Commandment of God vs. the Tradition of Men Pt.2

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 8 views
Notes
Transcript

Matthew 15:7-9

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu tulianza wiki iliopita kuhusu mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu na watu wanafundisha kama amri za Mungu. Tumeona wiki iliopita kwa nini sisi na Wakatoliki si kitu moja, tumeona kama wanaamini na akama wanaongoza kwa bibilia, sisi wakristo hatuwezi kufanya hii. Pia wiki iliopita nilisema tutaangalia Sevent Day Adventists. Leo nataka kuonyesha kama hawa wanaamini na sababu sisi si kitu moja. Kusema ukweli watu wingi hawajui vitu hivi labda hata watu ambao wanasema hawa ni sevrnth day hapa hawajui vitu hivi, labda wanajua ni kitu cha siku cha kuabudu tu, lakini ni mingi zaidi.
Saa hii kwa dunia nzima ni watu millioni ishirini na mbili wanasema hawa ni Seventh day adventist, wako na zaidi ya kanisa elfu tisini na tano, wako na shule elfu tisa mia tano na wanafunzi zaidi ya millioni mbili. Wako na dental clinics mia moja na hamsini na hospitali elfu moja mia tano. Wako busy, na wakati tunaangalia kazi wanafanya ni ngumu kusema hawa si mzuri lakini tunaongea kuhusu uamini wao na wanasema ni ya bibilia na Mungu na Yesu, na hii ni wakati shida inaingia. Swali lazima tunajiuliza ni maagizo ya wanadamu na wanafundisha kama amri za Mungu au ni ukweli wa neno la Mungu.
Tusome mistari yetu ya leo tena Mathayo 15:3,7-9 Yesu Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Vs7-9 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Tuombe:
Ni kitu moja sisi hatutaki kusikia Yesu kiusema kuhusu sisi na ni hapa. Hatutaki kusikia sisi ni wanafiki na tunasifu jina lake kwa mdomo wetu lakini miyoni wetu ni mbali na ibada yetu ni bure kwa sababu tunafuata mila au mfumo fulani ya binadamu na tunaanza kufundisha ile mfumo ya binadamu kwa watu kuliko neno la mungu.
Unajua wakati ninasoma vitu hivi ya madhehebu mengine nimeanza kuona ukweli moja na ni ukweli ambaye inaleta shida kwa wale wote na ni hii. Yesu haitoshi. Sisi wakristo wakweli tumeshika kwamba Yesu anatosha na Yesu peke yake. Lakini hawa wanaongeza mambo mingi sana kwa watu kufanya kupata wokovu au kuishi maisha amabye inampendeza Mungu. Shida ya hii ni kila kitu sisi binadamu tunaweza kuongeza kwa Yesu ni taka taka, ni chafu yetu. Nataka ninyi kusikia, Yesu anatosha, Yesu ni kila kitu na wakatu tunajaribu kuongeza kitu cho chote kwa yesu tunaleta yeye chini na hawezi kuletwa chini. Hata Paulo alikuwa na hii shida na watu, hii si shida ya wakati wetu, imekuwa tangu mwanzo. Paulo aliandika barua yake kwa kanisa la korintho na lile kanisa walikuwa na shida mingi, hii ni sababu barua zao ni mrefu na aliandika mbili. Walikuwa na watu wengi sana na makabila mengi. Paulo alifundisha hawa vizuri kuhusu Yesu na wokovu wake lakini ni kama Yesu hatoshi kwao. Angalia Waraka wa pili wakorintho 11:4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! Anasema hata baada ya ameona hawa Yesu wa kweli bado ikiwa mtu anaingia na anahubiri injili ingine, Yesu mwengine, Roho ingine wale wa kanisa la Korintho walikubali. NA shida hata mimi ninaogopa kwenu ni kama amesema kwa vs.3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Kama shetani aliingia ile nyoka bustani na alidanganya hawa ni kama walimu wa uongo, wanajua kudanganya watu sana. Kusema ukweli ni mafundi ya kudanganya. Na wanaongoza watu kufuata mfumo fulani na wanatoa fikira za watu na wakauacha unyofu na usafi wa Kristo. Hii ni shida hata ya siku zetu. Kufuata Yesu si kama watu wanasema na wanafundisha na wanaweka sheria mingi na wanalazimisha watu kufanya mambo ya maajabu kusema ukweli. Na iko hapa kwa hii mstari kusema ukweli ni unyofu na usafi wa Kristo. Ni hii tu, hakuna kitu kiingine.
