Doctrinal Statement Pt.15
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 18 viewsNotes
Transcript
God’s Decree 6
God’s Decree 6
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu kama sisi haoa kwa AIC Sekenani tunaamini au Doctrinal Satatement yetu. Natumaini sana umeanaza kujua kama bibilia inasema na kama kanisa lako linaamini na hata wewe mwenyewe unaweza kutetea kweli hizi tukonai kwa sababu ni Neno la Mungu wetu.
Kwa wiki tano tumeanagalia amri za Mungu au kwa kiingereza tunasema The Decrees of God. Tumeona kama Mungu wetu anafanya vitu, tumeona tabia ya Mungu wetu na pia tumeona sisi ni nani kwa hii yote. Tumeangalia sana jambo la wokovu kwa sababu ni hii watu wanachafua zaidi ya kila kitu kwa sababu kusema ukweli ni kuhusu sisi. Sisi tunaweza kuweka mungu juu sana na kukubali yeye anatawala juu ya kila kitu ni Bwana wa Mabwana Mfalme wa mifalmel, Muumba wa vitu vyote lakini wakati tunaongea kuhusu wokovu, sasa wokovu ni wetu, ni kitu sisi tumefanya, ni sisi tumepata Yesu, ni sisi tumeomba sali fulani. Wakati nina ona kama neno la Mungu linasema na ninaona kama watu wanafanya bila shaka Mungu hafurahishwi nasi. Hii ni tabia ya sisi wanadamu, sisi tumejaa na majivuno na tunataka kujiweka juu na kupata sifa tunafikiri tunastahili. Lakini tukisoma vizuri kama Neno la mungu linasema linpinga sana kila kitu tunachoamini. Tumeona hii kwa wiki tano hapa kwa masomo yetu. Ni mstari moja ukwlei moja ni mzuri tunaweka kwa mawazo yetu. Yona alikuwa tumboni la samaki kubwa na alsiema kwa mwisho ya Yona 2:9 Wokovu hutoka kwa Bwana.
Tusome kwa kitabu chetu mlango wa tatu namba 6. Just as God has appointed the elect to glory, so he has by the eternal and completely free purpose of his will foreordained all the means. Therefore, those who are elected, being fallen in Adam, are redeemed by Christ and effectually called to faith in Christ by his Spirit working at the appropriate time. They are justified, adopted, sanctified, and kept by his power through faith to salvation. No one but the elect are redeemed by Christ, or effectually called, justified, adopted, sanctified, and saved.
Tena tunasoma ya kwamba wokovu ni ya Mungu. Ni Mungualivyoteua wateule kupata utukufu. Ni njia mbili tunaweza kuagalia wokovu, njia moja ni kila kitu ni kuhusu sisi. Na watu wengi kwa hii dunia ambao wanasema hawa ni wakristo wanaona wokovu naam na hiyo. Njia ya pili ni kila kitu ni kumhusu Mungu, hii ni njia bibilia inatuonyesha, hata wokovu ni ya Mungu na ni yeye amwapea wale ambao amechagua kupata utukufu. Njia hizi mbili ni tofauti kabisa. Hi ya kwanza inaleta majivui kwetu kama ni sisi tumefanya kitu kuapata hii zawadi ya Mungu, halafu tunaanza kutegemea matendo yetu. Lakini njia ya pili inaleta nyenyekevu na inaweka utegemezi wetu kwa Mungu. Angalia Waraka wa pili wathesalonike 2:13-14 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Sasa unaona kwa hizi mistari Paulo anaongea kuhusu wokovu na hasemi pongezi wewe unafanya kazi njema na wewe umefanya hiii ama hii lakini kwa jambo la wokovu anasema sisi tunamshukuru Mungu, kwa sababu Mungu amekuchagua tangu mwanzo mpate wokovu. Vs.14 tunaona Paulo na mitume wengine wanahubiri injili, wanafanya kazi mingi kusafiri na kuonyesha watu njia ya kweli na anasema Mungu aliita wale watu kwa njia ya neno lake kuhubiriwa, Paulo na wengine walikuwa waminifu kufundisha wengine kuonyesha hawa ukweli wa Yesu kristo lakini bado ilikuwa Mungu kuiita hawa.
