Doctrinal Statement Pt.16

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 15 views
Notes
Transcript

Gods Decree 7

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu kama sisi hpa AIC Sekenani tunaamini au Doctrinal Statement yetu. Tumeangalia sana Amri za Mungu au Decrees of God na kama nimesema mara mingi hapa, hii yote ni muhimu sana kwa sabau kama unaamini ni kama utaishi maisha yako. Na akam tunaamini kuhusu amri za Mungu ni kama tunaamini Mungu ni nani na kazi yako ikoaje. Tukiamini sisi ni sababu ya wokovu wetu tutaishi tofauti sana, tutakuwa na majivuno na mambo mingi lakini tukiamini kama bibilia inasema kwamba wokovu ni ya Munngu na ni yeye anapea kwa watu ambao amechagua, tena tutaishi miahsa tofuati, italeta unyenyekevu, shukrani, na mambo mingi.
Leo ni mwisho ya kama tunaamini kuhusu amri za Mungu lakini natumaini sana umeona Mungu ni juu ya kila kitu na anafanya kama anataka, hata kwa wokovu wetu. Hata wokovu wetu ni yake na ni haki yake kupea kama zawadi kwa wale ambao anataka. Bibilia ni wazi kabisa kuhusu hii lakini binadamu hawapendi na wanaanza kufundisha tofuati.
Tusome pamoja sura ya tatu namba 7. The doctrine of the high mystery of predestination is to be handled with special prudence and care so that those heeding the will of God revealed in his Word and obeying him may be assured of their eternal election by the certainty of their effectual calling.18  In this way this doctrine will give reasons for praise,19 reverence, and admiration of God, as well as humility,20 diligence and rich comfort to all who sincerely obey the gospel.
Kwa sababu vitu hivi ni ngumu sana kuelewa kwa watu wengi na kusema ukweli sisi hatuwezi kueleza kila kitu kuhusu hii mafundisho kwa sababu hatuwezi kusema kwa nini Mungu alichagua huyu na hajachagua huyu mwengine kusema ukweli hii ni siri yake. Lakini tunajua kwa neno lake inasema vitu hivi, na Mungu na juu ya kila kitu na kila kitu hata sisi ni yake na anaweza kufanya kama anataka. Unaweza kukataa au kuamini lakini bado uchaguzi wa Mungu wa watu wake ni kama Bibilia inafundisha. Kwa sababu hatujui hii siri yake ya kwa sababu gani anachagua kama anachagua, sisi tunaamini inafaa kuangaziwa kwa umakinifu na tahadhari maalum, Hii ni kusema lzima tuchunge sana kama tunafunza na kama tunaongea kuhusu vitu hivi. Lazima si kama sisi tunafikiria lakini kama bibili inasema na hatutaki kuongeza au kutoa vitu kwa uchaguzi wa Mungu. Na tunaamini wakati tunafanya hii watu wanaozingatia mapenzi yaliyofunuliwa katika neno lake, na kupeana utiifu kwayo, wakaweze, kutokanana hakika ya mwitowao kikamilifu, kuhakikishiwa uteule wao milele. Na sasa hii ni muhimu zaidi. Mimi ninataka ninyi yote ambao unajua Mungu amekuokoa, bila shaka wewe mwenyewe unajua umebadilishwa na Mungu kuwa na hii uhakika ya kwamba wewe ni mmoja wa waliochaguliwa, na utaishi maisha yako bila shaka na kwa unyenyekvu kujua ya watu wote wa hii dunia mwanzo hadi mwisho mimi, nimepewa hii zawadi kutoka Mungu. Tuko na mstari moja Paulo aliandika na ni mzuri sana ni Wafilipi 2:12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Hii ni muhimu sana, Tafsiri nyingine wanasema kufanyia kazi wokovu wako hapa inasema utimizeni wokovu wenu, yote ni kusem ahakikisha wewe ni moja wa Mungu, hakikisha ni yeye amekubadilisha. Utajua naam na gani? vs.13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Si wewe ni Mungu ndani yako anatenda kazi yake.
Ni mahali ingine Paulo aliandika kitu kama hii na ni mzuri sana kwetu sote kufanya kama anasema hapa ni Waraka wa pili wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. Unataka kujua ikiwa wewe ni moja wa Mungu? Jijaribuni. Hii mtihani ni wewe mwenyewe unajua, hakuna mtu anaweza kuhakisha wewe ni Mkristo, hakuna mtu mwengine anajua moyo wako, mawazo yako ni wewe peke yako. Ni ukweli wengine wanaweza kuona matunda ya maisha yako lakini si kumaanisha bila shaka wewe ni mkristo. Jijaribuni kuona ikiwa imani yako ni ukweli. Ikiwa unajipima na unaona wewe ni fake, imani yako si ukweli umeanguka mtihani na ni mzuri unafanya kila kitu unaweza kujua Yesu kristo. Usiendelea kujidanganya kwa sababu ya majivuno au kufikiri watu watasema nini, usijali wengine sisi tunaongea kuhusu milele yako na roho yako. Lakini ukijijaribuni na unapata imani yako si uongo, pongezi sana, wewe ni moja ambaye kwa kwa sababu ya mapenzi yake amkekuchagua. na wakati unapata kweli wewe ni moja wake sisi tunaamini hii uhakika italeta sifa. Sifa ambaye inatoka moyo safi, unaweza kusema pamoja na Daudi kwa Zaburi 28:7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru. Utatembea kwa maisha haya na shukrani kwa kila jambo kwa sababu Mungu amehuchagua na uko sawa. Angalia Zaburi 118:6 Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Wewe ni yake, italeta faraka kwako italeta amani kwako na unaweza kutoa sifa kwa kila kitu.
Pia wakati umeshika hii ukweli italeta heshima na adha,a kwa mungu. Utajua ya kwamba ni neema ya mungu maishani yako, utajua hii yote si wewe ni Mungu wa kila kitu na amekuchagua kuwa mtoto wake. Ni yeye alilkuwa na umilele wako mikononi mwake. Ako na nguvu sana. Sulemani alisema kwa Mithali 9:10 Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Wakati umeshika Mungu wako ni nani kweli kweli inaleta heshima.
Wakati umeshika hii yote, Mungu ni nani na wewe unajua wewe ni nani inaltea Unyenyekevu. Uko na nini ukweli? Ni nini kwa jambl la wokovu wako inaweza kuelta majivuno? Mtru ambaye ni wafu anaweza kuchukua sifa gani? Angalia zaburi 69:32 Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Wakati sisi tuntii Mungu wetu kwa njia ya neno lake inaleta faraja, amani, inasukuma sisi kumpendeza Mungu na kila kitu. tamaa ya mioyo yetu itakuwa kumpends Bwana wetu kwa moyo wetu wote, kwa roho zetu zote, na kwa akili zetu zote. Kusema ukweli Mungu wetu ni waajabu. Na tunaona kazi yake yote kwa hii dunia na kila kitu ameumba na sisi kusema ukwlei ni kitu kidogo sana, kusema ukweli sisi ni punje ya mchanga katika mto mkubwa na bado Mungu wetu alinipenda, alinichagua kuwa mtoto wake na kupata baraka zote ndani yake, baraka za kumjua yeye na kupata msamaha na uzima wa milele. Huyu ni Mungu wetu.
Asanteni sana, kuna maswali?
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.