The True Church

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

1 Timothy 3:15

Kwa wiki tatu tuliangalia madhehebu mengine na kaa wanafundisha na wanaamini. Tuliona kama wakatoliki, Seventh Day na hata kanisa la Charismatic wanaamini na kama wanafanya. Tumeona kwa kila moja Yesu peke yake hatoshi na wanaongeza matendo na sheria mingi sana juu ya watu wao kufuata Yesu, kusema ukweli hii si Yesu wa bibilia, ni Yesu mwengine ni injili ingine. Yesu alisema wazi kabisa kwa kitabu cha Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Hii ni Yesu wa bibilia anaongea na anasema si sheria mingi, si matendo ya mtu lakini yote ni kuhusu Yesu, ndani yake tutapata raha nafsini mwetu kwa sababu nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi. Ukiangalia leo kwa makanisa na yale tumeanagalia kama wanafanya wanaweka uzito mingi juu ya watu wao na hata wingi wameanza kuuza Yesu na wokovu wake kwa wengine. Pia wameleta manabii wa uongo na wameweka hawa na maandishi yao sawa sawa na neno la Mungu. Nataka kukumbusha sisi ya kitu Paulo alisema kwa kanisa la Korintho. Waraka wa pili wakorintho 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Ukiweza kuweka hili akilini mwako itakusaidia maisha yako yote hapa kwa hii dunia. na sisi hatutaki kuwa kama vs.4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! Sisi hatutai kuwa kama kanisa la Korintho,Ikiwa mtu anakuja na anahubiri injili nyingine, roho ingine, Yesu Mwengine sisi hatutakubali.
Leo asabuhi nataka sisi kuangalia kanisa la kweli ya Yesu kristo ni nini. Mstari yetu ya leo ni Waraka wa kwanza watimotheo 3:15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kitu cha kwanza nataka sisi kushika ni kwamba sisi wakkristo ni kanisa la Yesu Kristo, si nyumba ya mawe, bao ama mabati. Roho Mtakatifu anaishi ndani ya kila Mkristo. Sisi wakristo ni hekalu ya Mungu. Waraka wa kwanza wakorintho 6:19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; Ikiwa sisi tumeshika umuhimu ya hii, tutaishi maisha yetu tofuati sana. Kila siku, kila dakika Roho Mtakatifu anaishi ndani yangu, Mungu akp pamoja nasi kila mahali, anaona kila kitu, anasikia kila kitu.
Wakati sisi wakristo tunakuja pamoja kuabudu Mungu wetu ni kanisa. Mara mingi mahali tunakuja pamoja ni nyumba fulani na tunasema hii nyumba si kanisa lakini ni mahali kanisa, Wakristo wanakuja pamoja kuabudu Mungu wao. Sisi ni nyumba ya Mungu. Ni kama hii kama dunia nzima. Tuko na kanisa la dunia ni kila Mkristo halafu tuko na kanisa ambalo ni area tunaishi, tunaita hii local church. Sisi sote ni sehemu ya local church. Ninyi ni sehemu ya AIC Sekenani au mara mingi tunasema Mshariki. Ni mahali unaenda kushiriki pamoja na wakristo wengine ambaye wanafikiri kama wewe kuhusu Bibilia, yesu, Mungu wokovu na hii yote.
Kwa mstari yetu ni mzuri tujue Paulo aliwaacha Timotheo kwa mahali inaitwa Efeso.Paulo alikaa karibu miaka mbili kwa efeso na watu wengi waliamini na walikuwa wakristo. Paulo alianzisha kanisa la kwanza hapo na wakati alitoka walikuwa kanisa saba kwa ile area. kama kawaida walimu wa uongo waliingia. Walianza kufundisha kama tumeona kwa wiki tatu kwa madhehebu mengine, vitu amabvyo si kwa bibilia. Walianza kufundisha mila na mifumo ya binadamu kuliko neno la Mungu. Aliwaacha Timotheo kwa Efeso kuwa pastor ya kanisa na kujaribu kuonyesha ukweli wa Yesu kristo na kunyorosha walimu wa uongo. Tunafika mstari yetu na tunaona Paulo kusema Kwa timotheo anaandika hii barua ili watu wanaweza kujua kuenenda katika nyumba ya Mungu. Kumaanisha wakati wakristo wanakuja pamoja iko na utaratibu wake kama inafanya. Hata kwa hii mlango Waraka wa kwanza watimotheo 3 tunaona vs.1-13 ni kuhusu wanaume ambao wataongoza wakristo. Paulo anatoa sifa za wale wanaume. Hata vs.11 tunaona sifa za bibi ya kiongozi wa kanisa. Na sifa hizi sio mapendekezo tu lakini ni amri. Tunasoma vs.2 Basi imempasa askofu. na vs.7 Tena imempasa. Imempasa ni lazima ako na vitu hivi maishani yake, lazima vitu hivi ni tabia ya maisha yake.
Kwa sababu tuko na neno la Mungu hakuna mtu ako na haki kufanya kanisani anataka. Kanisa ni ya Mungu na yeye anatuobnyesha kama anataka kuabudiwa. Hii ni sababu ni muhimu sana tunaweka viongozi ambao wako na sifa Paulo anasema, kwa sababu ikiwa wako na hizi sifa ni watu ambao wanajua neno la Mungu na watafundisha na kuongoza kundi la mungu kwa njia zake. Angalia kitabu cha Matedno 20:28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Kiongozi muzuri anafanya hii anachunga sana kundi la Mungu, kwa sababu anashika ya kwamba Yesu alilipa kwa kanisa lake na damu yake.
Halafu tunaona kwa mstari yetu Paulo anasema, Iliyo kanisa la Mungu aliye hai. Kwa nini atasema hii? Kanisa la Mungu wetu si kama ingine, Mungu wetu ako na uhai, anaishi hata saa hii. Kama tumeona kwa madhehebu mengine ni kama wanajaribu kusiaida Yesu kwa matendo yao, wanaongeza vitu vingi juu ya watu wa Mungu. Wanasahau kwamba Mungu wetu yesu Kristo alifufuka na saa hii ako mbinguni na anaona kila kitu na siku moja anarudi kuchukua kanisa lake na kuleta hukumu kwa wale watu amabo wanabaki.
Halafu kwa mwisho ya mstari yetu ya leo tunaona Paulo kusema kitu kuhusu sisi wakristo anasema nguzo na msingi wa kweli. Hii ni kanisa la kweli. Sisi hatutaki mila au mfumo fulani ya binadamu na hii dunia sisi tunataka Yesu na yeye peke yake. Kujua ukweli wake ni tamaa ya mioyo yetu. halafu sisi wakweli tunweka hii ukweli mbele ya dunia na watu wote kuona. Macho ya kila mtu wanaangalia na sisi tunaweka Mungu na ukweli wake wazi kwa wote kuona. Unataka kujua shida ya kijiji yetu, county yetu, nchi yetu? Ni sisi wakristo tumesahau sisi ni nguzo na msingi wa kweli. Watu wengi hawataenda kanisa watajua ukweli naam na gani? Angalia kitabu cha Mathayo 28:19-20 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Wengi wanasema hii ni ya wamisonari. Sasa yesu anaongea na wanafunzi wake na anasema wakati unaenda, kuenenda ni kila mahali unaenda kila siku ya maisha yako
Related Media
See more
Related Sermons
See more