Tunasoma kwa Doctrinal Staement yetu Mungu anachagua watu kwa utukufu naam na gani, Kwa kusudi huru kabisa la mapenzi yake na ameteuwa njia na namna zote za kufikia lengo hilo. Tena wokovu ni ya Mungu. Ikiwa umefikiri umeokoka na ni kwa sababu ya kitu fulani wewe umetenda, na unaweka imani yako katika ile kitu ulitenda, bado wewe hujaokoka. Lakini ikiwa Mungu amefungua macho na mawazo yako kuona ukweli wa neno lake na amekuleta kutubu na kuamini na umemkiri Yesu kuwa Bwana kwa sababu umeshika wewe ni nani na yeye ni nani, hii ni Mungu anafanya kazi yake moyoni mwako. Unaweza kuwa na uhakika wa wokovu wako kwa sababu ni Mungu amefanya kzai yake si wewe umefanya kazi fulani. NA umeshika kabisa ni neema yake ametenda hii kitu kwako, si lazima lakini ilikuwa kwa mapenzi yake. Na ni yeye ameweka mpango ya kila kitu ambacho itafanyika kwako kuokoka dakika ile. Labda rafiki yako ameingea na wewe kuhusu Yesu na badaye amekukaribusha kwa kanisa na ulisikia neno la Mungu kufundishwa hapo na uliamini na ulitubu siku ile, haikuwa kwa bahati ulikuwa hapo siku ile, dakika ile, ilishaa pangwa itakuwa kama hii.
Kwalo, wale waliochaguliwa , wakiwa wameanguka kiatika Adamu , wakaombolewa na Kristo. Tena sisi tumeanguka au tunaweza kusema kwa sababu ya baba yetu yote Adamu na dhambi alitenda tulikuwa wafu. baba yetu ya kwanza alituleta kifo lakini Yesu ametuleta uhai. Hata kabla ya alizaliwa ilitabiriwa Yesu atafanya hii anagalia Luka 1:68-69 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu. Ukisoma hii vizuri utaona kitu cha ajabu, Yesu alikuja amewajia watu wake, si kila kila mtu na inasema kuwakomboa, tena si kila mtu, ni watu amechagua kuokolewa. Tena ikiwa umeokoka leo asabuhi toa shukrani kwa Mungu kwa mapenzi yake amekuokoa, hatujui kwa nini, lakini unaweza kusema asante Mungu.
Sisi tunaamini Tumeitwa kikamilifu kufikia imani katika Kristo. Unasema uko na imani? Pongezi, hata hii imani uko nai ni zawadi ya Mungu amekupea Waefeso 2:8 mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; Na hii yote ilikuwa na mpnago na kupitia Roho wake afanyaye kazi kwa wakati ufaao. Wakati hii imefanyika kwako halafu umehesabiwa haki, umefanywa wana, kutakaswa, na kuhifadhiwa kwa nguvu zake kupitia kwa imani hadi wokovu. Sisi watoto wa Mungu ambao amechagua tunapata baraka mingi sana. Tumehesabiwa haki, Hi ni nini? Kwa sababu ya Yesu sisi tunasiama safi mbele ya Mungu. Na alituchagua sisi kuwa naam na hiyo kwa njia ya Yesu. Pia tumefanywa wana. Mungu alituchagua kuwa watoto wake. Wenye dhambi ambao hawataokoa si wana wa Mungu tunasoma hawa ni wana wa hasira au ghadhabu Angalia Waefeso 2:3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Hii mstari inasema sisi tulikuwa naam na hiyo halafu tunaona vs.4 kitu inafanyika, ilikuwa nini? Ilikuwa pastor alituombea! Sisi tuliomba sali fulani? Ulipata Yesu? Inasema nini? Vs.4-5 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Ukisoma vizuri unaona kwa hizi mistari Mungu anafanya hii kazi yote ndani yetu.
Pia sisi wakati tunachaguliwa tuko na baraka ya Utakaso. Wewe utakuwa toafuti kabisa. huwezi kuendelea kusihi kama ulisihi, huwezi kuishi kama watu wa hii dunia, wasioamini. Angalia Waraka wa kwanza wakoritnho 6:9-11 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Vitu hivi ni mbaya sana na anaendelea kusema Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu. Sisi kwa sababu Mungu alituchagua tumetakaswa kuwa watu ambao ni watakatifu kwa utukufu wa Mungu. Waraka wa pili wa korintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Baraka ingine ya kuchaguliwa na Mungu ni tumeokolewa. Sisi ni kondoo yake sasa, sisi tumetolewa kutoka ufalme wa giza na dhambi na kifo na tumewekwa kwa ufalme wa nuru na haki na uhai. Wakati Yesu alituma Paulo tulisoma kama alisema na sababu alituma Paulo kwa kitabu cha Matendo 26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. Tumeokolewa. Sasa kwa sababu tunaamini hii ni lazima tunaishi maisha yao tofauti, sisi tunataka kumpendeza Bwana wetu.
Asanteni sana, kuna maswali?
