God Revealed
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 14 viewsNotes
Transcript
John 1:18
John 1:18
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika mlango ya kwanza vs.18. Tumeangalia sana mistari kumi na saba ya mlangi ya kwanza na ninafikiri utakubali tumeona mambo mingi sana kuhusu Bwana wetu yesu kristo. Ikiwa tulikuwa kortini na tulilzaimishwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha Yesu ni Mungu hizi mistari zitatosha. Lakini kwa kitabu cha Yohana ataendelea kwa milango ishirini na moja mistari mia nane sabini na tisa kutuonyesha Yesu kristo alikuwa Mungu. Yohana hajakuwa na lengo inginge kuandika kitabu chake. Kama nimesema nitakumbusha sisi kila jumapili sababu Yohana aliandika hii kitabu. Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Natumaini sana ikiwa hujaamini, Mungu atafungua macho yako kuona ukweli wa kitabu hiki na utaamini na kuamini utakuwa na uzima wa milele.
Ikiwa unafanya search kwa google kuhusu Mungu utapata orodha kubwa sana. Na nimepata mingi tofauti lakini ukiangalia maswali kumi ja juu ni haya. 1.Mungu Yupo? 2. Mungu ni nani? 3. Mungu ni nini? 4. Kuna Mungu? 5. Mungu ni kweli? 6. Ikiwa kuna Mungu, kwa nini kuna mateso na uovu mwingi sana uliwenguni? 7. Mungu aliyeumbwa na Mwanadamu? 8. Tunaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu? 9. Jina la Mungu ni nani? 10. Mungu amekufa? ukiangalia hii orodha utaona maswali karibu yote ni watu wantaka kujua ikiwa Mungu yupo na ikiwa yeye ni ukweli. Jibu ni ndiyo. Na ikiwa mtu yo yote ameulizwa maswali haya kwa kanisa letu natumaini sana ninyi yote unaweza kujibu karibu yote na wakati unajibu utakuwa na imani na jibu lako, utajua ni ukweli kabisa na unaweza kuonyesha watu kwa bibilia.
Watu wengi kwa hii dunia hata watatumia mstari yetu ya leo kujaribu na kutusadikisha kwa bibilia yetu wenyewe, kwamba Mungu si halisi.
Tusome mstari yetu kwa muktadha yake. Kitabu cha Yohana 1:14-18 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Tuombe:
Sasa kama nilisema uko na watu watasoma hii mstari na watasema unaona! Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Kumbuka unaongea na watu ambao hawajui Bibilia na hawajali muktadha ya mstari, lengo yao ni kuthibitisha Mungu hayupo. Tuko mistari zingine kama Kutoka 33:20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. Kwa nini? Kwa sababu Mungu ni Mtakatifu na kwetu wenye dhambi kuona yeye itatua. Lakini utakuwa na watu kusema uonaona hata Bibilia unasoma inasema huwezi kuona Mungu wako au utakufa, nani anataka kumtumikia Mungu kama huyo? Halafu angalia kama Yesu alisema kwa kitabu cha Yohana 6:46 Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. Halafu Waraka wa kwanza watimotheo 6:16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina. Sasa wakati tunasoma hizi mistari tunaona Baba Mungu hakuna mtu ameona yeye na ni kweli, kwa nini? Angalia Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Roho haina mwili huwezi kiuona roho. Sasa ukianza kuketi na kufikiria hii na kama watu wanasema unaweza kufa moyo kidogo. Na hii ni hitimisho la Yohana kwa utangulizi wake kuhusu Yesu ni nani.
Lakini mstari yetu ya leo inaendelea Vs.18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Sasa kumbuka lengo ya Yohana tena kuandika vitu hivi na tena anajaribu kutuonyesha nini. Unakumbuka? Yesu ni Mungu!!! Anaanza kusema Yesu alikuwa Neno na alikuwa pamoja na Mungu hata alikuwa Mungu, tumeona vyote vilifanyika kwa Yesu, wala pasipo yeye hakikufanyika cho chite kilichofanyika, Ni kusema yeye kwa njia yake kile kitu kilikuwa, nani ni umbaji wa kila kitu? Mungu, hapa anasema Yesu ni Mungu. Tumeona vs.10 ulimwengu ulipata kuwako, tumeiona alikuwa Nuru halisi, Nuru ukweli. Tumeona aliwapa wote ambao walimpokea uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, tuliona Neno, Mungu alifanyika mwili na akakaa kwetu, Mungu alikuwa pamoja nasi. Alikuwa na mwili, miguu, mikono, mdomo, masikio, macho, na tuliona ni Yesu. Na tunafika hapa na Yohana anasema tena hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini, Mwana pekee. Mwana Pekee ni nani?