Ni vitu vingi sana kwa hizi madhehebu lakini ninajaribu kuonyesha nini chache tu na wewe wakati unaongea na moja wai unaweza kusaidia hawa kujua kama wanaamini pia. Kitu cha kwanza Seventh Day si kitu cha zamani. Walianza miaka mia moja sitini na moja iliopita. Sasa kwa miaka elfu mbili kanisa la Yesu Kristo limekuwa na kabla ya Seventh Day ilianza tulikuwa na na miaka elfu moja mia nane, ni kusema kwa hizi miaka yote watu hawajajua ukweli? Hawajakuwa wakristo? Chunga sana wakati dini au madhehebu mpya inatoka. Kwa nini inatoka na kwa nini tunahitaji kitu kipya?
Kitu kiingine na ni ile sisi sote tunajua ni siku ambaye wanabudu. Wanaabudu Mungu siku ya saba na siku ya saba ni Jumamosi. Seventh Day Adventists wanaamini siku ya kuabudu Mungu inaanza wakati jua inaenda chini ijumaa mpaka jumamosi wakati jua inaenda chini. Na wanaamini hii sana hata wanasema ikiwa unabudu Mungu siku ingine unavunja sheria yake. Amerkiani ni billboard mingi na ni kubwa wakati unaendesha gari kwa bara bara na ni ya Seventh Day na inasema Kuabudu Mungu jumapili ni alama ya mnyama, mark of the beast. Hii ni ajabu sana. Shida ya hii ni wanaanza kuabudu siku ya wiki kuliko Mungu mwenyewe. Kusema ukweli sisi wakristo tunaabudu Mungu wetu kila siku ya wiki, si siku moja tu. Hii ni shida ya watu wingi ambao wanasema hawa ni wakritso, wanaishi kama wasioamini siku sita na siku moja wanakuwa watakatifu kwa saa chache. Wakati tunaanza kuweka macho yetu kwa siku fulani tunaabudu Mungu shetani anapenda hii sana. Kwa sababu inatoa macho yetu kwa Yesu na tunaanza kujali mambo ambayo kusema ukweli hayana maana. Sisi kwa agano jipya tuko na mfano na si mfano tu lakini maagizo kutoka mitume ya siku gani kukutana kama kanisa la Yesu kristo na kumwaabudu Mungu.
Nataka kuangalia kama Neno la Mungu linasema kuhusu hii. Natumaini umeleta bibilia yako. Kitu cha kwanza Yesu alifufuka siku ya kwanza ya wiki, Jumapili Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. Baada ya yesu alifufuka alikutana na wanafunzi wake siku ya kwanza ya wiki, jumapili. Kitabu cha Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Halafu tunasoma vs.26 Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Walihesabu jumapili hadi jumapili na ni siku nane. Tena Walikutana na Yesu alikuja tena. Tunaona Roho Mtakatifu alikuja juu ya mitume siku ya kwanza ya wiki, jumapili. Kitabu cha Matendo 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Angalia vs.4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, Unasema sasa unajua hii ilikuwa siku ya kwanza ya wiki naam na gani? Kwa sababu vs.1 inasema walikuwa pamoja siku ya pentekoste. Angalia Kitabu cha mambo ya walawi 23:15 15 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; Sasa hapa anaongea kuhusu ilisherehe ya matendo mlango wa pili. Ni Pentekoste na tunaona hii ni sheria ya Mungu na anasema sabato saba hii ni siku arobaini na tisa au anasema baada ya jumamosi saba halafu tunasoma vs16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya. Sasa anasema siku iliyofuata jumamosi saba itakuwa siku hamsini na siku ile ni jumapili na wataleta bwana sadaka ya unga mpya. Na hii ni siku ile tunasoma kwa matendo 2:1 na ni ajabu Roho anakuja siku ile, si siku ya sabati lakini siku ya kwanza, jumapili.
Waraka wa kwanza wakorintho 16:1-2 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; Sasa hata kwa desturi la Wayahudi wameshaa anza kazi yao siku ya kwanza ya wiki, kwa nini watakuwa pamoja kuchukua sadaka au changizo ya watakatifu? Kwa sababu wamekuwa wakristo si wayahudi, na desturi imetoka na wanakutana kuabudu mungu wao siku ya kwanza ya wiki, jumapili kwa sababu Yesu, Bwana wao alifufuka siku ile. Angalia Matendo 20:7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. Hapa ni jumapili tena, Wakristo walikuwa pamoja, walikula pamoja halafu Paulo alianza kuhbiri. Ni kama wanafanaya kanisa hapa. Ni jumapili.
