The Lamb of God

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 8 views
Notes
Transcript

John 1:29

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika mlango wa kwanza vs.29. Kitabu cha Yohana imejaa sana na vitu vingi sana na tumefika vs.29 tu. Fikiria wakati tunafika mwisho ya kitabu hiki na vitu tutajua na tumeona. Natumaini sana hata ninyi tayari umeona vitu vingi na imesaidia maisha yenu ya mkristo kujua Bwana wako zaidi. Natumaini sana umeona lengo ya Yohana kuandika hii barua yake kama amesema kwa Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Tumeona Mtume Yohana, mwandishi ya kitabu hiki kutuonyesha hii sana kwa vs.1-5. Alituonyesha bila shaka yo yote, kwamba huyu mtu anaitwa Yesu ni Mungu. Pia tumeona aliandika kuhusu shahidi mwingine anaitwa Yohana Mbatizaji. Tumeangalia huyu sana na huduma wake alikuwa nai na kazi yake alifanya na sababu yake alitumwa na Mungu kufanya na ilikuwa kutangaza Masihi amekuja. Leo tuananza kutoka binadamu na tutaona huyu wanasema anakuja, huyu ambaye alikuwa tangu mwanzo huyu ambaye ni nuru ya ulimwengu, huyu amabye alikuwa uzima na vitu vyote vilifanyika kwa huyo, sasa huyu amefika.
Mstari yetu ya leo ni ajabu sana. mwandishi moja alisema “ KIFUNGU hiki kina mstari ambao unapaswa kuchapishwa kwa herufi kubwa katika kumbukumbu ya kila msomaji wa Biblia.”
Mwandishi mwengine alisema kuhusu mstari yetu ya leo “ Nyota zote mbinguni ni angavu na nzuri, na bado nyota moja inapita nyota nyingine kwa utukufu. Hivyo pia maandiko yote ya Maandiko yamevuviwa na yana faida, na bado baadhi ya maandiko ni tajiri kuliko mengine. Kati ya maandishi kama haya aya ya kwanza mbele yetu ni moja kuu. Kamwe hapakuwa na ushuhuda kamili zaidi uliotolewa kwa Kristo duniani, kuliko ule uliotolewa hapa na Yohana Mbatizaji.”
Kusema ulkweli hii mstari yetu ya leo ni tamu sana. Tusome mstari yetu Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Tuombe:
Ajabu sana! Kama Yohana Mbatizaji alisema hapa ilikuwa ajabu kwa sababu ya mahali ilifanyika. Mafarisayo walituma watu kuuliza maswali kwa Yohana, walifikiri labda yeye ni Masihi, Eliya au nabii. Hawa wanajaribu kutafuta nabii na tamaa yao ilikuwa atakuwa mfalme ambaye atatoa hawa chini ya uzito wa roma. Hawajataka Mwokozi. Kitu cha kwanza tunasoma ni siku ya pili yake. Sasa hii siku moja baada ya mafarisayo walitumwa watu wao kuongea na Yohana Mbatizaji. Ukihesabu hizi masiku, utapata siku walutimwa kwa Yohana na kufika mlango wa pili vs.1 Kwa harusi huko Kana ilikiuwa wiki moja.
Halafu tunasoma Yohana amwona Yesu anakuja kwake. Hapa ingekuwa ajabu sana kwa Yohana. Ni yeye tu alijua Yesu ni nani, fikiria furaha Yohana alikiuwa nai kuona Yesu, Masihi wao kufika uko nyikani. Tena Yesu alipata Yohana kama anapata sisi. Alikuja kwake, si yesu alipotea ni binadamu. Labda unakumbuka wakati Yesu alikuja kwako? Labda unakumbuka ulikuwa wapi au ulikuwa na shida gani na ulisikia neno lake na ulijua wewe ni nani na ulitubu na uliamini. Labda alikuja wakati ulikuwa chini sana, au labda wakati ulikaribishwa na rafiki kufika mahali inaitwa kanisa na Yesu alikuja kwako kwa njia ya neno lake na ulimwona, uliamini na alikuokoa. Kumbuka furaha, na amani na shukrani ulikuwa nai, kwa sababu ulikuwa mbele za Mungu. Nataka sisi sote kukumbushwa ya kwamba, kila siku sisi tuko kwenye uwepo wa Mungu. Na tunapokuwa katika uwepo wa Mungu, haya ndiyo mambo tunayopitia, furaha, amani, shukrani, upendo, faraja. Angalia Wafilipi 4:6-7 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Ingekuwa vizuri kwetu sote kukumbuka siku ile Yesu alikuja kwetu na alituokoa na tuishi kila siku kama ile siku. Ni kama watu wengi wanasahau siku ile na kama ilikuwa na unaona Mkritso ambaye hanafuraha, hanaamaini maishani yake, hakuna shukrani, analalamika kwa kila kitu. Tungeomba na Daudi kwa Zaburi 51:12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Watu wengi wanatumia hii mstari kusema unirudishie furaha ya wokovu wangu, lakini unaona inasema wokovu wako, ni ya Yesu. Mkristo kumbuka siku ile Yesu alikuja kwako na uzito wa dhambi zako ulitolewa na ulipata msamaha na rehema.
