Commandment of God vs. the tradition of Men Pt.3
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 4 viewsNotes
Transcript
The Charismatic Church
The Charismatic Church
Leo asabuhi tunendelea kuangalia masomo yetu kuhusu amri za mungu na mapokeo ya wanadamu. Tumeangalia kama Wakatoliki wanaamini na wiki ilopita tuliona kama Seventh Day Adventist wanaamini. Natumaini sana ikiwa uko na marafiki au famili wako ndani ya vitu vile unaweza kusaidia hawa kujua bibilia inasema nini ukweli na kufuata Yesu ni nini ukweli. Pia natumaini sana ninyi umeona na unajua Yesu anatosha, Anatosha kwa kila kitu, maisha, wokovu kila kitu na si lazima sisi tunaongeza vitu, si lazima sisi tunasaidia yeye. Kumbuka kama Paulo alisema kwa Waraka wa pili wakorintho 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Na kusema ukweli dunia nzima hii inafanyika sana na watu wametoka unyofu na usafi kwa Kristo. Wamedanganywa kufikiri Yesu hatoshi na ni lazima tusaidie yeye. Hii ni uongo sana. Watu wamedanganywa kufikiri kufuata Yesu kristo ni mambo mingi na huwezi kupata kwa bibilia.
Leo tutaangalia kanisa la charismatic au The Charismatic church. Sisi sote tunajua hawa, kusema ukweli karibu kila kanisa siku hizi hata kwa hii area ni Charismatic , tunaweza kujua naam na gani? Kwa sababu ya vitu wanafanya.Wanasema wanafuata Yesu Kristo, Wanasema wanatumia bibilia, kuketi na kuongea utafikiri unaongea na mtu ambaye anafuata neno la Mungu. Lakini ni vitu ambavyo ukianaza kuongea kuhusu unashangaa kidogo. Kama madehebu wengine wamechafua neno la Mungu, lakini lengo ya viongozi wao ni tofuati sana. Lango ya viongozi wao ni pesa na mamlaka. Nataka ninyi kujua ni vitu vi tatu vinafuata walimu wa uongo, pesa, mamlaka na wanawake. Kanisa la Charismatic ni ngumu sana kwa sababu watu wanakula kundi la Mungu, ni mbwa mwitu.
Hii yote ilianza miaka sitini na tano ilopita. Tena nitasema ikiwa kitu ni kipya chunga sana. Sisi tuko na miaka elfu mbili ya historia ya kanisa na kama wameaamini na kama wamefanya. Chunga sana kwa sababu ni walimu wa uongo au fraudsters wanapenda sana vitu vipya. Ni lazima sisi wakristo wafuasi wa yesu kristo tunajiuliza ukweli ni nini? Na ukweli inatoka wapi. Nini au nani ni mamlaka ya mwisho? Ikiwa hatujui halafu ukweli ni kama kila mmoja anasema. Mimi niko na ukweli wangu na wewe uko na yako, tukishi kama hii kama wakristo tuko na shida kubwa sana. Ikiwa wewe ni Mkristo wa kweli ni lazima unaamini ya kwamba mamlaka ya mwisho ni Mungu na kama anasema kwa neno lake. Wakati Yesu aliombea wanafunzi wake alisema kwa kitabu cha yohana 17:17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Nje ya hii hatuna kitu cho chote ya kusimama juu yake. Hii ni lazima sisi tunakuwa watu wa neno la Mungu wetu, tunajua kama anasema na kama anataka sisi kuishi na kufanya.
Kanisa la Charismatic, neno la Mungu si mamlaka ya mwisho kwao. Hawa wako na mamlaka inayoelea, inategemea hisia na uzoefu na ndoto wao. Wakati wanafanya kitu wanasema Mungu ameniambia, lazima alimwambia huyu kwa njia ya ndoto, au maono. Hata ni wingi wanategemea ishara kwa Mungu kuwaonyesha kitu. Sisi sote bila shaka tuko na story mingi tumesikia. Hata ni ajabu ni Mwanamke moja alisema aliona uso wa Mary kwa kipande cha Mkate ilikuwa 1994 na alikaa na mkate karibu miaka kumi na aliuza hii kipande cha mkate kwa shilingi millioni tatu na nusu. Ni wengine wanaona gari lao linatoa mafuta ya engio kwa ground iko na leak na wakati wanaona kumbe ni kama hii mafuta ina sura ya nchi na ni tanzania, hii ni Mungu ananiambia kuenda tanzania. Watu wale wanategemea sana vitu vingi nje ya bibilia.