Tuangalian Zaburi 2:17 Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Angalia Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Halafu angalia Mathayo 3:17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Ikiwa uko na shaka yo yote ya huyu ni nani angalia vs.16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, Ni nani? Ni Yesu. Angalia Mathayo 17:5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Tena ikiwa hujui hii ni nani angalia vs.4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; Ni Yesu! Wakati Gabrieli alitangaza kwa Mariamu kwamba atakuwa na mimba alisema kwa Luka 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Huyu ni nani? Angalia vs31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Sijui kwa nini hii ni ngumu sana kwa watu kushika, wasioamini wanakataa kabisa lakini hata mapepo walijua Yesu ni Mwana wa Mungu. Tunapata mtu kwa kitabu cha Marko alikuwa na mapepo mingi ndani yake hata tunaona jina lake ni Legioni kumaanisha walikuwa wingi na Yesu anaingia na angalia kama mapepo walisema Angalia Marko 5:7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Walijua yesu ni nani. Ni kitu cha ajabu sana tunasoma kuhusu mapepo kwa vs.6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; Mapepo wanajua Yesu ni Mungu na hata hawa wanapoga magoti mbele yake. Tunasoma Yakobo 2:19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Yesu ni Mungu bila shaka, Neno la Mungu inatuonyesha hii Mwanzo hadi Mwisho.
Yohana anasema Hatujaona Mungu wakati wo wote lakini Mwana Pekee aliye katika kifua cha baba, ni yeye akiyemfufua baba kwetu, aliyemfufua Mungu kwetu. Wakati tunaona Yesu tumeona Mungu. Wakati tunaona Yesu tunaona Mungu, Kumbuka neno ilikuwa pamoja na Mungu, Neno ilikuwa Mungu na Neno alifanyika mwili. Tuko na mistari kwa kitabu cha Hebrania ni zinatuonyesha hii vizuri sana. Wahebrania 1:1-3 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; Umeona kama vs. inasema? Yesu alikuwa mng’ao wa utukfufu wa Mungu, na chapa ya nafsi yake. Ni kusema alikuwa mwakilishi halisi wa baba, ni kusema yesu alutonyesha Baba kwa sababu walikuwa mmoja. Yesu alikuwa Mungu kwa mwili. Sisi tunaweza kujua Mungu ni nani kwa sababu yesu ametuonyesha, Yesu ni Mungu wetu. Wakati tunafuata yesu tunafuata Mungu. Kila kitu kimeandikwa kwa agano la kale ilikuwa kuweka macho yetu kwa Yesu, Kila kitu ni kumhusu Yesu.
Ni ajabu sana kufikiria mstari yetu lwa Yohana 1:18 kwamba hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Sasa ikiwa tumeishi maisha yetu yote na tumeongea na watu kujaribu kwaambia hawa kuhusu Mungu na tunaeleza hawa, Mungu yuko lakini huwezi kumwona, Itakuwa ngumu sana kwa hawa kuamini. Ni kama mimi kusimama hapa na kusema, niko na Fred hapa na ako na pesa kwako, unamwona? Lakini ako na ako na hii pesa kwa mkono yake, shika tu? Anasimama hapa nami saa hii. Utasema Travisa ameruka akili. Yesu Kristo alikuwa na Aliyemfunua Mungu kwetu.