Bila shaka Yohana Mbatizaji anakuwa kama hii saa hii, furaha tele na kumbuka sababu Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu kuwa sauti aliaye nyikani na tunasoma Yohana akasema Tazama! Wakati mtu anasema, Tazama! anasema kila mtu sikia, niko na kitu cha kusema naweza kuwa na usikivu wa kila mtu, Kumbuka ako na watu wengi sana wamekuja kwake na anawabatiza na anasema, Angalia, weka macho yako kwa huyu, Huyu ni Mwana Kondoo wa Mungu! Tumeona Yesu kuitwa vitu vingi kwa kitabu hiki lakini hapa kama Yohana alimwita iko na maaana mingi zaidi. Ni kwa maandiko ya Yohana peke yake tunaona hii jina kwa yesu, Mwana Kondoo wa Mungu. Wayahudi walijua sana maana ya mwana kondoo wa dhabihu, historia yao yote ilikuwa kuchinja kondoo, na mbuzi na n’gombe kwa sababu ya dhambi zao. Mungu alidhihirisha wazi, kwamba dhambi na kujitenga kwake kunaweza kuondolewa kwa dhabihu za damu. hakuna msamaha wa dhambi ungeweza kutolewa na mungu bila dhabihu ya damu. Yohana Mbatizaji hajatangaza yeye kuwa neno la Mungu, Kristo ya Mungu lakini Mwana kondoo wa mungu. Kama ametangazwa ilionyesha hitaji ya wayahudi sana. Mwandishi moja alisema “Huwezi kukaribisha Yesu Kwenye kiti cha enzi bila kumpokea madhabahuni.” Hata leo watu wanatumia Yesu kama mrekebishaji wa kijamii, tunatumia maneno yake wakati hatupedni kitu kwa hii dunia au kusaidia familia yetu, hatunashida na yesu kama nabii, ni mwalimu mzuri, lakini kitu cha kwanza tunahitaji ni Yesu ya Msalaba, mahali mwana kondoo wa Mungu alijitoa mwenyewe kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi.
Sasa Yesu, mwana kondoo wa Mungu anasimama mbele ya Yohana, huyu ambaye dhabihu zote za agano la kale zimeonyesha, walimtangulia. Kumbuka ilianza wakati Watoto wa Adamu na Hawa waliingia na tunaona Kwa kiatbu cha Mwanzo 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; Ilianza hapa kwa Mwana kondoo kuchinjwa kama sadaka. Halafu tena tunasoma Kuhusu Ibrahimu wakati alipanda mlima na Isaka na tunasoma kwa Mwanzo 22:7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Halafu tuko na unabii kwa vs.8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka. Yesu kristo alikuwa hii mwana kondoo Mungu alileta. kwa agano la kale kila asabuhi na kila jioni walichinja mwana kondoo hekaluni kumpendeza mungu, Hii yote ilikuwa kuonyesha watu ni Mwana kondoo wa Mungu anakuja na anatimiza hii yote kwa safari moja.
Kumbuka Wakati wayahudi waliishi kwa Misiri na Farao alikataza hawa kutoka, na Mungu alisema atatuma Malaika ya kifo kuua kila mzaliwa wa kwanza lakini alisema kwa Wayahudi kufanya kitu kuwaokoa kutoka na janga (plauge) hili. Angalia Kitabu cha Kutoka 12:5 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. Vs.7 Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. Vs.13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Wayahudi wote walijua maana ya hii na umuhimu wake, hata kila mwaka tangu siku ile mpaka leo wanafanya sherehe kukumbuka hii siku, walijua sana maana na umuhimu wa mwana kondoo.
Halafu tunafika kitabu cha Isaya na tunaina kitu ambacho inashangaza watu, mara ya kwanza tunaona mwana kondoo atakuwa Mwanamume. Isaya 53 yote ni kumhusu Yesu kristo na tunsoma Isaya 53:7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Wayahudi walijua sana hii unabii, Mafarisayo walijua sana hii unabii.
Tunafika kwa mstari yetu kwa Yohnaa 1:29 na Mwana Kondoo Alitambuliwa. Sasa tunajua ni nani. Ni nani Ibrahimu alisema, ni nani damu yake atapakwa juu ya watu wake ili Mungu atatusemehe. Huyu,Mwana kondoo wa Mungu tunaona kitabu cha ajabu kwa ufunuo 5. hapa tumeingia siku za mwisho, Mungu anafunga kila kitu na tunapata hii tukio (scene) mbinguni ambalo linatokea. na ni vitu vimeandikwa kwa kitbu na kimetiwa muhuru saba. Tunasoma kwa ufunuo 5:2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Sasa kwa mbinguni yote na dunia yote wanasema nani astahiliye kufungua lkitbu hiki, lazima ni moja? tunasoma vs.3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Tunasoma ni Yesu anastahili. Kwa sababu ya hii tunasoma vs.11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, Hii ni nambari hata ni ngumu kuhesabu na wanasema kwa vs.12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Halafu tunasoma si malaika peke yao vs.13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. Sasa na tumaini sana unaanza kuona Wakati Yohana Mbatizaji alitangaza Yesu na kusema Tazama, Mwana kondoo wa Mungu, ilikuwa kitu kubwa sana.