Ni kama watu wanatafuta sana ishara na maajabu siku zetu, Bibilia haitosho, Yesu hatoshi. Ni mzuri kukumbuka Udanganyifu wa mwisho katika siku za mwisha na dhiki itatokea kupitia ishara na maajabu. Mathayo 24:24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Hawa ambao wanataka vitu hivi watadanganywa rahisi sana kwa Kristo wa uongo na shetani. Hawa na misingi na maarifa ya ukweli.
Kusema ukweli tunaweza kuongea kuhusu kanisa la Charismatic jumapili tatu nne lakini nitajaribu kufupisha na kwako kujua wanaamini nini na kama kuonyesha hawa ukweli wa neno la Mungu.
Tusome mistari yetu ni Mathayo 15:3,7-9 Yesu Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Vs7-9 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu. hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Sisi wakristo hatutaki mapokeo au maagizo ya wanadamu, sisi tunatamani sana kujua Mungu anasema nini. Hii kanisa la Charismatic ilianza miaka sitini na tani iliopita lakini imeshaa kuwa desturi la watu wengi. Wengi wenu umezaliwa kwa lile kanisa na umeona mambo mingi sana na umefundishwa maneno mingi sana ambaye iko na wewe mpaka saa hii na ni neno la kweli peke yake inaweza kutoa ile uongo.
Kitu moja wanasema ni sisi tunaweza kupoteza wokovu wetu. Ni kama hawa wote wa uongo wanasema hii. Ni kama Yesu hana nguvu ya kutosha. Wanasema hii kwa sababu kukaa mkristo inategemea matendo yako. Wanasema ukipoyeza wokovu wako ni lazima unafanya matendo mingi kuoata tena. Shida ya hii ni sisi tunajua kwamba wokovu ni zawadi ya Mungu na inakuja kwa njia ya neema yake. Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kila kitu kuhusu wokovu wetu ni Mungu. Wakati unashika mistari kama Yohana 10:28 -29 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Wakati unashika kama inasema unajua wokovu wako ni mikononi ya Mungu, nani ako na uwezo kukutoa?
Kitu kiingine wanafundisha ni si kila Mkristo ako na Roho Mtakatifu. Hii ni sababu utasikia mtu kuuliza mwengine umepokea Roho? Au hii ni sababu kwa makanisa mingi snaa hapa unasikia hii manneo ya KUPOKEA, POKEA, POKEA. Hii ni mcheza wanacheza kuuza RPho Mtakatifu kwa watu, kufikiri hawa wako na nguvu fulani ya kuleta Roho kwa mtu na kumbuka, Roho Mtakatifu ni Mungu kabisa. Lakini Bibilia imejaa na mistari mingi sana kuonyesha hii ni uongo. Angalia Warumi 8:9-11 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, Ako wapi? Ako ndani yetu na anakaa hapo. ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Ikiwa Roho hayupo ndani yako wewe si Mkristo, wewe ni msioamini. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, Tena ako wapi? Ndani yetu na anakaa hapo. yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Tena anakaa ndani yenu. Kwa hizi mistari tatu tunaona kama wanasema kupokea ni uongo kabisa. Ikiwa wewe ni Mkristo ako ndani tayari. Na swali si ikiwa umepokea Yesu lakini ikiwa Yesu ni mwokozi wako, umeamini? Kwa sababu huwezi kuwa na Roho yake bila kutubu na kuamini. Mtu ambaye anaenda kwa kanisa la Charismatic atasema anajua Roho anaishi ndani yake kwa sababu nilipata uzoefu na nimepata ile ubatizo na ninasema kwa lugha. Lakini Mkristo wa kweli atasema ninajua Roho anaishi ndani yangu kwa sababu Mungu amesema kwa neno lake anaishi ndani ya waamini. Waraka wa pili watimotheo 1:14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. Ako wapi? anakaa ndani yetu.