Sisi wakristo hatusemi jumapili ni siku ya sabato, tunaita hii siku, siku ya Bwana. The Lords Day. Angalia Kitabu cha Ufunuo 1:10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; Tangu hii imeandikwa mpaka leo asabuhi sisi wakristo tumeita jumapili siku ya Bwana. Ni mzuri kujua siku ya sabati haijabadilishwa, imeondolewa. Angalia kiatbu cha Wakolosai 2:16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; Tunaona hapa Paulo anaongea kuhusu mambo mingi sana kuhusu chakula, vinywaji, sikukuu na mwisho anasema hata sabato. Na ansema mtu asituhukumu sisi kuhusu vitu hivi na kama tunafanya. Sasa hii ngumu sana kwa myahudi kusoma kwa sababu vitu hivi vyote ni maisha yao ya kumpendeza Mungu na kujaribu kufuata sheria ya Mungu. Agano la kale ilijaa na njia ya kufanya vitu hivi. Lakini unaona anaanza hii mstari na basi. Basi hapa ni kubwa ni kusema kwa sababu ya hii, hii hapa ni vs.14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; Yesu alitoa hii mambo yote ambaye ilikuwa juu yetu, kufanya hii ama hii ama hii kumependeza Mungu, sasa ameleta uhuru kwetu na ameleta njia ingine na njia ni yeye. Hii maneno yote ya kujaribu kupendeza Mungu kwa njia ya sheria au matendo alisema kwa vs.17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; Anasema hii yote ilikuwa kuweka macho yetu kwa ile ambaye inakuja na anasema , bali mwili ni wa Kristo. mwili ni kusema asili ya hii yote ni Kristo. Kila kitu ni yeye ni kuweka macho yetu kwa ule ambaye anaweza kufanya hii na kufanya kamili ni Yesu.
Hii jambo la kuabudu Mungu jumamosi imekula wakati wetu na ni kitu moja. Lakini waacha nijaribu kuenda haraka kueleza vitu vingine ambavyo ni muhimu unajua kama Seventh Day wanamini. Kitu kiingine ni Usingizi wa nafsi au Soul Sleep. Seventh Day wanaamini wakati unakufa huendi mbinguni kuwa pamoja na Mungu. Roho yako inalala kaburini mpaka Yesu atarudi. tuko na mistari mingi kwa bibilia zinatuambia tofuati sana. Lakini moja inatosha, kwa sababu ni wazi kabisa ni Waraka wa pili wakorintho 5:6-8 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Wakati sisi tunakufa, wakati huo tunasiamam mbele ya Mungu.
Kitu kiingine wanaamini ni Maanagamizi au Annihilation. na kwa sababu wanaamini hii wanasema Jehanamu ni ya muda si ya milele. Sasa bii ni mbaya sana. Wanasema wasioamini wataenda jehanamu kwa muda fupi halafu msioamini anaangamizwa. Kuteseka kwake si milele. Wanasema hakuna roho ya milele. Tena kumbuka tunaangalia mafundisho ya wanadamu na wanafundisha kama ni amri za Mungu au ukweli wa neno la Mungu. Kusema hii uamini wao wa maanagamizi unweka hata Yesu kuwa Mwongo. Angalia kama amesema kwa kiatbu cha Mathayo 25:46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. adhabu ya milele ni mahali wasioamini wataenda. Kusema hakuna jehanamu ya milele au utaangamizwa ni kusema hakuna matokeo ya dhambi na kama umeishi maisha yako. Bila shaka watu wengi wanataka hii. Wataishi kama wanataka hapa kwa maisha haya na badaye kwisha, hakua dhamiri, hakuna roho, hakuna kuteseka. Pia tuko na Yesu kuongea kuhusu ule Mtajiri na Lazaro kwa Luka 16:22-24 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Jehanamu ni ukweli kabisa na ni ya milele na ni mahali mbapo neno la Mungu inatufundisha watu ambao hawajatubu kwa dhambi zao na hawajaokoka , wataenda na watalipa bei kwa dhambi zao. Angalia Ufunuo 14:11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. Ni ya milele.
Kitu kiingine wanaamini ni Shetani atabeba dhambi zote za Wakristo. Zitawekwa juu yake. Hii ni shida kubwa kwa sababu dhambi zetu zote ziliwekwa kwa Yesu siku ile alikufa msalabani. Ni yeye na yeye peke yake anaweza kubeba hii uzito. Kwa nini dhambi zitawekwa juu ya shetani? Tena kumbuka, mafundisho ya binadamu inataka kutoa macho yetu kwa Yesu, lengo ya shetani ni kukoroga na kucafua ukweli wa neno la Mungu.