Wakati Yesu anaitwa hii, Mwana Kondoo wa Mungu, hii jina liko na maana mingi sana. Ni kusema alikuwa kamili, bila dhambi yo yote. Petro anaingea kuhusu kwa Waraka wa kwanza wa Petro 1:19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. Mara mingi sisi wakati tunafikiria Yesu tunafikiri yeye ni Bwana wetu na ni ukweli na ni mzuri tunamtumikia kwa uaminifu. na ni mzuri tumtii kwa uaminifu kama mfalme wetu, ni mzuri tunasoma mafundisho yake kama nabii yetu. yeye ni mfano yetu ya kufuata kwa maisha haya, pia tunaweka macho yetu mbele kwa siku ile wakati atarudi na ataokoa mwili na roho zetu, lakini ni muhimu sana wakati tunafikiria Yesu tunakumbuka ya kwamba alikuwa sadaka yetu, na sisi tunaweza kuweka uzito wote wetu juu ya kifo chake kwa sababu ilikuwa upatanisho kwa dhambi zetu. Kusema ukweli kila mwaka ya maisha haya tunaishi, damu ya bwana wetu ingekuwa tamu zaidi kwetu, tuko na baraka mingi sana atika bwana wetu Yesu kristo lakini zaidi ya yote ni mslaba wake. Ikiwa hatuwezi kuona Yesu kama Yohana Mbatizaji, ya kuwa alikuwa Mwana Kondoo wa Mungu, halafu sisi hatujui kitu cho chote.
Yohana anaendelea kusema huyu Yesu, mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! alifanya hii kwa njia ya kifo chake. Hapa ni mahali tunaweza kuseam Bwana Asifiwe na ni ukweli. Bwana wetu, Yesu hajakuja hapa kuwa mshindi ya Roma, Mwanafalsafa (Philosopher), hajakuwa mwalimu wa maadili. Alikuja kuokoa wenye dhambi. Alikuja kufanya kitu ambacho mtu hawezi kujifanyia mwenyewe. Alikuja kufanya kitu ambacho pesa, kazi, vitu haviwezi kufanya kutoa dhambi ya ulimwengu. Ni hii peke yake inaweza kuleta furaha ukweli kwa mtu. Ni ajabu sana wakati tunasoma maneno haya ni mambi mingi ndani yao. Yesu ni Mwokozi wetu kabisa. yeye hajakuwa mtu kuongea vizuri kuhusu msamaha kwa dhambi na kuhusu rehema . Bwana wetu Yesu kristo aichukuaye dhambi zetu. Alibeba juu yake mwenyewe. Waraka wa kwanza wa petro 2:24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti.
Sasa mstari yetu inasema alichukua dhambi ya ulimengu. Watu wengi wanaamini kwa mwisho kila mtu ataokolewa kwa sababu hii mstari inasema Yesu alichukua dhambi ya kila mtu kwa sbabu inasema ya ulimwengu. Hii ni uongo. Ni ukweli kifo cha Yesu kilitosha kwa wanadamu wote, kila mtu lakini siis tunajua, watu amabo wamekufa dhambini zao na wako jehanamu leo asabuhi. Kifo chake ilitosha kwao lakini haikuwa na ufanisi kwao kwa sababu hawajaamini. Kusema ukweli Bibilia inafundisha wengi zaidi hawataamini na watateseka kwa milele. Tunasoma mistari kama Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Hii ni ukweli. Halafu tunafika kwa mistari ambazi zinatuonyesha mbele kwa mbinguni angalia Mathayo 25:41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; vs.46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Swali nataka kuuliza leo asabuhi ni hii, Yesu kristo hi Mwana Kondoo wako? Umeaamini? Umetubu? Unafuata yeye kwa njia ya kutii neno lake? Ikiwa humjui yeye nitasema kwako kama Yohana Mbatizaji , Tazama mwana Kondoo wa Mungu, Aichukuaye dhambi ya ulimwengu. Leo asabuhi wewe unaweza kuweka imani yako katiak Yesu, leo asabuhi unaweza kutoka hapa kiumbe kipya, Mfuasi wa Yesu. Ikiwa unataka kuongea zaidi tuko hapa. Kuja mbele baada ya ibda yetu na ongea na mimi au kaa kwa kiti chako na mimi nitakuja kwako. Lakini tafadfhali usitoke hapa bila kujua Mwana kondo wa Mungu, yesu Kristo.
Asanteni sana, Bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.