Kitu kiingine ni kunena kwa lugha. Unajua ni mzuri kujua ikiwa unaenda kanisa la Pentecostal hii jina inatoka kwa Pentekoste siku ile wakati Roho alikuja kwa waamini na waliaanza kuongea kwa lugha tofuati. Kunena lugha ni kitu kubwa kwa kanisa la Charismatic. Wanasema ikiwa hujanena kwa lugha toafuti hujapata Roho bado. Shida ya hii ikiwa hujapata roho, bado wewe ni msioamini. Lakini nataka kuwa wazi kama bibilia kuhusu hii maneno ya kunena lugha. Wewe umeona kama hawa wanafanya na ni ujinga na maneno mingi hata watu hawaelewi kama mtu amelewa. Maandiko ni wazi angalia Matendo 2:1-8 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Mwisho ya vs.6 anasema nini? Kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Walikuwa kabisa mingi tofuati walikuwa hapo siku ile. Hata ukisoma vs.9-10 utaona karibu kabila kumi na tani toafuti. Ni kama Mimi saa hii nikianza kuongea kwa lugha ya kimaasai, na ninyi yote unasikia kama ninasema kwa lugha yenu, hii ni karama ukweli ya kuenena lugha, si kama watu wanafanya siku hizi. Vs.8 ni wazi wale wote wanasema hawa ambao wanaongea ni ya wagalilaya na sasa tunasikia hawa kwa lugha yao, lugha waliyozaliwa nayo. Si ujinga inafanyika hapa. Si fujo inafanyika hapa.
Halafu angalia Waraka wa kwanza wakoritnho 14. Sasa hii mlango mzima inadeal kuhusu hii mambo ya kunena lugha. Lakini angalia vs.13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. Hii liugha unanena ni lazima inaweza kutafsiriwa. Karibu mwisho ya hii mlango kuhusu hii tunaona vs.33 Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. Ukiingia kanisa fulani na unaona hii yote na ni kama watu wameruka akili, toka hapo haraka sana. Mungu wetu si Mungu wa machafuko. Kanisa lile si kanisa la Yesu kristo. Ni mzuri kujua hii kuenena lugha ilikuwa karama ya Mungu, haijafundishwa na mtu, lakini leo tuko na madarasa kufudisha watu kuenena lugha ya uongo. Hii si kama Bibilia inasema kuhusu hii.
Kwa haraka ni kuonyeshe utaratibu na miongozo kuenena lugha kwa Bibilia. Yote iko hapa kwa Waraka wa kwanza wakorintho 14. Ya kwanza Ilikuwa ishara kwa wayahudi ambao walikuwa wasioamini. Angalia vs.22 Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini. Tunaona ni kwa watu wa wili au wa tatu kwa ibada vs.27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lazima mtu anaweza kutafsiri vs.28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Haiwezi kuwa fujo kumbuka Mungu wetu si Mungu wa machafuko. Na kwa mwisho wanawake angalia vs.34-35 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Wakati unaangalia makanisa leo, wanafanya kama bibilia inasema?
Kitu kiingine wanafundisha ni upnuaji na miujiza. Kitu cha kwanza nataka ninyi kusikia ni hata leo Mungu wetu ni Mungu ambaye bado anafanya miujiza. Anajibu maombi na anaponyesha watu wakati ni mapenzi yake. Lakini kanisa la Charismatic wanafundisha bado wakristo wako na hizi karama za kupnyesha watu na kufanya miujiza. Kama kunena kwa lugha hii yote ilikuwa kwa muda fupi na zilikuwa kuonyesha wayahudi kwamba kama wanafunzi wa Yesu walisema ilitoka kwa Mungu ukweli. Agano kipya haijaandikwa bado na hizi ishara ilionyesha huyu mtu ni mtume, ni mtu Yesu alituma. Ukifuata vitu hivi kwa bibilia itaona wale watu wa leo wanafanya si kama watu wa bibilia. Kwa bibilia tunaona wakati mtu aliponyeshwa ilikuwa bila shaka yo yote. Si kama leo mtu ako na shida ya tumbo na huwezi kujua ikiwa nui ukweli wameponyeshwa. Pia wanaleta watu kwa wheelchaor au Crutches na wanasema simama na temebea na huwezi kujua ikiwa huyu mtu alikuwa naam na hiyo na kusema ukweli wengi wanaletwa, hawa na shida yo yote na wanalipwa kusema wako naam na hiyo. Kwa nini wale wa leo hawawezi kurudisha mkono au miguu ya mtu mbele ya macho yetu? Kwa nini hawataingia hospitali kuponyesha watu? Kitu kiingine ni mzuri unajua ni mitume hawajachukua pesa kufanya vitu hivi. Angalia Matendo 3:6 Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. Kwa vitu vya hii dunia mitume walikuwa maskini, walitoka kila kitu kufuata Yesu. Hizi karama zilikuwa kwa muda fupi sana, hata kabla ya Paulo alikufa zilianza kutoka. Timotheo alikuwa kama kijana ya Paulo alipenda yeye sana na Timotheo alikuwa na shida na tumbo lake. Ni mzuri Paulo aende kwake na kumponyeshe. Lakini angalia kama PAulo alimwambia Timothea Waraka wa kwanza waitmotheo 5:23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. Angalia waraka wa pili watimotheo 4:20 Erasto alikaa Korintho. Trofimo nalimwacha huko Mileto, hawezi. Kwa iingereza inasema alimwaacha Trofimo mileto, alikuwa mgonjwa. Paulo alikuwa naye, kwa nini hajamponyesha? Hii karama ilishaa toka. Kitu cha umuhimu sana ni mzuri ninyi unajua. Kwa sifa za viongozi wa kanisa Paulo anaadika kama lazima wanakuwa, tunapa kwa Tito 3 na waraka wa kwanza watimothoe 3 na huwezi kupata sifa moja anasema ni kupoyesha watu au nkufanya muujiza. Pia kwa tunda la Roho ya Mkristo kwa wagalatia 5 tunaona vitu tisa, na hakuna ni kuponyesha watu au kufanya miujiza.