Ni mistari nne ni mzuri sana zinatusaidia sana kushika ukweli ya Yohana 1:18. Ya kwanza tuangalia Kitabu cha kwanza cha wafalme. Hapa tuko na Sulemani na ameleta Sanduku la Mungu (Ark of the covenant) kwa nyumba ya Mungu. Na tunasoma kwa 8:12 Ndipo Sulemani akanena, Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. Pia tunasoma kuhusu Mungu kwa Zaburi 97:2 Mawingu na giza vyamzunguka. hii ni ngumu sana na ni kumaanisha huwezi kumwona Mungu. Na kwa agano la kale Mungu hakujidhihirisha chini ya sheria. Unaweza kujua nini kumhusu Mtu ambaye anakaa kwa mawingu na giza? Lakini sasa kwa sababu ya Yesu na ametuonyesha Baba tunasoma kwa agano jipya Waraka wa kwanza wa Yohana 1:5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. Tofauti kubwa sana hapa, Kwa siku za sheria Mungu alisema atakaa katika giza na mawingu, hataonekana lakini sasa kwa gani jipya kwa njia ya Yesu tunasoma Mungu ni Nuru na sasa kwa sababu ya Yesu vs.7 tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi. Ni ajabu sana. Kwa wakati wetu sisi tumebarikiwa sana. sisi tumezaliwa kwa wakati Yesu kristo ameshaa kuja, tunajua story yake, tuko na neno la Mungu mwanzo hadi Mwisho, sisi si kama wale wa agano la kale. Angalia kuhusu hawa kwa kitabu cha Wahebrania 11. Ukisoma hii mlango utaona mashujaa wa imani. Tunasoma kama wamefanya imani walikuwa nai na kusema ukweli inatii mioyo yetu kuona mifano ya kufuata Mungu. Vs.38 inasema wale watu ni watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Na tunasoma kuhusu hawa kitu cha ajabu sana kwa vs.39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; Ahadi gani? na tunasoma vs.40 mwanadishi wa kitabu cha Wahebrania alisema kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, hii ni nini? ama ni nani? Ni Yesu. Wale wote hawajaona Mungu lakini sisi tumeona Mungu kwa njia ya Yesu, Mwandishi wa Wahebrania kama Yohana anasema Mungu alikuwa pamoja nasi, alitembea nasi kwa njia ya yesu kristo. Hata saa hii Kila mkristo ako na ahadi kubwa sana na Yesu, Mungu mwenyewe alitoa hiio ahadi kwetu. Angalia Mathayo 28 na kwa mwisho ya hii kitabu Yesu anatuma wanafunzi wake nje kuhubiri injili na kufundisha watu kumhusu yeye na alsiema kwa mwisho ya vs.20 mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Sisi tuko na kitu ambacho watu hawajakuwa nai kwa miaka elfu mingi, Bwana wetu, mungu wetu ako pamoja nasi, hata saa hii.
Ni mahali ingine ni ajabu sana kuhusu hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tunajua hizi mistari ya Musa wakati Musa aliuliza Mungu kuoyesha yeye utukufu wake. Kitabu cha Kutoka 33:18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. Halafu vs.20-23 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba, kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana. Hata Musa hajaona Uso wa Mungu, Kama kawaida tunajua mtu wakati tunaona uso wao si nyuma yao. Ilikuwa wakati wa Musa, alikuwa kwa wakati wa sheria na Mungu hakufunuliwa katika sheria. Sisi tunaishi kwa wakati wa Neema. Sisi wakati tunaoa Mungu hatuoni nyuma yake lakini sisi tunaona uso wake. Waraka wa pili wakorintho 4:6 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Sisi tumeone utukufu wa Mungu kwa uso wa yesu. Hii ni ajabu sana. Yesu ametuonyesha mungu kwa sababu yeye ni Mungu.
Kama nimesema hizi mistari kumi na nane in utangulizi wa Yohana na kila kitu ni kumhusu Yesu. Yesu ambaye alikuwepo katika ushirika wa karibu na baba tangu milele, alifanyika mwili, alituonyesha sisi binadamu Mungu ni nani, alituonyesha neema na ukweli kamili. Na kama alifanya hii yote ni kama tutasoma kwa kitabu hiki cha Yohana. Kumbuka hii yote iliandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Leo asabuhi ikiwa hujui Yesu Kristo, hujui Mungu, Ikiwa hujui Mungu bado wewe ni msioamini na mbele yako ni hukumu. Nitaomba, tafadhali, waacha kucheza na vitu hivi na jikabidhi kwa Yesu, tubu kwa dhambi zako na amini kwamba yeye ni Kristo, mwana wa Mungu na utakuwa na uzima wa milele. Ukitaka kuongea zaidi sisi tuko hapa. Baada ya ibda yetu unaweza kukaa kwa kiti chako au kuja mbele na niambie unataka kuongea zaidi.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
