! Sasa nataka ninyi kushika umuhimu ya hii. Usio na mwisho ukawa na mwisho, Umilele iliingia wakati. Yasiyoonekana yakawa yanaonekana, Muumba aliingia katika uumbaji wake. Wakati tunafikiria hii natumaini unashangaa kidogo kwa sababu ni ajabu.
Tunajua Mungu alijifunua kwa umbaji wake, tunasoma hii kwa Warumi 1:18-21 na tunasoma kwa vs.19-20 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; Pia Mungu Alijifunua kwa agano la kale kwa njia ya Neno ambaye limeandikwa Tunaona hii kwa Waraka wa pili wa Petro 1:21 unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Lakini sasa Mungu Alijifunua ya wazi zaidi katika Yesu Kristo. Tunasoma kwa kitabu cha Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Hii ilitabiriwa miaka mia saba kabla ya ilifanyika. Manabii wote waliongojea hii siku kufika kwa sababu walishika maana yake. Walijua Mungu wao atakuja na atakuwa hapa na binadamu. Bila shaka walishangaa kidogo kwa sababu walijua bikira hawezi kuwa na mimba lakini walikuwa na imani na walijua Mungu anaweza kufanya kama anataka, kwa sabbau yeye ni Mungu. Halafu tunafika agano jipya na tunaona Malaika alikuja kwa Mariamu na alimwambia yeye atakuwa na mimba na alisema Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli na kwa sababu ya hiyo atakuwa na mimba na atakuwa mtakatifu atakuwa Mwana wa Mungu. Na tunasoma kwa kitabu cha Mathayo 1:23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. hii sehemu ya mwisho ni muhimu sana. Huyu Imanueli, Yesu atakuwa Mungu pamoja nasi. Mungu mwenyewe. Tunaona sababu ya hii kwa kitabu cha Luka 1:68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Alifanya hii kwa njia ya Yesu kristo. Mungu, mwokozi wetu alichukua asili ya mwanadamu juu yake mwenyewe, ili kuokoa wenye dhambi. Alikuwa kama sisi na kila kitu, bila dhambi. Alizaliwa na mwanamke kama sisi lakini yake ilikuwa muujiza, alikuwa mtoto mdogo kama sisi na alikuwa mtu mzima na alikuwa na njaa, kiu. Kama sisi alikula chakula alikunywa, alilala, alichika, alisikia uchungu, alilia, alifurahi, alikuwa na hasira bila kutenda dhambi, alikuwa na huruma. Aliomba, alisoma agano la kale, alijaribiwa na hajaanguka. Aliteseka, alotoa damu yake, alikufa, alifufuka na alienda mbunguni na kwa hii yote alikuwa binadamu na Mungu pamoja. Ni ngumu sana kushika kama Yesu anaweza kuwa Mungu kabisa na binadamu kabisa lakini lazima tuamini hii.
Ikiwa Yesu hajakuwa Mungu kabisa, halafu kifo chake msalabani ni bure kabisa, kwa sababu ikiwa alikuwa binadamu tu, hajakuwa kamilifu na ikiwa hajakuwa kamili alikufa kama mimi na wewe tungekufa siku ile na ikiwa hi ni ukweli kila kitu sisi tunafanya hata leo asabuhi ni bure kabisa. Na ikiwa Yesu hajakuwa binadamu kabisa, hatuna mwokozi ambaye anatufahamu. Kwa sababu bibilia ni wazi kabisa alikuja hapa na alikuwa kama sisi, alijaribiwa na mambo mingi lakini bado hajatenda dhambi. Anajua sisi kwa sababu alikuwa moja wetu. Kama mstari yetu inasema Naye neno alifanyika mwili. Neno la Mungu mwenyewe ilifanyika mwili na mwili ilikuwa Yesu.
Tunasoma Naye Neno Alifanyika Mwili, akakaa kwetu. Sasa hii ni ajabu tena. Mungu wenyewe alikaa na sisi binadamu hapa miaka thelathini na tatu. Neno hili, akakaa, iko na maana mingi sana. Inamaanisha kama mtu ameweka hema yake pamoja na wengine. Ni kumaanisha aliishi kama watu wake. Alikuwa moja wetu. Alikuwa na marafiki alifanya kazi alikuwa moja na sisi. Angalia Wahebrania 2:17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Pia tunasoma Akakaa kwetu. Hii kwetu hapa ni muhimu tena. Kwa gano la kale labda unakumbuka Utukufu wa Mungu ilikuwa na wayahudi katika maskani au tabernacle. Tunasoma hii kwa kitabu cha kutoka 40:34-35 Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani. Halafu pia tuko na mara mingi Mungu alijifunua katika Yesu kabla ya alizaliwa kama kwa Abrahamu. Ukisoma kitabu cha Mwanzo 18. Utaona kama vs.1 inasema Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Sisi tutasema hii ni Yesu kwa sababu Mungu ni Roho na tunajua tumeona Mungu kwa njia ya Yesu kristo. Hatujui sura yake ilikuwa aje lakini ilikuwa Yesu, hajakuwa kama sisi bado. Lakini Abrahamu aliongea na yeye. Halafu vs.20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, Halafu vs.22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Bado Ibrahimu anasimama mbele ya za Bwana, anasimama na huyu mtu na anaongea na yeye.
Halafu Yesu alizaliwa, Neno la Mungu akivaa mwili. Petro, Yakobo na Yohana waliona utukufu wa Mungu kwa Yesu, kitu ambacho wengine hawajaona.