Wakati inaenda lakini ni muhimu unajua vitu hivi. Kitu kiingine wanafundisha ni Theologia ya ustawi ( prosperity theology). Wanasema ikiwa wewe uko karibu na Mungu na ako karibu na wewe, na siku zetu ukitoa pesa za kutosha utabarikiwa kimwili na Mungu. Utakuwa na afya mzuri sana. na kwa sababu kila mtu anataka hii wanakimbia haraka sana kwa wale walimu wa uongo. Ni mzuri sana tunajichunga kwa sababu hata sisi tunaweza kuanguka kwa hii uongo ya ukaribu wetu na Mungu unatokana na hali zetu. Ni mzuri kukumbuka Wagalatia 6:7-8 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Ikiwa wewe ni mlevi bila shaka matokeo ya hii kuharibu ini lako (liver) ikiwa unalala na malaya unaweza kupata ugonjwa fulani. Hii ni matokeo ya kama watu wanaishi. Lakini si ugojwa wote ni sababu mtu anaishi dhambini au maisha mbaya. Kwa sababu ya dhambi hii mwili wetu inaoza kila siku. Mifupa yetu si kama wakati tunakuwa vijana, kupoteza kumbukumbu ni kwa sababu ya akili zetu zinazeeka. Unajua kuwa na ugonjwa au kiti kiingine mashani ya Mkristo inaweza kuwa mapenzi ya Mungu kwa ule mtu Warumi 5:3 ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; Ukisoma kitabu cha Petro anaogea sana kuhusu kuteseka lakini inaleta watu karibu na Mungu na ni ukweli. Pia ni mzuro kukumbuka Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Sasa hapa katika mambo yote ni nini? Ni kila hali ya maisha yetu. Shida ya kanisa la Charismatic ni wanatumia hisia ya watu na tamaa zao ya kutaka afya na baraka ya vitu vya hii dunia kudanganya watu. Chunga sana
Tunaweza kuendelea kwa muda lakini vitu viingine wanaamini ni kutoa mapepo kwa watu, hii ni hatari sana. Wanaweka nguvu ya Mungu ndani ya vitu kama maji, mafuta, binadamu, Man of God na wanaweka huyu mtu kwa nafasi ya yesu na wanabudu huyu man of God zaidi ya yesu. Shida kama nimesema ni Yesu hatoshi. Na mimi nitasema na Paulo kama tumeshaa soma Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Jua Bibilia yako, fuata yesu ya bibilia si Yesu ya hii dunia watu wameunda kufanya mapenzi yao na kuwapea watu tamaa zao.
Ikiwa uko hapa leo asabuhi na umeshikwa na hii uongo nitasema tubu na fuata yesu kristo wa kweli. Ikiwa hujui Yesu, hujaweka imani yako katika yeye nitasema tafadhali, Tubu, amini na fuata yeye. Ukitaka kuongea zaidi tuko hapa. Kaa mahali uanketu na tutakuja kwako au kuja mbele baada ya ibada yetu na uliza kama unataka, tuko hapa kujibu.
Asanteni sana, Bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo. hutaki kukosa wiki ijayo kwa sababu ni utangulizi wa kitabu cha Yohana.