Kitu Kiingine wanasema ni lazima kubatizwa kuingia ufalme wa Mungu. Ikiwa hujabatizwa hujaokoka. Ni ukweli Yesu anasema kubatiza watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu lakini hii ilikuwa ishara kuonyesha wasioamini na duni awewe unafuata Yesu. Maji haiwezi kuokoa mtu kutoka dhambi zao, ni Yesu Kristo peke yake. Kumbuka nimesema, kwa watu wengi Yesu haitoshi, hata wanaongeza maji, maji ile unakunywa, unafua nguo, unasafisha gari. Hakuna kitu inafanyika kwa hii maji wakati unaingia kubatizwa. Pia lazima tukumbuke ule mwizi alikuwa kwa maslabani kando ya Yesu. Aliamini Yesu ni mwana wa Mungu na Yesu alisema leo utakuwa nami peponi. Huyu mwizi alikufa hapo, bila kubatizwa. Ikiwa ubatizo ni lazima kupata wokovu, Yesu alidanganya yeye.
Wakati imeenda sana na bado ni mingi sana wanaamini lakini natumaini sana hii imekusaidia kujua kidogo tu na kukusaidia kuuliza hawa maswali kuhusu kama wanaamini na kuonyesha hawa ukweli wa neno la Mungu. Lakini kwa mwisho nataka kuongea kuhusu huyu mwanamke anaitwa Ellen White. Seventh Day wanaweka vitabu vyake pamoja na Bibilia. Ellen alikuwa na maono na ndota zaidi ya elfu mbili na wanasema alikuwa nabii. Kitu cha kwanza kuweka kitabu kiingine pamoja na neno la Mungu, haiwezikani. Lakini pia hii ilifanyika kama miaka mia moja na hamsini iliopita. Lakini kwa haraka ni vitu vichache Ellen aliamini na aliandika kwa vitabu sita na Seventh Day wingi wanaamini leo. Kitu moja alisema ni Yesu hajakuwa mzaliwa wa kwanza kwa mama yake. Ndugu zake walikuja kwanza. Hii ni shida kubwa sana. Kwa nini? Kwa sababu Isaya alitabiri kwa Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Halafu tunasoma Mathayo 1:24-25 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.
Kitu kiingine anasema ni Malaika wanahitaji cardi ya dhahabu kuingia mbunguni na kutoka mbinguni.
Kitu kiingine anasema ni watu ambao wameokoka wakati tunafufuka tutakuwa na mbawa.
Kitu kiingine anasema ni alijua kamili siku ile Yesu atarudi. Alisema Yesu atarudi mwezi wa sita 1845. Hajarudi. Bibilia inasema kwa Marko 13:31-32 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Kitu kiingine ni lazima tunatii amri kumi kuu kupata wokovu. Wagalatia 3:11 Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
Kitu kiingine anasema ni hakuna mtu anaweza kuwa na uhakika ya wokovu wao. Waraka wa kwanza wa Yohana 5:13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
Kitu kiingine alisema ni damu ya Yesu haiwezi kutoa dhambi. Waraka wa kwanza wa Yoahna 1:7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Alisema pia Yesu hajakuwa Mungu. Ni ajabu sana. Bila shaka Seveth Day wingi hawajui kama dini lao inasema.
Tena, sababu tunaangalia vitu hivi si kuchapa mtu lakini kusaidia wewe ikiwa umeingia na hawa ni mzuri unajua bibilia inasema nini na ikiwa uko na marafiki au familia ambao wameingia kwa vitu hivi, unaweza kuuliza maswali mazuri kwao kwa sababu unajua kama wanaamini. Natumaini imekusaidia kujua zaidi.
Ikiwa uko hapa leo asabuhi na umeshikwa na hii uongo nitaomba tafadhali tubu na fiata Yesu wa bibilia. Ikiwa hujui Yesu Kristo hujaamini katika yeye na kazi yake nitaomba tubu na amini na fuata Yesu kwa njia ya neno lake. Ukitaka kuongea na sisi tuko hapa, tutapenda sana kueleza zaidi na kutoa majibu kwa maswali yako. Unaweza kuketi na tutakuja kwako. lakini tafadhali ongea na mtu, ni muhimu sana.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe, na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more