Witnesses of God becoming Man
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 2 viewsNotes
Transcript
John 1:15-16
John 1:15-16
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 1:15-16. Kufika hapa tumeona mambo mingi sana kwa mstari ya kwanza hadi kumi na nne. Ikiwa tulikuwa na hizi mistari peke yao zitatosha kutuonyesha Yesu alikuwa Mungu. Natumaini sana umeona hii kwa hizi mistari. Ikiwa unaongea na mtu kuhusu Yesu natumaini utasoma hizi mistari kumi na nne na hawa. Ikiwa wanakataa, wanakataa ushuhuda wa Mungu mwneywe kwamba Yesu ni Mungu. tumeona ndani yake kila kitu kimeumbwa, tumeona yeye ni Neno la Mungu na Neno la Mungu alivaa mwili na waliita yeye Yesu. Tumeona ndani yake ni uzima na nje yake hakuna, nje ya Yesu Kristo ni giza peke yake. Tumeona ushuhuda wa Yohana Mbatizaji kwamba huyu Yesu ni Nuru na wote ambao wataamini na kuweka imani yao katika yeye na watakuwa watoto wa Mungu. Tumeona Yesu alikuja kwa watu wake na walimkataa. Na wiki iliopita tuliona Neno la Mungu ilifanyika Mwili na alikaa kwetu. Na tuliona mashahidi walikuwa na waliona utukufu wake. Ya kila kitu iko kwa mawazo yako saa hii, hakuna kitu ni muhimu zaidi ya kujiuliza Yesu huyu ni nani ukweli na ikiwa umeona jibu kwa neno la Mungu sasa lazima unajiuliza nifanyaje na hii yote. Unaweza kuamini au usiamini na haya yote mawili yana matokeo ya milele.
Leo tunaona mashadi tena ya Yesu kuwa Mungu mwenyewe. Ni mzuri wakati wewe unasema wewe ni Mkristo wewe unasema Yesu ni Mungu.